Anataka nifanye Masters pia niwe msiri-Ushauri

"Mpendwa dada Dinah. Mimi ni mwanamke wa miaka 23 naishi jijini DSM. Nimekuwa nikifuatilia na kusoma mambo mbalimbali na ushauri wako na comments za washirika tofautitofauti. Nimeona bora nije na hii yangu ambayo kwa ukweli inanichanganya kichwa.

Ninae boyfriend kwa hapa nitamwita X mwenye miaka 26, nimekutana nae chuoni mwaka 2006 nikiwa naingia mwaka wa kwanza na hadi sasa tumeshadumu miaka 3. Tulikuwa darasa moja huko chuoni ila yeye kwa sasa anaendelea na Masters ambapo kwa mimi plan ni next year ndiyo niisome hiyo masters kwani sikupenda kuunganisha.

Mwanzo alipoanza kunidate alikuwa mtu mzuri sana, muda wote alikuwa karibu na mimi na tulipoanza mahusiano mambo yalibadilika kidogo japo aliniambia kuwa yeye ni busy person. Tulikuwa tunaonana kwake siku za weekend tu tena mchana. Siku za kawaida na hata kama ni darasan ni salaam tu basi then kila mtu na muda wake.

Nilipomuuliza alinijibu kuwa yeye ni mtu anaependa privancy hasa kwenye mambo yake ya binafsi kama mahusiano. Tuliendelea hivyo japokuwa alinitambulisha kwa baadhi ya marafiki zake wa chuoni na hata wa kazini kwake akiwemo Boss wake. Kitu ambacho kilinishangaza katika usiri wake ambao ulikuwa ni chuoni tu, kwani tukishatoka chuoni alijitahidi kuwa close na mimi.

Mara moja moja tulipokuwa darasani alikuwa anakuja kukaa na mimi na mda mwingine hapana, japokuwa darasa zima lilikuwa likikujua kuwa tunadate na walikuwa wanatushangaa tunavyoact kama hatujuani.


Hapo ndipo mambo mengine yakaanza, akaniambia anataka watu wachanganyikiwe kwamba wasiwe na uhakika kama tunadate kweli au la. Akawa akiulizwa "mkewako mzima?" anawajibu "sina mke mimi" na baada a hapo anawaacha kwenye mataa na kuondoka.


Kitu kingine ambacho kiliniuma sana ni kuwa hata kwenye party za chuo kama za darasa ambazo ni za usiku alikuwa haongozani na mimi, bali na marafiki zake 3 wa kiume na msichana mmoja. Ndani ya party anakaa na hao watu ila mda mwingi anatoka nje na kurudi


Wakati party inaendelea msg zake kwangu haziishi kutumwa kuwa nisijali nivumilie na niact kiutu uzima. Ukicheza mziki na mkaka anakuja kukutoa na kuniambia nijiandae tunarudi nyumbani. Kwa maana hiyo party ndio inaishia hapo.


Siku zilienda mara nyingine alikuwa na mikutano ya kikazi mpaka saa sita za usiku ndio anaweza kuniambia anatoka kikaoni, nilikuwa najiuliza ni kazi gani usiku? Nijuacho mimi ni kuwa anafanya kazi kwenye makampuni 2 ambayo kote kuwili alinipeleka.

Hatimae nikaja kusikia tetesi kwa watu wengi wa darasani kuwa X anafanya kazi ya upelelezi, tena na hivi alikuwa anasafiri sana kwenda nchi tofauti na hamna anayemuaga zaidi ya mimi tu basi mi ndio nikawa nasumbuliwa "vipi mumeo kaenda kufanya upelelezi?" na maswalimengine mengi.

Siku moja nikamuuliza, akaniambia "kazi zangu zote mbili unazijua haya ya upelelezi sijawahi kukuambia na wala siyajui ndio mana nikakwambia watu wambea sana wanaongea mno, wewe nisikilize mimi na si wao".

Kwa kweli haya yote yalinisumbua sana kichwa changu na mara kwa mara niliongea nae ila jibu lake ni kuwa eti nahitaji kumwelewa na tupeleke mahusiano kiutu uzima na si kitoto. Basi kwa vile nilimpenda nikaka kimya.

