Ndoa ni Mwaka huu! Mwenzangu anatereza na mdada nimjuae!

"Habari yako,
Naitwa M*(Dinah amehifadhi jina) na ninaishi Sinza,
Kwa upande wangu sina swali ila ninapenda kupata ushauri kutoka kwako.
Nina umri wa Miaka 30 na nipo katika uhusiano kwa takribani miaka miwili na ninatarajia kufunga ndoa mwezi huu wa tano.

Tatizo linakuja kwa huyu mwenzangu anajihusisha kimahusinao na dada mmoja ambae namfahamu na kila nikimuuliza anakataa lakini Ofisini kwa huyu mwenzangu wanafahamu uhusiano wao, yeye na huyo mdada mwingine.

Sasa nashindwa nifanye nini na nikangalia ndoa ipo karibu,
naomba ushauri wako/wenu.

Hivi sasa amebadirika sana kitabia."

Comments

Anonymous said…
Kwanza pole sana.unajua tabia haina dawa na mapenzi hayalazimishwi kwa mtazamo wangu huyo jamaa hana penzi la dhati kwako lakini inavyoonekana hataki pia kukuacha ni mtu asiyeelewa hisia zake ziko kwa nani hasa,mara nyingi watu kama hawa utakuta ni huyo dada ni mpenzi wake wa tangu zamani kabla yako lakini kutokana na sababu moja au nyingine akaona wewe unaweza kuwa mkewe lakini sio kwamba anakupenda kwa dhati ila mapenzi yamelemea kule asikotaka kuacha sasa ukiolewa uwe tayari kuendewa kinyume maana haitokuwa rahisi jamaa kumuacha kimada><
Anonymous said…
Pole dada M* kwa maswahiba unayopitia... Mwanaume hata siku moja hawezi kukubali ukimkabili kijinga hivyo, kinachouma ni hiyo hali ya kuwa upo katika mchakato wa kufunga ndoa alafu mwenzako anakuwa hivyo, inauma sana. Me naona uandae mtego ambao utathibitisha hicho usemacho la sivyo utaingia katika ndoa kwa kuwa tu ndoa ipo karibu na pengine hutaki kuitia familia aibu kwa kuivunja kabla ingawa ni hatari sana uwezekano wa kuvunjika kwa ndoa yako ni dhahiri usipokuwa makini katika hili kwani hujui mwenzako nae kaahidiwa nini na baada ya kugundua mwenzake kaoa ataibuka na lipi?

Kwa kuwa umeshamuuliza na kukataa shughulika mwenyewe ili uwafume, acha kazi fanya kazi ni rahisi kuivunja ukiwa na uthibitisho waziwazi na si kumuuliza na kuamini akuambiacho, wengi tunaumizwa ndani ya ndoa na wakina dada wenzetu kwa kusubiri umuulizapo mume aseme "NDIO ILA NIMETELEZA" usikubali neno hilo kupenya maskioni mwako.. Kila la kheri..
Anonymous said…
dear, endelea na mipango yako ya ndoa, huyo kicheche anamrubuni huyo mtu wako, yaani kwa kifupi usiulize chochote kuhusiana na uhusiano wao, nina hakika huyo jamaa yako anakupenda ndio maana kaamua kutangaza ndoa, na pengine huyo bidada hajaambiwa kuhusu hiyo mipango yenu ya marriage. kifupi ni kwamba, wanaume wa tanzania ni ngumu kuwa faithfull ktk mahusiano, naona ni kama ulimbukeni maana kila kona matatizo ni hayo hayo. na kwa taarifa yako, ukivunja hiyo mipango, ndio umempa go ahead huyu kicheche, nakuhakikishia utamuumiza sanaaaa. yaani fro now, usiulize chochote, subiri kwanza ukishapata ganda lako, ndio umbane jamaa
Anonymous said…
achana na maneno ya watu..cha msingi kuwa close na mumewe na kama anakuwa mbali kikazi kimajukumu make sure communications inakuwepo ..talk to him about it..mi naamini hujamfumania ila kuna maneno unayasikia pia wasiwasi wako...

muamini na jiamini...itasaidia kuboresha ndoa na kukuset free..pia usichunguze saaaana...

