Mambo vipi!
Hebu leo tulizungumzie hili suala la Wivu, natambua watu wengi wanaamini kuwa Wivu ni chanzo cha kufarakana na kutokuelewana. Baadhi huamua kuficha hisia hizo za wivu kwa vile wanaogopa kuachwa na wenza wao.
Vijana wa sasa ndio wanaongoza kwa kupinga hisia hizi za wivu, lakini tukirudi nyuma enzi zile za Hayati Bibi yangu kumfanya mtu akuonyeshe wivu ilikuwa ni sehemu ya mapenzi na ikiwa mpenzi wako hakuonyeshi wivu ni dalili kuwa humvutii tena (namna ya kumfanya mume awe na wivu ni somo kwenye kufundwa).
Pia wapo wanaopenda kuweka "Wivu" kama ubora wa hali ya chini sana kwenye uhusiano wa kimapenzi na hata ndoa. Ukifuatilia kwa ukaribu utagundua kuwa sehemu kubwa ya watu wanaopinga hisia za Wivu kwenye uhusiano ni ama wanawapenzi zaidi ya mmoja au hawajui Wivu ni nini? kama sio wanachanganya wivu na kuwa "obsessed"(kwa kiswahili ni?).
Inashangaza unapomkuta mtu anataka mpenzi wake awe mlevi wa penzi lake (addicted) lakini hataki mpenzi huyo awe na wivu juu yake....hapo huwa najiuliza ikiwa unamkolezea mwenza wako mapenzi motomoto kiasi kwamba unakuwa "tiba" yake na bila tiba hiyo hajiwezi tena, kwanini asiumie kihisia ikiwa haupo karibu yake au umechelewa kurudii nyumbani?
Wivu ni hisia kama ilivyo penzi, hupangi au kuchagua bali inatokea tu. Wivu mara zote uhusisha mtu wa watatu, inaweza kuwa jirani, rafiki, mfanyakazi, mpenzi wa zamani n.k.
Wivu hauna tafsiri wala sababu kama ilivyo kwenye hisia za kimapenzi, anaekupenda siku zote huwa hana sababu ya kukupenda bali hutokea tu anakupenda, japokuwa kukupenda huko kunaweza kuongezeka siku hadi siku kutokana na matendo mema au mapenzi unayompa n.k basi hata wivu ni hivyo hivyo na huongezeka kutokana na matendo mema na mapenzi unayotoa.
Wivu unaweza kuwa maumivu ya hisia (mtu unakonda tu...lol), hasira, Uoga, hofu, na huzuni. Vilevile wivu unaweza kujionyesha kwa mhusika kuwa mfuatiliaji, muuliza maswali, uhakiki wa muda/mahali au kutaka kujua maisha ya mpenzi wako ya kimapenzi kabla yako.
Wivu unahimarisha uhusiano na kukufanya uhisi/ujue kuwa mwenza wako anakujali, inakufanya wewe mpenzi kuona namna gani unamrusha roho japokuwa mmekuwa pamoja kwa miaka mingi.
Wivu mzuri nii ule unaokwenda sambamba na na mapenzi na kujaribu kumsukuma mtu wa 3 ambae labda humuamini mbele ya mpenzi wako kutokana na mazoea yao.
*Kuna ila hali ya kutomuamini mpenzi kwa vile tayari amewahi kukutenda, au umewahi kumfuma na mtu mwingine "wakidukuana", hali hiyo sio Wivu kama wengi ambavyo huita bali ni kutomuamini mwenza wako.
Pia kuna ila hali ya "umilikishi" kwamba kwa vile tu ni mpenzi wako basi hutaki awe karibu na mtu yeyote....yaani ni marufuku hata kwenda kwao, shughuli zote za kutoka unazifanya wewe kwa vile unahofia watu wengine watamuona na kumtamani....wengi huita wivu, lakini kiukweli sio wivu ni kuwa "obsessed".
Kila la kheri.
*Samahani L inagoma-goma kwani mwanangu kaing'oa hivyo nahitaji kubonyeza kwa nguvu na mie nasahau kutokana na mwendo wa haraka wa kuchapa.....

