Nataka kuolewa lakini nashindwa kupenda kila anaenitokea-Nifanye nini?

"Hello dada Dinah mimi ni binti in early twenties, ninatamani sana kuolewa na kupata japo mtoto mmoja soon. Bado niko shule lakini sielewi why I feel this way now! kwasababu nilikua against kuolewa kabla ya kumaliza masomo.

Niliwahi kuwa na Mpenzi ambae nilimpenda sana ila nilimuacha kwasababu nilidhani hakunipenda kwani we were breaking up and makingi up all the time, yaani maisha yalikuwa ndio hayo kwa muda wa miaka mitatu mpaka nilipoamua kuwa sasa I have had enough and called it off.

The guy bado ananitafuta kwa simu akitaka tuonane lakini mimi namchunia. Baada ya kuachana na huyo nikaanza kutoka na mwanaume mwingine ambae amenizidi umri kwani anamika 37 sasa. Tatizo ni kwamba jamaa anataka tufunge ndoa haraka iwezekanavyo.

Nyumbani hawamfahamu kwani bado sijamtambulisha, nilihakikisha anamjua rafiki yangu mmoja tu ambae nae alibahatika kwani aliomba lift. Baadhi ya ndugu zake wananifahamu na kufahamu uhusiano wetu kwani huwa ananikaribisha kwao na mwezi wa Pili kwama huu alitaka tuvalishane Pete.

Sina mpenzi mwingine na ninataka kuolewa lakini kusema ukweli simpendi huyu jamaa kihivyo, sura yake, na anavyoongea kwangu ni kero na pia he's terrible in bed. Nimekuwa nae kwasababu ya pesa, na kila ninapohitaji hunipatia pesa. Jamaa amejijenga vizuri kwani ana Kampuni yake na nyumba nzuri tu, pia huwa ananiachia niendeshe gari yake.

Nikaamua nimwambie kuwa siwezi kuolewa nae kwa sababu ni mkubwa kwangu na some other reasons which I cooked up but they sounded concrete. Yeye hataki tuachane kwani anadai kuwa ananipenda na anataka kuishi maisha yake yote na mimi pia anasema kuwa familia yake itamuona muhuni kama tutaachana.

Mie nimeshangaa jamaa bado anang'ang'ania kuwa na mimi wakati tangu tumekuwa pamoja sijawahi kumuonyesha mapenzi, yaani hata kumpa K ni ishu!! Mpaka anibembeleze kwa Wiki na wakati mwingine miezi. Mfano mwaka huu tumefanya ngono mara tatu tu.

I mistreated him kwa kumponda, kumnunia hata miezi miwili bila sababu ya msingi ili aniache lakini wapi! Kila kitu anachonipa na kuahidi ni perfect isipokuwa yeye. Nipo nae kwa vile hivi sasa sina kitu na sina mtu wa kuniangalia (money wise) kwani nina mzazi mmoja na kipato chake ni kidogo na sijawahi kumuomba mzazi huyo pesa kwa vile namuonea huruma.


Wakati niko kwenye Dilema hiyo, kuna kaka wengine wawili wanaonyesha interest kwangu. Wote wanasura nzuri na wanavutia na pia wana kazi nzuri ila mimi sina hisia za mapenzi, napenda sura zao na kazi zao. Mmoja ndio anaonekana mwema na anaweza kunioa ila naogopa kutoka nae kwani sina uhakika kamanitawapenda au itakuwa kama huyu Mjamaa, sitaki kuumia.

Dada Dinah naogopa nitakosa mwanaume wa kunioa kwani umri nao unakwenda lakini kila anaenitokea sivutiwi na sina hisia za kimapenzi, lakini rafiki zangu wakiwaona jamaa wanapagawa kweli.

Najua Email yangu ni ndefu sana, lakini am in desperate need for help na nilitaka nigusie yaliyopita na ninayokabiliana nayo hivi sasa ili nieleweke.

Nifanyeje?"

Comments

Anonymous said…
Wewe mshamba tu. Tena ngoja wenzio wasiki eti unamchunia na kumnunia jamaa. Kama ulikuwa humpendi kwanini unachukua vitu vyake na hela zake? Kwa taarifa yako wanawange wengi wanaojifanyaga hivyo hujuta maana wenzio wekipata huo mwanya wee utakuwa unatoa chozi kwenye umati mwenzio akiwa anvikwa pete. Halafu hii tabia yenu wanawake ya sitaki nataka huwa inatukera sana wanaume, maana hata mkishaolewa ndani ya nyumba huwa ipo. Nina mifano mingi sana ya wanawake wanaotoaga hizi excuses halafu wakiachwa wanalia kama paka mwizi. Tuambie huyo jaama anakaa wapi tumtafutie binti leoleo, Nyambafu wewe. Na kama ushasema humpendi unatuuliza nini sasa na wewe ndio utakaeishi nae? sisi hatupo humo ati ni wewe na yeye !!

