"Dada Dinah, umri wangu ni miaka 33 miaka miwili tangu nimefunga ndoa nilibeba mimba lakini kwa bahati mbaya iliyoka baada ya miezi mitatu tu, mpaka leo sijashika tena mimba. Nimeenda Hospitali zaidi ya mara moja kwa ajili ya uchunguzi lakini nimeambiwa sina tatizo lolote.
Vilevile nimejaribu kutumia dawa za Kienyeji lakini sijafanikiwa kushika mimba mpaka leo, je kuna njia nyingine yeyote inayoweza kunisaidia kushika mimba tena bila kunywa dawa za Clomid? Naomba mnisaidie....
Nimefurahi sana kupata email yako.
Asante."
Vilevile nimejaribu kutumia dawa za Kienyeji lakini sijafanikiwa kushika mimba mpaka leo, je kuna njia nyingine yeyote inayoweza kunisaidia kushika mimba tena bila kunywa dawa za Clomid? Naomba mnisaidie....
Nimefurahi sana kupata email yako.
Asante."
Comments
Punguza pombe pia kama ni mywaji na angalia vyakula unavyokula, pata mapumziko ya kutosha.
Wakati mwingine dawa hizi za uzazi wa mpango zinaweza kufanya uchelewe kubeba ujauzito hata kama umeacha kwa kipindi cha miezi nane dawa inakuwa na nguvu mwilini.
kwa kifupi ili mimba ishike miongoni mwa mambo muhimu ni pamoja na uzima wa kizazi cha mama pamoja na uzima wa mbegu za mume wake. Kingine ni tarehe za kukutana na mwanamme, kwa sababu hata kizazi kikiwa kizima na mbegu za mwaname nzima sio tarehe yoyote mimba inaweza kushika. Kitalaamu kama hamuwezi kulenga zile tarehe za kushika mimba basi unatakiwa angalau mkutane mara nne au tatu kwa wiki.
Lakini pia umesema kuna mimba iliwahi kutoka. Hivyo yawezekana lile tatizo lililofanya mimba ikatoka ndio hilo ambalo linazuia usishike mimba, au wakati mwingine mimba iliyotoka imeacha madhara ambayo hayajatibiwa na haya madhara yanachelewesha kushika mimba. Jingine wanawake wa umri wako ambao hawajapata watoto huwa wanakabiliwa na matezi ya kizazi (fibroid)Matezi hayo yanaweza sababishwa na kutokupata mimba mapema lakini pia yakisha tokea nayo yana tabia yakuzuia mimba kushika. Nenda hospitali pamoja na mumeo mkachunguzwe kwa pamoja. Msikate tamaa. Waweza pata ushauri zaidi. Email- hiishkamili@yahoo.com