"Pole Dada Dinah kwa kazi ya kutushauri, mimi ni mwanamke mwenye miaka 26 nina Mchumba wangu mwenye umri wa miaka 36. Tumekuwa pamoja kwenye uhusiano wetu kwa mwaka mmoja.
Mchumba wangu huyu kwa mujibu wake ni kuwa anaishi kwenye nyumba yake, lakini toka tuanze kuwa pamoja kwenye uhusiano hajawahi kunipeleka kwake japokua ameniambia sehemu anayoishi. Kwa kawaida huwa tunaonana kila siku na pia mara nyingi tunaenda out kwa ajili ya diner n.k.
Naomba mnishauri, je anamapenzi ya kweli au ananidanganya tu, ningependa awe mume wangu Mungu akitujaalia. Asante"
Comments
Maanake hana longterm objective in this relationship. Fanya upelelezi or time to move on kabla hajakuliza
Hilo ni swala la kumshauri kuwa ni vyema nikajua kwako, ili kuimarisha mahusiano mema, kwani kuna leo na kesho. Kama ana nia njema na wewe atakupeleka!
Anakutumia tu.utakuja kutuambia kwenye blog hii hii.
Jua kuwa anaogopa kukuleta home kwake kwa sababu anajua atafumaniwa na msichana mwingine aliyenaye ila wewe hujui hilo tu.
Kama unaona anakupa raha unayoitaka endelea ,lakini kama una malengi mahususi kwa maisha yako basi chomoka bila kuangalia nyuma usije geuka nguzo ya chuma.
Wanaume walaji bibie anakula kuwili na kutakatisha kumoja tuuu!! Kama huamini hebu jaribu kuwa ngenge hivi mkomalie unapenda sana umembelee home au mwambie unataka ukamsaidie kazi za usafi huko kwake halafu uone atakavyojikanyaga Period
G
Mi nakushauri fanya uchunguzi wako kimyakimya ambapo ni pamoja na:
Mwinde akitoka kazini, jaribu kumfatilia mpaka atakapofikia yeye kwani yawezekana Jamaa ana FAMILIA YAKE YENYE MKE NA WATOTO na labda yupo na wewe kwa ajili ya kujiliwaza tu na HANA MPANGO WOWOTE NA WEWE kwani watu kama HAWA WAPO WANAKUTUMIA KISHA MWISHO WA SIKU ANAAMUA KUKUFUGIA VIOO.
Njia nyingine nathani jaribu kujenga mazoea ya kutaka kujua marafiki zake, ndugu na jamaa kwa hili nathani nalo litakusaidia.ku kujua ndugu, jamaa na marafiki zake.
Yote yakishindikana haya, mi nakushauri ACHANA NAE mana HAILETI SENSE WATU MUWE KATIKA RELATIONSHIP then hata kwake hanapoishi husipafahamu. Dada una MOYO SANA KATIKA HILI, MAANA NI WACHACHE WENYE UVUMILIVU WA AINA YAKO.
katika MAELEZO yako haukusema kama huyo Jamaa ana mazoea na NDUGU, JAMAA NA FAMILIA.
Poa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
TUMEJARIBU KUMSHAURI MARA KIBAO KWA KUMWAMBIA KUWA HUYO NI MUME WA MTU,
ILA HAAMINI WALA ASIKII AMETUAMBIA MAMBO MENGI KUHUSU HUYO MWANAUME.
ME BINAFSI SIMJUI ILA WATU WALINIAMBIA KUWA NI MTU MZIMA KWAKE HATA WAKIONGOZANA ANAONEKANA NI MWANAYE
ALISEMA KUWA WATAOANA MWEZI WA 12 MWAKA HUU HAPO ILIKUWA NI MWEZI WA TATU ANATUAMBIA HIVYO NILIPO MWAMBIA NAOMBA NIONYESHE AKANIKWEPA MPAKA NIMEGHAILI.
KWA KIFUPI MAISHA NI KUAMUA
AMEAMUA KUISHI HIVYO MWENYEWE KWANI YEA ANAONA KWENDA DINNER NDIO MAUJANJA KUMBE HIYO NI FANI YA MACHANGUDOA.
MWACHENI AKIJA KUAMBIWA SIKU YA SIKU KUWA SIKUTAKI TENA NINA MKE WANGU NDIO ATAMUACHA.
By:- Kingi
By:- Kingi
Mwambie tu kwamba unahitaji kupajua kwake otherwise muachane. Sikufichi wangu,ataona bora muachane kuliko kwenda kwake. Halafu wanaume wa aina hiyo ndio hao wanaopenda kuhongwa. Atakuambia umkopeshe hela na hatakulipa,Uongo? Achana nae hata kama unampenda vipi maana hana mpango na wewe tena ole wako huyo mwingine akijua(it's obvious haupo pekeako)mbona utanikumbuka best! Acha rafiki yangu hata humu wapo wanakushauri ila nao yamewakuta wanajikausha tu. BORA KUACHA KULIKO KUACHWA MAMA...
Mwambie tu kwamba unahitaji kupajua kwake otherwise muachane. Sikufichi wangu,ataona bora muachane kuliko kwenda kwake. Halafu wanaume wa aina hiyo ndio hao wanaopenda kuhongwa. Atakuambia umkopeshe hela na hatakulipa,Uongo? Achana nae hata kama unampenda vipi maana hana mpango na wewe tena ole wako huyo mwingine akijua(it's obvious haupo pekeako)mbona utanikumbuka best! Acha rafiki yangu hata humu wapo wanakushauri ila nao yamewakuta wanajikausha tu. BORA KUACHA KULIKO KUACHWA MAMA...