Mzigo Mzito akak MM
Anonymous said…
Kuchamba kwingi mwisho utagusa mavi.Sweetheart, you need to ask yourself seriously what you really want in life before making any decision. Unaangalia sura au the way the person treats you with utmost respect? Remember all that glitters is not gold - kama umri unakwenda utakuja juta mdogo wangu. Sometimes it what is inside the person that matters and not outside. Think careful before jumping into conclusion.
Mama 2 said…
Acha ujinga mdogo wangu, sura kitu gani, utapata mwenye sura nzuri halafu akutese na hiyo sura yake,au hana maisha mazuri, sasa sijui utakula hiyo sura. Kaa na mtu ambaye unaweza hata kumsaidia mzazi wako. Sura kitu gani bwana! watu wanaolewa na walemavu, itakuwa sura! shauriro!!!!! Utaja juta baadaye.
Anonymous said…
ndoa si sura mdogo wangu, tulioolewa tunakufumbua macho funguka!Unaweza ukaoelwa na sura nzuri lakin ikawa vipigo na matusi kila siku. Mi nakushauri mshike huyo uliyenaye, utamkumbuka na itakua too late
Anonymous said…
we dada unashangaza watu sana,Yaani kuna wasichana wanatamani kuwapata hata hao wa kutongozwa nao lakini wapati,nashangaa wewe unatuelezea upuuzi wa kuwa huna hisia,nahisi utakuwa na jina mahaba nenda kombewe sio bure,halafu mwanaume wa kukuoa wewe ni yule mwenye umri wa miaka 37,hao vijana ni VICHECHE TU hawana lolote zaidi ya kukulamba na kuondoka,chezea bahati wakati wengine hapa tupo kwenye maombi ya kupata mume mwema,mungu kakupendelea lakini hujagundua hilo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Anonymous said…
wewe bint soma achana na wazee. Mtu wa miaka 37 kwako ni mtu mzima. Uwezi kujiuliza kwa nini akung'ang'anie wkt umeonyesha humuhutaji. Tena anakuambia ndugu zake watamuona muhuni. kwanini aonekane muhuni?inamaana ndio tabia yake.Pia jiulize ujana alikula na nami mpk uzee wake akutafute wewe. Binti fikiria kwa mapana usiwe na mtu kwasababu unataka kuolewa au pesa yake. Maana pesa ikiisha ndoa itakuwa shubiri na ndipo utaambiwa undoka na begi lako la nguo maana vyote ulivikuta hivyo ni vyake peke yake. Kuwa na mtu kwasababu umempenda toka moyoni hata kama hana ela ela zinatafutwa na Mungu hubariki pale penye amani na upendo wa kweli.
Anonymous said…
wewe bint soma achana na wazee. Mtu wa miaka 37 kwako ni mtu mzima. Uwezi kujiuliza kwa nini akung'ang'anie wkt umeonyesha humuhutaji. Tena anakuambia ndugu zake watamuona muhuni. kwanini aonekane muhuni?inamaana ndio tabia yake.Pia jiulize ujana alikula na nami mpk uzee wake akutafute wewe. Binti fikiria kwa mapana usiwe na mtu kwasababu unataka kuolewa au pesa yake. Maana pesa ikiisha ndoa itakuwa shubiri na ndipo utaambiwa undoka na begi lako la nguo maana vyote ulivikuta hivyo ni vyake peke yake. Kuwa na mtu kwasababu umempenda toka moyoni hata kama hana ela ela zinatafutwa na Mungu hubariki pale penye amani na upendo wa kweli.
Rehema said…
Mdogo wangu mimi nachangia mada kuhusu shida yako, yaani ukiangalia kwa maelezo yako inaonekana huyo jamaa ambayo akuvutii kwa sura uongeaji waje n.k ndio mwema. Maisha siku hizi ni tambala bovu onaweza ukapata mtu wa sura nzuri na kipato kikubwa lakini baadaye kero yake utaiona. UTAJUTA NA KUSAGA MENO mimi nakwambia kwani ni mkubwa kwako nimeshaonja maisha na najua. Wako watu walichagua wazuri na matokeo yake mwanaume analeta ukimwi ndani. Usiangalie sura chagua huyo huyo mwenye sura mbaya ndio atakufaa cha msingi MUULIZI MASWALI HAYA (1) KAMA UKIONANA NAYE HATAENDELEA KUWA MKWELI AU VIPI? MAANA DUNIA YA SASA IMEJAA MAGONJWA HASA GONJWA LA KUTISHA NI UKIMWI) MWAMBIE TUTADUMISHA UHUSIANO WETU BILA WEWE NA MIMI KWENDA NJE YA NDOA. HICHI NI KITU CHA MUHIMU SANA KULIKO KUINGILIWA NA BALAA LA GONJWA BAYA.

(2)AKIKUJIBU NDIO SASA MKUBALIE NA MUOANE NA MPATE WATOTO)

Wako waliochagua wenye sura nzuri na wenye sura mbaya lakini mwisho wake ni majuto.

MAANA ANAWEZA PIA AKAWA NA SURA MBAYA LAKINI AKAWA NI MOTO WA WANAWAKE. NA NDIO MAANA NIKAKUSHAURI UMUULIZE HILO SWALI NILILOANDIKA JUU.

AU KAMA UNAONA HUMTAKI KABISA BASI CHAGUA YULE MWENYE SURA NZURI LAKINI PIA MUULIZE SWALI HILO HILO NILILOKUANDIKIA JUU.

Maisha ni amani ya Mtu na utulive uliajaa mapenzi na kuoneana huruma.

