"Mimi ni mwanamke ambae niko kwenye ndoa miaka minne sasa. Ila ninatatizo naomba mnipe maoni na ushauri. Mume wangu ambae nilimpenda kupitiliza nimegundua amekuwa akitoka nje ya ndoa yetu pale nilipoanza kumufatilia sana ingawa alikuwa mjanja sana.
Kinachoniuma saaana huyo mwanamke aliekuwa akitoknae nilianza kumuhisia kipindi hatujafungandoa, kila siku nilikuwa nikiona msg zake akimtukana mtu fulani ila nikijaribu kumuuliza mume wangu anasema kuwa ni mambo tu ya kazini. Lakini kila nilipokuwa nikiona msg nahisi kusutwa!
Hivi sasa tuna watoto wawili na nilikuwa muamini zaidi mume wangu nakila ninapo shitukia ishu kuwa labda anatoka kusaliti ndoa yetu na kumhoji kama ni kweli, mume wangu anakasirika na kuniomba nipige magoti nisali na kuomba Msamaha.
Nilikuwa nikifanya hivyo na hata yeye kuomba pamoja nami huku maombezi yake yakiwa Mungu atupe tuweze kuaminiana. Hajawahi kupunguza mapenzi kwangu wala kuonyesha ila siku moja nimekamata msg nyingine nikajifanya mimi ni mume wangu na hapo ndipo nilipogundua mwanamke huyo anavyo enjoy na mume wangu.
Kinachoniumiza sana alikuwa akitumia rafiki yake huku mara nyingi nyingi kujifanya kuwa ni mgonjwa anahitaji kwenda hospitoli anadai asindikizwe na mume wangu kumbe ilikuwa njia yakumtoa tu. Akitoka asubuhi kusaliti ndoa yetu anahubiri Kanisani kama kawaida na huku akisukuma Injili.
Yaani nikifikiria hapo nahisi kumchukia, hata mida mingine sijisikii kumpikia kutokana na ahadi nyingi tele tele na huku akionya watu wengi kuhusu ndoa. Naombeni jamani mniambie nifanye nini kumsamehe sijamsamehe ila aliishaomba msamaha nakunieleza kuwa kila nililoligundua ni ukweli! ninaumia sana.
Nilimwambia asubiri nitampa jibu. Sasa mawazoni mwangu najiandaa na nikipata kazi nitamuacha kwani nikifanya uamzi mapema naweza kuumia sijuwi niko sahihi au nakosea?
Hii yote ni kwasababu hakuna njia nyingine ya kumuamini hasa pale anaponiambia yote "tumkabizi Mungu" nahisi hata hilo jina asiwe analitaja. Nikiwa mbali na yeye ninajihisi kufurahi nikimuona nahisi kujinyonga sasa jamani mnasemaje hapo naombeni ushauri wenu. Asante"

Comments
Kwa kuwa amekiri yote, please msamehe na mwambie akirudia utamsemea huko Kanisani hadhrani.
Kosa si kosa bali kurudia kosa.Chukua muda kutafakari na kumhurumia yeye pia kwa dhambi hiyo kwani kuna kutenda kwa kuzingirwa.Tamaa huponza wengi.Mhurumie kwamba hajajijua katika hilo na uone jinsi mnavyoweza kuanza ukurasa mpya wa kuaminiana.
Usimhukumu kwa hilo tu maana umesema anakujali na hajapunguza upendo,huyo ni shetani tu kamzidi kete.Hata wewe una makosa japo hujaambiwa nini na nini unakosa.Hutakujwa kupata malaika asiyekosea. Na abda utakujapata mbaya zaidi ya huyo.
Samehe saba mara sabini na ndoa yako itadumu na kurekebika sana.Ukichukua uamuzi wa kumchukia na kumkimbia utapata mabaya zaidi kwa sababu suluhisho la tatizo ni kukaa ndani ulishughulikie.Ukitoka nje unaongeza ugumu wake zaidi.
Pole dada najua inaumiza sana lakini ndiyo hivyo ulikiri kuwa naye katika shida,huzuni,furaha nk.
Na kwa taarufa yake,mwambie Mungu hajaribiwi wala hadhihakiwa,huo unafiki anaofanya kwa Mungu wakati sio mkweli,atakufa haraka sana,we mwombee tu Mungu atajibu.
