Mchumba ana UTI isiyoisha-Ushauri!

"Pole na kazi dada Dinah
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 27 sasa na nina mahusiano na nataka sasa nifanye maamuzi hasa kwenye maisha ili niweze kuoa, maana nafikiri kila kitu nimemaliza kwani nimeshapata elimu kwa kiwango cha degree moja na nimepata kazi nzuri .

Kwa sasa nimeshatoka nyumbani najitegemea na nimeshafikiria maamuzi ya kuoa, ila tatizo kubwa linaloniumiza kichwa ni huyu mpenzi wangu karibu kila baada ya miezi 2-3 lazima atalalamika kuwa tumbo linamuuma sana na akienda hospital anaambiwa kuwa ana UTI sasa mimi nashindwa kuelewa.

Tunakaa pamoja na nyumba ina choo cha kuflash na sasa ni zaidi ya mara 5 amepatwa na huo ugonjwa, napata wasi wasi sana japokuwa nilipomwambia tukapime HIV alikubali na wote tulikuwa safi, sasa najiuliza maswali haya

1.Huu ugonjwa ukiachilia uchafu wa chooni tatizo lingine linasababishwa na nini?

Dinah anasema: Maambukizo kwenye njia/mfumo wa Mkojo unasababisha na wadudu wanaoishi sehemu ya kutolea haja kubwa na sio uchafu wa chooni, japokuwa uchafu chooni unaweza kusababisha maambukizo mengine ukeni.

Mgonjwa akipata UTI na kuanza matibabu ni lazima amalize Dozi aliyoandikiwa na wakati akiendelea na unywaji wa dawa lakini akawa mzembe kunywa maji kwa wingi tatizo hilo litaendelea kujitokeza mara kwa mara kwa vile wakati alipokuwa akitumiia dawa alipaswa kunywa maji kwa wingi ili kusafisha njia yake ya mkojo kwa kukojoa mara nyingi.


Msemaji aliyesema kuwa UTI ni kichocho sio kweli, kichocho ni maambukizo mengine ambayo husababishwa na wadudu wanaishi kwenye maji yaliyotuwama/simama. Mtu mwenye kichocho hukojoa mkojo wa damu wakati mtu mwenye UTI anakojoa mkojo wenye rangi ya kama brauni hivi....yaani mkojo wake sio msafi na huto aharufu mbaya na kali sana.

2.Je akifanya ngono tatizo hili alimuathiri ?

Dinah anasema: Mhusika napopatawa na UTI hata kama ni mwanaume, unatakiwa kutumia Condom wakati wa kufanya ngono ili kuepuka maambukizo. Lakini ni vema kutofanya ngono mpaka mgonjwa amalize Dozi na kuponakabisa. Utajua umepona baada ya kwenda kumuona Daktari kwa vipimo vingine na pia mkojo kuwa msafi (unatakiwa kuwa kama maji).

3.Kwanini hiyo UTI inamtokea mara kwa mara?

Dinah anasema: Kuna sababu chache ambazo nimezigusia hapo juu na nyingine ni kwa vile anaendelea kungonoka wakati wewe ambae nadhani utakuwa umeambukizwa. Mlipaswa wote kupimwa na kutumia dawa za kutibu UTI.....ugonjwa huu sio kwa wanawake tu, bali hata wanaume.

4.Ni njia zipi zinaweza kuchukuliwa ili asipate tena ?

Dinah anasema: Kuhakikisha anapimwa tena, anatumia dawa na kumaliza Dozi yote bila kuruka siku, masaa. Kujenga tabia ya kunywa maji kwa wingi kila siku, kujifunza kuwa msafi na kujua namna yakujisafisha sehemu zake nyeti.

Kutokubana mkojo kwa muda mrefu, wanawake tunauwezo wa kubana mkojo kwa zaidi yamasaa manne na huwa tunajisifu sana kwa hilo lakini kama umewahikuwa na UTI hakikisha ukibanwa tu mkojo unaenda kukojoa haraka.