Mimi Dada yako
jipanguse said…
"nataka kuolewa" umeona eh? ila huna mapz ni ile tu kiu yako ya kutaka kuolewa nakushauri usiolewe na mtu usiempenda km uyo bwege unaemchuna mana utaishi nae milele sa km humpi kuma itakuwaje kwenye ndoa nyie c ndo mnatoka nje mnashukiwa alafu badae mnatusumbua kuomba ushauri km humfeel mwache atapata anaempenda ila kumbuka bahati haijimara mbili hao mahandsome wako watakuvuruga wakuache maana wapo wengi wanaowatamani km hao marafiki zako ni hayo tu.asenti
Anonymous said…
Kila linalotupata kwa hakika ni kichumo cha mikono yetu wenyewe. Hayo unayoyafanya kwa mwenzio nawewe pia yatakukuta na wala usilie kwani ndio umepanda mbegu inaota, nawewe utapenda usipopendwa na utatumia rasilimali zako pale usipopendwa.
Inshort nataka nikujuze maana ya mapenzi, Mapenzi sio sura kwani unaweza kuwa mzuri lakini usipendwe, mapenzi sio kazi na wala sio pesa kwani unaweza kuwa na kazi nzuri na pesa nyingi lakini usipendwe ikapendwa pesa tu!!! Sasa mapenzi ni nini????
Kwa hakika MAPENZI ni HISIA sanjari na RIDHIKO LA MOYO la moyo. Kama huna hisia, hakika hapo hujapenda, na kama una hisia na hujaridhika hakika umependa lakini tabia na asili yako ni mbaya kwani c mridhkaji. Kuridhika yeyote anaweza kujifunza, bt u can nt learn to love coz love is Feelings.
USHAURI. Mwacha huyo bwana haraka sana kabla hujamuumiza zaidi. Kwa hakika tusipende kuwatendea wenzetu yale tusiyopenda kutendewa. Hebu jaribu kufikiri hw much it hurts kama wewe ndo ungekuwa huyo mkaka halafu yeye awe ndo wewe?? Hebu tuache unafiki ktk mapenzi. Sifa za mnafiki ni tatu, 1. Akiaminiwa hufanya hiyana 2. Akiongea hasemi ukweli 3. Akiahidi huvunja miadi. Hizo sifa zote unazo, kwa kifupi wewe ni MNAFIKI.
Swala la umri sio tatizo, Tulia, kwa hakika mpenzi wa kweli utampata ktk umri wowote ule ila mradi uwe na haiba ya kike na heshima na hekma cku zote. Tunza utu wako, waheshimu watu, muheshimu na umuogope Muumba wako, uwatendee ihsaani wanaokuzunguka na wanaokupenda, heshimu hisia za watu na usiwatendee watu usilolipenda kwa hakika litakurudia. Mfano. Saddam Hussein aliua mamia ya watu kule Iraq huku yeye akilindwa na mamia ya askari, Lakini Muumba we2 ni mkubwa mno kwani mwisho wa yote na yeye alikufa kifo dhalili kabisa cha kunyongwa huku wanyongaji wakimcheka na kumfanyia istizai mbalimbali, huo ndo ulikuwa mshahara wake.
Nawewe pia ondoka hapo acha kumuumiza mkaka wa wa2, kama shida yako ni pesa basi nenda kauze mwili kwa wanaume wakware sio kuwatapeli wanaume waliotulia.
Its me M.
Anonymous said…
Maliza masomo halafu utuletee hiyo hoja yako. Tukushauri nini zaidi ya kusoma na wewe ni mwanafunzi?
Acha usumbufu S O M A... Kizito!!!
Anonymous said…
Wewe bibie si ajabu una pepo.

Umeelezea vema sana jinsi jamaa huyo anavyokujali na kujikita nawe sawasawa na hata kumchuna ngozi ya mapesa yake bila hiana na matanuzi ya gari yake.

Mimi nadhani kama humpendi na hujisikii kuwa naye achana kabisa na matumizi ya mali yake.Uwe mkweli na muwazi usiendelee kummaliza mtu wa watu wakati unajua fika moyo wako haupo hapo.

Ni hatari sana kumtumia mtu kihivyo kwani siku zimwi likicharuka utalipa kwa majeraha makubwa sana.Usicehze na moto maa siku ukilipuka nyumba nzima itaungua.Mwambie mtu wa watu kuwa huna upendo kabisa kwake.Na ikiwezekana hama mji bila taarifa yake ili ukwepe shari hilo.

Pia kama hao wengine wanakuja na bado huna upendo nao tafadhali achana nao ungoje mtu ambaye moyo wako utaridhika na kuridhia kuliko kupapalika na wanaume ambao hujisikii nao.Ni hatari pia kama unaogopa tu kwamba miaka inaenda na labda hutapata mtu wa kukuoa na hivyo ukaamua kuolewa na mtu roho haipendi hapo utakuwa umejichukulia mzigo ambao utashindwa kuubeba na itakuwa soooo la kukumaliza kabisa.