Ilimradi mapenzi niliyapata, nikiumwa yupo,nikiwa na shida ananisaidia, akiwa less busy naenda kwake na hata nikitaka kulala huko yeye sawa tu, pia yeye alikuwa anakuja kunitembelea nilikokuwa naishi na wakati mwingine analala. Marafiki zangu walimjua na aliwajua vizuri japo alikuwa ananiambia nisiongee nao kila kitu kuhusu mapenzi yetu kwani hataki umbea.


Siku moja nikamuuliza hivi una mpango gani na mimi wa mbeleni? akanijibu "nataka usome hadi masters mana kamwe sitaoa mwanamke asie na masters" na akaniambia kwa yeye ana plan ya kumaliza masters na kuendelea kusoma na ana mpango wa kuoa mwaka 2015 ila kwa sasa nijue tu kuwa sisi ni wapenzi mungu akipenda basi tutafika mbali.


Ila akaniambia ukitaka tuwe wapenzi zaidi inabidi ujifunze kuwa privancy person hiyo ndiyo sheria yangu,ukianza kuongeaongea sana mambo yetu na mengineyo tutaishia hapo.

Kwa saa tupo mbalimbali na huwa nafunga safari kumfuata chuoni na ninakaa nae siku tatu au mbili kisha narudi kazini. Mambo si rahisi kwa huu umbali ila najitahidi kumtembelea na hata mapenzi ya simu yanachukua nafasi kubwa zaidi kama nikiwa nimekosa kisingizio cha kuomba ruhusa kazini, maana kazi nazo si kila mara uombe ruhusa.

Basi mara nyingi mimi ndio nikawa nampigia simu kila siku jioni, inaweza kupita hata siku mbili kama sijapiga basi tena. Siku moja nikamwambia sipendi hiyo tabia kwa nini hapigi simu?akanijibu kuwa huwa anasahau kuweka credit basi nikamwambia "kama hunipendi uniambie kuliko kunipotezea muda".Tukaagana.

Kesho yake yeye akapiga simu ila sikuchangamka kama siku nyingine.Siku iliyofuata usiku akanitext "hujambo umeshindaje?usiku mwema", mimi nikamwendea hewani tukaongea vizuri tu mwisho nikamwambia "i love u",akanijibu "me too".


Nikamuliza "una uhakika?" akanijibu "sina budi ya kurudia kitu kwa miaka yote 3 tuliyokuwa pamoja hujakua tu?kua basi tuwe na mapenzi ya kiutu uzima" na akaniambia "kusema i love u kila siku haimaanishi ndo unapendwa naweza nikakuambia hivyo na bado nisimaanishi. Kwa kweli sikumwelewa, akaniambia mwisho tukagombana bure na yeye hataki hilo litokee bora tulale,basi tukaagana.

Huyu ndie mwanaume ambae ninae dada Dinah kwa miaka 3 sijapata jibu ni mwanaume wa aina gani huyu na kama kweli ananipenda na ana mpango na mimi. TAFADHALI NAOMBA UNISAIDIE KWA USHAURI NIFANYAJE.
Na washiriki wengine nahitaji maoni yenu tafadhali.

Ni mimi dada F"

Dinah anasema: Dada F, shukrani kwa ushirikiano na uvumilivu wako as nachukua muda mrefu kujibu kutokana na uwingi wa majukumu mengine ya kikazi na maisha. Nimefurahishwa na maelezo yako ya kina na kumfanya yeyote kuelewa picha nzima bila kuwa na maswali.....hongera kwa hilo.

Suala la Ushushushu sio muhimu sana as long as wewe unajua kazini kwake, na akitoweka siku zote huwa anakuambia kuwa anasafiri hivyo huitaji kujipa hofu na mimi binafsi sina uzoefu na masuala ya wapelelezi. Nitakupa maelezo kuhusiana na issue ya uhusiano wenu wa kimapenzi ambayo naamini yatafungua macho yako kwa kiasi fulani.

Mimi binafsi ninaamini kuwa sisi wanadamu lazima tupitie hatua sita za maisha ya kimapenzi na mahusinao. Ila tatizo la wengi huwa tunakurupuka na kutaka/kutegemea jambo fulani kabla ya wakati.

