Miaka 10 kwenye uhusiano na mtoto moja bila ndoa, je nimuache?

"Habari dada Dinah,
Pole kwa majukumu na hongera kwa kuelimisha jamii. Mimi ni mdada nina miaka 32 toka Arusha. Nina uhusiano na mwanaume kwa muda wa miaka 10 na nimezaa naye mtoto mmoja.

Kabla ya kuwa na mimi huyu mwanaume alishawahi kuwa na wanawake tofauti na amezaa watoto wawili kila mmoja na mama yake.Katika uhusiano wetu tumefanikiwa kununua nyumba moja yeye alichangia hela nyingi kuliko mimi ila mimi niliifanyia ukarabati mkubwa, hati nilisaini mimi na alinikabidhi.

Nyumba hiyo ninaishi mimi na mtoto wangu, yeye anaishi nyumba nyingine na watoto wake hao wawili na huwa nafika hapo ila hajawahi kunikaribisha ndani wala kunitambulisha kwa watoto wake.

Alishawahi kunitambulisha kwa baadhi ya ndugu na rafiki zake na kwa staff wenzie ofisini. Huyu mwanaume amekuwa msaada sana kwangu na familia yangu, kwetu wanamfahamu kama baba wa mtoto wangu.

Mimi nataka kuachana na huyu mwanaume kwa sababu naona ananipotezea muda pamoja na kwamba ananisaidia. Ila kuna ndugu zangu wananishauri nisimuache. Mimi binafsi naona hayupo serious kwani angekuwa serious na mimi au kuwa na mpango na mimi sidhani kama angekaa nyumba tofauti na mimi.

Pili, muda wa miaka kumi ni mrefu sana kama angekuwa na mpango na mimi nadhani angenioa. Nimejaribu kuongea naye mara nyingi takribani miaka 6 sasa kuhusu suala la ndoa lakini kila siku jibu lake kuwa ana mipango anaikamilisha kwanza lakini haniweki wazi ni mipango gani hiyo.

Tatu, Pamoja na kwamba huwa anakuja kwangu na tunafanya mapenzi lakini si kivile na mara nyingi huwa nakuwa mpweke, kwa kifupi huwa anakuja anavyotaka yeye so nakuwa sipo uhuru na mapenzi.

Nne hakuna relation yeyote kati ya mtoto wangu na watoto wake yaani kwa kifupi mambo yake mengi haniweki wazi hizo ndio sababu ambazo zinanifanya niamue kuachana naye pamoja na kwamba ananihudumia kwa kila kitu.

Binafsi bado nampenda sana, tena kwa dhati ila kwa kweli nimechemsha kwa hilo. Nilishawahi kumwambia kuwa nimechoka na ninataka tuachane, aliumwa presha mpaka akalazwa. Toka nimekuwa na uhusiano naye sijawahi kuwa na mwanaume mwingine nje ya uhusiano wetu na nilishawakataa wengi kwa ajili yake lakini kwa sasa nimechoka.

Hofu yangu ni kuwa baada ya kuachana itabidi tuuze hiyo nyumba na nitahangaika na makazi mimi na mwanangu. Pia nahofia usalama wake maana bado atabaki kuwa baba wa mtoto wangu.

Ninaomba wana-blog wenzangu mnishauri katika hili ili niweze kuchukua maamuzi sahihi. Samahanini sana kwa maelezo yangu marefu, Madada wa Arusha".

Comments

Anonymous said…
kweli kutokujua haki yako inagharimu sana! sasa uuze nyumba kwani huyo si mtoto wake ama? ndo ushapata na wewe urithi wamwanao mapema haijarishi yeye kangia nyingi ama vipi kwani si kafanya kwaajiri ya mwanaye?!
Anonymous said…
usimwache kwani unataka kwenda wapi wakati mwanaume unaye?Jaribu kuwa mvumilivu kama mambo yote anakufanyia tulia,kwani hilo la kuoana litafikia tamati mtaoana.

