"Dada Dinah na wachangiaji wote, tafadhali naomba ushauri au mawazo kwani nipo kwenye kipindi cha kufanya maamuzi magumu.
Nina mchumba wangu ambae tunataka kufunga ndoa, lakini nitakapofunga ndoa nitalazimika kuhama kutoka Nchi moja kwenda nyingine na kuacha ajira yangu.
Kinachonichanganya hasa ni suala la kuacha kazi, yaani mawazo juu ya hilo hunipa maumivu ya tumbo na huonga huniingia.
Naomba ushauri kutoka kwa yeyote aliyepitia hii hali katika maisha yake, asanteni"

Comments
Kuna nchi zingine ukienda utasota hata kama una madigrii na kuna nchi zingine ukienda utapata kazi hata isiyo ya fani ulionayo.Na pia kuna nchi zingine zina kipato kizuri zaidi kuliko zingine.Kuna nchi zingine maisha ni magumu sana hata kama ungekuwa na kazi pesa inaishia kula na kulipa pango.
Ukituambia kwa kinaga ubaga uko wapi na unatarajia kwenda wapi ukiolewa tutakupa msaada wenye manufaa zaidi kuliko hivi sasa tutakuwa tunaelea hewani bila real facts.
Hongera kwa kupata wa kuishi naye milele.