Mume kanitelekeza kisa Ndugu zake, Je nina ndoa au sina Ndoa?-Ushauri

"Pole na kazi Dada Dinah,
Mimi ni Mama wa watoto wawili, nilifunga ndoa 2004. Kwenye ndoa yetu ikatokea upande wa mume wangu hawajanikubali sana. Siku zilivyosonga mbele kukawa hakuna maelewano kabisa nyumbani kati yangu na mume wangu.

Mwaka 2008 December, Mume wangu akahama nyumbani na aliniachia mtoto ambae kwa wakati huo alikuwa bado ananyonya, nilijaribu sana kumbembeleza arudi nyumbani lakini sikufanikiwa, kwa sasa anaishi Arusha.

Mwaka 2009 July mtoto wetu mdogo aliumwa sana kiasi kwamba nilichanganyikiwa, nilimueleza baba yake ambae ni mume wangu alienikimbia lakini hakuja kabisa kumuona mtoto. Toka 2008 alivyoondoka mpaka leo amesha kuja kututembelea kama mara mbili tu kwa madai kuwa Dar na Arusha ni mbali sana, hivyo hawezi kuja mara kwa mara kwani huwa anachoka.

Mara chache anatuma zawadi kidogo za watoto. Na toka aondoke ameshatuma kama laki tatu hivi na watoto wote wanasoma sasa, hajui naishije na watoto wanakula nini, yaani kwa kifupi hana habari na watoto wake.

Sasa dada naomba ushauri wako, unaona hapo kuna ndoa tena?
Mimi ninafikiria nitafute makazi yangu nihamae na watoto wangu kwani ninapokaa ni kwake yaani ni nyumba yake.

Kama watoto wakimkumbuka sana baba yao huwa nawadanganya, ila huyu mkubwa (5yrs) naona ameanza kuelewa kwani akiniuliza huwa namwabia hali halisi namuona kama ananza kuelewa na anapata uchungu sana.

In short naona kuliko niendelee kuumia moyo wangu ni better ni give up, nianze maisha mapya, nifanye juu chini nisomeshe hawa watoto na nijihesabu kuwa ni single parent.
Unanishaurije?"

Dinah anasema:Pole sana kwa yote unayokabiliana nayo, inasikitisha kuwa mumeo amefuata matakwa ya wazazi wake na hivyo kukuoa na kisha kukuacha "solemba". Kwasababu tayari mmekwisha funga ndoa na bado of course mko kwenye ndoa kwa vile hakuna Talaka iliyotolewa na kwa mujibu wa Imani za Dini, wewe kama mkewe na mama wa watoto wake unahaki zote za kubaki kwenye nyumba hiyo. Hiyo nyumba ni yenu na sio yake.

Kutokana na maelezo yako nadhani kinachomshinda kuja kuwaona watoto mara kwa mara ni mwanamke/mke mwingine anaeishi nae huko, Arusha na Dar sio mbali kiasi kwamba mtu ukatembee mara moja kila baada ya miaka miwili! Lazima kuna kitu kinamzuia kuja huko mara kwa mara bila "sababu ya msingi" hasa kama mwanamke alienae hajui kama jamaa alioa/anawatoto.

Kibinaadamu Dada mpaka sasa huna ndoa, ni kama vile jamaa amekuweka spea tairi kwamba yakimshindwa huko Arusha basi wewe upo hapo kwa ajili yake (wapo wanaume wengi tu wa Kitanzania wanafanya hivi).



Huyo mwanaume kama anajali maisha mema ya watoto wake hakika hawezi kukufukuza kwenye nyumba hiyo, lakini kwa vile sio muaminifu (amekukimbia) hivyo kumuamini kwenye masuala mengine sio kitu rahisi. Inawezekana kabisa siku moja akaamua kuiuza nyumba yenu alafu wewe na watoto kuhamishwa bila kupenda.

