Mwaka 2010 nikapata post ya kwenda nje ya nchi kwa mkataba wa miaka 2 , baada ya kuondoka nilikuwa napata likizo ya siku 21 au wiki moja. Chakusikitisha tangu mwaka jana mume wangu alianza kubadilika.
Nikirudi likizo mara ananiambia nenda kwenu ukawatembelee. Naweza kukaa wiki nzima lakini anafanya sex na mimi mara 1 tu mpaka naondoka.
Mwaka jana mwezi wa kumi na mbili nilipata taarifa kuwa amezaa na mwanamke wa pale mtaani kwetu na mtoto anamiezi 3.
Mwezi wa kwanza tarehe 12 alikwenda kumtabulisha kwao kijijini pamoja na mtoto na pia hapo hapo ana mwanamke mwingine anamimba anakaribia kujifungua na hao wanawake wote huwa anawaleta pale kwenye nyumba kwetu wanalala kitandani kwangu!
Mimi nategemea kumaliza huu mkataba mwezi wa sita mwaka huu, nimejaribu kuongea na mume wangu na amenitamkia kuwa hanitaki tena.
Nimeongea na wazazi wake mpaka sasa sijapata jibu lolote, roho inaniuma sana kwani nilipokuja huku tulikubaliana vizuri.
Sasa hivi nikienda likizo anafunga chumba hataki nionane naye, nikipiga simu ananikatia,nikituma sms hajibu, naomba ushauri wako dada maji yamenifika shingoni dada.
****************************
Dinah anasema: Pole sana kwa matatizo unayokabiliana nayo. Sina hakika ni kitugani hasa kilipelekea ninyi wawili kufunga ndoa...kwani si ndoa zote zinafungwa chini ya misingi ya mapenzi...wapo wanafunga kwa ajili ya kuanzisha familia? Kurahisisha maisha(pesa), Umri, Mkumbo, kuondoa mkosi n.k
Kutokana na maelezo yako inaonyesha kuwa hamkuwa na muda wa kuzungumza au kuwasiliana kama pea na pengine hamkuweka au hamkuwa na nia/mipango inayofanana ya kimaisha hapo baadae.
Inaonyesha mumeo alitaka sana kuanza familia na wewe ulitaka career vyote ni vizuri na ni muhimu ila vimekutana wakati mbaya na labda kwavile hamkujadili haya mwanzoni kabisa mwa uhusiano wenu kabla ya ndoa.
Hongera kwa jitihada zako za kutaka kurudisha ndoa yako, hakika inauma lakini suala zito kama hili huwezi kulizungumza wakati wewe mwenyewe uko mbali.
Ni vema kuzungumza na mumeo na wakati huohuo kujaribu kuwasiliana na aliewafungisha ndoa Kanisani au wale waliowapa Semina kabla hamjafunga ndoa.
Natambua Ndoa za Kikatoliki zina hatua zake, basi ni vema ukijaribu kuzifuata mara utakaporejea nyumbani.
Umejaribu kuzungumza na wazazi wake ambao kwao kidogo inaweza kuwa ngumu kufanya chochote kwani hujui mtoto wao(mumeo) amekuzungumziaje kabla ya kutambulisha mwanamke mwingine na mtoto.
Muombe Mungu akutie nguvu kipindi hiki uko mbali kikazi lakini pia shukuru kuwa mumeo anakukwepa kwenye kufanya mapenzi...:uwezi jua anakuepusha mangapi.
Maneno yangu sio sheria, lakini nashindwa kujizuia kusema haya:-
Mwanaume aliekosa uaminifu kwa mkewe na kungonoka na wanawake ovyo na hata kuwapa ujauzito hafai kuwa Mume.
Unaweza kushawishika kupigania penzi lako na hata kushika mimba ili umpe mumeo mtoto so that ndoa iokolewe lakini baadae ikakuongezea matatizo zaidi.
Hatua mliyofikia sidhani kama kuna umuhimu wa "kupigania penzi" ni vema kuanza maisha yako upya.
Kisheria unaweza kumtaliki mumeo lakini Kikristo huwezi kufanya hivyo. Sasa kwasababu imani yako ya Dini inakataza Talaka haina maana uendelee kuishi mpweke ndani ya ndoa.
Tusikilize wengine watasemaje...
Pole na kila la kheri!!
