Baada ya Ultrasound na kujua umri wa mimba Mpenzi kaikataa!

Habari Dinah,

Mimi ni mmoja wa waenzi wa Blog yako ila leo ndio mara ya ngu ya kwanza kukuandikia nikihitaji ushauri au msaada wa kimawazo. Nina umri wa miaka 25, na ninamshukuru Mungu kuwa nina Ujauzito ambao siku yeyote naweza kujifungua kwani tayari niko kwenye my due date.

Tatizo ni huyu baba mtoto ambae anaumri wa miaka 28. Nilipokuwa na mimba yangu changa about a month nilitokea kumchukia sana na nikawa na hasira za karibu karibu kitu kilichopelekea mimi na yeye tukatengana.

Nikaendelea kutunza mimba yangu hadi ilipofikia miezi minne then nikataka kujua mwenzangu anampango gani, hivyo nikamuuliza. Yeye akaniita tukayaongea na kukubaliana kwamba tutalea mwanetu nahivyo penzi likaanza upya.

Tukaenda kuangalia Ultrasound ikawa inasema Mimba ina miezi mitano na sio minne, tukarudia tena ikasema hivyo hivyo, yule mwanaume akaanza ku-doubt nakujiweka mbali kidogo na mimi. Kumbe sisi tulivyokuwa tunahesabu ni tofauti na wanavyohesabu wataalam.

Kumbe mimba inahesabiwa kuanzia siku ya mwisho ya Hedhi (last date of period) na sisi tulikuwa tunahesabu kuanzia siku ya kwanza ya kukutana kimwili (Date of Conception) so ikawa inatusumbua ila mimi nilikuwa na hakika kuwa yeye ni baba kwa sababu yeye ni mwanaume pekee niliyefanya nae mapenzi, sina mwanaume mwingine.

Cha kushangaza mwenzangu akaanza visa na pia nikagundua kuwa anatoka na mwanamke mwingine, nilipouliza kulikoni? akanijibu kuwa yuko serious na huyo mwenzangu, pia akadai kuwa hana uhakika kama mtoto ni wake. Kaendelea kusema kuwa hayupo tayari kuzaa kwani hajajipanga.

Niliumia sana, nikatafuta Daktari nakumuelezea na yeye akanielewesha namna ya kuhesabu tarehe kwa mara ngingine tena nikagundua kuwa mimi na baba mtoto tulikuwa tunakosea kuhesabu tarehe, basi nikamuandikia Email ndeefu baba mtoto wangu na kumueleza yote na pia kumuomba aende kwa Daktari yeyote ampe tarehe zetu za kukutana kimwili then tarehe yangu ya mwisho ya kupata hedhi ili apate ukweli. Naamini kuwa alifanya hivyo ila hakutaka kuniambia ili akwepe majukumu.

Baada ya muda nikawa namcheki ili aniambie amefikia wapi? akadai hawezi kuamua sasa mpaka mtoto azaliwe, cha kushangaza kazini kwao na kwa marafiki zake anatangaza kuwa mtoto ni wake. Nimehangaika mpaka sasa nakaribia kujifungua bila msaada wowote kutoka kwake, nilipokuwa najaribu kuomba msaada alikuwa akinijibu kijeuri au kukaa kimya.

Kanifanya niwe mpweke sana kwani kipindi cha mimba ni kigumu na kinachohitaji support ya hali ya juu. Nasikia kutoka kwa watu wengine kuwa anataka kuja kuomba amjue mtoto atakapo zaliwa, ila mimi nina hasira sana na sitaki hata kumuona.

Naomba ushauri wa kujenga na sio kubomoa wala sio matusi, huyu mtu ni wa kumsamehe kweli? na je tunahitaji mtu kama huyu kwenye maisha yetu (mimi na mtoto)?

Asanteni"

