Sio pesa....Lol!!
Hakuna mtu asiependa kuwa na uhusiano wa kimapenzi mzuri na wenye afya, mimi binafsi napenda sana kuona watu wanapendana, huwa napata maumivu na wakati mwingine hasira ninaposikia au kupata kesi ya uhusiano au ndoa kuvunjika.
Wakati wa kufundwa mara zote niliambiwa kuwa ukizubaa mapenzi kati yako na mumeo hayatokuwa kama mtakavyoanza hivyo basi unahitaji kuwa mstari wa mbele kuhakikisha hakuna kuzoeana bali kujuana.
Sasa kwa vile Mfundaji mwenyewe alikuwa ni Hayati Bibi yangu aliezaliwa na kukua enzi za Mfumo Dume aliwakilisha somo kwangu kwa kusema “hakikisha unakuwa mstari wa mbele” lakini kutokana na maisha yalivyo sasa mimi nitasema kwako HAKIKISHENI (wake kwa waume) kuwa hamzoeani na badala yake mnajuana kiundani zaidi.
Uhusiano huwa mtamu kweli kweli unapoanza, hakuna hata mmoja kati yenu anaekumbushwa na mwenzie kufanya mambo/jambo, unajikuta tu unafanya mambo mazuri-mazuri kwa mpenzi wako, uhusiano unaendelea mnafikia mahali mnakubaliana kuishi pamoja part time(mf: mwisho wa wiki tu) au full time kwavile inakuwa ngumu sana kupitisha siku nzima bila kumuona Asali wa Moyo na baadae
ndoa.
Baada ya kuishi pamoja au kufunga ndoa mmoja wenu au wote mnaanza kupunguza speed na hatimae inafikia mahali wote kwa pamoja mnajikuta mnadharau kufanya mambo mliokuwa mkifanyiana awali kwa sababu ya mapenzi......hatua hii ni mbaya sana na ndio huwa chanzo cha ugomvi au kutafuta mtu atakaekufanyia mambo bila kumkumbusha, hatua hii inaitwa KUZOEANA.
Baada ya kuzoeana na ku-miss hamasa, chachu ya mapenzi kutoka kwa mwenza wako, unaanza kulinganisha uhusiano wako na uhusiano wa watu wengine na kuanza kuona wivu na hata ku-wish kuwa mkeo au mumeo angekuwa kama yule au
tungekuwa kama wale n.k.
Sasa nini siri ya mafanikio kwenye uhusiano?
1-Usijisahau na hakikisha unarudisha uliyokuwa ukimfanyia mwenza wako miaka 4 iliyopita, kabla hamjafunga ndoa, yafanye tena sasa. Inawezekana
maisha yenu yamebadilika na sasa mmekuwa familia kwamba kuna watoto,
bado watoto hawakuzuii wewe mume/mke/mpenzi kuwa wapenzi. Ndio ni
baba na mama lakini pia ni Wapenzi.
2-Jipende ili uvutie, usipojipenda wewe mwenyewe na kuvutia itakuwa ngumu kwa
mwenzio kuvutiwa nawe. Kwavile tu mmefunga ndoa au mnaishi pamoja
haina maana ndio mwisho wa kuvutia.
3-Penda/pendezwa,
kukubaliana au kubali mchango wa mawazo yake kwenye jambo mnalotaka
kufanya, mshirikishe mwenza wako kabla ya kufanya uamuzi wowote,
peaneni matumaini na ushirikiano inapobidi....sio kila wakati wewe
ndio msemaji mkuu na muamuzi wa mwisho na yeye ni wa kupokea tu, hata
akichangia mawazo yake huyafanyii kazi(unadharau).
4-Muda, kazi na watoto huchukua muda mwingi na hivyo kutopata muda wa
kuzungumza na kuonyeshana mapenzi, hivyo kutenga muda wenu kama
wapenzi ni muhimu. Ninaposema muda wenu kama wapenzi sina maana ya
kufanya ngono kwani ngono inaweza kufanyika watoto wakiwa wamelala,
nazungumzia ule muda wa ninyi wawili kama ilivyokuwa mf: miaka 4
iliyopita kabala hamjafunga ndoa.
5-Mawasiliano kwa maana ya kuzungumza ni njia pekee ya kumwambia mwenza wako vile unavyojisikia, unataka nini, kwanini umefanya jambo fulani, usaidiwe
vipi, kwanini uko hivyo ulivyo n.k. Hii ni njia pekee ya kuwekana sawa na kuepuka maumivu ya kihisia ambayo yanaweza kukupa upweke ndani ya uhusiano/ndoa.
6-Kubali mabadiliko,
jinsi miaka inavyozidi kusonga ndivyo ambavyo tunabadilika/tunakua,
maisha yetu yanabadilika....japokuwa wakati mwingine mabadiliko hayo
hayaji kama tulivyotarajia bado hatuna budi kuyakubali na kwa pamoja
ku-adopt badala ya kulalamika na kufananisha.
*Mabadiliko yanaweza kuwa upungufu wa hamu ya kungonoka, kupendana zaidi, kuwa wazazi, kuishi maisha ya chini au ya juu kuiko ilivyokuwa hapo awai,
kuugua, ulemavu n.k
7-Kuzozana/gombana kwa maneno, kubishana sio ukorofi inategemea mnabishanaje na kuhusu nini? Katika hali halisi kubishana kwenye uhusiano kunahashiria afya ya uhusiano wenu....ikiwa kuna watu wanaishi pamoja kama wapenzi na hawajawahi kubishana basi ni either wanadanganya au mmoja wao anamuogopa mwenzie.
