Nampenda Mdada alienizidi miaka 9, je naweza kuoa?-Ushauri

"Dada Dinah pole na mihangaiko ya hapa na pale ya kila siku. Mimi ni mwanaume wa miaka 23 naenda 24 sasa. Nimetokea kumpenda dada wa miaka 32 ambaye ni rafiki yangu kipenzi. Lengo langu ni kutaka kumuoa kwani moyo wangu umeridhika juu yake.

Sijamtamani kingono but I feel that I am in love with her. Hajawahi kuolewa na wala hana mtoto. Bado sijamweleza nia yangu ya kutaka tuhame kutoka kwenye urafiki tulionao kwenda kwenye uhusiano wa kimapenzi. Kwasasa mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu chuo kikuu hapa Tz, mwenzangu yeye ni mwalimu.

Tumekuwa pamoja kama marafiki kwa mwaka mmoja sasa. Urafiki wetu ni zaidi ya urafiki kwani tushafanya romantic talk/romance kwa njia ya simu. Naogopa kumweleza nia yangu kwani nahofia kuumiza hisia zangu ikiwa atanikatalia.

Moyo wangu unapata faraja na mateso juu yake. USHAURI ninaoomba kwako dada Dinah na wanablog wengine ni, Je kuna athari zozote yinazoweza kujitokeza kutokana age gap iliopo ikiwa tutaoana?

Na je nimweleze nia yangu au nifute wazo hilo? Wanawake mnalichukuliaje swala la kuolewa na mume mdogo kuliko mke kwa gap kubwa? NAOMBENI MAWAZO YENU NA HEKIMA ZENU. Facts are sacred, opinion are welcome and ideas are respected.

I love u All,

NB. Kilichonivutia kwake ni akili yake iliyokomaa, upendo alionao juu yangu na uelewa mkubwa alionao. Sura huwa si kigezo cha muhimu sana kwangu".

Comments

Anonymous said…
bro.dah nilishawahi kuwa na case kama yako hiyo..wakati nikiwa na miaka 18 nilimpenda msichana aliyenipita miaka 6. ila nilizaa naye tu hakuna ndoa. kama utavumilia maneno ya watu. vijembe, maneno ya pembeni kuwa umeoa mzee. hata ndugu zako watasema hayo. kama hutayajali maneno yao basi usigope kumuoa. kumbuka kuoa ni decision nzito sana na unatakiwa kufikiria kama mtu mzima unataka kuoa kweli? na unayemuoa ni binadamu kama wewe na lazima nawe uwe na ubinadamu..sio umuoe siku mbili then umuache utakuwa umeshamwekea doa na kumchafua dada wa watu.. mana ye akiwa na miaka 40 we utakuwa na 31.na miaka 40 kwa mwanamke ni mzee sana hata sura yake itajionesha. hapo ndio utaanza kumsalit na kumuona mbaya. imagine utakuwa na miaka 41 ye 50 ..41 kwako ni kijana sana tena hata ukikutana na mwali ataona kweli we ni mwanaume wa nguvu. je miaka 50 kwake ataonekana vip? bro tafuta mtoto wa saiz yako tu nakushauri. huyo mwacha atafute mtu wa miaka 40. acha tamaa kijana wangu, najua unamtamani tu japo unasema hujamtamani. ungekuwa hujamtamani msingefanya romance yoyote.umenisoma hapo? so kinachokupush kuwaza kufunga naye ndoa ni tamaa. kama unampenda kaeni miaka 5 bila ndoa then ukiweza muone after hiyo 5 yrs.
mdau german
Anonymous said…
Mmmh! athari hamna mdogo wangu, ila ninachohofia ni wewe kuja kumuumiza huko baadae utakapoanza kutamani au kuona umuhimu wa kuwa na wasichana ambao mnaendana umri au umewazidi, kwasasa huwezi kuona hilo kwani desire juu ya huyo mwanamke imefunika macho yako na moyo wako, Naita desire kwani am not sure kama kuna love hapo, kwa experience yangu Wanaume huwanza kwa KUTAMANI then kupenda baadae, so ni mapema sana for u to claim u r in love with her. Ila hiyo hali itakapoisha, na ukaja ukagundua u r not in love with her ndo hapo unapokuwa mwanzo wa kumuumiza, tena inaweza kutokea muda mfupi tu baada ya kuwa umemwambia hisia zako na yeye akakubali then mkaanza uhusiano na ukapata kile unachokihitaji the most kwenye mwili wake. The idea of having someone or something especially when u knw its hard or imposible to have it always feels better than having it in reality. Be careful for her sake
Anonymous said…
Oooh we brother hongera sana kumatch na mdada mkubwa kama huyo,dah safi sana kwa hilo.
Kwanza age aint a thing just a number,so sio shida hata kdg isipokuwa jamii yetu ndio vile kukuelewa sio rahisi kwani wakati woote toka mababu zetu man should alwyays be superior to his wife,infact kwa issue zote kama kipato,umri,hata size(urefu vs ufupi). So kwako mwenyewe na wwngine waelewa kama mimi hakuna shida bt for majority big NOOOOO. So check na moyo wako kuwa nae na kuhimili outsiders or please outsiders kwa kuachana nae.