Vilevile kukojoa kila baada ya kufanya ngono ( ni muhimu kunywa kimiminika) sio uji, Soda wala pombe bali juisi iliyochanganywa na maji mfano maji ya Ukwaju, Ubuyu, Squash (hii lazima uzimue na maji) au aina yeyote ya kinywaji ambayo inachanganywa na maji asilia. Yote kwa yote maji ni mazuri zaidi ya vimiminika vingine.

Anapojisafisha baada ya kunya asijisafishe mpaka ukeni kwa wakati mmoja. Kama amekojoa wakati anakunya na anataka kujisafisha "kwa mpigo" ni vema kuanza kujiswafi uke na kumalizia sehemu ya kunyea kwama viungo viwili vinavyojitegemea kwamwe asisafishe kwa wakati mmoja. Pia kuepuka kuchangia vyombo/vifaa/sehemu za kuongea au kujisafishia nyeti zake.

Ikitokea amjemaliza kujisaidia (kunya) kisha akaenda kuoga (baada ya kuchamba) ahakikishe kuwa amesafisha mikono yake kwa sabuni kabla hajagusa uke wake nakujisafika ukeni (kuondoa utoko).

5.Madhara gani makubwa yanaweza kutokea baadae?

Dinah anasema: Kama ataendelea kutumia aina ya Antibaotics kutibu UTI kwa muda mrefu, inasemekana dawa hizo husababisha tatizo lingine la kiafya, pia kama UTI itafikia kwenye kiwango cha mgonjwa kukojoa mkojo mzito (uliochanganyikana na usaa) au usaa kuteremka wenyewe kama Utoko basi ni wazi kuwa mrija wake wa mkojo unaweza kuzima na hivyo kushindwa kutoa mkojo kawaida.....unabanwa mkojo lakini huwezi kukojoa.

Ikifikia hatua hii mhusika tahitaji kufanyiwa upasuaji ili asafishe na pengine kuwekewa Catheter (mrija wa mpira) kwenye Kibofu cha mkojo nahivyo kutumia Mfuko wa nje wa kutunzia mkojo.

Nitashukuru sana nikipata majibu kutoka kwako hili nitoe wasiwasi wangu
Ni mimi nduguyo Jm."

Dinah anasema: Asante sana JM kwa uwazi na ushirikiano. Ni matumaini yangu maelezo ya wachangiaji na haya yangu niliyo ongezea yatasaida wewe na mpenzi wako kwa pamoja kwenda kwa Daktari ili kupata matibabu na kutibu tatizo.

Kila la kheri.

Comments

Anonymous said…
Wanawake na wanaume tuko tofauti kimaumbile.Wakati wenzetu njia yenu ya mkojo ina sentimita 20 sie yetu ina nne so hapo maambukizo ni rahisi sana.Pia kuna vitu kama mate ya mwanamme yanaweza kuchangia sana katika kuleta matatizo ya mirija ya mkojo.

Pi tatizo jingine kubwaaaaaaaaa sana ni kuto kukojoa mara baada ya kufanya mapenzi.Wanawake tuna shauriwa tuwe tunaenda kukojoa mara tu baada ya kufanya mapenzi ili kusaidia kusafisha njia ya mkojo.Na hata mwanamke na mwanamme mkimaliza kufanya mapenzi kama mna pumzika kwa muda mrefu wote mkiwa bila nguo ni vizuri mkajisafisha kwanza kabla ya lile tendo hasa kwa wanaume vile nyie uume wenu unakuwa uko exposed zaidi.Kuwa makini mambo ya kulambana ukeni haya mana mdomo una wadudu wengi sana na mara nyingi watu ndani ya usingizi tukikurupuka na kuvamia tendo la ngono ina ongeza chance ya infection.Pia wataalam wanasema kuwa kuna condom nyingine pamoja na vyakula vinavyo changia matatizo ya mirija ya mkojo so ni vizuri kuangalia sana vitu vingi badala ya swala moja tu.

