"Thanxs dada dinah kwa ushauri unaotupa wanawake wenzio. Ila dada naomba ushauri wako pamoja na wachangiaji wengine. Mimi nina mahusiano na mume wa mtu na nampenda sana naye ananipenda sana na pia ndio mwanaume wa kwanza kwangu.
Ila dada naogopa mke wake asije kujua, huwa namwambiai huyu mwanume lakini yeye ananipa moyo kuwa hilo halitotokea. Huyu mwanaume ananitunza vizuri tu na pia kaninunulia nyumba na full furniture. Nyumba hii iko mbali na anapoishi na familia yake.
Tatizo wakati ninapomuhitaji huwa simpati kwani unakuta muda mwingine yupo bisy na kazi au familia yake. Dada nifanye nini wakati nampenda sana?"
Dinah anasema:Natambua kuwa hii Post itawakera wengi, Mimi binafsi sikubaliani na tabia hii kwani kitendo cha kutoka na mume wa mtu ni Kosa kubwa. Lakini tukumbuke matusi na maeno makali hayatosaidia huyu dada kufanya uamuzi wa maana. Tafadhali mshauri kwa busara bila kum-attack huyu Binti.
Asante!
Ila dada naogopa mke wake asije kujua, huwa namwambiai huyu mwanume lakini yeye ananipa moyo kuwa hilo halitotokea. Huyu mwanaume ananitunza vizuri tu na pia kaninunulia nyumba na full furniture. Nyumba hii iko mbali na anapoishi na familia yake.
Tatizo wakati ninapomuhitaji huwa simpati kwani unakuta muda mwingine yupo bisy na kazi au familia yake. Dada nifanye nini wakati nampenda sana?"
Dinah anasema:Natambua kuwa hii Post itawakera wengi, Mimi binafsi sikubaliani na tabia hii kwani kitendo cha kutoka na mume wa mtu ni Kosa kubwa. Lakini tukumbuke matusi na maeno makali hayatosaidia huyu dada kufanya uamuzi wa maana. Tafadhali mshauri kwa busara bila kum-attack huyu Binti.
Asante!
Comments
Moto ukishakolea kwa kweli kuuzima ni mbinde sana, na hasa kwa kitu kinachoitwa "mapenzi" asikwambie mtu na kama ndio hivyo anakujali na kukutunza na kakununulia house.Hapo mwanamke hata umwambieje hatakusikia.
Na unacholalamika kama nimekuelewa vizuri ni kukosa muda wa yeye kuwa na wewe hasa unapomuhitaji akupe chakula chako cha usiku.Mambo mengine kama vile kuwa ni mume wa mtu hilo sidhani kama linakusumbua.
Ushauri wangu tangaza ndoa naye uwe mke wa pili maana mtafichana hadi lini dada?Ni afadhali kuhalalisha kabisa kuliko kuiba na kula kwa wasiwasi kila kukicha.
Sidhani kama kutakuwa na ushauri wa kukwambia achana naye halafu uone kama linakufaa hilo?Na umesema yeye ndiye wa kwanza,kwa kweli hata ukiondoka hapo bado utarudi tu bibie bora kujenga nyumba ya kutambulika kabisa.Kumbuka siku za mwizi ni arobaini.Hata ufiche vipi vitatokea peupe muda si mrefu.Wewe mwambie tu jamaa kuwa muweke mambo hadharani.Siyo peke yako unayekula bata wa waume wa wenzio mko wengi na kwa style tofautitofauti.Wanawake mko wengi sasa ukingoja wa kwako utampata wapi na lini?
Hizo siku unazomkosa vumilia kwa sababu unajua ana mke mkubwa wewe ukipata moja kwa mwezi au wiki inatosha maadamu anakupa mahitaji mengine mengi.Kakununulia nyumba unafikiri mchezo?Huyo jamaa anakupenda mwenzangu!!!
Ukimwacha utavuna gundu wewe kaa hapo hadi kieleweke.Kama jamaa anakupenda na naamini anakupenda mwambie aingie Uislamu ili akuhalalishe na wewe uwe mke wa pili.
Mimi nadhani umebahatika umempata akupendaye na umpendaye,hilo la mume wa mwenzako potezana nalo nani alikwambi wanaume wanakuwa na mke mwanamke mmoja?Kama ana mke nyumbani , basi ana mwingine nje kwa kujivinjari.