Tafadhali tulia na achana na jamaa usiendelee kutumia mali yake wakati unajijua kabisa huna upendo naye.Du kumbe wadada wengine hamna huruma jamani?kweli mtu hujisikii naye lakini unaendelea kumchuna tu kisa eti kwa sababu anampenda yeye.
Anonymous said…
Wewe unajua una tamaa sana, kwanza unafanya dhambi kwa kumkatili huyo jamaa wa watu, na una tamaa au nikuite malaya na mwisho wa yote utambulia zero au waswahili wanakwambia kijua ndo hiko usipouanika baba utautwanga mmbichi, acha tamaa olewa na mjamaa wa watu sio unakula pesa yake tu kama humtaki mwambie uone wenzio watakavyochukua uzuri si hoja shost.
Anonymous said…
jamani ww dada kuwa na huruma utaki kuumia lakini unataka kumuumiza mwenzako.
unatakiwa kujifunza kujitegemea acha kuwategemea wanaume au mtu mwingine soma tafuta kazi ujitegemee na kupenda sio sura, dada.hata hao unao waona wazuri sura zao zinaweza kuharibka je utawakimbia ukatafute mwingine mwenye sura nzuri?au ww ukiharibika sura yako utajisikia je? usiwe hivyo.just tell him da truth and work hard to earn your own money. ubarikiwe
Anonymous said…
NIMEKUSOMA, NA KWA KIFUPI HUTAKAA UJE UPENDE NA HATA UKIOLEWA UTATOKA NJE TU YA NDOA. MAANA AKILI YAKO UMEIFUNGIA KWENYE MAWAZO HAYO HAYO TU, U DONT WANT 2 OPEN UP TO NEW PERSPECTIVES.......POLE ILA MWISHO WAKO KAMA UTAENDELEA HIVO NASIKITIKA KUSEMA KUWA HAUTAKUWA MZURI SANA, UNLESS UBADILIKE.
Anonymous said…
kwa haraka naona kuna mambo kadhaa makubwa yanayokusumbua, 1.ni hali ngumu ya kiuchumi inayokukabili na kutokana na hilo 2. unawataka wanaume kwa fedha zao 3.hujiamini wewe binafsi hivyo kufanya usijue aina ya mwanaume anayekufaa bila kuangalia uwezo wa kifedha.

USHAURI.
Kwa sababu huyo mdingi uliyenaye sasa upo naye sbb ya fedha, ni bora uachane naye, then usianzishe uhusiano na mtu eti sababu anafedha au sura nzuri utaishia kutoa uchi kwa watu tofauti na usiolewe. Pia umedai unasoma ongeza juhudi kwenye masomo, kupata mtu mtakayependana bila sababu za nje inawezekana, kipato kidogo cha mzazi wako kinaweza kutosheleza ikiwa hutakuwa na tamaa na vitu.
AJABU
Unadai jamaa huwa anakuachia gari yake unadrive,mzazi wako anachukulia poa tu???? wala haulizi gari ya nani
Anonymous said…
we mdada, mume/mke anatafutwa kwa kuomba mungu akuoneshe. mwanaume anayetaka kukuoa hlf wewe unakataa, yuko na mungu ndio maana anaepushwa kwa ww kugoma. atakayetaka kukuoa na ww ukaridhika nae bila lakini.... basi mtaishi kama mume na mke. mie yalishantokea. nilimpenda sana, sana yaani kupenda mwanamke 1 na nilitaka nimuoe lkn kumbe alikuwa kama ww alikua hanipendi na wala hakutaka nimuoea. yy alinifanyia hivihivi, alikua hanipi pusi, ananiudhi mara kwa mara ili tugombane, simu hapokei n.k hatimaye alikuja kuolewa na mwanaume aliyempenda na alianza mambo yake ya harusi bila mm kujua. in short, omba mungu akupe mume, usijilazimishe mume/mke. ukilazimisha mtaishi kwa furaha max 2 years baada ya hapo ni kuanza majuto. mie nashukuru mungu nilipewa mke, kwa kweli nashukuru mungu, ananipenda.
Anonymous said…
sema na moyowako,lakini tahadhari usijependa usipopendwa,wanaume ni wasanii tena usaniiwao ni mkubwa huwezi gundua maramoja.Mawazoyng midhali huyo kaka unahisi anakumpenda kweli basi huyo ndio wakuanae,maisha ya sasa bora mtu umuendeshe sio akuendeshe,ww uwe ndie mshika usukani wa moyowake.Mm mwenzako nlitendwasana lakini sasa nashkuru kunajamaa kanizimikia vibayabibaya ni aged na simzuri,nilkua akiongea mm naonakaraha,nikilalanae anaguruma kama simba,yy amelala mm natulia namuangalia umbolake kwani anajitumbo na hana matako ila maboswafi,sikuwa nkimpenda hatakidogo ila jamaa hasikii kwamimi basi nikaona nijilazimishe,huwez amini sasa nami siskii sioni sitaki hata mtu anikaribieasijenitiliamchanga kitumbua changu, natanua,nimetulia najilia vyangu wale wote walionipetezea muda sasa wanaionea gere kwani jamaa ananitunza kisawasawa,nnagara napeta.
all in all,ishi na anekupenda,kasorozake fanya kuzisahau penzi litameatu wakati anakupenda kwadhati na mbolea ya penzi anayo(pesa)laa unataka kwendateseka kwa utaowapenda ila hawakupendi sikulaumu,fuata moyowako
Anonymous said…
Mume wa kukuoa ni huyo unayembexa na kumchuna kishenzi.Yeye ameonyesha mapenzi makubwa kwako pamoja na mali zake unazozitafuna ingawa unamchunia hata kumpa penzi huku ukifurahia kuzitafuna pesa na mali zake.

