Bado nampenda Mume wangu lakini Dini imetutenganisha-Ushauri!

"Dinah mdogo wangu hujambo? Nawasalimia wanaGlob wote, nami naleta shida yangu ili nisikie wanajamii wa Dinahicious itanishaurije. Mimi ni mmama mkubwa tu, ni Muislamu na niliolewa na Bwana ambae alikuwa Mkristo nikiwa na umri wa miaka 23. Alikuwa ni mwanaume wangu wa kwanza tukiwa wanafunzi wa Chuo.

Uhusiano wetu uliendelea vizuri na baadae tukapata mtoto mmoja, Mpenzi wangu alikubali kufunga ndoa ya udanganyifu ya Kiislamu ili wazazi wangu wamkubali hivyo alislimishwa na tukafunga ndoa, baada ya siku tatu akaungama na kurudi Kundini.

Tuliendelea kuwa pamoja kwa miaka kadhaa kama mume na mke na tulipofikisha miaka mitano alidai tuende tukabariki ndoa yetu Kanisani lakini mimi sikuwa tayari kwa hilo hivyo akatafuta mwanamke mwingine kama nyumba ndogo na akasema kuwa anaoa.

Mimi sikumkatalia lakini nilimuambia kuwa nitaondoka nyumbani kwake, hapo tayari alikuwa ameanza ratiba ya kulala huko mara tatu kwa wiki, iliniuma sana Dinah. Lakini nilivumilia hali hiyo kama mwaka na kila nikimuambia kuwa naondoka kwake wala hakuwa akionyesha kujali yaani hata kusema usiondoke hasemi.

Ilipofika siku maudhi yamezidi, nikatafuta nyumba nikapanga, kabla sijahamia nikamueleza kuw animepta nyumba na nitaondoka nyumbani kwake kama kawaida hakupinga wala kuonyesha kujali basi mimi nikaondoka na kuanza maisha mapya huko nilikopanga. Baada ya muda mfupi nikaenda masomoni na niliporudi nilikuta tayari amefunga ndoa ya Kanisani na yule Mdada.

Mimi na yeye hatuna maswasiliano ya mara kwa mara lakini tunapowasiliana huwa anadai kuwa hana amani na inamuuma sana na itaendelea kumuuma mpaka anaingia kaburini. Kuna wakati maneno yake hunigusa sana hasa ukizingatia bado nina hisia nae.

Kwa sasa sijaolewa lakini akanibariki kwani kuna watu wawili-watatu wamejitokeza kutaka kunioa lakini mimi bado sijaamua kuolewa tena. Moyoni nahisi ingekuwa inawezekana kumrudisha Mume wangu ili tumkuze kijana wetu basi ningefanya hivyo, Ila nitakuwa tayari kama atakubali kurudi kuwa Muislam.

Da Dinah nimeileta hii ili nisikie ushauri wako pamoja na wachangiaji wengine. Je nimshauri aingie Uislam ili turudiane kwani nahisi bado nampenda au nikaze tu Moyo ili niolewe na mmoja kati ya hao wengine wanaotaka kunioa?

Naomba ushauri wenu tafadhali, natanguliza shukrani."

Dinah anasema: Mimi sijambo kabisa mdada, vipi wewe. Asante sana kwa ushirikiano wako. Dini ni Imani au mfumo wa maisha hapa Duniani ambao tunaufuata baada ya kukuta wazazi wetu wanauabudu lakini ukweli unabaki palepale kuwa wewe unapozaliwa na wazazi wenye kuamini Imani fulani haina maana na wewe ukiwa mtu mzima mwenye uwezo wa kufanya maamuzi juu ya maisha yako bila kutegemea wazazi uendelee kuiamini Imani hiyo.

Mfumo huu wa maisha unatusaidia sisi kuwa karibu zaidi na Mungu ambae wote tunaamini kuwa anatulinda, kutusaidia na kutuepusha na mabaya yote hapa chini ya Jua (Duniani), lakini linapokuja suala la mapenzi Dini huwa haina nafasi kwa sababu hujui ni mtu gani utamdondokea kimapenzi na yeye akakupenda jinsi umpendavyo!

