"Heshima yako dada Dinah.
Napenda kutoa pongezi kwako na kwa wachangiaje wote ambao wapo bega kwa bega kutoa ushauri katika topic mbalimbali. Mimi ni mmoja wa wapenzi wa blog hii, nimekuwa nikifuatilia kwa karibu sana mada mbalimbali na kujifunza mambo mengi kwakweli.
Dada dinah kama unavyojua matatizo tumeumbiwa nayo binadamu hasa katika barangeni hili la mapenzi. Mimi ni kijana mwanaume, umri miaka 22. Kusema kweli mpaka sasa mwenzenu nipo njia panda kuhusu msichana ambaye ninampenda sana ila simuelewi hata kidogo kama kweli ananipenda ama la.
Ni miezi sita tangu ni mueleze hisia zangu juu yake bahati nzuri alinielewa na akanipa jibu zuri ambalo lilinifanya nisijute kumpenda. Tangu hapo nilikuwa nimechizika kwake nilipenda kila wakati eidha nimuone au nisikie sauti yake tu. Hapo ndipo nilipo fikia uamuzi wa kumnunulia simu ili mawasiliano kati yangu na yeye yawe rahisi.
Tangu hapo nikawa nampigia simu mara kwa mara wakati mwingine anapokea wakati mwingine hapokei, basi ninaamua kumtumia sms ambazo pia hakuona umuhimu wake, nasema hivi kwasababu ninapo muuliza kama amepata sms yangu hunijibu sms ipi? Ilikua inasemaje? Basi tu ilimradi.
Haya yote sikuyatilia umuhimu kwa kuwa nampenda ila wasiwasi wangu umeanza kuja hapa, tangu niwe na mahusiano nae sijawahi kukaa nae tukajadili kuhusu mapenzi yetu kwa kuwa huwa anakataa na kudai kuwa anashughuli nyingi.
Pili sijawahi hata kumkiss shavuni achilia mbali romance nimejaribu mara kadhaa kumuomba tutoke out japo twende hata beach lakini huwa ana kataa sababu ni hizo hizo. Nimemjali kwa mengi bado haoni umuhimu wangu kama mpenzi wake. Pia nikakubaliana na yote hayo hivyo mapenzi yakawa ni ya kwenye simu tu hakuna kuonana.
Kikubwa kinacho niumiza mimi mara kadhaa ninaweza kukutana nae katika mizunguko lakini cha ajabu huwa hana muda na mimi hata salamu mpaka nianze mimi. Nikikaa kimya hunipita kama hanioni. Dada dinah kiukweli nimekuwa sina raha muda mwingi nawaza kwanini ananifanyia hivi lakini nakosa jibu, hata yeye mwenyewe ninapo muuliza huwa hanijibu chochote.
Sasa sijui amedhamiria au ndio mapenzi yenyewe! naweza kusema alibadilika pale tu nilipo mnunulia simu na ilikuwa ni wiki moja tu baada ya kunikubalia ombi langu. Anayo nifanyia ni mengi mno ila sipendi kuwachosha wachangiaji kwa kusema yote.
Hivyo mwenzenu mpaka sasa nipo njia panda, neno nakupenda limebaki kuwakumbukumbu kwangu. Nimeshajaribu kufikiria kumuacha niwe alone lakini nashindwa, je nifanye nini mwenzenu.
Ahsanteni".

Comments
Gg
na kusema ukweli kua umemnunulia ni vigumu ,na akachimbwa biti akaamua kuachana na wewe kuepusha shari, na kuku ambia ukweli hawezi kwakua inaelekea anakupenda lakini hawezi kwakua bado yupo chini ya wazazi na anaogopa kuwaambia ukweli ,fanya uchunguzi katika hili inawezekana ika ndio sababu hasa yakufanya hivyo .
maana nakumbuka hata mimi nilianza uhusiano nikiwa na umri kama wako nikutana ma mpenzi nilikua naogopa hata kumsalimioa maana naogopa mtu asije akaniona akapeleka umbea nyumbani ika tabu,hata busu nilikua sitaki akilazimisha basi nitaangalia kila upande nikiridhika kua hakuna mtu basi ndi kiss nasio kwamba nilikua sipendi lakini niliogopa sana kuwapa wazazi stress ,na hata swala la beach nilipinga vikali maana nilifikiria nitaaga vipi kwenda huko na sikupenda kuwa danganya wazazi wangu ,na nilijisemea hivi nidanganye kua naenda mahali alafu niende beach mara nikifika huko nikutane na mtu wa familia kaenda huko nitakua mgeni wa nani mimi ,kwahiyo sikuthubutu hata kidogo ,inawezekana na yeye akawa na tatizo kama hilo .uhusiano wenu bado ni mchanga humja juana vizuri ,jari kuchunguza kwa makini utaujua ukweli.nakumbuka mimi nilimwambia baba watoto wangu ,mashari kua mimi sitakuja kwako labda uwe una umwa ndio nitakuja kukujulia hali tena kwa muda wa dakika 30 tu ,sitapata muda wakutoka na wewe, sihitaji zawadi zako zaaina yeyote ile hasa durable goods kama sim ,nguo etc. kweli nilimpa wakati mgumu sana lakini nikua sina jinsi maana nilikua mwanafunzi japo wa kidato cha sita ,na wazazi hawana tabia za kizungu kwahiyo ilibidi iwe hivyo .kwahiyo inawezekana na yeye inashida hiyo. fanya uchunguzi
Dogo, go back and re-write your objectives
Cha kufanya ni kukaa kimya, tulia look around utakutana na mwingine tu na mambo yataenda sawa. After all bado mdogo sana, 22 ni bora utumie muda wako kujisomea au kufanya mambo ya msingi ambayo yatakupa shavu baadae. Inawezekana anakuona mdogo ndo maana yuko hivyo. Kwa kifupi achana naye.