Pamoja na kuwa ninyi ni wapenzi bado mnatofautiana kijinsia, kimawazo,
kikazi, kipato, matumzi binafsi ya pesa, kimalezi na hata kasoro zenu
hazifanani....hivyo kubishana ni lazima ikiwa kunatofauti hizo na
nyingine ambazo unazijua.
Kubishana kunaweza kuwasaidia mmoja wenu kujirekebisha kwani itawawezesha
kutambua kosa lako ni lipi hasa kama mwenza wako sio mtu wa kukosoa
papo kwa hapo (kosa linapotokea), pia itakuwa nafasi nzuri ya kutambua au kugundua nini hasa mwenzako anafikiria kuhusu kosa/tendo ulilofanya au tabia yako na nini anataka kifanyike ili kuepuka mabishano ya mara kwa mara.
8-Shukuru, omba radhi ni maneno mafupi na pengine unaweza kudhani kuwa hayana umuhimu wowote, licha ya kwamba yanaashiria kuwa umelelewa katika maadili mema pia yanauzito na maana kubwa sana kwenye maisha yetu kuliko unavyofikiria.
Unapohisi kuwa umemuudhi mwenza wako, sio mpaka akununie kwa wiki moja au
akufokee ndio uombe radhi, akionyesha tu kuwa hajafurahia tendo lako
au maneno yako basi omba radhi.
Shukuru kwa kila jambo unalofanyiwa na mpenzi wako....unakumbuka wakati
mnaanza uhusiano akiku-check during the day unasema “asante mpenzi
kwa kunijulia hali”, sasa kwanini ushindwe kusema asante kwa chakula mpenzi?!!
Kila la kheri!

Comments
Welcome back. Happy New Year. Tulikumiss sana sana na naona umeanza mwaka na siri ya mafanikio kwenye uhusiano. Hii ni nzuri sana na inatupa raha wadau wako. Mungu akubariki sana
Ukweli uliyosema theoretically ni rahisi ngumu kuimplemnt kutokana ubinadamu unautufanya "hili nana aanze na kukubali kuwa chini au hali ya umeshindwa"Taasisi hii ni ngumu tumuachie mwenyewe MUUMBA
Ugumu WA YOTE UNATOKANA NA UKWELI WE ARE LIVING ARTIFICIAL LIFE. ZAMANI HAKUKUWA NA TOFAUTI YA MAISHA BAINA YA FAMILIA AU KIJIJI NA UNAPOOA NYOTE MKO LEVEL MOJA NA MLINGANO WA MALEZI. LEO SI RAHISI BINTI ALIYEKULIA KWA WAZAZI WAKE NA MAISHA YAO AJE KWAKO ULIYELELEWA KIVYENU MKAMATCH.USHINDANI NI LAZIMA UJITOKEZE NA ASIPOKUWEPO WA KUSUCCUMB IMETOKA HIYO!!!!
watu wanajisahau sana...mwisho wa siku mtu anacheat
gluv
Umempenda mtu na mkakubaliana kuishi pamoja wote mkiwa wazima (bila kilema) na maisha mazuri.....Mara mwenza wako anapata ajali na kupata ulemavu....penzi ako itaisha na utamterekeza au utakubali mabadiliko na kuendelea kuishi nae?
Au ikitokea wote mmepoteza kazi au bishara hazijaenda vema na hakuna pesa, je mtaachana au mtakubali mabadiliko na kuendelea kuwa pamoja na kujitahidi kuinuka tena kama wapenzi?
Mimi kama Dinah na Mume wangu tumepitia mambo mengi magumu, tulikubali mabadiliko na kuendelea kuwa pamoja mpaka tulipoweka mambo safi na sasa tuko sawia kabisa.
Nilichokisema ni kutokana na uzoefu, hivyo sio ngumu kama unavyofikiria.
Ikiwa hiyo dawa imetibu na hatimae kuondoa vipele vidogo ni wazi kuwa ndio dawa unayotakiwa kuendelea kuitumia mpaka hivyo vikubwa viondoke pia.
Inawezekana vimechelewa kutondoka kutokana na ukubwa wake nje na ndani, ni vema kurudi tena kwa Daktari ili umueleze matokea ya Tiba uliyotumia na yeye atakushauri kama unahitaji kuendelea kutumia (pewa nyingine) au la.
Uvumilivu ni muhimu ili upone kabisa. Kila la kheri.
Kufanya ngono mara kwa mara hakukufanyi umchoke mwenzio unless other wise hakuna mapenzi ya dhati kati yenu na pia sio wabunifu/watundu.
Kuna namna nyingi sana za kungonoka hata kama mnangonoka kila usiku kwa mwaka mmoja bado hamuwezi kurudia yale yale, hivyo suala la kuchokana nadhani ni la individual.
Kama umejaaliwa uwezo wa kawaida au ule wa hali ya juu wa kungonoka huwezi kufanya ngono mara 2 kwa wiki(HAITOSHI)....Lol!
Asante kwa ushirikiano.
Suala la kukumbukana kwenye uhisano linategemeana na mtindo wa maisha mlionao, uzito wa mapenzi yenu na mahitaji yenu ya kimwili na kihisia.
Mf: kama mna watoto na wote mnafanya kazi sidhani kama mtahitaji muda wa ku-miss-iana kwani huo muda wa kuwa pamoja tu hamna kwani wote mko busy, ninaposema kuwa pamoja sio kuishi nyumba moja bali kutumia muda mmoja kama wapenzi.
Pia ikiwa mnafanya kazi za shifts mmoja anafanyakazi usiku na mwingine asubuhi lazima mta-miss-iana tu.
Kuna watu wanaishi pamoja lakini wakiachana ile asubuhi kwenda kazini huwa wanakumbuka sana kama vile hawajaonana wiki nzima.
Asante kwa ushirikiano.
DAVID, arusha.