Ni kazi sana kumuacha mtu unaempenda ila pia inawezekana...
Kutoka na mume wa mtu hatari yake huwezi jua mkewe akijua atakufanya nini au atamfanya nini mumewe..hatari sana...
Kama ni waislam basi akuoe uwe mke wa pili sheria ya dini inaruhusu ila kila upande uwe wazi na kupunguza kujificha ...
Pia tafuta mwanaume mwingine wa kuwa nae na achana na mume wa mtu..wanaume wa kupendana nao ni wengi..huyo hadi kaoa sio wako...
pia ni rahisi kupata maradhi kama ukimwi kwani ni hivi mwanaume anaetoka nje ya ndoa huwa hapati muda wa kuwa na mkewe hivyo mwanamke anaweza tafuta wa kumridhisha na matokeo yake anaweza leta magonjwa home na kumbuka wanandoa hawatumii condom na wewe ni wazi hutumii condom na jamaa..mtakufa na ukimwi
pia kuwa na roho ya huruma kwa mwanamke mwenzio..muachie mumewe wakae walee watoto..
Kama unakazi basi fanyakazi yako pata kipato na jiendeshe maisha yako..kukujengea house sio issue kwani wanawake wengi tuu wamejenga na kununua magari na wanasomesha kwa jasho lao ..punguza utegemezi kwa wanaume na jiamini kuwa unaweza jenga na kuendesha maisha yako kama utafanya kazi au business...
kama huna kazi mwambie akupe mtaji na atambae zake
..Ila jaribu kumpa nafasi mwanaume mwingine anaekupenda na achana na huyo kwani hayo ni mapenzi hatarishi kiusalama na kiafya...
karibu
Gluv Love
gluv100@yahoo.com
NOTE:MME WA MTU NI SUMU(AND VISEVERSA)
asante from manyagag@gmail.com
Ila nina wasiwasi kwani wengi ambao walifikia kujengewa majumba huwa CV zao zinakuwa zimeshaenea mitaani hivyo kupata mwanaume wa kukumiliki jumla inaweza kuwa ngumu. Uamuzi ni wako. Ila ulichifanya si kizuri dada na kama na wewe unaamini kuwa si kizuri basi anza sasa kufikiria kuacha hiyo tabia. Kuna magonjwa. Kukununulia nyumba haina maana mko wawili tu (na mkewe). Kuna wanaume wana pesa ya kujengea nyumba jata wanawake wanne. Fikiria magonjwa mdogo wangu. What if the wife is also a cheater??? Chan hiyo ndugu. Huoni kinyaa kuchangia??? Huoni wivu kuwa the other woman??? I wish ungekuwa mdogo wangu I would have stopped you from the beggining. Anyway I hope it is not too late.
Back to the topic; mie ni m/ume na nimeshawahi kutoka nje ya ndoa ila nakiri kabisa kuwa ili ni tatizo kubwa na ninajutia sana kwani w/wake siku hizi utongoza w/ume hasa wakiona ana kipato kikubwa. Binti achana na mme wa mtu inaleta mtafaruku sana kwenye familia ya m/mke mwenzio maana usaliti uonekane kwa wasiwasi tu wa m/ume si lazima akujue sasa kama huyo dada akihamua kufuatilia nyendo za mme wake atajua tu na unaweza kufanyiwa kitu kibaya hivyo vyote ulivyofanyiwa vikakutokea puani
me natamani wanawake wote wanaotembea na waume za watu wapate what they deserve kwa sababu kiukweli inauma sana mumu wako kutembea na mwanamke mwingine..
isitoshe unajidhalilisha sana kuvunjwa bikira na mume wa mtu you are so cheap
am sorry am being so harsh but that the truth though it hurts the only way to escape being called someones' misstress is to quit the relationship with him kwa sababu hapo hakuna real love ni money love na ikiisha utacheka kichina my dear. Pole
Liz
Umeniboa kama nini huna adabu
myzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzz
PS: wisen up! utakuja kuolewa wewe siku moja na mumeo atafanya ivyo ndio utajua utamu wake ***** (nimetukana hapo). haya bye