"Dinah mdogo wangu, hujambo?
Mimi ni mama wa miaka 41, niliolewa na kukaa na ndoa kama miaka 10 hivi na kupata mtoto mmoja. Mwamaume yule akaanza vituko na hata akanza kulala nje yando ayetu. Nilivyoona karaha zimezidi nilimueleza kua nitahama nyumbani kwake lakini hakuonyesha kujali na wala hakunibembeleza ili nisihame.
Siku ya siku nikatafuta nyumba, nilipofanikiwa nikamueleza kuwa nimepata nyumba na nategemea kuhama, lakini hakuniomba nibaki. Nikajua hakua ananihitaji tena basi nikahama. Baada ya mda mfupi nikatafuta shule nikaenda nje ya nchi kusoma.
Huku nyuma yeye akafunga ndoa na yule hawara yake (sisi ni Waislam). Nikadai Talaka akaitoa bila ubishi. Nikaendelea na masomo na Mungu akanisaidia nikamaliza salama na sasa nimepata PHD yangu tayari.
Hivi sasa kuna wanaume wawili mamekuja wanataka kunioa, mmoja kaishia form two na mwengine form four, shida yangu ni kua viwango vyao vya elimu ni vidogo mno na ndio kitu pekee kinanipa hofu kuingia kwenye hayo makubaliano ya ndoa na mmoja wao, ingawa nahisi bado nahitaji kuwa na mume.
Naomba mnishauri wanablog, Jee mwanaume ukimzidi elimu sana na hata kipato haiwezi kuwa tatizo ndani ya familia? ili kuwe na amani ndani ya ndoa ya hivyo mtu ufanye nini? Nahitaji kufanya maamuzi kati ya mmoja wao. Nahitaji sana kuolewa kama Mungu akinibariki. asanteni wote".

Comments
Ni vizuri zaidi watu kuwa na elimu/ufahamu unaofanana ili kufurahia maisha. Hii ni kutokana na kwamba mume na mke pamoja na mambo ya kindoa husaidiana pia katika mambo mengine ya kikazi na kijamii. ili uweze kutimiza majukumu yako ya kila siku kama Ph.D holder ni lazima uwe na mwanaume ambaye anatambua na kuelewa kile unachokifanya.
Ushauri ni ingawa ka umri kameenda kidogo, you still have a good chance of meeting Mr. right. Tuliza ball
na wewe na PHD yako itakuweje uingie kwenye mapenzi na mtu wa form two? ndoa si masuala ya ngono tu, kuna mambo mengi sana ya kushirikiana na mengi kwa kweli kwa dunia ya leo yanazingatia elimu. nashauri wote wawili uachane nao inshaallah mungu atakupa angalau mwenye digri,
Lucy
TINA-MOROGORO
na umri je isije ikawa unataka kuwa fataki wa kike?
well, vijana/wanaume wamekuwa wajanja sana haswa wakijua unakipato? fikiria mara 2 ndugu yangu, kwanza jiulize haya una watoto? kama unao au huna 41 unataka kuzaa? si utazalia ICU muhimbiliii teh teh ok then jiulize unataka mume wa nini hata kukera km wa kwanza? na nyie wamama wasomi mna matatizo yenu nyie mpaka hapo ushayaanzisha matatizo kabla ya ndoa kufungwa hilo lakutaka kujua tofauti zenu za kielimu ni tatizo pia ambalo utalijenga hata kwenye hiyo ndoa mchwara unayotaka kufunga
the thing is fanya mazoezi na kumrudia mungu wako mawazo ya ndoa za uzeen na watu wanao taka fortune zako achana nao sawa mama, hii huu ujumbe ufikirie mara 2.
Hilo gap la elimu ni kubwa mno na sijui labda uwe an angel lakini mkishaoana utakuja mdharau mmeo bila hata wewe kujua au kupenda kwa sababu vile itakavyoanza its a process which will take time and before you know it, it is already there. Na tatizo ni kwamba kuirekebisha hii ni ngumu kwa sababy hao jamaa kwenda tena shule ni.
Ingekuwa rahisi kidogo kama mwanaume ndo angekuwa na elimu kubwa kuliko mwanamke. Naturally and this is a proven scientific and pyschological finding, women tend to prefer having a man who is at least slight clever/educated/smart/intelligent whatever you may call it.
I am talking about utopia theories here, this is a fact and although most people may be in denial at the beggining, they often find it too late when they finally come to terms with its implications and eventualities.
So if its advice you need from me, please dont do it. I know now its a bit emotional because you want to get married but think aloud for the sake of your future. Hata hivyo mtu kama ulishaolewa kwa hiyo im not expecting you to be overly excited about marriage and this puts you in a very good position for you us both your mind and heart to make decisions like these rather than been driven by emotions only.