Pia mwanamke anapojitawaza siku zote anashauriwa kuanza kujichamba toja mbele kwenda nyuma.Sasa mfano sie kwetu huko bongo kujichamba kwa maji kunaweza kuwa changio zaidi katika kuleta wadudu.Kwanza sometimes maji tunayotumia si salama na mkono wa kujichambia mmoja so yale maji yanasafiri kihurahisi kutoka njia ya haja kubwa kwenda kwa haja ndogo.Ushauri tawaza njia ndogo kwanza osha mkono na sabuni then tawaza sehemu ya haja kubwa kama ukiweza jikaushe na tissue badala ya hapo ili kuzuia usambaaji wa wadudu.
Ngono ni changio kubwa sana kwa UTI ni jukumu la mume na mke wote kuhakikisha sehemu nyeti ziko safi kabla na baada ya tendo la ndoa.
Jambo jingine muhimu la kuzingatia ni umalizaji wa dozi ya UTI.kama tatizo la jirudia ni vizuri kama ukipewa dawa uwe wamaliza dozi yote kuzuia kujirudia kwa wadudu.Mie nishamkataza mpenzi wangu kulowanisha uume wake na mate kama niko dry bora asubiri mana ilikuwa yaniletea matatizo sana.
Goodluck.
Anonymous said…
Kuongezea katika jibu langu refuuuuuuuuu, ni muhimu kunywa maji ili kupata mkojo wa kutosha unaosafisha njia ya mkojo.Maji yanasaidia sana kufanya mtu ukujoe kwa wingi na kuzuia bacteria kujiwekeza kwa njia ya mkojo.Matatizo mengine kama sikoseli na kisukari nayo pia yana changia kuleta UTI.Hata watoto pia wanapata tatizo la njia ya mojo sababu hawatawazi vizuri na hawanywi maji kwa wingi.Usimfikirie vibaya mmeo hilo ni common problem.Wadudu wa UTI wanapatikana sana kwenye nyama pia.Kama unakula nyama haijaiva vizuri na usafi wa sehemu nyeti si fresh ni rahisi sana kupata maambukizo.
Anonymous said…
hi....pole sn kaka nina elimu ndogo tu kuhusiana na UTI na si vibaya nikishare,kwanza hongereni kw kucheki afya,pili elimu yangu ndogo juu ya ugonjwa huu ni kama ifuatavyo; UTI husababishwa na uchafu,uchafu huo c lazima uwe wa choo pekee yawezekana ni usafi wa muhusika pia,kwenye kusafisha nguo zake za ndani,kipindi cha hedhi jinsi anavyojihudumia nk. vilevile pengine ni ufatiliaji wa doz zake kwa ajili ya kutibu maradhi hayo,kuto kunywa dawa kwa wakati au kuacha kabisa hvy kusababisha tiba ishindwe kupambana na vijidudu hivyo,nimegusia uchafu mana hata watoto wadogo hupata UTI kama hawahudumiwi ipasavyo,na pengine alishakuambukiza wewe kwani UTI inaambukiza,sasa anajitibu halafu anaupata tena kwako kwa njia ya kujamiiana,kuchangia choo nk,ni vema ukacheki na wewe kama vp upate tiba kwani kwa mwanaume UTI inachukua muda kujitokeza.
madhara;kwanza ni hiyo hali anayoipata ambayo huambatana na homa mara nyingine,kubwa zaidi UTI ikimla sana inaweza ikaathiri kizazi chake.ni hayo tu.ahsante