Itakuwa ni mara chache sana kukutana na mwanaume mwenye Imani kama yako na mkapendana kwa dhati unless mnajumuika pamoja kwenye shughuli za kiDini au wazazi wake na wake wawaunganishe AGAIN itakuwa bahati sana kwako wewe kumpenda huyo uliyetafutiwa ili kufunga ndoa.

Sina uhakika na jinsi ndoa za Kiislamu zinavyofuatiliwa ili kuidhinisha "Talaka" ukiachilia ile ya "kisheria za kijadi" ambayo wenza hujulikana wameachana ikiwa hawajakutana kimili kwa muda fulani.

Nina uhakika na ndoa ya Kikristo kuwa haina Talaka, japokuwa siku hizi kuna sheria inayomruhusu mtu yeyote kumtakili mwenza wake Kisheria ili kuepuka usumbufu na unyanyasaji ambao unatokana na umilikishi (mume wangu, mke wangu) vinginevyo ndoa hiyo itaendelea kujulikana kuwa ni wanadoa waliotangana na kila mmoja hatoruhusiwa kufunga ndoa tena mpaka mweza wake afariki Dunia huko aliko.

Ndoa ya Kiislam uliyofunga haikuwa halali kwani wote mlikuwa mnajua kuwa mnafanya hivyo ili wazazi wako wamkubali, lakini kama kuna uthibitisho kuwa mlifunga ndoa basi hata ndoa yake aliyofunga Kanisani ni batili kitu ambacho kinaweza kurahisisha mambo kama wote wawili mtakubaliana kuhusiana na Imani zenu za Dini.

Kutokana na maelezo yako inaonyesha kuwa Imani zenu za Dini ni muhimu zaidi kuliko uhusiano wenu wa kimapenzi na kama ukweli ndio huo basi itakuwa ngumu sana kwa ninyi wawili kuishi pamoja kwani wote hamtaki kubadilisha Mfumo wa maisha yenu kiimani.

Natambua unampenda mzazi mwenzio na ofcoz anakuwa wazi sana kwako na comfortable kuongea na wewe mambo mengi kwa vile mmekuwa pamoja kwa muda mrefu na anatambua kabisa kuwa wewe ni mwanamke unaemuelewa vizuri kuliko Mkewe wa kanisani. Pia inawezekana anataka kuwa na uhusiano mzuri na wewe kwa faida ya mtoto wenu.

Kama kweli unampenda na unataka kurudiana nae basi utafanya lolote ili kurudiana na "mumeo", tunapozungumzia kufanya lolote ni pamoja na kubadili Dini na kufuata Imani anayoiamini yeye.

Wapenzi huwa radhi kubadili Dini, wengine hata Kukana wazazi wao kwa ajili ya wapenzi wao, sasa kama kweli wewe unampenda Jamaa na una uhakika anakupenda kwanini usifanye atakacho ili kuwa nae?

Ndoa yake ya Kanisani sio batili kama unauthibitisho wa aina yeyote kama vile cheti cha ndoa n.k...hivyo isikutishe kabisa. Huyo mwanamke aliefunga nae ndoa ameingilia ndoa yako na hakika huyo ni mume wako wa kudumu kama utaamua kuafiki na kubariki ndoa hiyo Kanisani.

Lakini kama Dini yako ni muhimu zaidi na labda hutaki kuwaudhi wazazi wako ambao mimi naamini kabisa kuwa hawahusiki na maisha yako ya kimapenzi basi kubali kuolewa na hao wanaume wengine waliojitokeza.

Natumaini sehemu ya maelezo yangu na michango ya watu wengine yamesaidia ktk kufanya uamuzi wa busara.

Kila la kheri!

Comments

H said…
Kama ndoa ni ya kiislam mmoja akitoka tu tu ktk Uislam basi na ndoa hakuna, kwa hiyo ulikuwa unazini kwa muda wote huo!!! wewe ni mtu mzima na akili zako jiulize itakufaa nini kama utaipata dunia yote na kuipoteza akhera yako???

Huyo wa kubadilibadili dini ni mdanganyifu ameshakudanganya vya kutosha wala usibabaike naye tena.

Ni upumbavu ulioje kununua Jehanamu kwa gharama za eti "mapenzi" na kuikosa Pepo.

Sina maana ukimuacha ndio utaingia peponi la, kuna mengine mengi tu ya kheri lazima uyafanye kama muislamu yeyote ikiwa ni pamoja na kuswali Swala tano kila siku lakini nina uhakika kwa wewe kuendelea KUZINI haina mjadala lazima utaishia Jehanamu (Mwenyezimungu apishie mbali).