Secondly,cencus research reveals that,ther are more widows than widowers,this means ili kubalance age btn man and a woman inatakiwa wanaume woootw duniani waoe wanawake wakubwa ili kubalance wdws vs widowers,kwa sababu wanaume hufa haraka kuliko wanawake. So ili at least mkeo asibaki mda mrefu wa kuwa alone ni vyema mwanaume ukawa mdogo at least mfe kwa tofauti ndogo ya miaka.

Otherwisw am leaving the stage to other fans,all the best young bro,ila mie nlioa msichana younger than me 9yrs.
Anonymous said…
Kaka kwanza pole sana kwa kuficha feeling zako kwake, ila ww kama unampenda kidhati mwambie tu ukweli, na elewa swala la kukupita miaka it doesnt matter, is just a number, watu wanaolewa au wanao wazee na vijana wadogo sembuse ww, mueleze tu ukweli umsikie nae, kwanai inavyoonekana nae pia anakupenda sana pengine anasubiri tu umtamkie ww kwanza.
Anonymous said…
Kwanza kabisa nakupongeza kwa kuwa muwazi kwetu. Mungu akubariki sana.

Maoni yangu mimi. Sioni kama kuna tatizo kwa hilo, wewe kumpenda mtu mwenye umri mkubwa - Age is a number. Cha msingi ni kwamba, ni vizuri kumueleza huyo mwenzio nia yako, ili ujue na wewe analichukuliaje hili swala. Lakini mi naona pia na yeye atakuwa anakupenda tu ili labda anashindwa kukutamkia juu ya hili kutokana na desturi za kibantu. Msichana si rahisi kusema kwa mtu ampendae kwa mara ya mwanzo kuwa nakupenda ila utaona dalili tu za mapenzi.
Sasa huyo mwenzio akikubali sioni kama kuna tatizo hapo. Ila kama umependa kweli unatakiwa uwe strong kweli kweli kwenye hayo mapenzi yenu. Si unawajua watu huwa hawakose la kusema, na huwa wanapenda sanaa kufuatilia vitu vya watu vyao duh!!! Sasa wewe akili kichwani kwako. Wewe si wakwanza kutokewa na hilo. Wapo wengi sana wamewapenda au wameoa au wanaishi na wake ambao wamewazidi umri, ili mladi mnaheshimia na kupendana kwa dhati basi ndoa yenu itadumu bila tatizo. mbona wenzetu wazungu wanaoana hivyo? Hizi ni mila na desturi za kibantu tu, eti kuoana ni lazima mke awe mdogo kwa mme. Au niseme mme amzidi umri mke.
Kwa mimi sioni kama hilo ni tatizo, wewe endelea tu, na muombe Mungu na Mungu atakubariki sana.
Usiitese Nafsi yako. Mwambie huyo dada usikie nae anasemaje.