Comments

EDAMO said…
Pole sana dada kwa yaliyokukuta kutokana na maelezo yako inaonekana huyu mwanaume anakupenda.Tatizo limekuja kwenye umri wa mimba na inaonekana pia hamuaminiani na kwa kuwa hamjaoana na ianaelekea vilevile yeye anafahamu tabia yako ama mahusiano yako na wanaume wengi hivyo anaogopa kujikuta analelea mtoto wa mwanaume mwenzie.Ni wewe ndiye unayejua undani wa haya yote hivyo kabla ya kumuhukumu angalia mazingira yaliyopelekea mpaka mkaamua kwenda kupima umri wa mimba maana inaelekea kuna jambo lililopelekea mkaamua kwenda kupima.Kiukweli anayejua baba wa mtoto ni mama lakini kwa mwanaume inakuwa ni vigumu kuamini endapo mwanamke alikuwa na mahusiano na watu wengine ama anahisi tu maana inakuwa kama mpira wa kona mtaruka wengi lakini atakayepiga kichwa ni mmoja na ili ajijue ni mpaka mpira utue kichwani mwake.Kwa hiyo anapokuambia anasubiri mtoto azaliwe anamaanisha kuwa anataka apate uhakika kama mtoto ni wake au la kwa hiyo usimlaumu wa kujilaumu ni wewe kwa tabia uliyokuwa nayo ambayo inamnyima mwenzio uwezo wa kujiamini kuwa mimba ni yake maana inaelekea anajua kuwa hakuwa peke yake pamoja na kwamba wewe una uhakika ni mimba yake.Vilevile hamjaoana unabeba mimba inaelekea na wewe mambo yako yana walakini.Cha msingi akija kuomba kutambua mimba/mtoto mpokee na hata mtoto akizaliwa ni vema mkapime DNA ili kumtoa wasiwasi maana anaweza kuwa wake na asifanane nae kwa muonekano wa nje nayo italeta malumbano.Mwisho nataka ufahamu kuwa chanzo cha tatizo hili ni wewe hivyo usiishie kumlaumu mwenzio tu lakini pia ujiulize nini ulichofanya/tabia gani uiyonayo ambayo inakuondolea uaminifu kwa mpenzi wako maana wewe unalaumu kwa kuwa una uhakika ni mimba yake lakini je ni kweli kuwa ndiye mpenzi wako pekee au ndo yaleyale ya mpira wa kona?
Anonymous said…
Sasa hivyo unavyomchukia mtoto atatoka kopiraiti baba yake yani wala hatauliza jinsi watakavyofanana muombe mungu ujifungue salama.msamehe tuu mlee mtoto
Anonymous said…
inawezekana ana hali ngumu hivyo kuogopa majukumu, na ww pia inawezekana una hasira kutokana na hali uliyonayo, tafuteni msaada wa kimawazo kwa wazazi kama mnapenda muoane au kila mtu ajue msimamo na kuhusu malezi ya mtoto.
Anonymous said…
inawezekana ana hali ngumu hivyo kuogopa majukumu, na ww pia inawezekana una hasira kutokana na hali uliyonayo, tafuteni msaada wa kimawazo kwa wazazi kama mnapenda muoane au kila mtu ajue msimamo na kuhusu malezi ya mtoto.
Anonymous said…
Kwanza kabisa nakupa pole kwa yaliyokukuta na pia nakupongeza kwakuweza kustahimili hadi hapo ulipofikia ww ni mwanamke shujaa.ninachokushauri mm kama mwanamke mwenzio usiweke hasira juu yake kwani huyo ni baba mtoto wako tu na ukumbuke kuwa mtoto anahitaji malezi ya wazazi wote wawili.msamehe bure ili hata mtoto asiwe na kinyongo kwa mzazi wake.ila umweleze ukweli wa jinsi ulivyopata shida kulea mimba na hata mtoto na umwambie kuwa hutohitaji kuona makosa yakijirudia.msamehe na mjenge familia yenu.mm mwenzio nilibeba mimba na muhusika akaikubali lkn hakutaka kunihudumia hadi sasa namlea mwanangu mwenyewe na hamjui baba yake hadi leo,ana 3 yrs sasa.pamoja na yote aliyonitendea nilishamsamehe ingawa siko nae tena.
Anonymous said…