Umesema unampenda na anakutimizia mahitaji yako yote,ni vema sana hilo lingine liwekee mikakati ili liwezekane.Kama ulivyosema kuwa hayupo mara zote home kwako anakuja tu kukupa raha,nadhani inatosha mama, kwani unaweza kurukka matope ukaenda kukanyaga mavi.Tena umezaa naye na umenunua nyumba pamoja naye,hayo mengine yatajiri taratibu bibie.
Anonymous said…
Wewe jamaa una tatizo kama langu.Huwa na mimiminanitokea hivyo.Kuna siku hata kama sijatomba siku tatu lakini mzee mzima anakataa kabisa kusimama.Na siku nyingine akisimama basi natomba vema tena kwa mfululizo kabisa bila shida na mwenzangu anafika kileleni mara tatu mfululizo mimi nikiwa bado sijamwaga.

Na ikiwa nimemwaga basi nakaa kidogo tena mzee anakuwa yuko fit.Lakini nyakati zingine natomba kimoja nikikojoa wakati yeye amefika kileleni mara mbili tatu mfululizo mimi mzee hasimami tena hapo hadi asubuhi,lakini ninakuwa nimemtosheleza mwenzangu vizuri kabisa.
Nilichogundua mwenyewe ni kwamba kuna siku huwa nakuwa na mambo mengi kichwani ambayo yanahitaji utatuzi wangu na labda mambo ya kazi yananichukulia muda mwingi kuyawazia namna ninavyoweza kuyafanya na kuyakamilisha.Wakati huo nikiwa na hamu au mwenzangu akiwa na hamu kudu basi mboo haiwezi kusimama kabisa wakati huo hadi nipupoteze hayo ndipo inanyenyuka yenyewe.na hii imewahi hata kutokea nikiwa katika ya gemu nashangaa tu kitu imesinyaa.

Kwa hiyo ndugu yangu wchangiaji watusaidie.Hasa lile la kuzimikia moto ukiwa tayari game limekolea. Hilo la kukosa kukojoa kwenye round ya pili nadhani ni uchache wa sperm zinakuwa bado hazikutengenezwa za kutosha baada ya kumwaga mara ya kwanza.
Anonymous said…
Ndoa muhimu shoga, asikudanganye mtu eti ndoa ndoano, tulio kwenye ndoa tunakwambia ndoa ni tamu ndo maana hatutoki. Unakua na rafiki na company permanent, upweke unausahau. Kimbia achana nae na ubinafsi wake. Akamilishe mambo yake kivyake na wewe anza kivyako. Mtu gan hata watoto hawajuani! heee!!!!
Anonymous said…
Umama huruma ndo unawaponza mnaend up single forever, mwenzio anaoa! akili mukichwa!!!
Anonymous said…
ukiamua kuachana naye basi ujue kila utakayempata utamwacha tu, hakuna mwanaume asiye na mapungufu. miaka kumi ni mingi sana ktk mausiano ya mapenzi mmeshafahamiana vya kutosha ila sasa wewe unataka kutafuta vizuri zaidi bila kujua kuwa utaharibu au utaaribikiwa. Mwite ongeanae na mrekebishe tofauti zenu.Hayo ndio maisha.
Anonymous said…
NI TATIZO KAMA LANGU, HEBU TUNAOMBA USHAURI NAUNGANA NA HUYU DADA.

MAWAZO YENU NITAYAFANYIA KAZI KWA KWELI NIMECHOKA KUISHI NA MTU AMBAYE HAYUPO SERIOUSE NA MAISHA MIMI NI MPIGANAJI KWA KWELI LAKINI HANA MSIMAMO MARA UMFUMANIE NA WANAWAKE WENGINE MARA VURUGU TUUUUUU.