Kila la heri kaka.
Anonymous said…
Kaka kama unampenda huyo dada ,ni muhimu umuulize ukweli kwanza, mwambie jinsi gani unavyofeel. Miaka sio issue, kikubwa ni mapenzi, na miaka 9 sio mingi sana ila mkija kuoana inabidi wewe uwe mwanamme ndani ya nyumba,sio kwamba sababu mwanamke ndio mkubwa kwako ,aje kutawala nyumba.Kweli wanawake wanapenda wanaume ambao ni warefu na wenye age kubwa kushinda wao but the most important thing is ,just be a men,and age is not a big deal :)
Anonymous said…
wewe hacha uo upumbavu,angekuwa amekuzidi 2 au 1 sawa,lakini 9!!!!!.ebu kaangalie usitaarabu mwingine na vizuri umeomba ushauri kabla hujamtongoza,KATAFUTE MKE WA KUOA NA SI HUYO,Ukimuoa huyo mkimaliza miaka5 tu humtamani tena utatafuta unayelingana naye,na ndo mwanzo wa kujutia.
Anonymous said…
kaka age aint nothing just a number, kwa ushauli wangu if you really love her to death, go ahead and express your feelings na kumbe mshafikia ya kuongelea romantic talks am sure the lady loves you as well but as you know a woman most of time can not approach or express their feelings.

and concering age there is no any problem, there are so many couples with age differnt women being older than their husbands and are leaving so happly. matatizo mengine ya kindoa yapo ingawa a marriage is between two people.

in short follow you hearts wishes brother
Anonymous said…
Umri ni namba tu usikusumbue hata kidogo mwambie tu na lazima atakubali kwani unasema ni marafiki wa siku nyingi hii ni itakurahisishia wewe kumuingia.

Au hujui uanzeje tukufundihe? Kwa hiyo usimuogope zungumza nae. Sikiliza dogo hatali ya kutokumwambia atajitokeza mtu atataka kumuoa utaanza kulalamika ooh alikuwa wangu sijui oooh jamaa kanikatili ili haya yasitokee wewe ongea nae Mwaga sera..........Kizito!!
Anonymous said…
Miaka 32 bado sio mdada mkubwa hasa ukizingatia maisha ya sasa sio ya kuzaa watoto wengi..huyo bado ana nafasi ya kukuzalia watoto hata wa3 kama mtapanga..kizuri zaidi yeye yupo kwenye age ya kutulia kiakili na kimaisha..

Ni wewe kuwa tayari tu kumuoa na inatakiwa haraka kwani kwa huo umri wake ukichelewa kumuona ni kama nan yeye anaogopa umri unaenda..

Cha msingi ni je yeye yupo tayari kuolewa na wewe..je mpo free inpublic?..yaani kutembea pamoja na kufanya mambo ya kijamii pamoja na kila mtu kufahamu bila mmoja wenu kujistukia..kama jibu ni yes from both sides..basi Ndoa itakuwa tamu sana na ya kuheshimiana..

Mimi niliwahi kiwa na girlfriend alienizidi umri sema tu hakutaka kuwa na mimi sana inpublic so tukaachana ila wadada wakubwa they are so sweet sio kingono tu hata kukaa kuongea nae kuishi nae...

chukua mzigo kijana..