Best of luck. If you would like to get more info/advice my contact email is Marchnov2008@ymail.com
Mwanaume ambae hajasoma/hana hela, akioa mwanamke msomi/mwenye hela huwa anatumia nguvu kudifence, so atakuweka kwenye wakati mgumu sana unasafari kikazi hataelewa ataona una mambo yako. Before you engage your self plz plz AMUA MWENYEWE.
Tuwasiliane kupitia kp21p@hotmail.com kuna issue nataka kukuuliza kuhusiana na masomo nje ya nchi.
Tafuta level yako dada - apples with apples or pears with pears.
jambo la pili pole sana kwa kuchafuliwa maisha ya ndoa na mume wako hadi sasa inakupelekea kuingia mkenge na ndoa nyingine.
Tatu, kwa kiwango chako cha elimu ulichonacho sasa unahitaji kuwa makini sana.Kwa sasa hivi unatazamwa na jamii kama msomi mahiri katika uwanja fulani, hivyo jamii inategema sana kujifunza kutoka kwako.Kwa hiyo usifanye makosa hasa kama hayo yanayohitaji uangalifu na umakini zaid kuliko aidha kuwa na haja sana ya kuwa na mume.
Nne, nikija kwa hao wanaume, ninapata wasiwasi nawe kwamba tayari unavinjariwa na wanaume wawili kwa wakati mmoja.Inakuwaje kuonyesha kama unakubaliana na watu wawili at a time licha ya kwamba labda hujaingia nao kwenye mahusiano ya kimapenzi.lakini tayari inaweza kukupa dosari sana utakapokuwa umeamua kuchukua mmojawapo.
hata hivyo mimi ningekushauri kwamba tatizo la kuolewa na mtu aliyechini kielimu kuliko wewe linaweza kuwepo au kutokuwepo kwani itategemea sana jinsi wenyewe mtakavyochukuliana.Na hasa wewe ambaye ndiye kinara wa elimu unahitaji kujishusha sana na kujua namna ya kumchukulia mumewe hasa kwa mambo ya kifamilia na kinyumbani.lakini unapotoka katika lango hilo ukiwa nje ya hapo nadhan i utabaki kuwa mwenye PhD.
Jambo lingine ambalo naliona na mumewe kujiamini kuwa ninyi hamtaoana kwa sababu ya elimu bali upendo unaowaunganisha.Na najua hao wanaume wameishajua kuwa kuwa wewe ni msomi na ni wajibu wako kuwaambia bayana kuwa elimu yako imewazidi mno, na kwamba wanaionaje hiyo na watachukuliana nawe vipi?hapa nina maana wafumbuke MACHO na akili kwamba uwanja ulio nao utakuweka wewe kwenye nafasi nyingi ambazo hatimaye wanaweza kukwazwa kwazo kama hawajiamini.
Muhimu ni kujua hayo na kuweka bayana mambo yote.lakini mambo ya mume/mke na familia hayana shida mradi wewe msomi utajua namna ya kubadili mazingira kuwa sasa uko wapi na kwamba nahitaji kuwaje.
Kipato pia kitatofautiana, ingawa siwezi kusema wewe utakuwa na kipato kikubwa,maana inawezekana hao wanaume ni washika mapesa kwani kutokuwa na kisomo hakuna maana huwezi kushika nafasi zingine za kipesa.mfano wafanya biashara hivi.lakini hayo unayajua wewe zaidi wakoje hao wanaume.Penye upendo mambo mengine hujitenga mbali.
Kuna mwanaume ambaye alioa mke mwenye elimu ya kidato cha sita wakati yeye alikuwa wa darasa la saba.Baadaye huyo mwanamke aliendelea na masomo hadi nikawa naye hapa marekani kusoma PhD na tulipomaliza yeye mume wake akabaki hajiendelezi.Mke karudi bongo na kapata kazi za kimataifa.ndoa ikaanza kuteteleka kwani huyo mke kakutana na wanaume lukuki wa kufanana na kichwa chake.Kwa hiyo itategemea sana na wewe mama na wala siyo mwanaume.
Mwisho wewe kama msomi mwenzangu nakushauri uweke umakini sana katika kilichekecha hilo licha ya mashauri mbalimbali utakayoyapata hapa lakini jibu sahihi litakuwa ndani ya moyo wako.La muhimu uwe muwazi sana na hao wanaume na kaa na kila mmoja umweleze the whole situation ili ujue wanajiamini vipi katika hilo. ila nakuomba usiwatishie kwa elimu yako bali uwaeleze hali yako na wajibu wako kama msomi katika jamii.
nakutakia kila la heri dada na uitumie elimu yako vema.
mi nashauri kama unamapenzi ya dhati chagua mmoja ufunge ndoa dear.Elimu si tatizo but jaribu kuchagua yule mwenye upeo zaidi wa maisha ingawa ujasema hao wanaume wanafanya shughuli gani kwa sasa. kama hana kazi basi jaribu hata kumfungulia biashara ili nae awe nakipato chake si unajua wanaume wengi hawapendi kuonekana magolikipa? so chagua mmoja ujinafasi nae elimu si tatizo unaweza ukampata huyo mwenye elimu akakutenda tena! poleee!