------------------
Comments
inaelekea kwa namna fulani mumeo alikubali uende ughaibuni either kwa wewe kulalamika sana, nae akakosa uwezo wa kukuzuia na kwa wakati huo bado ndoa yenu ilikua mbichi sana ambapo alikuhitaji kupita kiasi.
kwa kusema hili sio kwamba nakubaliana na ushenzi alioufanya...lah no, amefanya makosa makubwa hasa kuzaa na mwanamke mwingine, kumtambulisha kwao wakati akijua kua ndoa yenu haijavunjika na bado kumpa mimba mwanamke mwingine kwa hili sidhani kama anayosababu yoyote ya kukueleza kwani ni umalaya na uhuni.
yapo mengi ninayoweza kukueleza ila kwanza tuliza akili zako kwa kila njia unayoweza and then umalize mkataba wako na urudi nyumbani
jiweke katika mazingira ya kujiamini na kua na msimamo thabiti kwani hata kama bado unampenda huyo mtu, yakupasa ukumbuke kua kwa sasa atakua na watoto wawili wenye mama tofati, unaweza ukampenda yeye na kumsamehe ila itakapokuja ishu ya hao watoto waweza ichukia ndoa yako daima.
ukiwa jasiri na msimamo utagundua pia msimamo wake na hivyo itakusaidia zaidi kufanya maamuzi kulioko kung'ang'ania penzi mfu.
njia zote muhimu zikishindikana as you want mpe talaka na uanze maisha yako mapya. kila kitu kinawezekana hata kwenye bible kumeandikwa "waweza mtaliki mkeo kwa uzinzi tu" so the same alichokifanya huyo ni uzinzi mkubwa sana and as per your wishes waweza mtaliki.
ila mengineyo angalia upande wako pia coz sometimes matatizo yanapotokea kama hayo waweza kuta mnahusika kwa pamoja kwa namna moja ama nyingine kuyasababisha.
Eddy
Kingine, hakuna mahali katika maandishi matakatifu katika dini yoyote inakulazimisha uishi na mtu kama huyo wakati hatari unaijua...japo lengo la kuoana ni kuishi pamoja milele kwa raha na shida lakini kiliwekwa kikomo...kwahiyo sheria inayobana ni ya kanisa tuu lakini kwa mungu una haki zote mamii....unaweza kutemana naye tuu ukaanza maisha mapya tena mungu akayakubali na kuyapokea...sio hayo mnayoishi sasa ambayo sidhani hata kama anayapenda...kwanza ni hatari, pili ni magumu utaendelea kuumia tuu, tatu jamaa ameshasema hakutaki, shukuru mungu kwamba amefunguka moja kwa moja japo inauma lakini ukweli ndio mzuri...sasa ukiendelea kung'ang'ania yanayofuata ni majuto..utatamani bora ungejiengua mapema...
Mapenzi yanauma lakini amini hapo huna chako, kubali hasara yaishe uanze upya wangu....
-Imani yenu hairuhusu ndoa ya mke zaidi ya mmoja
-Imani yenu haijui kutalikiana,kuachana...imani zote haziPENDEZEWI NA HILO,ILA IKIBIDI ...
Kwahiyo ndio maana naona kamainawezekana, mkutane wazazi wa pande zote na hawo wakuu wa dini zenu, ili wajadiliane..na hatima itajulikana. Ndio ushauri wangu huo
Tupo pamoja ndugu yangu muda sijaongea hapa kijiweni, lakini tupo pamoja
Kuhusu wewe mpenzi, nakushauri uachane na huyo mwanaume. Kwa sababu amna watoto hence wewe huko mre free to move on. Pili mumeo hakupendi na amekutamkia wazi.
Wanaume ni wengi na huyo si wa mwisho. Wewe mchukulie kama ilikuwa mistake wewe kuolewa nae. Na wala usijutie kuwa wewe ni sababu ya ndoa yako kuvunjika kwa kuwa umeenda kufanya kazi mbali kwani wewe si wa kwanza na si wa mwisho kufanya hivyo.
Mwache ahangaike na hao wanawake zake. Huyo ni malaya maana kama suala lingekuwa wewe huko mbali basi angekuwa na mmoja; sasa iweje kazalisha wanawake wawili???
Hata ungekuwepo huyo bwana angekupa za uso live. Mwache utanambia baada ya miaka mitano jinsi dunia itakavyomfunza adabu; wakati huo wewe akha maisha yanakunyookea ukiwa Mrs fulani na watoto juu.