Gluv
Anonymous said…
Jamani dada wa watu,
Mpaka nywele zimenisisimuka kwa ujumbe wako. Kama anateleza sasa hivi mu wachumba, akikuoa ni hatari zaidi.
Sasa, kabla hajakuvurugia maisha achana naye. Wanaume ni washenzi mwisho, hasa wenye tabia hiyo. Huwa hawaachia. Akikuoa atazidi zaidi. Roho itakuwa inakuuma karibia kufa na wala hashtuki. Kwa nini ujitafutie kufupisha maisha yako, achana naye. Mungu atakujalia wa uhakika. Tafdhali usiulazimishe moyo.
Ushauri tu
mama wawili said…
pole sana dada, ila hayo ni mitego ya shetani! always kitu chema kinapotangazwa eg. ndoa, shetani nae huzidisha mikiki yake ili kusambaratisha ila muendelee kuwa katika kundi lake la wazinzi. hivyo dada kaza buti weka pamba masikioni kesha ukisali na kumuomba mungu akunusuru na mitego ya shetani ili apitishe baraka zake muwe katika ndoa impendezayo mwenyezi mungu. shetani anamtumia huyo mdada mwingine ili kuwavuruga. mi nafikiri ukifanya maombi ndoa yako itakua na amani tu. hata mie yamenikuta kama haya. nilikua na jamaa yangu soon baada ya kutangaza ndoa mambo mengi ya kuvuruga yalitokea hadi nilianza kukata tamaa. lakini badae nilikaza buti kwenye maombi. mambo yakawa sawa. omba mungu atakusaidia.
Anonymous said…
Mimi nilijiingiza kwenye ndoa ya jinsi hii sikuwahi kuhisi ka mme wangu ana hizo tabia kwani wakati wa uchumba hakuonyesha dalili zozote za kucheat. Baada ya harusi tu safari za mara kwa mara kwenda head office kwao ambayo iko mkoa mwingine zikawa zimezidi.

Ila inauma sana na wala hajaacha na sijui ka ataacha. Mimi nashindwa kujua kwa nini alinioa sababu gani. Hata siku moja mke wa shemeji yangu aliniambia iko siku alimuuliza mme wake kwa nini mme wangu anafanya hivyo na kwanini kama anampenda huyo kimada hakumuoa basi, eti akasema hata yeye aliwahi kumuuliza ndugu yake hilo swali akasema hakutaka huyo kimada awe mke wake basi. Nikimuuliza anasema umekosa nini hapa kila kitu unacho wasiwasi wako nini. KWELI ROHO INAUMA DADA BORA UOMBE MUNGU KA UMEONA MAPEMA NI RAHISI SANA KUVUNJA UCHUMBA LAKINI NI NGUMU SANA KUVUNJA NDOA HASA UKISHAKUWA NA WATOTO. Nikijiangalia nasema hata nilimkosea nini Mungu na uzuri wangu wote.
Anonymous said…
Mhhh...katika riadha, yaani athletics, hii inaitwa "False start". Hebu muulize akueleze seriously matarajio yake katika ndoa ni nini na muweke bayana kanuni za msingi za hiyo ndoa kabla hujajitosa kichwa kwanza.
Anonymous said…
Ni sawa kuwa usichunguze saaaana, lakini lazima ujadili na huyo mchumba wako kuwa yeye anaonaje ishu ya uaminifu na ukweli ndani ya ndoa ili muwe close zaidi. Mwanasiti.
Anonymous said…
Yaani mwenzangu pole, lakini nisingekushauri uendelee kufunga ndoa, vinginevyo msigoze tarehe ya ndoa mbele, labda mwakani. Hakuna kitu kinauma kama kugundua mme wako anatoka nje!!! its real pain! kwa sababu atabadilika tu, tena itokee bahati mbaya huyo mwanamke wa nje kamkolea, mbona utakonda uishe na mapressure! me nipo kwenye ndoa hata sijamaliza mwaka lakini nimeshachoka, mme wangu hataki niguse simu yake ila yangu anaishika, kila siku anachat na namba moja ambayo ni ya mwanamke, ukimuuliza ni ugomvi namnyima kuwa na marafiki!! urafiki gani huo kwa mtu mmoja masaa yote hadi usiku? inauma ndugu yangu, please be careful, hawa watu ni washenzi tu, tunaishi nao tu.
Anonymous said…
Walaaniwe wote wanaotembea na wauume na wachumba za watu. Yaani kuna watu wanapenda ligi. Wakiona mtu kaoa au ana mchumba basi ndio wanamuona ana mvuto. Ila bidada hacha woga muulize huyo hubby to be. Tena fanya mpango uwaite wote wawili, si umesema unamjua huyo bidada. Waite waulize kweupe, kama wana uhusiano. Na kama vipi wewe waambie waoane wewe utatafuta ustaharabu kwingine. Wanaume wako kibao
Anonymous said…
anony wa 08:01pm naungana na wewe amuite huyo mchumba ake na huyo bidada kweupe awaulize maana ukiingia kwenye ndoa atakuwa anakurudia asbh nyumban na atakudharau huwezi mfanya chochote coz ulikuwa unafaham kabla hajakuoa kwanin usichukue hatua?