Chunga sana wewe utaruka matope na kukanyaga mavi.
Anonymous said…
Bibie nenda kwa waombaji wakakuombee bila shaka una pepo fulani linakuzingira.Haiwezekani ule mali za mtu na kuzitumia lakini usimpende na hata usitake kumpa penzi.Hiyo noma sana iweje uwe tayari kutumia mali za mtu wakati humpendi?? Hebu wadada wote mnaotembelea humu jaribu kutafakari hali hiyo sijui wote kama mnaweza kuwa na tabia hiyo kikawaida???

Usipompenda mtu na mali zake usizipende pia!!!
Anonymous said…
Ni bora umuache huyo jamaa pia mueleze ukwel kua humpendi kuliko kumpotezea muda.pia usimtamani mtu kwa sura tu bali kwa penzi toka moyon.
A,Dar said…
Da, mamie unawakati mgumu sana,but siwezi kukwambia sana ila nadhani unahitaji muda wa ziada kumpenda huyo mwanaume kwakuwa me naona bora mwanaume akupende yeye sana kuliko wewe umpende sana.Hata mimi kuna wakati napatwa na hali kama yako nina mchumba ananioa soon but simfeel kivile sana'na si kwamba simpendi but siumizi muda wangu sana kwake,nilimpenda mtu once labda amenifanya hivi,nashindwa kupenda sana vile.Nakuomba umpende kama ni mpango wa mungu no matter what utampenda tu.
A,dar
Anonymous said…
Me nahisi kama sijakuelewa maana maelezo yako na hisia zako ni vitu viwili tofauti, kwanza kwa msichana alie desparate kuolewa, then akapata jamaa wa hivyo sizani kama atathubutu kufanya unavyofanya wewe, au hujui kuwa desparate na kuolewa kukoje? Then unasema uko nae kwa jili ya pesa tu kwa kuwa uwezo kwenu mdogo, sasa hayo mapozi unayomfanyia akisema akubwage, hizo hela zake ambazo ndo zimekuweka kwake utazipata vipi? Then unasema kuna wenye sura nzuri na wana kazi nzuri wanaokupenda , ila wewe huwapendi sijui huwataki, mbona havieleweki? Inshort nilichokisoma kwako ni utoto na ulimbukeni, tulia ukue kwanza uyajue maisha, cha msingi for now kwako soma umalize hicho chuo, pata kazi yako
Anonymous said…
He! ww dada una bahati lakini unazipiga mateke my dia, mm nakushauri usali sana kwa imani yako. u knw wat? may una jini mahaba thats y huna hisia za mapenzi, yani unapenda ukiona tu, lkn kuolewa, kumake love hutoweza kufeel coz inasemekana hayo majini mahaba hayapendi shea. so plz sugua magoti sali sana dia.
Anonymous said…
sasa my dia usiangalie sura ya kuvutia. mwanaume shughuli, mwanaume kipato, sura nzuri ya nn? mm nnae mmoja ananisumbua sana, ningepata mwingine alie criazi km huyo fasta ningekubali kuolewa nae.
Anonymous said…
Wewe dada naomba upige magoti, funga na umuombe Mungu kwanza akusamehe makosa ambayo unayafanya. Mchumba ambaye unatarajia kuwa ndiye awe MUME wako huwa hapatikani kwa njia hii. Njia unayotumia ni ya kiumalaya kabisa maana unatafuta sura, pesa na vitu vya thamani. Mapenzi yako MOYONI na si kwenye hivyo nilivyovitaja.

Wewe bado ni msichana mdogo kwa nini umemvulia chupi babu yako kama si baba yako?? Kama haitoshi unaendelea kuvua chupi yako kwa kila mmoja???? ACHA KABISA HIYO TABIA. Katubu uanze upya. Mungu ni mwema na ni mwaminifu ANASAMEHE na ATAKUSAMEHE.

Mume wako bado hajapatikana kati ya hao hata huyo babu yako ni muongo tu. Kama unatafuta UKIMWI aaah!! njia unayotumia ni sahihi kabisa.