Sasa kazi kwako Kheri na Shari zote ziko wazi ni wewe kuchagua unafuata nini, ushauri wangu ni wewe ufuate KHERI na uachane na Shari kwa kisingizio cha mapenzi.
Anonymous said…
unatakiwa uwe na msimamo dada,huyo mumeo anaonekana hana msimamo,unatakiwa uangalie mbele sasa hivi,kama kuna aliyejotokeza anania ya kukuoa olewa tu,usikae unamfikiria mtu mmoja ambae tayari ana ndoa ya kanisani na mwanamke mwingine. ukae ukijua huyo ameshaoa,.....mom
Anonymous said…
hebu nikuulize swali kwanza!
ulikubali ajifanyishe muislamu lakini wewe hauko tayari kujifanyisha mkiristo?
kweli unampenda mumeo wewe au umemzoea tuu? na unashindwa kuachana nae kwasababu unaogopa maneno ya watu?
ulivokubali ulitegemea mwisho wake ungekuaje?

acha ukoloni kwa mungu ni kulekule hata uwe mpagani mfate mumeo kanisani kama alivokufata msikitini maana nyie mnavoishi n full komed sasa tatizo nin i mbona yanakushinda katikati?
Anonymous said…
dada pole kwa mkasa ulikokuta.. bt kwanini hamkufunga ndoa ya serikali tuu mkaendelea na life yenu km kawaida, mie kuna watu nawaona wanaishi miaka mingi tuu na wameoana bomani kila mtu anadini yake and there doing just fine.
now is too late kuishi nae huyo kwani anandoa ya kanisani tayari, ushauri wangu ni tafuta mtu mwingine uolewe tuu..is not that bad..
mie nikimpenda mtu bwana hakuna cha dini,kabila wala rangi kitakachonizuia kuwa nae as long as tunapendana kweli na kuheshimiana..
all the best in putting ur life back together.lily.
Anonymous said…
Pole kwa kupoteza mume wako kwa sababu ya dini. Kama unavyoona wewe vigumu kuondoka katika dini yako ndivyo hivyo hivyo ilivyo vigumu kwake kuondoka katika dini yake. ushauri endelea na maisha yako kwani kikristo ndoa ni moja tuuuuuuuuuu na ameshaoa. kwa hiyo mkubali wa dini yako mtaishi kwa amani tu kama utakubali kumwondoa huyo baba wa mwanao rohoni
Anonymous said…
Bibie pole sana, ila nikuambie jibu mbona unalo wewe mwenyewe, alidiriki kuwadanganya watu ili akuoe na akarudi kwenye dini yake ukiwa unaona kwa macho yako sio? akatafuta nyumba ndogo hadi akaoa kwa ajili ya mgogoro huohuo wa dini, na mtoto mlikuwa mmeshazaa unafikiri leo hii huyohuyo mwanaume atakubali kumwacha mke wa ndoa ya kanisani ili aje arudie uislmu alioukana kweli! HAIHEZEKANI ENDELEA NA MAISHA YAKO BWANA HANA MPANGO NA WEWE TENA LABDA KWA KUIBA LAKINI MKE NA MUME NI IMPOSSIBLE!!!!!!
Anonymous said…
Weeeeeee dada,

kwanza pole sana kuingia kwenye ndoa ya udanganyifu.Mimi ni mkristo,kwa kweli ni nadra sana mkristo kuoa mwislamu kwa mapenzi ya dhati kuingia uislamu.Hii hutokea kama ilivyotokea kwako kwamba ili akupate kwa kuwa alikupenda sana ilibidi aigize kuwa mwislamu.Mtaka cha uvubguni shartii ainame akikipata si atainuka tena?

Nakushauri kama wewe pia unampenda kubali kuingia Ukristo ndipo mambo yataiva.Sahau kabisa kwamba mwanaume wa Kikristo ataingia uislamu.Nimeona kwa waislamu wanawake wakingia ukristo kwa sababu ya ndoa,lakini wanaume wanaishia njiani baada ya kuwin tu basi.