Wewe pamoja na huyo mlimbwende ni wachanga mno kuparamia mastress ya mapenzi.
Miaka 22 uko mchanga huhitaji kujikita mno nayo,take mapenzi as simple as you can.usipoteze muda kujikita nayo yatakuaharibia mwelekeo hatimaye ukajikuta unajiumiza bure.
Huyo binti inaelekea kabisa ni mtoto sana na pia amekuona una papala naye sana kiasi kwamba unapoteza muda wako kummingulia saa zote.Wewe huoni anadhiriki kukupita bila kukusalimia?
Ushauri wangu ni kwamba kaa kando kabisaaaaaaaa fanya kama hummaindi kabisaaa atakutafuta yeye.Hata sielewi kama uko chuo au unafanya nini, nilitaka kukuambia kuwa mapenzi ni sumu hasa ukijirembesha na mtu asiyekujali kama hivyo.Achana nayo kwanza endelea na mipango inayokuhusu wewe kama wewe tu hasa shule kama unasoma chuo au vipi.
Mbona watoto wa kike wamejaa kibao, ni vile labda hujatembea mahali pengine upo hapo ulipo hivyo umejifunika blanketi zito hata huwezi kuona wengine kando yako.Mbaya zaidi msichana akigundua kuwa unampenda sana atakutesa hadi ujinyonge.Achana naye tulia kwanza.
STRAWBERRY
Pili nyie ni marafiki tu, usikimbilie yale ya uchumba na ya ndoa kabla hamjaewana. Nasema hivyo kwasababuu mapenzi wkati mwingine ni kama ulimbo, ukikunasa itachukua muda kuubandua, na athari yake inaweza kukuumiza kabisa.
Cha muhimu kikujuana kwanza, na kujuana sio lazima kuingiliana kiundani, hapana, kujuana tabia,na kama ikiwezakana kuelezana nini wewe wapenda na nini mwenzako apenda.
Huyu mwenzako anaweza akawa anakutega ili ajue msimamo wako kwake, kwahiyo hapo na wewe unatakiwa uwe makini, kama utataharuki kuwa hataki mapenzi ya undani basi atagundua uzaifu wako mapema, kuwa wewe nia yako sio njema kwake.
Peaneni muda, na ikifikia muda hutaamini, mabo yatakuwa saafi kabisa. Tusipaparikie makubwa kwanza, tufanye subira, kwani subira huvua heri
Kuhusu maswala ya kumkiss na romance achana nayo kwani yaweza kukupelekea kufanya zinaa, na sote twajuwa kwamba zinaa ni haraamu. Take care and be happy always.
huyo mpenzi wako amshapata mtu mwingine ndio maana kaamua kukubadilikia au alikuwa naye kabla ya kuwa na wewe na kaamua kukuficha tu mdogo wangu umri wako bado ni mdogo sana mi nakushauri achana na hayo mambo yana muda wake kwa sasa kama ni mwanafuzi soma au kama unajishughulisha na shughuli binasi kuwa busy na kazi kwanza mambo mengine yanafuata baadaye
1.Mtafute mkae muonge mueleze mabadiliko yake kwako, hata akijidai yuko rightway jaribu kumkumbusha alivyo kuwa mwanzo na alivyobadilika sasa
2.jiulize kwani amebadilika sasa wakati mwanzo alikuwa poa pengine kunavitu anavikosa sasa kutoka kwako achiliia mbali zawadi nalega sana mahabati au havutiwi na unavyo ilipuka(pamba) maana mabinti wanavutiwa sana mwanaume nadhifu
3.jaribu kufuatilia historia yake kwani ni vema kujua background ya mwenzio HALAFU KUMBUKA KUTATUA TATIZO SIO KULIKIMBIA BALI NI KUKA CHINI WOTE 2 NA KUTAFUTA SULUHISHO.TONY
Lakin anyway jaribu kutafuta faragha uongee nae ujaribu kumweka wazi nini unapenda!!
Ikishindikana move on kwanza wewe ni kijana mdogo una mambo mengi ya kufanya tena ya msingi kuliko kuumizwa na mapenzi ambayo kwako muda wake bado!!!!!!!!!!
na kama anakupenda basi atakutaft ila ukiona kakaa kimya ujue hakupend na yuko na mwanaume mwingine,namalza kusema kuwa mwanaume mwenye roho km yako ni kumi kwa mmoja,ila pole sn kaka yng amin ipo cku na ww utapata yule unayemhitaj