Sali sana na MUME wako atapatikana. Acha kabisa UMALAYA.
Anonymous said…
Lav i 1st red ur qn n repit t over th 2nd tym. Ur jus lyk me az am in the sem sem c2atn ver bothered n don kno wea 2 go an ask n get a guinine advice. Pole sana lav wish cc dina wil advice u n ol tht hu r in nid as me. Wish lucky n hp u wil tek a yz dcsion wch wil mek u a hapiest person in the world. Xo xo xo xo
Anonymous said…
kweli wa moja yake moja,wa mia wa mia 2.mama dunia imebadilika,mke/mume atafutwi kwa sura,kuna wanawake wangapi wazuri kweli kweli wapo mtaani? mke/mume tabia,mapenzi.huyo jamaa,ww ndio humfayi coz mambo ya dunia yamekutawala,ujui nn unataka,then unasema utaki kuhumia while unaumiza wengine.kama kitu ukipendi usimfanyie mwenzio,what kind a woman r ya.unaweza kumake love na mtu usiempenda for money then unataka kuolewa? ya aint ready mama,ya have to change first,before ujafikilia hilo swala,coz wapo wenzio kama wewe wamekimbilia ndoa now they want out.dear unategemea kuenjoy sex wakati hata moyo wako haumkubali huyo kaka?then unasema his not good in bed.kila kitu kianzia kichwani mama.hata sisi wanaume kama sikukubali kabisa i wont feel nothing,atauume unaweza usisimame labda ulazimishe.so mama mwenye tatizo ni ww,umepata bahati msera anakuzimia,unaleta mambo yako ya kizamani,sometime things happen once,usije hishia story,kunakaka alitakaga kunioa.na wauza sura wako.be careful mama.
Anonymous said…
mmhhhh sijui kama nitakua nimekosea, ila nadhani wewe hauko kwa ajilia ya mapenzi uko kwa ajili ya fedha, maana hainiingii akilini unampenda mtu kwa ajili ya kazi yake, nyumba yake, kukupa gari uendeshe mmhhh , kama ni pesa dada tafuta zako
Anonymous said…
Huyu Mdada mkorofi sana unajua ndoa ipo tu leo kesho na hata mwakani. usiikimbilie maisha hayako hivyo. Uchi ulionaso ni wa heshima sana hutakiwi kuupa misukosuko wakati bado unasoma. Tulia soma kwanza maadam umekili bado uko shule endelea na masomo.
Kama hamu yako ni kutombeka yutatombeka tu muda ukifika......Kifuna!!
Edamo said…
Pole sana bidada km nimekusoma vizuri tatizo lako kubwa ni kushindwa kutofautisha kati ya kumpenda mtu na kupenda alichonacho mtu.Usikubali kuwa mtumwa wa mapenzi kwa sababu ya shida zako za fedha na tamaa ya kutaka mambo makubwa usiyoyamudu.Wewe huna hisia za kimapenzi kwa hao wanaume wote kwa kuwa unashobokea pesa na kazi ya mtu na wewe ni sawa na malaya anayejiuza maana huwa haangalii kupenda mtu bali pesa za mtu tu.Wewe ni mchunaji na utakuja kujikuta umeolewa na mtu usiyempenda mwishowe utaanza kuja tena hapa bloguni kutusumbua kwa ushauri wakati ni tamaa yako inakusumbua.Vilevile unaweza kuzalishwa na kuachwa kumbuka pesa unazopewa na mwanaume haziendi bure itakutokea puani.Nakushauri achana na huyo mwanaume haraka sana kama huna mapenzi naye na hata hao wengine wawili achana nao ikiwezekana rudi kwa yule wa awali maana huyo unampenda lakini mlikuwa mkigombana hovyo kwa sababu ya tabia yako ya kushobokea wenye pesa,kumbuka thamani ya pesa huja baada ya mapenzi ya dhati.Usiwafanye wanaume mtaji maana nao watakufanya biashara yao na mwishowe utakuwa wa kumegwa na kuachwa mpaka utajiona huna thamani duniani,tulia vuta subira umalize masomo yako utampata umpendae kwa dhati kuliko kuwa mtumwa wa mapenzi kwa mali ama kazi ya mtu.
Edamo said…
Pole sana bidada km nimekusoma vizuri tatizo lako kubwa ni kushindwa kutofautisha kati ya kumpenda mtu na kupenda alichonacho mtu.Usikubali kuwa mtumwa wa mapenzi kwa sababu ya shida zako za fedha na tamaa ya kutaka mambo makubwa usiyoyamudu.Wewe huna hisia za kimapenzi kwa hao wanaume wote kwa kuwa unashobokea pesa na kazi ya mtu na wewe ni sawa na malaya anayejiuza maana huwa haangalii kupenda mtu bali pesa za mtu tu.Wewe ni mchunaji na utakuja kujikuta umeolewa na mtu usiyempenda mwishowe utaanza kuja tena hapa bloguni kutusumbua kwa ushauri wakati ni tamaa yako inakusumbua.Vilevile unaweza kuzalishwa na kuachwa kumbuka hakuna pesa unazopewa na mwanaume haziendi bure itakutokea puani.Nakushauri achana na huyo mwanaume haraka sana kama huna mapenzi naye na hata hao wengine wawili achana nao ikiwezekana rudi kwa yule wa awali maana huyo unampenda lakini mlikuwa mkigombana hovyo kwa sababu ya tabia yako ya kushobokea wenye pesa,kumbuka thamani ya pesa huja baada ya mapenzi ya dhati.Usiwafanye wanaume mtaji maana nao watakufanya biashara yao na mwishowe utakuwa wa kumegwa na kuachwa mpaka utajiona huna thamani duniani,tulia vuta subira utampata umpendae kwa dhati kuliko kuwa mtumwa wa mapenzi kwa mali ama kazi ya mtu.
Anonymous said…
You'll never know what you got till it's gone!! Hakuna mtu perfect, so please dada, take stock of what you have, accept, take it and trust God to make you love it. Most importantly, these issues are two way trafic...as you analyse them, surporsing someone analysed you; are you that perfect person you are trying to create?? We are all human, each with our own flaws; Stop the pride, accept what you've got and make a decision. Good luck!