Anonymous said…
Uncle J,
Pole kwa tatizo hilo. Ushauri wangu ni mdogo na sijui utasaidia kwa kiasi gani, lakini upande wangu ulisaidia "like magic"!
Mchumba wangu aliwahi kusumbuliwa kama hivyo, mara kwa mara mwaka juzi (2008). Alitibiwa kwa kuchomwa sindano mara ya kwanza, akapona, ukarudi, akachoma mara ya pili, akapona, ukarudi akanywa dawa. Sambamba na hiyo, daktari alishauri ANYWE MAJI KWA WINGI.
Alishauri hivi toka mara ya kwanza, sasa tulipoona ugonjwa hauishi, akaanza kunywa maji LIKE CRAZY. Kwa siku lazima akate lita 3 au zaidi.
Since then, mpaka leo hii, HAJAWAHI KUUMWA TENA.
Pamoja na kufuata ushauri mwingine, jaribu kuzingatia hili, then utoe feedback after like 6 months tujue.
Asante.
B
Anonymous said…
POLE SANA kaka tatizo inaonekana anatumia dawa yeye wewe hutumii ushauri nendeni wote kwa daktari mpime na dawa mtumie wote inavyooneka wewe ndio unamwambukiza kwani yeye anatumua dawa then mkingonoana wewe unamwambukiza bila wewe kujua kwani unakuwa hujatumia dawa
Anonymous said…
Naombeni msaada na mimi jamani nina tatizo hilo hilo pia na fungus nakuwa nawashwa sehemu za siri. nikiwa mjamzito sipati hilo tatizo kabisa na ile miezi miwili baada ya kujifungua kabla sijaanza kusex nakuwa OK nimeanza tu ku do miezi miwili nikapata tena hii inasababishwa na nini? Ila mume wangu hata siku moja hajawahi kupata hilo tatizo.
Anonymous said…
nenda kwa mtaalamu wa magonjwa ya akina mama ikiwezekana umshauri na uyo dada yawezekana iyo UTI hamuitibu bali mnaituliza kama vile mtu anaumwa maralia unamtuliza maumivu ya kichwa na maralia inabaki palepale. Hutampata kirahisi mwingine ambaye hana virusi sasaivi dunia imejaa virusi CHA MUHIMU NENDENI HOSPITALI MPIME WOTE MAGONJWA YA ZINAA, yawezekana wewe ndo unayo na mkisex unamrudishia vijidudu. USIMUACHE HUYO NDO ATAKUFAA KAMA KWELI WAMPENDA NA MNARIDHISHANA
Anonymous said…
yani huyu mkaka amesema hii mada yake ni kama mimi jamani. sipitishi miezi 3 cjapata tatizo hilo. ila mie nimeshawahi kwenda kwa dr akaniambia coz mie ni mnene so nikitembea na kuchubuka so mvuke unapanda juu kwenye uke so inaleta kama fungus flani. ila inaniboa sana coz kila baada ya miezi 4 lazima niumwe, mpaka naona ntashidwa kuzaa sasa. najua wadau watatusaidia wote. thanks
Anonymous said…
Naombeni kama kuna mtu anajua UTI unaitwaje kwa English anisaidie tafadhali. ili nikienda kwa dr, nijue vya kuanza! Asanteni
KKMie said…
Anony @ 09:11 UTI ni neno la kiingereza (English), ni kifupi cha Urinary Tract Infection.