Mimi nakushauri tu kama ameoa mke mkristo basi wewe chukua zako.hapo huna ndoa dada yangu,tena mlifunga huko basi imekwisha hiyo.Ikibidi kama unamkomalia basi kubali kubaki mwislamu na yeye mkristo na uwe mkewenza inatosha.Au la basi chukua maisha yako kivingine na wewe upate mume wako kama ulivyosema kuwa kuna majamaa wanakuwangia basi mega mmojawapo anayekupa machale ya kutosha.

Lakini la muhimu zaidi ni kuanza maisha mapya sahau huyo mwanaume kwa sababu kwanza alikudanganya kubadili dini akawa mwislamu wa siku tatu then akageukia alikotoka.Tafuta mwislamu mwenzako kama yupo kati ya hao wawili unaozengeana nao.

Nakutakia kila la heri ufanikiwe kutatua tatizo hilo kwani unaonyesha wewe ni mama mwenye busara sana.
Anonymous said…
Achana na huyo mwanaume ataendelea kukutomba tu na kukupotezea muda kama uliopoteza naye.

Kwanza mdanganyifu wa nini sasa na ameoa mke mwingine?

Hizo hisia umesema unazo juu yake kwani wengine hawana hizo tools zikakuondolea manyege hayo?

Usirudie kosa ulilofanya mwanzo utajuta tena.Pata mmojawapo wa hao wawili umesema wanakunyemelea.Mwanaume anayebadili dini kwa sababu ya kumtaka mwanamke si wa kweli hata siku moja.Atarudi alikotoka tu.
sada said…
Pole sana dada yangu kwa msiba uliokupata. Kwa kweli inaonyesha ya kuwa huyo jamaa hana mapenzi tena na wewe. Ila kikubwa dada yangu muombe mungu atakusaidia kupata mbadala wake kwani hata mimi ilikuwa hivyo hivyo lakini hatukufikia kwenye hatua ya kuoana tuliishia njiani kwani mara ya kwanza nilimkataa kukutana naye kimwili kwa sababu alikuwa dini tofauti na mimi na sikupenda kufanya mapenzi kabla sijaolewa na ukifikiria nilikuwa bikira. Lakini yeye kwa kujua hivyo akanirubuni kuwa nyuko tayari kuwa muislamu na tutaoana. Cha hajabu baada ya kunitoa bikira yangu tu, mambo yalibadilika akasema kuwa wazazi wake wamemkataza kubadili dini hivyo kuoana nami haitawezekana. Nikabaki ninaugulia sina la kufanya na kumwomba mungu anipatie mume wa kweli. Dua zangu zilisikika na nikampata mume huyu niliye naye sasa.
Hivyo Dada yangu wanaume walaghai haina hii wako wengi sana inabidi tuwe makini ili yasije kutokea kwa ndugu zetu wa karibu. Muombe mungu utamsahau huyo jamaa, na kati ya hao waliojitokeza kuwa tayari chagua mmoja wapo muoane ila kuwa makini isiwe ikawa kama mwanzo kwani waswahili walisema aliyeumwa na nyoka akiona ung'ongo hushtuka.
Anonymous said…
atakuumiza sana baadae kwani hakuwa na sababu ya kukuacha, kukulalia nje na kuslim kiuongo,kama unamaisha yako na una mwingine endelea ila umchunguze sana2 kabla ya kukubali kuolewa
Anonymous said…
Kwanza he is a married man already so sijui hapo unatafuta nini tena. Second Kwani uliyokuwa nae hukufikiria wewe kubadilisha dini kuwa mkristo? Na kama haiwezekani ama hutaki kwann unataka kumlazimishe mwenzio kubadilisha when wewe haupo willing kubadilisha japokuwa unasema unampenda? Vitu kama hivyo havilazimishwi ni mtu mwenywe ndio anaweza kuchagua kubadilika au la. Waangalie hao wengine huwezi jua kati ya hao kuna mmoja wa dini yako au amabaye yuko willing kubadilisha kuwa nawe. cku njema
Anonymous said…
Dada inaonekana wazi kuwa umemsahau mola wako utawezeje kufanga ndoa na mtu ambae muko tofauti kidini na ulijua kuwa anaingia kwenye uislamu kwa unafiki ni hata ukimshawishi ingie tena kwenye uislamu itakuwa km mara ya mwanzo sio mkweli huyo kwako ni bora uachane nae na uolewe na mtu ambae dini zinaendana ni hayo tu.