-Uzoefu/kutambua ujinsia wako kwanza (hapa unakuwa kwenye umri mdogo so jaribu kufurahia maisha na kupata uzoefu zaidi wa kimaisha na wakti huohuo unazingatia masomo/kazi, sio lazima ungonoke).

Pili:-Unapenda na ku-commit (hapa utakuwa mkubwa kiumri na umetulia kiakili).

Tatu:-Chumbia na Ndoa (kuwa na uhakika wa kuishi na huyo mmoja tu maisha yako yote).

Nne:-Familia(Uamuzi au kukubaliana kuzaa).

Tano:-Kufanya uhusiano wenu wa kimapenzi na ndoa kusimama Imara.

Mf-ninyi wawili bado wadogo, mnapendana sana tu (kutokana na maelezo yako bado mko hatua ya kwanza)...ila wewe unategea au unataka zaidi ya unachokipata kutoka kwenye uhusiano wenu, huenda ungependa siku moja ufunge ndoa na huyo mpenzi X hasa ukizingatia kuwa owte mnafanya kazi na mmeshakuwa pamoja kwa muda mrefu. Lakini yeye hayuko tayari kufanya hivyo kwani anachotaka yeye kwa sasa ni kurekebisha maisha yake na wakati huohuo kuongeza Elimu.

Kitu ambacho sisi wanawake huwa tunakikosea ni kuharakisha mambo, labda kutokana na " msukumo" kutoka kwa jamii inayotuzunguuka kuwa ukiwa kwenye uhusiano baada ya muda fulani basi lazima uolewe au hata kuzaa.

Lakini katika hali halisi tunatakiwa kujua nini hasa wapenzi wetu (wanaume) wanakitaka kutoka kwenye uhusiano husika na je ni hatua gani hivi sasa uhusiano wetu upo? kabla hatujaanza kurukia/harakisha hatua inayofuata kama sio kuziruka zote na kwenda hatua ya mwisho.

Sasa ninachokiona hapa ni wewe kutaka commitment na kuhakikishiwa nafasi yako, wakati yeye bado anajaribu ku-have fun. Kweli anakupenda lakini hiyo hamfanyi yeye kuwa na uhakika kwa 100% kuwa wewe ndio mke wake.......anahitaji muda.

Kwenye suala la wewe kuwa msiri, mimi sioni tatizo kwani naelewa kuwa kuna baadhi ya watu wanaaibu sana yanapokuja masuala yao ya kimapenzi.....yaani hawapendi kujionyesha wa watu wengine kuwa wao ni wapenzi. Sasa kwa vile mpenzi X ni mmoja kati ya hao watu ni vema wewe kuheshimu takwa lake hilo.

Nini cha kufanya: Jiulize nini hasa unataka out of the relationship with X, mawasiliano yenu yako bomba kama wapenzi, unapewa mapenzi yake yote, mnaonana kila mnapohitajiana, anakujali, kila mtu yuko huru kwenda kwa mwenzie, mnaoneana wivu (which ni dalili nzuri) X anaonyesha ameji-commit kwako.......nini kingine unataka?

Kama ni ndoa ndio utakayo ni wazi hutompata kwa sasa kwani yeye anadhania takuwa tayari akiwa na miaka 31 (2015) which wanaume wengi ndio hupenda kujipangia hivyo kuanzia 31-36 wawe wamefunga ndoa, huamini by that time wanakuwa somehow wamekamilisha "mipango" yao kimaisha.

Hivyo hapo kuna maamuzi 3 tofauti;
(1)-Endela na uhusiano huku ukimsubiri tumia muda huo kwenda kufanya hiyo Master yako au

(2)- Endela na uhusiano, furahia maisha yako na chukulia kila siku kama inavyokujia (mkifunga ndoa poa isipotokea ndoa poa).

(3)-Toka kwenye uhusiano ili kupata utakacho kwenye uhusiano mwingine (kama unaharaka sana na maisha ya wawili).

Nakutakia kila la kheri.