Pole sana dada!! najua ni kwa jinsi gani ujauzito unachosha!! coz naona kwa wengine. angetakiwa kujua kuwa unapokuwa mjamzito lazima hali itabadilika kwa kiasi fulani n aunaweza hata kuchukia kumuona aliyekupa mimba unakuwa una hasira mara zote. Ninavyo ona mimi huyo jamaa kwanza ni mjinga sana na pili wala hakujali!! na inonyesha kuwa hakuamini kwani kama ni mpenzi wake hawezi kusema kuwa eti ana subiri mpaka aone sura ndio a jue huo ni upuuzi shame on him!! kama akitoka kafanana na shangazi au mtu mwingine toka kwenye familia yako atajuaje!! bore hata angesema mkapime DNA lakini anasubiri aone sura!! huyo hana mapenzi ya kweli dada yangu kwangu mimi huo ndio mtazamo wangu japo unaweza ukatofautian na wengine pole dada kuwa mvumilivu katita dakika hizi za mwisho umejitahidi sana kuilea.
false said…
msamehe tuu dada dinah kama akirudi na kutubu. naamini anafanya hivyo kwa kutokujua ukweli. atakapojua ukweli na akitaka kurudi mpokee
Anonymous said…
Sasa bibi hasira hazijengi zinabomoa.kwanza baada ya kuwa mjamzito, ulipoona unamchukia ungejikaza na kujizuia, kwa njia maja ama nyingine japo ni ngumu,kumbuka kesho na keshokutwa mtoto akikwambia baba utamjibu nini. kama unamuoana anamsimamo masamehe, jifanye hamnazo kichwani, flash anza upya. Ni kwa faida yako, unajua kipindi cha ujauzito kinabadilisha tabia kupita kiasi, unaweza ukawa na tabia mbaya mno au kama mtoto, au ukawa normol tuu,Mimi nilikuwa namtukana baba wa watu, halafu baadae najilaumu, mpaka nikaona hapa nisipobadilika nitaachwa kwenye mataa nilijitahidi nikabadilika na nilimuomba msaamaha nilijizuia mno, ukitaka ndoa kama ndiyo umebeba mimba kabla ya ndoa unyekee mwanamme, hatukanwi.Kuusu kukosea tarehe hilo ni tatizo lakawaida kwa watu wengi huwa wanakosea, ndiyo maana ukienda klinic ukiwaambia tarehe ya kubeba mimba wanakupa kitu kinaitwa makisio. Sasa unaweza pitisha makisio au ukajifungua tarehe ile ile uliopewa au mtoto kuwahi.
Anonymous said…
dada pole sana kwahayo yote kwani siwewe pekeyako wako wengi mabo kama hayo yametokea maranyingi saana ,
kitu ninacho kushawishi nikuwa kama wataka jenga ndowa yako kwaza mukaee muongee muelewane vizuri ,then muende kwa daktari mukapime D.N.A a prove kwani mambo sikuhizi ni kizungu dada kama ni mtoto niwake mwambiye akulipe kwanzia mwezi alipohama nyumbani, akikubali zote hizo basi muregeeyane mimi yangu nihayo nakushawishi dada pole saana ,
GOOD LUCK FOR YOU MARRIGE, TRAYING D.N.A DADA USIOGOPE KAMA UNAVOJUWA MTOTO NIWAKE ITAKUJA APROF ,
MOMBASA KENYA .
Anonymous said…
Pole sana mdogo wangu. Mimi ni mama mwenye watoto 3 sasa. Na kabla ya hapo nilipata mtihani kama huo, nilipata mimba ya mtoto wa kwanza na baba watoto wangu, na tulikuwa tunaelewana vizuri tu. Na nisipo muona nilikuwa sina raha kabisa. Nilijifungua mtoto wa kike. Baada ya mwaka nilijikuta nina mimba nyingine, hapo ndio matatizo yalipotokea. Kwanza nilikuwa sipende kumuona kabisa, pili nikimuona nakuwa na hasira mno. Na yeye aka-take advantage hiyo akaondoka kabisa. Kuja kupeleleza nikasikia kuwa alikuwa na mawasiliano na mwanamke mwingine. Hakujali mimba wala nini. hata matumizi alikuwa haleti. Mpaka siku ya kwenda kujifungua ndio nae alitokea. Na alinisaidia kunipeleka hospitalini tu. Lakini cha ajabu kaniacha hapo hata pesa za matibabu hakutoa. Ila nashukuru Mungu nilikuwa nafanya kazi, nililipa hiyo pesa na kurudi home. Niliishi kwa shida sana na watoto wangu lakini Mungu Mkubwa. Siwezi kukwambia mengi. Ndio maana nakwambia usikate tamaa. Mimba zinasababisha mambo mengi sana. Hasa ukipa mimba kabla ya ndoa. Kwani wanaume hawajui mimba ina mambo mengi. Kwa vile hawajafundishwa hayo. Ndio maana siku hizi wanafanyiwa(Bed-Party).

