Mume kung'ang'ania picha za Ex wake ni kawaida?-Ushauri

"Habari Dada Dinah, Mimi ni mwanandoa ambaye nakaribia kumaliza mwaka sasa kwenye ndoa yangu. Tatizo langu ni kuwa mume wangu ana picha alizopiga na wapenzi wake wa zamani na hataki kabisa ziondolewe kwenye albam.

Ukigusia hilo suala ni ugomvi mkubwa, je Dada Dinah hiyo ni haki? au nichukue maamuzi gani? Nizitoe tu hapo na kuzichoma moto au nijifanye sijaziona na akiniuliza nimjibu kuwa sijui zilikokwenda na kumbe najua?

Maana yake kwa kweli zinanitia kichefuchefu. Tena kibaya zaidi ni za wasichana wa kizungu wawili tofauti, Je ndoa ndiyo zilivyo Dada Dinah au huyu mwenzangu ana lake jambo? Hao wasichana wako Ulaya yeye aliendaga kusoma huko siku za nyuma kama miaka mitatu ilopita na ndipo aliporudi akakutana na mimi tukaanza mahusiano na mpaka kufikia ndoa.
Naomba ushauri wenu jamani mnisaidie."

Dinah anasema: Ni njema tu Mdada, Unauhakika kuwa ni wapenzi wake au walikuwa marafiki tu wa Chuoni? Maana kuna Watanzania wengi wajinga wajinga wanadhani ni sifa kuwa waliwahi kutoka na Wakoloni (Wazungu) kimapenzi au kuthibitisha kuwa alisoma nje basi anatunza Picha za wanafunzi wenzake.


Ikiwa ni kweli ni wapenzi wake hakika anachokifanya sio haki, si hivyo tu mumeo hana heshima na wala hajali hisia zako kama mkewe. Katika hali halisi unapokuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi wa kudumu na mtu hapaswi kuwa na Picha za wapenzi wake wa zamani let alone kuwa kwenye ndoa.

Picha za maisha ya shule/chuo yaliyohusisha wapenzi huwa tunaziacha nyumbani kwa wazazi, album za wanandoa huwa na picha zenu mlipokuwa wapenzi na zile za ndoa, za wazazi wenu ndugu, jamaa na marafiki sio exes.

Unapoingia kwenye ndoa unaacha kila kitu huko nje na kuanza maisha upya, ndio maana huitwa maisha mapya ya ndoa. Wote wawili mnaanza upya sio tu kama wapenzi/familia bali pia kama individuls.

Kama umejaribu kumuomba kwa ustaarabu aziharibu Picha hizo na yeye kuwa mkali na hata kuibua ugomvi basi kuna mawili ya kufanya;

(1)~Ziondoe na uzifiche mahali kisha tafuta njia ya kumfanya aongeze picha kwenye album ambayo ilikuwa na hizo Pics za Exes. Asipoziona ni wazi kuwa atakuuliza au kukushutumu kuwa umezitupa na kuibua ugomvi kama kawaida au anaweza kuuliza tu picha fulani ziko wapi? Mwambie ukweli kuwa Picha hizo zinakunyima raha, zinakufanya usijiamini n.k.

Kama ugomvi utakuwa mkubwa sana, basi mwambie "naona hili suala la picha za wapenzi wako wa zamani limekuwa ni tatizo kubwa kwenye ndoa yetu, hivyo naomba tuliwakilishe kwa wazazi wa pande zote mbili" katika hali halisi ni jambo dongo sana kulipeleka kwa wazazi wenu sio hivyo tu litamfanya asikie aibu na ku-give up....then acha siku mbili zipite alafu zipige kibiriti.

(2)~Tafuta picha za the hot guys kuliko yeye lakini wabongo na wewe ziweke kwenye album yenu. Au kama kuna picha ambazo ulipiga zamani ukiwa na wanaume ambao sio ndugu na yeye hawajui ziweke kwenye album hiyo....so he can learn the hard way.