Comments

Anonymous said…
Huyo mwanaume mhhhh!! Haya anakwambia kuoa yeye hadi 2015, hivyo kweli wewe inakuingia akilini? Dalili ya mvua ni mawingu shost wangu, huyo mie naona hana hata upendo na wewe.Be careful wanaume kama hawa ndio wanapotezeaga wasichana muda, wewe utakuwa unamsubiri kumbe mtu mwenyewe wala hana upendo nawe. Akili kumkichwa mdada.
Anonymous said…
Dada yangu pole sana kwa yaliokukuta na unatakiwa kua mstahamilivu kwani safari ya mapenzi ni refu na ina vikwazo vingi. ushauri wangu ni kwamba ww usichoke kumuomba Mungu msaada wake kila wakati na km upo tayari kuolewa mwambie huyo jamaa afanye hivyo na akikataa ww fanya kama huna time nae nayeye atahisi maumivu kwani ni binaadamu na ana hisia na maumivu ya mapenzi pia sishauri muachane kwani kuachana kutapelekea maumivu makubwa kwenu nyote ila ukiona haheshimu mawazo yako ni vizuri kuwa na msimamo wa dhati nadhani na yy atajifunza. lkn pia jitahidi kua makini nae kwani inawezekana kua anafanyakazi ya usalama kweli km watu wanavyofikiria. mm nakutakia kila la kheri ktk maisha yenu Mungu abariki penzi lenu lidumu milele.
Anonymous said…
Huyo mwanamme akija kukuoa utajuta,mapenzi gani ya masharti hivyo utafikiri mume wa mtu,raha ya mapenzi na yeye ajali feelings zako inaonyesha hazijali kabisa,kama usomi wenyewe ndio huo,hayo sio mapenzi umri bado unakuruhusu achia ngazi mapeeeema asikupotezee muda wako. Inaonyesha hiyo tabia hatoiacha kabisa.mkioana mambo ndio yatazidi.Najua kupenda kubaya lakini bora achia kabisa mungu atakupa mwengine na utakuja kumsahau huyo mwenye kupenda kwa masharti.
Anonymous said…
kwakeli huyo mwanaume wako haeleweki,mbona ana mapenzi ya kizamani sn tena ya kitoto,inawezekana ni kweli anafanya kazi ya upelelezi ndo mana ana act like that,inabidi uwe mjanja sn umchunguze kwa makini ujue anachokifanya zaidi ya hizo kazi za kwenye makampuni mawili utapata jibu
Anonymous said…
unajua mara nyingi mtu anaedili ktk masomo(msomi) huwa muda wake wa kushughulika na mapenzi ni mchache sana,kama ameamua kusoma kwake ni kumpotezea muda2, cha msingi dada yangu kama uko tayari kuolewa akitokea mchumba kubali tu.Mapenzi ya kweli hayaekewi vikwazo kama hivyo...kwa sasa hana mpango na mapenzi huyo achana nae kabla hajakuchoma jiti...
Anonymous said…
Dada mwenye tatizo, nafikiri vuta subira. Jaribu kufanya uchunguzi zaidi juu ya bf wako. Si wanaume wote wanaopenda kuweka mambo yao open...especially tena ktk umri huo wa 26...Kuna vitu vingi vinakuwa kichwani mwa mwanachuo.

Kuhusu jamaa kukutaka usome Masters, nafikiri ni wishes ambazo angependa ziwe..haimaanishi kweli hatakuja kukuoa kama hutapata Masters... Nilikuwa mwanachuo kipindi fulani, na nilifikiria kama bf wako...lakini thru time, mambo yanabadilika, akili inakuwa na options/flexibilities zinaongezeka.

Kuhusu kazi ya usalama...sidhani kama bf angeweza kukubali kwamba anafanya kazi ya usalama..especially when u two are in bf-gf relationships. Hujui wale jamaa huwa wanakula viapo?? Kama jamaa yuko makini atakuja kukwambia siku ukishakuwa mke wake rasmi.

Bottom-line, usifanye haraka na maamuzi. Jaribu kuchunguza kama jamaa anakupenda hasa kutoka moyoni au la...hilo najua unaweza kufanya - women insincts zitakusaidia.