USHAURI PLEASE!!!!!!!!!
Anonymous said…
Nilivyokuelewa Madada wa Arusha,
(1)umechoshwa na uhusiano na mwanaume kwa miaka 10 bila ya ndoa. Unajiuliza kwa nini miaka yote hiyo hajakutambulisha kwa wanaye japo amekutambulisha kwa ndugu zake, rafiki zake na staff wanzake.
(2)Hakupatii ngono vizuri na hivyo mara nyingi u mpweke , lakini pia unasema amekuwa msaada sana kwako na familia yako, kwenu wanamfahamu kama baba wa watoto wako!!!
(3)Unatamani kumuacha lakini unahofu juu ya makazi na tena usalama wake!!!
(4)Kwa kuwa umesema umewakataa watu wengi kwa ajili yake na sasa umechoka, basi binafsi naamin unaimani kuwa ukiachana nae leo kesho utaolewa!!!
Naomba nitoe mawazo yangu kama ifutavyo.
Kwa maelezo yako mwanaume huyu aliisha zaa watoto wawili kwa mama tofauti na watoto hao anaishi nao, hii ina ashiria ni mwanaume ambae katika maisha yake alipanga kuoa na kuishi na mke hadi kikomo cha maisha yake, lakini kwa bahati mbaya wale ambao alitegemea kuishi nao walikuwa na tabia ambazo hazikumpendezea hivyo wote aliwashtukia mapema na kuwaacha. Hata hivyo alihakikisha watoto wake anawatunza yeye mwenyewe mpaka hapo atakapompata atakaekidhi vigezo vyake.
Miongoni mwa watu ambao nahisi aliamini wanakidhi vigezo vyake ni wewe, na hiyo inajithibitisha kwa kile kitendo cha kukutambulisha kwa ndugu zake, watumishi na marafiki zake, (lakini sio kwa watoto wake!) wanaume wanampomtambulisha mpenzi wake kwa watu ujue kaisha mkubali labda kutokee tatizo lingine.
Hata hivyo kuna kigezo kingine ambacho naamini alikiweka na ikawa ndio mtego kwako utakaoamua au akuoe au la. Kigezo hicho ni cha wale watoto alionao. Na hili naomba wanawake wanaosoma makala hii wawe makini nalo. Ukiona mwanaume anaishi na watoto wake tu, halafu ukapendana nae, na ukawa unatamani ufunge nae ndoa basi fanya bidii ya kuonesha mapenzi yako kwa watoto wake. Usipolifanya hilo kwa wanaume wengi walio makini ujue ndoa haipo hata kama ungalikuwa mzuri kama nini. Kwa sababu huwa wanahisi kuwa huenda baadae ukawanyanyasa watoto wake.
Kitendo cha kutokutambulisha kwa wanae ilikuwa ni mtego kwako, ulipaswa wewe mwenyewe uwatafute uoneshe mapenzi kwao, halafu wao wangepeleka ujumbe kwa baba yao.
Hata hivyo bado naamini atakuoa, lakini kwa kuwa mtego uliowekewa haukutegua mapema itakupasa usubiri mpaka watoto wale wawili watakapokua na kuondoka pale nyumbani iwe kwa masomo au mambo mengine.
Suala la ngono. Nafahamu umuhimu wa ngono katika ndoa, lakini naomba uamini mwenendo wa ngono hauboreshwi kwa kufunga ndoa. Na tena baadhi ya watu ambao walikuwa wanafanya ngono sana kabla ya ndoa , wakishafunga ndoa kasi ya ngono hupungua!!! (mwandishi moja katika kitabu cha society in the doc anasema: marriage or love has nothing to do with sex…..)
Suala la nyumba sidhani kama ni vizuri kulichanganya na upenzi na mwenzako. Ni maana kama unampenda au humpendi nyumba isiwe kigezo. Ukiwapenda watu kutokana na vitu kuna siku utanasa.
Suala la wanaume wanakutaka, hapa ndio unapotaka kufanya makosa mabaya, dada yangu sisi wanaume ni walaghai. Hakuna mwanaume atakayetaka kukuoa wewe hali ya kuwa una mwenzako. Baadhi ya wanaume wanapenda wanawake wanaohudumiwa kwa sababu hawana gharama, sehemu nyingine wanaita huduma ya afya wakati wa Nyerere!! Ukitaka kuamini mwache huyo halafu nenda kwa Yule anaekutaka, kama mapenzi yenu yatafikisha wiki moja bahati.
Samahani kwa maelezo marefu.
Anonymous said…
wewe dada huyo mchangiaji kakueleza vizuri sana siwezi kuongeza zaidi nawewe anon wa mwisho hongera kwa ushauri mzuri dada zingatia hayo jamaa kaweka mtego mzuri hapo