Natumaini unafanyia kazi ushauri wa wachangiaji wengine.
Nakutakia kila la kheri

Comments

Anonymous said…
He is just selfish, je na wewe ukiamua kuwaweka maX-boyfriend wako kwenye hiyo family album atakubali, hebu muulize kama kweli hataki kuziondoa basi na wewe huoni kosa kuziweka za kwako za wapenzi wa zamani uone kama hatazitoa?.
Anonymous said…
Jamani wee bibie, ya nini hayo kuhangaika na picha hizo?

Mimi ni mwaume na nimeoa miaka imepita,nina album mbili zenye picha mbalimbali za marafiki zangu wanaume na wadada kutoka vyuoni na sekondari hadi makazini na nilikuwa na mpenzi wa kizungu pia huku ughaibuni.Na nilimwambia mke wangu wadada wawili ambao niliwahi kuduu nao na huyo zungu.

Nimetunza picha zao bila hiana na wala sina nafasi ya kuwarudia, ila ni marafiki wazuri tu maana hatugombana kwa lolote.Na mke wangu ameridhia kabisa na hana wasiwasi nami.Rafiki ni rafiki hata kama walikuwa wapenzi,hiyo hatua ilikwisha sasa ni mambo ya ukubwani na huwezi kumtupa rafiki.

Kwa hiyo bibie mwachie uhuru wake huyo mumeo kwani angetaka kuendelea na hao wazungu unadhani una uwezo wa kumzuia hata kama utachoma picha zao? Wwe umeolewa naye kwani hakuwaona kuwaona hadi akaja kwako?Jua kuwa hiyo ni safari tu aliyopitia la mwisho ikaishia kwako,period.

Kumbukumbu ni muhimu bibie haijalishi nani na nani unatunza picha yake.Tulia mama utachemsha haraka hapo usipooangalia.
Anonymous said…
pole sana dada, nawe chukua za x wako ziweke kwenye album then utaona kama atapenda. hawa wanaume wanajua wao tu kuumia ukiwatendea lkn kwa wenza wao wanaona poa. CHUKUA ZA X WAKO MAMA WEKA NA WEWE
Anonymous said…
mh shost pole aisee haiwezekani kwakweli hamna reason yoyote ya yeye kukeep hizo picha coz mnapooana ni wazi mnaanza mwanzo mpya we na yeye that means hizo background zenu zinakufa sasa inakuwaje aendelee kuzingangania?mimi binafsi ilikuwaga hivyo kwa mume wangu wakati huo mchumba tunakaribia kuoana akawa hataki eti picha ya ex wake niitoe basi siku alienda job alivyorudi mi nikazichoma moto kila kitu cha huyo dada na kadi zote basi alivyorudi palichafuka kwelikweli nikamwambia achague moja mimi au huyo ex wake mbona alicool ila kwa undani zaidi kunakuwa kuna kitu kinaendelea kati yao be careful, we choma hizo picha sasa ndo atoe huo uamuzi whatever coz hata mkienda kwa wazeee au kanisani au msikitini utamshinda
Anonymous said…
mimi nilifikili hao wazungu wapo hapo bongo,kumbe wapo mbali kabisa na huyo jamaa!
Mimi nakuomba tu uwe unajiamini ukizingatia jamaa ameshakuoa sasa izo picha zinakusumbua nini? labda anatunza kama kumbukumbu tu ya kuwa alikuwa huko masomoni na hao labda ni rafiki zako wa siku izo,au amewahi kukutamkia kuwa anataka kuwaoa? au anawasiliana nao?
Sasa kama hakuna na wewe si upo kwenye ndoa yako shida ya nini kujiumiza kichwa?
Naomba jiamini na umwamini jamaa yako!
Anonymous said…
Jiamini dada yangu iyo ndio silaha kubwa sana,ukizingatia hao vimada wapo mbali na ww sioni kaa kuna shida hapo!!
Anonymous said…
Mpenzi mweleweshe tu kuwa hizo picha zinakukosesha amani. Ila tafuta siku ambayo mna raha wote sio mtu hana mudi unaanza kuropoka. Mweleze kwa upole kama ni mwelewa na anakupenda hataki ukwazike atatoa ILA KUWA MPOLE USIWE UNAMWAMBIA KWA KUFOKA AU KWA UKALI HAWA VIUMBE UNATAKIWA UKAE NAO KWA UPOLE
Anonymous said…
tena wako mbali hivyo, wala usigombana nae, wadharauuu, ujifanywe huwaoni maana kiukweli hamna wanachokupunguzia wangekua hapa bongo tungesema labda bado yuko nao...we tulia, tena muonyeshe mapenzi motomoto, atajiona mjinga mwenyewe!
Anonymous said…
c kawaida kabisa inaonyesha hakuthamini, yani km hapendi kukupoteza lazima angezificha ama kuzichoma kabisa, ameshaona huna any means ya kumtoka yani ndo umefika, tena huyo mumeo ana dharau sana,(muhaya nn?) hana adabu kabisa. unajua kuna v2 unawaza found for bad lucky lkn hivyo anakuonyesha live dah! bidada FURUKUTA ucmchekee hata kidogo huyo.
Mama 2 said…
Hayo siyo maisha ya ndoa. Kwa kuwa mnapoamua kuoana ina maana kila mtu ameachana na mambo yote ya huko nyuma. Sasa kama yeye anazing'ang'ania maana yake kuna kitu bado kinaendelea. Zichane uone atafanya nini. Kama kweli wewe ni mkewe na alikupenda na anakupenda toka moyoni mwake hawezi kukasirika au kukuacha sababu ya picha. Au la nawewe kama una picha ulizopiga na wapenzi wako wa zamani ziweke peupe azione uone kama hajakasirika. Vinginevyo atakuwa hakupendi bali alikuoa kwa bahati mbaya.
Polee! dada. Ningekuwa mimi siku nyingi nishazichana.
Anonymous said…
Picha ni ukumbusho tu jamani, kwani wewe amekukataza kuziweka za kwako?