gluv100@yahoo.com
Anonymous said…
Kama kweli mumependana na mnaweza kuishi kwa furaha MUOE! Zile mila na desturi za kusema eti lazima umuoe mke mdogo kuliko wewe zimepitwa na wakati. Kama watu wawili (bwana na bibi) wako 'compatible' kwa kila hali na wanapendana wana haki ya kufunga ndoa. Vitu muhimu ni (1) mapenzi ya dhati (2)kila mmoja kuvutiwa na mwenzake (ikiwemo ku-'match' kitandani) (3)mtazamo wa maisha unaofanana (4) maelewano. Mwisho wa usiku, wewe ndio utaishi na mkeo. Cha muhimu ni haki yako ya msingi ya kibinaadamu ya "pursuit of happiness".
Anonymous said…
Mke wangu amenipita kwa miaka minne. Tuko pamoja kwa zaidi ya miaka 20 na tuna watoto. Ndoa bado ni nzuri. Lakini kumbuka kuwa uhakikishe kuwa unataka kuwa naye kikweli na yeye pia anataka kuwa na wewe kikweli. Kila la heri.
Anonymous said…
Ni kweli kuwa zile mila za wanaume kukatazwa wasioe wanawake wakubwa zao zimepitwa na wakati. (1) Katika dunia ya tatu (nchi zilizoko nyuma kimaendeleo) utakuta wazee wa miaka 70 wanaoa visichana vya miaka 15! licha ya kuwa matarajio ya kuishi (life expectancy) ya wanawake duniani kote ni juu zaidi ya wanaume. Kwa wastani, wanawake wanaishi kati ya miaka mitatu hadi saba zaidi ya wanaume (kutegemea na nchi); lakini dunia nzima hamna nchi hata moja ambako wanaume wana maisha marefu zaidi ya wanawake.
(2) Hamu na uwezo wa ngono kwa mwanamume wa kawaida iko juu kabisa (peak urge and strength) akiwa na umri wa kati ya miaka 19 na 35 wakati hamu na uwezo huo kwa wanawake wa kawaida ni kati ya miaka 33 na 48. Matokeo yake ni kuwa wanaume wengi wazee wenye wake vijana wanashindwa kuwaridhisha wake zao na kuwafanya wake zao watoke nje na ma-'gigolo' vijana. (3)Wanaume wanaojiamini wako tayari zaidi kuoa wanawake wakubwa zaidi yao kuliko wanaume wasiojimini. (4) Katika nchi zilizoendelea kisayansi, kiuchumi, kiutamaduni na hata kidini huo "mwiko" wa karne ya 19 [wa mke kumzidi umri mume] unapuuzwa kwa kuwa hauna msingi wowote wa busara bali inaakisi masalia ya mila za kizamani ambapo watu walikuwa wakidhani radi inaletwa na mizimu kupiga chafya au vinyamkera vinaletwa na vibwengo kukoroma!!!!!!! (5)mdau mmoja hapa juu ametaja haki ya "pursuit of happiness". Haki hii imo katika Universal Declaration of Human Rights ya 1948 ya UN. Katika maisha haya ya mpito hapa duniani, binaadamu wote tuna haki ya kutafuta furaha ili mradi tusivunje sheria wala tusiwaumize watu wengine. Kwa hivyo bro do the right thing. (6) Katika soma yangu ya Taurati, Talmud (kanuni za wana wa Israel) Zaburi, Injili na Kurani, sijaona hata sehemu moja ambapo Mwenyezi Mungu amesema ni hatia kumuoa mwanamke aliyekuzidi umri. Nakubaliana na mdau aliyesema kitu kikubwa uwe na uhakika kuwa unataka kuwa na mkeo kwa maisha yako yote hapa duniani, isije tena baada ya miaka kumi ukaanza kupapatika nje. Yaani uwe na uhakika wa mapenzi yako. Kama wanavyosema wenzetu "Love conquers all". Wadau mkiweza kukipata kitabu kinachoitwa "In Praise of Older Women" kisomeni. Nakutakia maisha ya upendo na furaha.
Anonymous said…
Why not? Ni wewe ndiye utaishi naye na si majirani zako wambeya.
Anonymous said…
Katika utafiti wangu wa Sociology nilitazama suala la ndoa baina ya watu weusi na weupe USA. Mwaka 1967 states karibu zote zilihalalisha ndoa hizo, ya mwisho ilikuwa Alabama 2000. Ndoa za aina hiyo ziliongezeka kutoka 50,000 hadi kufikia karibu 500,000 mwaka 2005 ndani ya miaka 40. Ninachotaka kusema ni kuwa 'taboos' [miiko?] za zamani zilizokuwa zinatokana na ujinga zitaendelea kutoweka kadiri ya watu wanvyoelimika na kuendelea. Hali kadhalika utafiti unaonyesha kuwa asilimia [percentage] ya wanaume wenye kuwaoa wanawake waliowazidi umri ['cougars'] pia inaongezeka kila mwaka. Kama miaka 40 iliyopita mtu yeyote angetabiri kuwa mtu mweusi angelichaguliwa kuwa Rais wa USA 2008, mtu huyo angelichekwa. Kwa hivyo, kama wewe na huyo bibie mnapendana na mnataka ndoa, endeleeni tu. Msio watumwa wa mawazo yaliyopitwa na wakati. Penye mapenzi na upendo wa dhati, basi pia baraka za Mwenyezi Mungu zipo. God bless you all.
Anonymous said…
Karibu kwenye Ulimwengu Malidhawa:Mungu akipenda 2011 hii nafunga ndoa na aliyenizidi zaidi ya miaka 5 amenizalia mtoto wa kiume:
kuna busara sana juu ya hili.kikubwa jiamini tu
Anonymous said…
annons 1:08:00 PM and 2:36:00 AM
mmenifurahisha sana na mna akili sana safi sana mnajua kutia watu mioyo,,,ata mie nna iyo ishu ya umri ila nilikua nawaza naazaje lol
kweli ndoa ni ya 2 waliopendana na si wazazi wala majirani wambeya
nimeeelimika now
Anonymous said…
NIMEOLEWA NAMWANAMME ALIYENIZIDI UMRI MIAKA 6 NAISHI KWA AMANI AMBAYO SIJAIFIKRIA KWENYE DUNIA .NDOA MBILI ZA WALIOANA KWA UMRI WA MWANAMKE MDOGO NA MWANAUME MKUBA ZIMEVUNJIKA NIKIONA AKILI KICHWANI MWAKO MRADI UMPENDE KWA DHATI
Anonymous said…
Kaka,
Unatakiwa kuufuata moyo wako! Unampenda, mwambie. kama mnaafikiana sioni sababu kwanini usimuoe! bottom line mnaenda kuishi wawili usiangalie wambea wanasemaje!
Anonymous said…
Yeah man unaweza kuendelea nae japo kwa kawaida wanawake wanaokuzidi hata kama unamliza kitandani atataka akuendeshe kama mdogo wake kitu ambacho ndo mwanzo wa kuachana..