Ni mtazamo tu!
Ni mimi Muti Mukavu aka MM
Nways,Mimi pia natafuta mwezna na nna PhD labda tutaendana, au wasemaje. Ni mtazamo wangu tu.
Kwa upande wangu sioni shida katika kutofautiana kielimu katika mapenzi ila tatizo ni kwamba wanaume wengi huwa na tabia ya kujishuku pindi pale mwanamke anapomzidi hasa kwa hivi vitu viwili
1. PESA
2. Elimu
Mimi binafsi na ndoa yangu ni mfano wa hayo ninayokuambia maana mim i ni graduate na mume wangu wa miaka minne sasa ni form six lever lakini amekuwa akitaka ubishani na kufuata atakalo simply nikijibishana naye anaona namdharau, imefikia mpka ameanza chuo kwa kutaka naye apate degree. pia mimi namzidi kimshahara kiasi cha kwamba nikifanya mambo yangu anaona natumia hela vibaya na anataka nimpe yeye iliaweze kupanga na anavyodai mipango ya kimaendeleo,ninachoweza kukushauri ni kumchunguza huyo umpendaye na muweze kuwekana wazi juu ya tofauti zenu na ni kwajinsi gani yeye anazipokea. Mapenzi hayachagui mamii ila inabidi uwe mwangalifu usije teswa nayo sababu tu yakuwa desparate take ur tym na uolewe na mwaume umpendsaye no matter what naumweleze mpenzi wako awe huru juu yako kama mkewe na yeye kama mume mambo ya elimu,vyeo na pesa yabaki nje ya mahusiano yenu yasiwakwaze, nakutakia kila la heri, E
dada yangu kwanza napenda kukwambia kuwa mapenzi ni maua huota popote kama ulivyo amua kuwapenda hao mbwana wawili pamoja na elimu zao kuto fikia kiwango ulicho nacho wewe lakini moyo umependa, nakwambia hayo kwa sababu nataka uelewe kuwa kwa hali yoyote uwe na elimu usiwe na elimu,uwe tajiri au masikini utapenda tu, hivyo basi nakushauri kati yahao mabwana wa wili tafuta mmoja ambae unampenda zaidi funga nae ndoa usijali mambo ya elimu au kazi aliyo nayo kwa ni baadae kama una uwezo unaweza kumshauri ajiendeleze sio mbaya ila kikubwa ni upendo na maelewano ndani ya nyumba.
nacho kuomba kama utakubali kuolewa nae akiwa na elimu hiyo ndogo tafadhali usije ukamnyanyasa maana sisi wanawake sijui tuko vipi wengi wetu wakijiona tu wanauwezo kumzidi mumewe basi manyanyaso moja kwa moja mpaka mwanaume ananza kutafuta mwanawake nje ili kuepuka kero za ndani. nakutakia uchaguzi mwema na maisha mema pia katika ndoa mpya ijayo.
Mohdy
Kwanza hongera kwa kuwa muwazi.
Nitakuwa mfupi ( brief, ha ha ha ) kuwa hapo ni kitendawili. Better safe than sorry my dear.
Gap ni kubwa na kwa vile ni ndoa ya pili, vikishindikana, vitakutia doa na watu watadhani ni wewe una shida.
Yamenikuta so naongelea kwa uzoefu.
Kwa vile una watoto, kaa kimya usubirie wakati wa Mungu akupatie mtu 'mtayefanana ' naye.
That's too wide a gap na ina translate a lot katika maongeo, mafikira , maamuzi na perceptions.
Ndimi Mama Kiduku

kwamjibu wa swali lako tayari inaonyesha kuwa kuna walakini ndani ya moyo wako kinachokusuma nidesire to have sex na hapo upendo haupo.
inaonyesha hao wanaume hawakufai yawezeka hata wao wanalitambua hilo ila wanataka kukuchuna tu
it my comment, changanya na za kwako
Nashauri ni vyema ukamchagua Mume ambaye amekuzidi Umri ingawa si kigezo kikubwa sana lakini katika saikolijia ya maisha tunatambua kuwa UKUBWA NI BUSARA NA HEKIMA.
"EVERY WOMEN NEED A MEN" kwani utafiti wa kisayansi ulifanywa na WANABAIOLOJIA umebaini kuwa UPWEKE WA KIMAPENZI NI SUMU KWA WANAWAKE WALIO WENGI, fanya hima MAMA Mpate Mwenzio NA HATIMAYE UIREJESHE FURAHA YAKO YA MOYO.
Thanks.