Sasa ili kujiondolea hofu na kuwa na uhakika wa mahali pa kuishi na watoto wako ni vema ukawahi kumtaliki mumeo (mpe Talaka), kisheria ndani ya Tanzania una haki hiyo. Ni vema ukienda Ustawi wa Jamii lakini tatizo la hawa jamaa wanakalia kesi za watu kwa muda mrefu sana. Pia TAMWA inawanasheria wazuri ila wanazile za "njoo kesho" nyingi na hivyo kucheleweza mambo.

Mimi kama Dinah nakutokana na uzoefu wangu na "Mahakama" ningekushauri uende moja kwa moja Mahakama ya Wilaya ya hapo unapoishi na kuomba kumuona Hakimu anaeshughulikia masuala ya Familia na ndoa. Ukipata nafasi ya kumuona (inategemea how busy she/he is) then muelezee matatizo yako ya kindo tangu mwanzo, maisha yalivyo hivi sasa na nia yako ya kutaka kumtaliki mumeo.

Mumeo anaandikiwa barua ya kuitwa Mahakamani ili Hakimu aweze kusikiliza upande wa pili na kupata ushahidi au sababu zilizomfanya jamaa akukimbie, baada ya hapo unaweza ukapewa nafasi ya kueleza nia yako ya kumtaliki mumeo au Hakimu anaweza kuisema moja kwa moja (kwa vile tayari umekwisha mueleza nia yako).

Kesi itaendeshwa kwa muda wa kati ya wiki 2 mpaka mwezi mmoja, inategemea kama mumeo atakuja Mahakamani na kuwa mbishi kuchukua/kubali Talaka kwa sababu zake azijuazo yeye au atataka kurudiana na wewe n.k.

Kutokana na urefu/umri wa ndoa kisheria mali zinagawanywa kwa manufaa yenu wote wawili na watoto mliozaa, lakini wewe utapendelewa zaidi kwa vile umekuwa ukilea watoto peke yako kwa muda wa miaka miwili hivyo ni wazi nyumba itakuwa yako pamoja na mali nyingine zinazowahusu ninyi kama wanandoa tangu 2004-2010.

Vilevile mumeo atalazimika kisheria (Mahakama itaamua) kuwa anatoa kiasi fulani cha pesa kila mwezi kwa ajili ya matunzo na elimu ya watoto, hata kama wewe unuwezo huo bado kisheria atalazimika kuchagia unless otherwise wewe mwenyewe ukatae.


Ikitokea umefanikiwa kuachana na mumeo kisheria, hakikisha hujengi chuki na mpe nafasi ya kuwaona watoto wake au watoto kumuona baba yako kila anapopata nafasi ya kufanya hivyo. Hakikisha watoto wanakuwa na uhusiano mzuri na baba yako.

Kumbuka tofauti zenu na chuki ya wakwe zako haziwahusu watoto waliozaliwa. Ikitokea watoto wanataka kujua kwanini baba hakai hapo nyumbani unaweza kuwaambia tu kuwa anafanya kazi mbali na siku akipata likizo atakuja kuwaona. Kamwe usiwaambie watoto kuwa baba yenu hawaenzi ndio maana hayupo hapa.....hakikisha unajenga uhusiano mzuri kati ya baba na watoto hata kama baba huyo anakuja kuwaona mara moja kila baada ya mwaka.

Talaka sio suluhisho na siku zote wanaoteseka ni watoto, lakini kutokana na unayokabiliana nayo Talaka itasaidia wewe kuwa huru kiakili na kuendelea na maisha yako kama mwanamke na vilevile kuwa na mahali penye uhakika ili kukuza watoto wenu.

Hongera kwa kuonyesha msimamo wako kama mwanamke, hongera kwa kusimama imara kwa watoto wako kama mama.

Nakutakia kila la kheri katika maisha yako na watoto wako.