Nakumbuka niliwahi kuwa na mwanamke alonizidi zaidi ya mika 12 ila nlidum nae kama miaka miwili tuu tukaachana,na sababu kubwa ya kuachana ni kutaka kuniendesha kama mwanae,so kuwa makini japo mie napenda wanawake wanaonizidi umri maana wataoto wadogo sometimes wasumbufu tuu...Shemeji yako nlonae sasa hivi kanizidi miaka 5 ila napima kama kawaida na anakwenda hadi tiGo kama kawaida utadhani mtoto wa miaka 14.
Anonymous said…
Age ain't nothing but a number! kama kweli umempenda OA kaka, usisikilize maneno ya watu.
Anonymous said…
bro. tnere is nothing wrong with that.. ge nuttin but a number fall your feelings.... kama umempenda bora umwambie ajue kuliko kukaa kuumia moyo ..utaumia zaidi pale utapoona kaja jamaa mwengine kachukua goma kisha huyo jamaa anaanza kukata mawasiliano yenu kati yako na huyo dada.. tell her now while u have a chance n time... if u gotta a gutts just spit dat shit get it out ya chest... thanks.. there is no problem becoz ya umri different...akama angekuzidi 15 okey lakini 9 poa tu mtu wangu huyo anajua nini kinacho ni mkubwa si msichana kiruka njia.. thnks...
Anonymous said…
kaka nakuchauri umwambie uyo dada jinsi unavyo mpenda labda nayeye anakupenda vilevile,mm nimeshaolewa na limwanaume zee makamo ya babangu na amenipa mtoto wa kike baada ya kujifungua mtoto mwanaume akaniacha na kutafuta wanawake wengine na kunitesa sana mpaka nikamuacha sio kusema ukioa mwanamke mkubwa ndiyo utakuwa umekosea sio mm nakuchauri muoe huyo mwanamke usichelewe mapenzi akili ya mtu sio umri unaweza ukapata mke mdogo akakutesa sana na mkubwa akakupenda sana,
Anonymous said…
Ww muoe 2 mm mwenyewe mke wangu kanizidi miaka 10 sasa hivi nina 25 yy ana 35 na bado tunaishi kwa raha mustarehe namuheshimu na yy pia ananiheshimu