Kwa Kiswahili (sio chakitibabu) ni maambukizo kwenye mrija unaotoa mkojo kutoka kwenye Figo kwenda kwenye kibofu cha Mkojo a.k.a system ya mkojo.

Natumaini maelezo haya yatasaidia kwa sasa.
Anonymous said…
Pamoja na mawazo ya wachangiaji wengine,Stile ya sex pia hua inasababisha, kwa mfano kama mnapenda chuma mboga mara nyingi huleta hio. jaribu kuacha tumia kifo cha mende
Anonymous said…
Dinah , mimi ndio niliouliza niambiwe UTI kwa English unaitwa vp. Ahsante sana dada, Japo sijawahi kuusikia huu ugonjwa kwa kiswahili or English, lkn waliotoa maona na wewe Dinah mmenielimisha kiasi flani. Keep up the gud work. THANX AGAIN
Anonymous said…
Mdau kweli mh! UTI ni english/kiingereza Urinary Track Infection na kiswahili ni ugonjwa wa kichocho.Unapokuwa na ugonjwa wa kichocho unapata maumivu makali ya tumbo pamoja na maumivu katika njia ya mkojo.Ukienda kukojoa kama imefika hatua mbaya unatoka damu na unakuwa na maumivu makali kwa njia ya mkojo.Mara nyingine unakuwa unajisikia kama unataka kukojoa lakini ukienda chooni hakuna mkono ni chumvi tu inafanya ujisikie kama wataka kojoa.We ukienda kwa daktari ukimwambia tu una maumivu kwa njia ya mkojo wakati wa kukojoa yeye atajua ni nini.Hope mbaka sasa umeelewa UTI ni kifupisho cha maneno matatu ya kingereza ingawa inasomeka kiswahili.Kama UDSM kirefu chake ni University of Dar es salaam na UTI NI URINARY TRACK INFECTION jaribu kuunganisha maneno hayo matatu kutumia herufi za mwanzo utaona yanakupa neno UTI.
Anonymous said…
Anayesema UTI ni KICHOCHO kakosea, ila ni "maambukizi katika njia ya mkojo" Kichocho ni ugonjwa tofauti japokuwa una uhusiano na njia ya mkojo.

Anayetaka maelezo ya kidaktari kuhusu UTI aweke wazi e-mail yake nitamtumia, wadau mmegusia baadhi ya sababu zinazisababisha lakini ni nyingi zaidi ya hizo.
Anonymous said…
mi nashauri kwenda hospitali ya uhakika na kupata ushauri mzuri,kwanza ajitahidi kunywa maji mengi sana.
mwanamke yeyote akikaribia period au akimaliza mkojo huwa mchafu,kama unaumwa tumbo au unataka jua afya ukienda pima lazima wapandikize ili kujua ni wadudu gani na wanatibika na dawa gani. ndo sehemu nyingi wanavyopima,pia kwenye haja kubwa kuna wadudu kama akikosea wakati wa kujitawaza wadudu huja mbele(ukeni)pia huleta mkojo mchafu tumbo kuuma.
NASHAURI MKOJO UPANDIKIZWE ILI KUJUA NI WADUDU GANI NA WANATIBIKA KWA DAWA GANI
Anonymous said…
dada dinah nashukuru sana kwa post yangu kuwekwa maana nilikuwa nasubiri sana majibu yake ingawa imekuwa ni ya muda kidogo najua una kazi nyingi na pia nashukuru wadau wote kwa kunipa ushauri mzuri ulioenda shule lkn bado sijapata majibu mawili ya msingi yaani swali namba 2 na 5 sijaelewa kwakweli ni naomba wadau wanieleweshe maswali hayo
jm
Anonymous said…
Kwa mdau wa 7.02. Huyo mtu alieomba kuambiwa UTI kwa English sio kama hawezi kuunganisha URINARY TRACK INFECTION, bali alikuwa hajui huo UTI ni nini. iwe kwa kirefu or kifupi. Soma vizuri, ombi lake usijifanye mjuaji sana. Asante
Anonymous said…
Fwata ushauri wa aliyekwambia mkojo upandikizwe kwa sababu kuna UTI sugu. Fika TMJ hospital uombe kufanyiwa kipimo cha culture kwa ajili ya UTI, utaacha sample ya mkojo na kupewa tarehe ya kuchukua majibu. hayo majibu ndiyo yataonyesha dawa specific kwa ajili ya UTI inayokusumbua wewe.
Anonymous said…
naomba kuuliza mafhsra yske ya uti katika mwili wa binadamu