Harry from Kenya!
Anonymous said…
Mpenzi unaonekana uko very selective na tatizo ukichagua sana utakuja kosa kabisa, angalia usikute unademand vitu visivyokuwa na msingi kwenye mapenzi. La msingi ni upendo wa kweli and not good in looking, educated man, money etc. no love is love na kuna wakati unahisi humpendi mtu lakini ukikaa nae the way anavyoongea na kutake care tu ukampenda mpaka basi yani ukakuta unampenda kuliko. so be careful usije baki njia panda mwenzangu nimeona wengi wakilia kwa kuchagua weeeeeee mwisho wanatafuta hata chongo hawampati.
Anonymous said…
Nadhani unahitaji msaada wa kisaikolojia kwa sababu kwanza unaonekana una ubinafsi ndio maana unafikiria kupata mtoto mmoja tu.Pili una mtu ambaye umesema humpendi na ni mbaya kitandani, sasa unataka ujitese kwa kuwa naye muda wako wote uliobaki duniani kwa sababu ya pesa au gari au nyumba?.Hivyo ni vitu ambavyo unaweza kuvipata na yule unayempenda na kufurahia maisha naye.Uko kwenye early twenties weka priorities zako right kwani unaweza kuendelea na masomo ili uje kupata kazi nzuri na ndoa nzuri zaidi na mtu ambaye mtachuma wote.Na uliolewa na mtu mmtakayependana na kutaka kuanzisha familia haitakuwa kwa ajili ya mtoto mmoja tu bali kadiri mungu atakavyowajalia na kwa kutaka kwenu. Ufanye nini? Jipe break, sali,uache vya bure,na jipange upya
Anonymous said…
Penda unapopendwa usije penda usipopendwa. Sura , pesa sio ishu sana kwenye mapenzi muhimu ni mapenzi ya kweli.
Mimi kwa mtazamo wangu angalia tabia yake, anakuthamini? ni muadilifu? mambo ya kitandani anaweza kujifunza...hata wewe inawezekana ukawa hauko perfect. Je ni mcha Mungu? Je ni mtu responsible? Ndoa zina kazi mdogo wangu usione waatu wanatembelea mabenzi...wanalia machozi. Ila nafikiri pia una utoto fulani hauko tayari kuolewa. Nakuomba sana usimdharau huyo mwanamme...unaweza kumwambia tu akupe muda.
Anonymous said…
Penda unapopendwa usije penda usipopendwa. Sura , pesa sio ishu sana kwenye mapenzi muhimu ni mapenzi ya kweli.
Mimi kwa mtazamo wangu angalia tabia yake, anakuthamini? ni muadilifu? mambo ya kitandani anaweza kujifunza...hata wewe inawezekana ukawa hauko perfect. Je ni mcha Mungu? Je ni mtu responsible? Ndoa zina kazi mdogo wangu usione waatu wanatembelea mabenzi...wanalia machozi. Ila nafikiri pia una utoto fulani hauko tayari kuolewa. Nakuomba sana usimdharau huyo mwanamme...unaweza kumwambia tu akupe muda.
Majoy said…
Chonde chonde we dada unaejisema upo kwenye dilema...dunia ya leo wanaume kama huyo unaemponda wapo wachache sana kwani wengi wanatafuta wanawake wenye kipato au source ya income.Angalia sana ucje ukajuta maana wahenga walisema mkataa pema pabaya panamuita.huyo kaka ni mwema na ameonyesha mapenzi ya dhati kwako rudisha moyo wako na ujifunze kumpenda nina uhakika utafanikiwa dear usipoteze hiyo bahati kwani wakati utakapoihitaji haitakuwepo tena.
Ni hayo tu mdogo wangu na nakutakia kila la kheri katika maamuzi yako kwani ni wewe pekee unaeweza kujenga au kubomoa maisha yako.

Majoy.
emu-three said…
Swali la kujiuliza ni je nini unataka katika maisha yako, pesa na mali, sura nzuri au upendo!
Nasema hivi kwasababu sio rahisi kumpata `mr world' handsome guy with plenty of everyting!
Ukimpata mwenye pesa anaweza akawa kibogoyo, sura kama limau. Ukimpata mwenye sura nzuri anaweza akawa hana kitu,mifuko ipe nje!
Ukimapata mwenye upendo anaweza akawa hana mvuto! Ilimradi binadamu wote hatujakamilika.
Ndoa ni bahati yako, ukimpata mnayeivana, kwa tabia basi mengine mtayapanga pamoja, kwani siku hizi karata mnazicheza wenyewe, mwisho wa siku mnaweza mkajenga hekalu.
Kwanini usubiri mwenye pesa, au tajiri kwanini msitafute wote huo utajiri, je wewe ni tajiri mapaka umtafute tajiri? Ni maswala ya kujiuliza.
Cha muhimu ni upendo wa dhati!
Anonymous said…
Your too young my dia, plz tujuze anaishi wapi na namna ya kumpata. i think a will fit for him, am 30 years old. tutaendana.
Anonymous said…
Thanx people nitazingatia mliyonambia, as of now nimeachana nae......ila bado he does not want to let me go. nimebadilisha namba ya simu nasina mtu yeyote and life feels good na natafuta alternative ya kupata temporary job......thank u
Anonymous said…
KUNA WATU WA AINA MBILI
1. NI WALE WANAOWEZA KUISHI NA MTU KWA VITU ALIVYONAVYO.
2.NI WALE WANAOISHI NA WATU KWA KUWAPENDA SIO KWA MALI ZAO.