Unachohitaji kufanya ni kuwa mvumilivu na pia ujue kusamehe maana usiposamehe sijui wewe utakuwa mwanadamu wa namna gani kwa sababu hata wewe una makosa japo hayajabainika wazi.
Msamehe mumeo na mwambie siku ya siku akirudia makapi utampeleka mbele ya kanisa zima ili limjue kuwa anawahubiria uongo.Ni muhimu chukua biblia halafu mwite kaa naye na muulize ni wapi pameandikwa utoke nje ya ndoa yako? Halafu mwambie kuanzia leo nimekusamehe kabisa,na usirudie.kama K yako ameichoka akuambie nini kinapungua ili ukiboreshe na wala si kubemenda nje.
Kumbuka hasira hasara,ukizidi kumshupalia na hasira utamfanya aendelee kufikiria kupata lishe hiyo huko nje,kwa hiyo mkaribishe na mlishe chakula kitamu yaani ongeza manjonjo katika mchezo, maana inaelekea labda hata wewe hujui kujishughulisha kitandani unabaki kulalama tu.
Kusamahe na kusahau ni muhimu na ndipo ndoa itadumu.
Kwani wewe huna makosa kiasi kwamba umemchukia kiasi hicho licha ya kukuomba msamaha?
Kama anahuburi huyo ndiye mzuri sana kwa sababu anajitega mwenyewe hivyo ni rahisi sana kumtegua na akarekebika na ndiyo maana amekuomba msamaha kirahisi.Wanaume ni wagumu kuomba msamaha.lakini wa kwako amekiri yote na kukuomba msamaha, sasa ulitaka afanye nini zaidi ya hilo?
Yaani wewe unaona hilo ndiyo kosa kubwa hasa kuliko yamkini makosa unayofanya wewe? MSAMEHE MUMEO MAISHA YAENDELEE!! usidhani kumkaushia utatatua tatizo labda ndo utaendelea kumfukuzia mbali zaidi.
Pole lakini maana inaumiza,ila kumbuka kuwa kukosa ni kila mtu anakosea muhimu ni kurekebisha, na lazima ujiulize kwa nini kaenda huko nje,labda wewe ndiye kikwazo.
Ukishindwa kutunza wa ndani watakutunzia wa nje.Wewe utabaki kutunza ndoa wakati wenzio wanakutunzia penzi.
Nimeshamfuatilia sana hadi sasa nimechoka, sina mpango naye kabisa tena na sasa najitahidi kujenga makazi yangu ili nijiandae kuanza maisha mapya. Suala la tendo la ndoa nimesimama kwa sababu sitapenda niache wanangu yatima. Mungu alinisimamia nikawa na nguvu ya kwenda kupima HIV hatua ya awali ni salama, nasubiri nirudie mara ya pili wiki ijayo ili kupata uhakika wa afya yangu then nimpe uhuru afuate hao malaya wake kabisa milele. Nimeshamvumilia sana,ameomba msamaha mara nyingi sana huko nyuma ila mara ya mwisho (mwaka jana 2010 Septemba) alimpata tena binti wa mwaka 1991 muuza duka la nguo na nilipomuuliza alinijia juu hadi kunikaba. Nimemlaani kwa Mungu hata kaa afanikiwe chochote milele. Mungu ataniwezesha mimi kuwatunza watoto kwa kazi yangu na biashara zangu ndogo. Yaani aliiba hadi jewelery zangu (almasi, dhahabu, tanzanite, etc) anaenda kuhonga na kuuza ili apate hela za kuhonga nakupanda ndege kufuata malaya. Kuna mchangiaji amesema pengine unashindwa kumtimizia mwanaume ndo maana anatoka nje,nasema hapana, ni tabia na hulka zao tu kwa maana huyu mume wangu ameishi na wanawake ndani mimi ni wa nne na hakuna aliyeweza kuishi kuvumilia mateso yake hata kwa miaka mitatu, mimi nipo naye miaka saba ya uvumilivu na mateso na nilikuwa namfanyia huduma zote anaonekana barabarani, chupi yake siku zote inaonekana mpya, chakula safi, kumsaidia biashara zake kimawazo maana Mungu amenipa nafasi na uwezo au upeo mkubwa kielimu na kufahamu mambo. Yote hayo sasa nimeacha na sitakaa kabisa kujishughulisha na maisha yake. Kwa hiyo jamani wanume mtakaosoma hii habari ninaomba sana wapendeni wake zenu kwa ukweli, tunaumia jamani mkitusaliti. Mimi nina muda mrefu sijui tena mboo ya mwanaume wangu na wa nje naogopa magonjwa na si tabia yangu kutembea nje.Naumia sana kisaikolojia, nalazimisha nature. Nami nisaidieni jamnani.
mama nakupa pole sana kwa kisa chako!!