Mbona mimi naona unasumbuka na mambo yasiyolipa bibie?Suala kama hilo ni la kukukosesha usingizi nalo wakati hao walimbwende wenyewe wako looooongi hasa?

Hata Dina namshangaa eti anakuambia asipoziondoa upeleke shauri kwa wazazi wote pande mbili,jamani kitu picha tu,kwa nini unakosa kujiamini hivyo?Ukipeleka suala la picha na mengine makubwa utapeleka wapi?

Kuanza maisha mapya ya ndoa hakuna maana kwamba wa zamani huwezi kukutana nao huko mitaani au mahali popote,na je ukikutana nao utawatukana kwa sababu sasa una mume/mke wako?

Umekosa moyo wa kujiamini kwamba uko kwenye ndoa.Tena nikwambie wazungu wakishajua mtu kaoa hawana tabia ya kurudi huko hata iweje kwani wanaheshimu sana ndoa ya mtu,labda awadanganye amekutaliki.

Mke wangu aliikuta album ya marafiki wangu wote wa zamani huko wanaume kwa wanawake,haidhuru nani alikuwa mpenzi au vipi.Hiyo haimpi shida kwa sababu na yeye ana ya kumbukumbu pia.

Wanawake mna shida sana,huwezi kummiliki mwanaume kihivyo akiamua kwenda out atakwenda na hasa ukionyesha wivu wa kijinga kama huo atakufanyizia kikweli hata kama hakuwa na mawazo hayo.
Anonymous said…
Huyo anonymous wa mwisho asijidai kusema wanawake, kama yeye mkewe alikubali inategemea jinsi walivyokubaliana, kila nyumba na mpangalio wake. Na kuhusu mwanaume kutoka nje ya ndoa atoke tu, ila asimvunjie heshima mkewe, anayofanya huyo bwana ya kumkataza mkewe kutoa hizo picha, ni kumuonyeshea kwamba yeye kidume, siyo vizuri. Sisi tunajua kama wanaume asilimia kubwa mna wanawake wa nje, hata wewe mwenyewe naamini unaye, lakini fanya mkeo asijue. Kwa nini mvunjiane heshima wakati uliamua mwenyewe kumuoa?
Anonymous said…
Bibie, usikubali kuzichana au kuzichoma picha hizo kwani utazua tafaruku kubwa zaidi ya hilo unalosuza nalo.