Comments
Maana yangu ni hii..
-Kuwa ni GF/BF or wife/hb pasipo walau kuonyeshana a piece of wivu is direct show that 'there is no true love in somehow' becouse inamaanisha kwamba no one anayemjali mwenzake or kuumia kumwona mpenzi wake kuwa na 'kirambas' mwingine..
Dada Dinah kiukweli kabisa 'bibie wangu' akipea mkono na jidume lolote na wasipoachia mikono kwa muda kidogo,huwa ninachafukwa vibaya...Ni sawa ninamwamini but kuwa na doubt mara nyingi muhimu kwa maana wapo wanaoweza kushawishika..
'regards to all'
Pia kama mtu upo katika mahusiano, ni vizuri kuhakikisha kuwa ukaribu wako na marafiki zako wa jinsia nyingine unapungua kupita ukaribu wako na mweza wako, kuna mipaka ambayo rafiki anatakiwa aiheshimu katika mahusiano yako...kupiga simu usiku wa manane kutuma sms zenye sexual content si uungwana!!!!
Wivu uwe wa maendeleo lakini isiwe kila unapomuona mume/mkeo anaongea na mtu fulani basi kiroho juujuu na maswali juu yake kibao.Please bear in your mind that "Humans beings are social beings. Unapokosa imani na mpenzio.mume/mkeo ni dalili za kwamba una kasoro fulani hivi.Kuna rafiki yangu anaulizwa na mkeo kila saa anapigiwa simu uko wapi, ukona nani?unafanya nini na mambo kibao kiasi cha kuleta kero. Juzi aliamua kumwambia ikiwezekana awe anafuatana naye kila aendako.
Naamini kama kweli kuna upendo wa kweli kati ya watu wawili basi wivu wa maendeleo utakuwepo ule ambao unakaa na mpenzio.mumeo.mkeo mnaona mambo ya watu mema na yenye tija katika mahusiano ambayo mnaweza kuyafanya pia mkijiweza.lakini ya kuulizana ulikuwa unaongea na nani sijui ulimpa nani ride nk ni upuuzi tu.
Namshukuru mke wangu hana mambo ya kijinga hayo.Na siku moja aliniambia kuwa wewe ni mtu wa watu wengi, nami nimekukuta ukiwa ulikuwa na watu wengi uliosoma nao mashuleni, vyuoni, nk,hivyo sina muda wa kuchunguza nani na nani unawasiliana nao kwani umuhimu wangu ni kuangalia mambo yetu tunayoweza kuyapanga pamoja kwa ajili ya afya ya ndoa yetu na maendeleo yetu ya kimaisha.Na aksema sitaki kujianzishia magonjwa yasiyo na sababu bure.
Hajawahi kugusa simu yangu wala nini, hata nikiiacha siku nzima hapo chumbani itaita hatapokea.Kinachompa ujasiri huo ni vile anavyoniamini na kunipenda na anavyojilinda kwa nafsi yake pia.Kwa kweli namheshimu sana kwa hayo na niko muwazi kwake kwa jambo lolote.
Nina picha nyingi za marafiki zangu toka huko nyuma waume na wanawake wengi wao aliisha wajua na hana taabu nao hata nikiongea nao.Imesaidia sana kumjali na kumheshimu sana kupita kiasi.
Si rahisi kumzuia ndege kupita juu ya kichwa chako, lakini ni rahisi kumzuia ndege asijenge kiota juu ya kichwa chako.
..pia kuna watu sio kwamba wana wivu ila ni kwamba hawajiamini na wanahisi penzi lao lipo cuz wamelazimishia hao unaweza dhani wana wivu na wanakupenda kumbe walaaa...wanaangalia life security tu na sio love..
so mtu kuwa na wivu na wewe muangalie kwa jicho la tatu haimaaniishi anakupenda sana na anatrue love au hacheat ..anaweza kuwa na wivu wa kuzuga tu ili kuwa na wewe for his/her own reasons..hasa wanawake wanazo sana hizi...
Gluv
gluv100@yahoo.com
,,,wivu wa wastani hudumisha mapenzi,,,
,,,i like it