Comments

Anonymous said…
Dada move on haraka hakuna ndoa hapo tena mshukuru mungu wako kwani lazma kuna jambo kakuepushia. anza maisha mapya songa mbele, kuhusu hiyo nyumba yake kama hakubugudhi usiondoke hakikisha unajenga kwako kwa siri asijue so badala ya kulipa kodi tafuta kiwanja uanze ujenzi ili ukianza maisha yako isikuwie vigumu. pili shughulikia talaka haraka, imagine ukipata mtu anayekupenda utafanyaje?
Anonymous said…
hapo umenena mpenzi wangu somesha watoto wako kwa nafasi yako muache na maisha yake unajua yeye alipaswa kujenga msimamo hatakama ndugu zake hawakukubali angefiria watoto tuu iko siku atakukumbuka kama sio kwa jua ni mvuampenzi wangu na watoto wakikua waeleza ukweli siku awakute ni maofisa sehemu fulani ndiyo atalijua jiji wakati huo kafulia
Anonymous said…
kama unayoeleza ni sahihi huyo mume hakupendi ,na kama umeamua kujitoa nenda kwa wanasheria au ofisi za ustawi wa jamii wakupe mwongozo
Anonymous said…
kama unayoeleza ni sahihi huyo mume hakupendi ,na kama umeamua kujitoa nenda kwa wanasheria au ofisi za ustawi wa jamii wakupe mwongozo
Anonymous said…
pole sana dada kwa yaliyokukuta,mimi nakushauri umfuate huyo mumeo huko aliko ukajuwe kulikoni! inawezekana amepata nyumba ndogo! nakama hakuhitaji akupe taraka yako dada magonjwa mengi! na kama anakupenda asingesikiliza maneno ya ndugu! hicho ni kisingizio tu,huyo kapata mwingine arushaaaaaaa!
Anonymous said…
Hai dada pole kwayote mpenzi,kumbe tuko wengi wenye matatizo kama haya jamani,ila hujasema mlifunga ndoa gani kama yakiislam sawaa lkn kama ya kikiristo ni ngumu.hapa nilipo ninamawazo nashinwa hata kuchangia nasi tunaachana nilifunga ndoa 2004 pole mwenzangu acha tu
Anonymous said…
POLE NA MATATIZO IAL MIMI NAKUSHAURI KWENYE HIYO NYUMBA USIHAME....KWANZA HIYO NYUMBA KUMBUKA UNAISHI BUE HIYO ITAKUSAIDIA WEWE KUPUNGUZA UKALI WA MAISHA SASA KAMA WATAKA UZIDI KUJIONA UNA MATATIZO MAGUMU HAMA HALAFU UANZE KULIPA KODI ZA NYUMBA, HUKU WATAFUTA CHAKULA HUKU UNATAFUTA ADA ZA WATOTO, HUKU BADO HUJAJUA WATOTO UTAWATIBU VIPI...UKIHAMA UTAFANYA KOSA KUBWA ANAWEZA AKAJA AKAWEKA MWANAMKE MWENGINE UKAWA UMEPOTEZA HAKI ZAKO KUMBUKA HIYO NYUMBA HATA KAMA AMEJENGA KWA PESA YAKE ILA NI MALI YA WATOTO WAKO...WEWE USHAPOTEZA PENZI KWAKE SASA UANTAKA POTEZA MALI ZA WATOTO!!

KWENYE HIYO NYUMBA USITOKE WEWE ENDELEA NA MAISHA YAKO KWANI MAISHA HAYAWEZI KUENDELEA MPAKA UHAME HAPO KWENYE NYUMBA?// LABDA KAMA UNA MPANGO WA KWENDA KUTAFUTA MWANAUME MWENGINE HAPO NTAKUELEWA....