Mimi kama mwanaume, nimesoma maelezo na vitimbwi vya mumeo hadi nimelia kwa kuziona tu hisia zako kimaandishi jinsi ulivyosimulia.
Kwa kweli nashindwa hata nikushauri nini bibie maana hapo ulipofikia naona umeishakata tamaa na mumeo.Moja tu dada, MUOMBEE naamini hajitambui wakati fulani unaweza kulaani mtu usijue kilichomshika huko akilini.
Nimefurahi sana kwa dada mmoja ambaye amepiga mbiu ya kufanya maombi kutuombea wanaume. Ila sikubaliani naye kabisa anaposema ataomba wengine wafe au waangamizwe.Kama Mungu angekuwa na hasira kiasi hicho sisi sote tusingeishi hadi leo kwa makosa mengi tulimtendea. Pia hata wewe mwenyewe si ajabu ni mama wa ajabuajabu maana mtu unamhukumu kwa maneno ya kinywa chake.
Kosa katika ndoa haliko moja tu la kutoka nje ya ndoa, bali yako makosa mengi yanayoambatana na hilo.Muhimu ni kama ulivyosema kuombeana ili Mungu aingilie kati katika kunyoosha mioyo ya wana ndoa.
Lakini nisema pole sana kwa wamama wote ambao waume zenu ni jeuri ya chama.Kusema ukweli inaumiza, ni sawa na mwanaume naye anaposikia mke wake anatembea na mwanaume fulani huko nje. Poleni wadada zetu ndiyo msalaba wa ndoa jaribu kumuomba sana Mungu anweza kuingilia kati.
Umenigusa sana na kilio cha mumewe ambaye umesema umemvumilia sana na sasa umeamua tangu mwaka jana asiguse kuma yako.Pole sana mwaya.Ndoa ni ndoana kweli!!!
Ila usahihishe usemi wako wa "Nimemlaani asifanikiwe" kama utashupalia usemi huo na fikra hizo hata wewe utazidi kulaaniwa na yeye atazidi kubarikiwa.
Kama ulijua alishindwa kuishi na wanawake watatu waliotangulia, ilikuwaje wewe ukaingia kichwa kihwa hapo?Ulidhani wewe utambadilisha kirahisi kama hivyo?
Je mara ngapi umeshauriana naye na hata ungempeleka kwa hao wachungaji wake wakakusadia kutatua tatizo lako kwa sababu ni mzee wa kanisa kuliko kulia kilio barabnarani na kuamua kumnyima chakula cha usiku wakati na wewe una njaa.
Mimi kama mwanaume nakupa ushauri, nenda kwa mchungaji wenu mweleze kila kitu na umuombe msaada wa kukaa na mume wako. Ukichukua nafasi ya kumlaani haitakusaidia hata kidogo.Kama Mungu angehesabu maovu yetu sisi sote ni wakosaji japo makosa yetu yanatofautiana.Muombee mumeo usimlaani kihivyo kwani mlipendana na ndiyo maana mkaoana na mlikiri kuvumiliana katika tabu na huzuni na katika raha pia.
Ann wa 12:41 usiwe muongo, wanaume hawatangulii kufa eti kwa sababu ya vilio vyenu??? Wewe ni nani hata useme hivyo?nani kakuambia hivyo?Hivi unajua kuwa wanaume wanaoa wake walio na umri mdogo kuliko wao?Unategemea mtakufa siku moja? Hujui kuwa wanaume wanaumiza sana vichwa katika mahangaiko ya maisha na kazi za suluba nyingi?
Vilio vya wanawake havina uhusinao na vifo vya wanaume na kuacha wajane.Je kama ni hivyo ni wanawake wangapi wanapenda kubaki wajane na kuwaombea waume zao wafe?
Waombeeni waume zenu kwani hata ninyi mna makosa mengi sana ambayo yanawafanya waume zenu kuwakimbia.
Msome sana Ann3:22:00pm ameongea mambo ya maana sana na ushauri wa maana sana utawasaidia mkizingatia kuliko kelele zenu hizi na hasira hazitawasaidia kamwe.