SASA WEWE JIULIZE NI KUNDI GANI LAKO, ILI UNAPOCHAGUA UJUE NDIO MAISHA YAKO NI UISHI KIUKWELI KUTOKANA NA CHAGUO LAKO.

ILA NINGEKUSHAURI CHA MUHIMU NI KUCHAGUA MTU ANAEKUPENDEZESHA MOYO WAKO, MAANA KAMA UTAOLEWA NA HUYO JAMAA NA ANAKUKERA TENDO LA NDOA LITAKUWAJE? MAANA HUWEZI KUIDANGANYA NAFSI YAKO.
KAMA UNAPENDA CHUNGWA KWANINI UKALE LIMAO? CHAGUA CHUGWA LINALOKUTAMANISHA KABLA HATA YA KULILA HATA KAMA UMELIOKOTA NJIANI. G'D LUC
Anonymous said…
hauna tofauti na malaya anaesaka wanaume kwa MAPENZI Vs MALIPO.WEE binti umekosa sifa za kuwa mke,unataka watu wenye pesa na kazi nzuri,siku pesa zikikata utakimbia nyumba,sifa kubwa ya mke ni UVUMILIVU KWENYE SHIDA NA RAHAA...wee bado mtoto hujui kitu kwa maisha..kubali hali yako ya umaskini ishi maisha uliyopewa na mwenyezi..j. arusha
Anonymous said…
Ama kweli punda wake mzigo.Wewe dada unataka aje mtu wa namna gani?Ninyi ndo wale baadaye mnajuta na kubaki mkikomaa baada ya kukosa bahati acheni hizo! Huyo unayemtaka madam sasa hayupo basi aliyekuja ndo wako!
Anonymous said…
yani kichwa cha habari kimenivutia kukusoma,ila uliyoyaeleza ni upuuzi mtupu,kwa kifupi hujatulia wewe dada,na akili ya maisha haijakukomaa,
amgali sana!!!!
Anonymous said…
there we go!! material girl is what you are...olewa na sura uone cha moto! wenzio waliambukizwa kwa kukimbilia sura tu
Anonymous said…
JAMANI MIE NAKUSHAURI HIVI
USIJILAZIMISHE KUOLEWA NA MTU AMBAYE HUMPENDI HAJAKUOA UNAMFANYIA VISA ILI AKUCHE JE AKIKUOA SI ITAKUWA BALAA USIKU WA MANANE AKITAKA URODA?
MAPENZI YA KULAZIMISHANA SI MAZURI UKWELI NI HIVI KILA MTU NA CHOICE ZAKE JAMANI MSIMSEME DADA WA WATU KAMA ANA PENDA MTU HANDSOME KILA MTU ANAPENDA MTU HANDSOME SEMA WENGI WA MAHANDSOME NI MAPLAYER WACHCE SNA WAOAJI.
MI NAKUSHAURI USIMPOTEZEE KAKA WA WATU MUDA HUYO SI CHAGUO LAKO YANI MI HAPA NIMEKUELEWA SNA. KWA UFUPI SO CHAGUO LAKO SO WLA SUIFE MOTO IPO SIKU UTAMPATA MTU AMBAYE NI CHAGUO LAKO.

MSIZINGUE DADA WA WATU KUMUAMBIA HUYO NDO MUME WA HERI KWAKE USIJILAZIMISHE KAMA MOYO HAUTAKI. KUJILAMISHA KUMPENDA MTU NIKUBAYA SNA

ACHNA NAYE MSAHAU ENDELEA NA MASOMO HOPE U WILL FIND SOME ELSE CHOICE YAKO GO GAL ACHANA NA WASWEMA HOVYO.

TWISHENI
Anonymous said…
kama huyo mwanaume haumpendi niachie mimi maana anaonekana ni mwaminifu na anaroho nzuri, hao wauza sura ni waongo sana tena sana unachotakiwa kuangalia ni kama kweli unapendwa mengine utamrekebisha maana hakuna mwanaume wala mwanamke mbaya ni jinsi unavyo muweka fikiria marambili dada shauri zako utaja juta sana
Anonymous said…
Dah!!
(i)_Kwa mujibu wa maelezo yako we unaonekana hata kutombana hujui
nasema hivi coz nawajua mademu wa jamii yako yaaani mnaboaaa!!!
(ii)Huna urembo wakutisha hata uwezekumpagawisha m2 yaani mi nilichokiona kwa jamaa ni kwamba yawezekana ametoka kwenye familia yenye maadili tofauti na wewe.Nilicho gundua kwako we ni aina ya
(i)nitombe nikale i mean upo kishida zaidi
(ii)Aina ya mademu wanao jifanya marketable huku michoko tu. ...na namalizia kwa kusema unaendeshwa na hisia zaidi na sio akili na ni hatari sana kwa maisha ya sasa-Hofu yangu ni kwamba upo uwezekano wa kumuua mshkaji na NGOMA kwa mfumo wako wa kisen***-Ushauri_fanya maamuzi sahihi though kuolewa sio lazima,mfumo wako ni hatari unamadhara sana kwa wakati tulio nao.Black mu2.
Anonymous said…
omba mungu akujalie upate mume ataekupenda na ww umpende zaidi yameshaongelewa so kuwa na huruma mtu anakupenda na we hufeel chochote so angalia!