Sidhani kama mumeo amewarudia hao walimbwende kujenga nao mahusiano ya kimapenzi.Suala la picha lisikuhangaishe kwani uko kwenye ndoa.Picha ni picha tu mama!!

Wee jaribu kufuata ushauri huo wa kuzichana au kuzichoma utaruka matope na kukanyaga mavi bibie?Kama yeye amezitunza zina maana yake kwake wewe mwachie uhuru wake.Na wewe weka za kwako kama unazo uone kama ana shida nazo.

Mbona kuna watu waliwahi kuzaa na watu fulani nje huko kabla ya kuoa au kuolewa, lakini baada ya kuoa au kuolewa bado wamekuwa ukaribu tu wakishirikiana katika mambo mengi tu kama kawaida.Suala la picha halina atarudi tena huko kudoea.
Anonymous said…
Nadhani tunatakiwa kuwa makini tunapowapa watu ushauri maana ushauri mwingine unapotosha badala ya kusaidia. Wanawake wengi wameongelea kuwa mume wa huyu dada ni selfish kwa kutojali hisia za mke wake na kudai achane hizo picha, lakini wanasahau kwamba kwa kuchana picha mke atakuwa amekuwa mbinafsi zaidi kwa kutokujali hisia za mume na umuhimu wa hzo picha kwake. Assume umezichana alafu akakuambia hao watu ndio waliomsaidia wakati akiwa na matatizo huko alikosoma na kumbukumbu yao kwake ni muhimu sana utafanyaje? Acheni kutokujiamini na kushabikia mambo yanayoweza kuvuruga ndoa badala ya kujenga, we jaribu kuchana alafu moto wake utauona, mume wako atajua huthamini hisia zake na yeye hata kuthamini pia.
Anonymous said…
Nadhani tunatakiwa kuwa makini tunapowapa watu ushauri maana ushauri mwingine unapotosha badala ya kusaidia. Wanawake wengi wameongelea kuwa mume wa huyu dada ni selfish kwa kutojali hisia za mke wake na kudai achane hizo picha, lakini wanasahau kwamba kwa kuchana picha mke atakuwa amekuwa mbinafsi zaidi kwa kutokujali hisia za mume na umuhimu wa hzo picha kwake. Assume umezichana alafu akakuambia hao watu ndio waliomsaidia wakati akiwa na matatizo huko alikosoma na kumbukumbu yao kwake ni muhimu sana utafanyaje? Acheni kutokujiamini na kushabikia mambo yanayoweza kuvuruga ndoa badala ya kujenga, we jaribu kuchana alafu moto wake utauona, mume wako atajua huthamini hisia zake na yeye hata kuthamini pia.
Anonymous said…
Wadau mnaomdanganya huyu dada atoe picha, achome hizo kumbukumbu za mwenzake hamtendi haki. mimi ni mwanamke napenda kumthibitishia dada huyu kuwa mapenzi ni ndani ya nafsi endapo bwana huyu bado anapenda alikotoka au pengine popote ni maamuzi ya nafsi yake na wala huwezi kumbadilisha, tusitazame upande mmoja wa shilingi jamani, kwani madam ww huyo mumeo anaweza kuondoa upendo na kumbukumbu ya mtu wako kama ulikuwa nae kwa kuchoma picha au kupiga kelele? siri ya mwanadamu imejificha ndani ya moyo wake hakuna mwenye mamlaka ya kubadilisha chochote cha matamanio yake ila mwenyewe,jali kama anakuheshimu na kukutunza mengine ni mapito tulia angalia maisha yako mapya na mumeo.