Ni vizuri uzungumze naye kuhusu issues inavyoziona (ur perspective) na kwamba anakuambia kuhusu 'utu uzima', u dont find it cool, na ungetaka aweze kujua ur own side of the story.
Anonymous said…
Pole kwa penzi lenye utotoro wa giza.

Kwa kweli wewe mdada ni mstaarabu sana na unathamini mahusiano vizuri kabisa.Nakupongeza sana kwa ustahifu wako.

Kuna usemi unaosema "Akufukuzaye hakuambii toka" Nina mambo mawili ambayo napenda nikuambie ambayo umeyaeleza katika stori yako.

Jambo la kwanza ni lile ambalo amekwambia kuwa yeye hapendi kuoa mdada aliye chini ya kiwango cha elimu ya Uzamili, na naambatanisha hapo na lile la kwamba yeye anatarajia kuoa mwaka 2015. Kwa mtazamo wangu nadhani huyo jamaa anweka vikwazo hivyo ili yamkini vikukatishe tamaa na ukimbie.Kama kweli ni hivyo bila shaka hana mpango wa kukuoa na isitoshe amekuambia kuwa kwa sasa ni mambo ya mapenzi tu,no anything else right now just remaining in relationship.Hicho ni kitendawili hasa kwa watu kama ninyi ambao mumefikia kiwango cha elimu mliyonayo.

Jambo la pili ni lile umetuambia kuwa anataka sana privacy na hataki uongelee sana masuala ya mahusiano yenu, na pia hataki sana uambatane naye. Mimi nadhani huyo jamaa yako ana lake jambo.Inawezekana kabisa(sina uhakika) kwamba ana mpenzi mwingine ambaye naye anam-treat in the same manner na hivyo kumpa yeye mwanya wa kutowachanganya kiurahisi na kuendelea kutunza matakwa yake.Kwa muda mliokaa kwenye mahusiano sidhani kama angekufungia nje kiasi hicho.Kule wewe kwenda kwake kulala au kuja kwake kwako kulala mnachofuata wote wawili na hasa yeye ni kukumega/kukutomba na anapokuwa hana shida hiyo kwako anakuwa mahali pengine.Kuna dhambi gani kujiweka wazi na kuambatana na wewe?ni privacy gani hiyo ambayo hawezi kuambatana na wewe na hata kwenye muziki anakuweka kando. Nikuulize swali Je unafurahia nini sasa katika mahusiano ya namna hiyo?Au kutombana tu ndiyo chance yenu kubwa mnapohitajiana?

ushauri wangu ni kwamba wewe kama mtu msomi usiwe kipofu wa mapenzi.Sikwambii achane naye lAKINI NATAKA UWE MWANGALIFU na mtafiti mkubwa juu ya uhusiano wenu huo kama kweli una manufaa kwako wewe kwa maisha yako unayoyatarajia.Usipoteze muda wako mwingi kuendelea na mtu mwenye vikwazo vingi visivyokupa picha yoyote ya unakokwenda na unayoyatarajia. Umri wako ni mzuri sana nina imani unaweza kuvumilia miaka mitano ukingoja kuolewa na huyo jamaa,lakini je kweli anakufaa huyo na ni kweli ana mpango wa kukuoa, na je kweli hana mtu mwingine?au ndiyo lile nimesema hapo juu "akufukuzaye hakwambii toka"

Umefanya vema kuleta hapa maana najua utapata mawazo mengi yatakayokufungua kichwa na kuuona ukweli.Nakutakian kila la heri.Usimsahau Mungu kumuuliza kama kweli una future na huyo jamaa.Omba sana hilo.
Anonymous said…
huyo jaa yako ni mafia a.k.a shushushu wa serkali!fta anavyokwambia kwan anaweza kukupoteza maishani!
Anonymous said…
Its PRIVACY honey & not PRIVANCY!
Faith said…
Habari yako dada F. Hii ndio mara yangu ya kwanza... Habari yako dada F.

Hii ndio mara yangu ya kwanza kutembelea hii blog, na kwa bahati nzuri nikakutana na post yako ambayo ipo very interesting.