Anonymous said…
Dada inaonekana wazi kuwa umemsahau mola wako utawezeje kufanga ndoa na mtu ambae muko tofauti kidini na ulijua kuwa anaingia kwenye uislamu kwa unafiki ni hata ukimshawishi ingie tena kwenye uislamu itakuwa km mara ya mwanzo sio mkweli huyo kwako ni bora uachane nae na uolewe na mtu ambae dini zinaendana ni hayo tu.
mkewangu said…
Mimi kidogo umenichanganya uliposema je nimrudishe kwenye uislam ili tuoane?? kiukweli ni kwamba tangu awali alishakataa kubadili dini na ndio maana alikuwa tayari kudanganya tu ili afunge ndoa..kiukweli alionyesha upendo hapo awali ila asikudanganye mtu kwamba ati anajilaumu au anaumia kwa yeye kuoa NI MUONGO HUYO kama aliweza kwenda kutafuta kimada ni wazi kwamba aliamua...labda sasa hivi kama anakutaka tena labda kama una kipato kizur...USHAURI WANGU TAFUTA MUISLAM MWENZAKO AKUOE..Huyo mtoto anaweza hata kulelewa na bwana mwingine na akakua vizuri..na usikute ndo RAID WETU MIAKA 30 IJAYO..Pole kwa matatizo.
Anonymous said…
pole dada kwa yote yaliyokupata,
umefanya uamuzi mzuri wa kutowadanganya ndugu zako kwa kubadili dini au kubariki ndoa kanisani.kitendo cha kuoa mke mwingine ni kuthibitisha kuwa anawajali ndugu zake kuliko wewe {mapenzi yamekwisha kwako}nakuomba usirudi nyuma muombe mungu akupatie mume mwema.achana nae huyo anakupotezea muda huyo.ndoa za kanisani hawaachani anakudanganya huyo.anakuona mjinga kaza kamba vumilia mungu atakupa.unajuaje mungu amekunusuru na nini kwa mume wa mtu huyo
Anonymous said…
we dada nawe, mtu mlishaachana tena kashafunga na ndoa wanini sasa???????? jamani mbona hivyo? kama ulikuwa unampenda si ungefunga nae ndoa nae! mambo mengine jamani twajitakia.
Anonymous said…
Pole sana Dada yangu kwayaliyokukuta ndio dunia hiyo duniani kuna mengi
kwaushauri wangu
huyo mwanaume tayari keshafunga ndoa kanisani na mwanamke mwingine na kwaimani yetu wakristo hakuna talaka lamda kama umemkamata mwenzako kwenye uzinzi.
nyie tayari mna tofauti za kididi na ndio mana tangu mwanzo huyo mwanaume aliona it cant work btn u ndiomana akaamua kwenda kutafuta wanaoendana kwa imani yakidini.
mimi ningekushauri tafuta mwanaume mlio na imni sawa za dini muoane na mungu atakubariki mtaishi maisha ya amani na upendo kuliko kuanza complication nakuanza kuingia tena kwenye ndoa na huyo ex wako .Piga moyo konde msahau kabisa mpotezee
Anonymous said…
Kasha oa mke mwingine tena kwa ndoa ya kanisani aliyokuwa akitaka toka mwanzo, songa mbele shost kurudi nyuma ni kwenda kujitia presha za moyo.Huyo mumeo alisha kusahau zamani ndo mana ana mke mwingine.Mie binafsi nimejifunza hilo.Move on!
Anonymous said…
Pole sana dada.moyo wako unaonyesha wazi hauko tayari kuacha dini yako ya uisilamu.mie nakushauri achana na huyo mume coz hakufai wala hakupendi.alikuwa anakudanganya tu.kubali uolewe na muisilamu mwenzako ili moyo wako uwe na amani.tubia kwa Mola wako na inshalah utapata maghfira.soma sana quran mungu ataleta kheri yake kwako.na utamsahau huyo mdanganyifu.naomba tuwasiliane kwa email nikupe ushauri zaidi muhimu sana dadangu my email is mustayoo@yahoo.com
Anonymous said…
me nadhani huyu mwanamke anakichaa kama sio mwenda wazimu!!kajitizame mara mbili hospital!!usiyeweza kutofautisha zuri na baya mwanaizaya