KIUFUPI HUYO HAKUHITAJI..ENDELEA NA MAISHA YAKO NA KWENYE NYUMBA USITOKE...USITAKE KUWAPATISHA TABU WATOTO UNA UHAKIKA UTAYAMUDU MAJUKUMU YOTE??
Anonymous said…
Pole sana dada yangu,ila hiyo ni mitihani tu!Mimi nakushauri anza upya,kuanza upya c ujinga my dear!Kwanza nakushauri wacliana nae akueleze msimamo wake juu ya ndoa yenu,watoto na wewe mwenyewe,akishakupa msimamo wake wewe usiache kuanza upya,wewe ni binadamu una haki ya kuishi kwa furaha na mapenzi pia!Hiyo nyumba kama ni yake tafuta mwanasheria atakueleza jinsi ya kufanya ili iwe mali ya watoto iweze kuwasaidia hapo baadae!
Anonymous said…
Du! Pole sana dadangu. unataka kugive up kuhamia kwako kwa nini? kwani huyo mumeo ni mume wa ndoa au alikuwa ni hawara tu? kama ni mume wako halali wa ndoa kwa nini uhame na kuhamisha watoto kwenye nyumba yako na yao kihalali? utakuwa unakosea sana ndugu yangu. una haki zote na mali mlizochuma pamoja ukiwa kama mke wake. isitoshe amekuwa mstaarabu kidogo hajakutoa kwenye hiyo nyumba alichofanya ni yeye kuhama na kukuacha uwe huru. ninachoweza kukushauri ni kuendelea kukaa hapo nyumbani kwako. sana sana fanya bidii ya kuhakikisha watoto wako wanaendelea vema, kuliko kuanza kuwazururisha kwenye nyumba za kupanga zenye kila karaha. funguka akili na utambue haya ninayokuambia. Fikiria zaidi maisha ya wanao kwa sasa kuliko kukaa na kuumia kwa ajili ya mumeo. Labda kuna siku Mungu atamrudisha aje muendelee kulea watoto wenu. uamuzi hapo utakuwa sasa ni wa kwako kumpa tena nafasi au vipi.

Claire
Anonymous said…
pole mpenzi, huyo ni shetani tu anataka kuujeruhi moyo wako,mimi ushauri wangunyumba usihame wala usifikirie kuhama maana ungekuwa mwenyewe ungekuwa na right za kuhama lakini hiyo ni nyumba ya watoto, ukihama utamfurahisha tu, ninachokushauri ni kwenda kanisani sali sana atarudi tu huyo ni shetani kamfunga moyo wake na mumeo akikuona anaona kaona kibogoyo nenda kanisani wakakuombee wakakutoe hicho kitu ulichowekewa ambacho kimefanya mumeo akuchukie, kama asingekupenda asingekuoa na kukuzalisha watoto wawili usichoke kuomba Mungu utaona majibu yake.
Anonymous said…
pole sana dada hapo hakuna ndoa tena kama unao uwezo wa kupanga nyumba hama wala msionane pengine itakupunguzia machungu huyo bwana inawezaikawa ana mwanamke anaishi nae sasa tabu ya nini kukaa na mtu asiyekupenda anaweza hata kukudhuru haikuwa ridhiki yako muombe mnyazi mungu akupe nguvu na utaweza tu sio kila kitu lazima mwanaume hata sisi kina mama tunaweza
Anonymous said…
Pole sana dada kwa yaliyokupata.Mimi naweza kuwa t... Pole sana dada kwa yaliyokupata.Mimi naweza kuwa tofauti na wachangiaji wengine naona ungewezesha wanablog wakupe ushauri utakaokusaidia na utaoendana na tatizo lako.Umesema tangu muoane ndugu wa mume wameonesha kutokukubali je hoja yao ni nini katika kukuchukia maana haiwezekani usiwe unajua hawakukubali kwa sababu zipi-labda tabia mwenendo na matendo yako yamechangia.Vilevile mumeo alipokwenda Arusha alitoroka au alikwenda kikazi na je alikuaga maana kama ulikuwa na maelewano mazuri naye hata kama ndugu zake wanakuchukia angekuwa upande wako.Tafadhali tueleze kwa mapana chanzo cha ugomvi huu ili tuweze kukushauri ipasavyo.