(Hicho kitu nakijutua sana ktka maisha yangu, sina budi kuwafundisha watoto wangu, wasije kurudia hilo kosa.)

Lakini sasa ndio niko nae na tuna watoto watatu. Kwa vile sikupenda kuzaa huku na kule. Ndoa ni uvumilivu tu. Nimekupa hiyo stori kwa ufupi ili ujifunze kitu hapo. Kwamba wewe sio wakwanza, na usikate tamaa kama Mungu kaandika kuwa huyo ndie mme wako, atakuwa wako tu, hata iweje.

Mawazo yangu mimi ni kwamba wewe omba Mungu ujifungue salama tu. Kwani kila kitu ni Mungu ndiye anapanda. Ila usiwe na hasira ya kumlani kwani kumbuka kuwa bado una kiumbe chake tumboni. Na mtoto huyu uliyenae tumboni anaona kila kitu kinachoendelea. na kujifunza kitu kwenu. Ukikasirika sana utamuathiri huyo mtoto tumboni. Wewe sali muombe Mungu tu. Na kwenye sala zako umuombee na yeye pia. Kwani ukimlaani utalaani na kizazi chako chote. Kama Mungu amepanga binadamu hawezi kuzuia. (Ni mapito tu) Ni mitihani tu ya maisha, ndio maana ya maisha. Tukiwa wadogo haya hatuyajui, sasa ndio tunajua maisha ni nini. USIKATE TAMAA na wala usiongope. MUNGU NI MWEMA.

Pole kwa kuandika msg ndefu, na kukuchosha kusoma, ila ni kutaka kukupa mwanga fulani, ktka maisha mdogo wangu.

Ni mimi mama T
Anonymous said…
msamehe bure huyo mtoto ni wake na ni wa kiume,bado anaogopa majukumu lakini baadaye atakuwa sawa, wote tumepitia huko-msoweto
Anonymous said…
mwache aje amwone mtoto wake best
Anonymous said…
Pole sana dada mungu yupo upande wako atakusaidiatu huyo anataka kukwepa majukumu
Anna said…
My Dear,nina umri kama wako na nimeshawahi kupata tatizo kama lako but wakati mwingine mwanaume si mtu wa kueleweka wako kama upepo leo unavuma kesho hakuna mvumo.Nakushauri mpigie mungiu goti hakuna amblo linashindiokana katika dunia MUNGU ni mwaminifu anajibu na atajibu imani yako iweke mbele god is thre na huyo mwanaume achana na e kwani anaonekana haeleweki,TUNZA MIMBA YAKO MTOTOT AKIZALIWA MUNZE THEN UTAMWONA ATAHAHA
Anonymous said…
jamani....hii habari inasikitisha kwakweli ushauri wangu kama atajirudi msamehe fanya hivyo kwa ajili ya mtoto wako.kwani mtoto wako ataitaji kupata malezi ya pande zote na itamsaidia kumjengea msingi bora wa maisha...jua kusahau na kusamehe Mwenyezi Mungu ni mwema atakusaidia...ni hayo tu
Anonymous said…
mie naboreka sana na tabia za wanaume wa bongo wanavitafuta visababu visivyo na msingi kukimbia mimba kaa, Mie sikulaumu hasira wkani ujauzito unabadilisha mtu vibaya mno anayetakwia kukusupport ni huyo mwenzako. Na kingine hizi utra sound huko hamani mjue zinavyofanya kazi na mahesabu unavyosema madaktari wamesema ni kweli kabisa watu wanakosea kuhesabu. Sasa anachosema mtoto sio wake anamaana gani? mie nashidnwaga kuelewa kabisa hapohapo ameshapata kimada nje tayari for short periso mliyotengana hapo anauzuri gani? mume wa hivyo mie walaa nisingeumzia kichwa lea mwanako MUngu atakusaida akituliza kichwa na kumwa mtu mzima atarudi na usimfungulie miguu bila kujua kama mpo salama ndio mnamalizana na magonjwa tu !
Anonymous said…
Pole sana, usiseme uko mpweke, wewe si ni mjamzito ongea na mtoto wako japo angali tumboni, muimbie nyimbo, ongea naye maneo mazuri ili tabia ya baba yake isimuathiri kisaikolojia. Kitu kingine naomba ujiandae kisaikolojia, manake inonekana huyo mwanaume ameshaoona huna jinsi namna nyingine ya kuishi bila yeye ndio maana anakuumiza, nakutia moyo hutaumia tena, na hata kama unajua bila huyo mtu hutaweza kumudu maisha, muombe Mungu, atakapozaliwa mtoto akupatia njia nzuri ya kumlea. Wanaume sio watu nakwambia mdogo wangu, kama wana laana vile, na hii dunia ipo kwa sababu tu ya wanawake, wanaume wamekuwa chanzo cha machozi ya kila siku kwa wanawake, haki ya nani ipo siku watajuta. Mungu akutie nguvu mdogo wangu.