Mpenzi mdogo wangu ningependa kukushauri kuwa wewe bado mdogo sana kiumri na hata kimaisha, kama huyo mpenzi wako alivyokushauri usome Masters na kuwa msiri ni vitu vizuri sana... Lakini katika suala la mapenzi na la kutaka kujua msimamo wako kati yake wewe na yeye mimi ninge kushauri ulichukulie taratibu sana tena sana don't take the love issues too serious as you have a long way to go... haya mambo ya mapenzi yanaweza kukupatia stress za maisha bila hata ya kuelewa. When time comes everything will set it self on its position...Suala la kukwambia I love you too anaweza akawa anamaanisha kutoka moyoni mwake au la kwani wanaume wapo tofauti sana na wanake emotionally.. pia suala la kujificha hataki watu wajue kuwa ana mausiano na wewe au la cha msingi watu wako wakaribu wanafahamu inatosha haina haja ya ulimwengu mzima kujua (msiri)...Kwahiyo nacho kushauri take one step at a time soma, jiendeleze, panga mipango ya maisha wewe binafsi na dont invest so much into him, mapenzi ili yapendeze yanatakiwa yatoke pande zote mbili, mpe muda na yeye akutafute akutembelee pia mpe muda wa kuweza kupanga maisha yake vizuri kwani wanasema if a man has not archieved his goals that means if he cann't provide he wont be able to profess and protect...

Kila la heri dear.
Ohh swali very interesting but refu mnoo..DINAH ITABIDI UWAAMBIE WADAU WAJIFUNZE KUSUMMERIZE...YAANI KUSOMA NATAKA LAKINI MUDA UNANIISHIA ...IMEBIDI NIPRINT KESHO NDO NIJE CHANGIA...AMBAPO INAKUWA HAINOGI
KKMie said…
Wee Zeze acha uvivu!

Samahani washauri, watembeleaji na wasomaji. Nimejaribu kadri ya uwezo wangu kuhariri Malezo haya na kufikia hapa yalipo.

Ningekata zaidi ningepoteza maana nzima ya Walaka huu na wala msingeweza kumuelewa.

Sasa ili muelewe the whole story bila kumuuliza maswali nikakomea hapo kuhariri.

Asanteni kwa ushirikiano!
Anonymous said…
Wewe zeze hii story ina urefu gani hasa hadi uone kama inachosha? Kweli wewe ni mvivu hasa... wink!
Anonymous said…
Faith umeongea point nzuri MNOOO!!! Kula tano!
sio uvivu dinah si wajua sie wengine waajiriwa na tunaumiaga muda wa mwajiri kupita huku ndo maana

but nimekuelewaa
Jane said…
Du!!! the same story like mine. pole dada ndo mahusiano yaliyo mengi ya siku hizi so mtangulize mungu katika hilo mpenzi nae si mchoyo atakuonyesha njia pale pasipo na njia. All the best
Anonymous said…
DU hi kali
huyu jamaa hafai kuwa mune wako atakuyumbusha na amegundua unampenda ndio maana analeta za kuleta
kwanza katika mapenzi haitakiwi kuwe na usiri wa aina yoyote hiyo
hayo sio mapenzi
pili haitakiwi kuwe na masharti ya aina yoyte yale
tatu kwa umri wako na wake na jinsi mlivyo wasomi hiki kipindi mlichOnacho kilikuwa ni kipindi kizuri cha kupanga mambo ya maisha yenu yaani ajitambulishe kwenu rasmi kama mchumba
kama ni ratiba za kusoma master mpange kwa makubaliano wote pamoja
mpange kuhusu maisha yenu ya familia yatakavyokuwa ili hiyo 2015 anayotarajia kuoa muwe mkombali kimaisha ni kimaendeleo
sasa yeye yupoyupo tu wala akupi mwelekeo wa mapenzi yenu anaishia kusema sina mpango wa kuoa sasa labda 2015 wala haonyeshi kama yupo silias mapenzi yanaumiza kuachana na mtu hasa kama umemzoea lakini angalia kuhusu maisha yako kwani usipokuwa makini utateseka maisha yako yote kwa mistake ndogo ya kushindwa kufanya maamuzi
ushauri wangu usijiingize sana kwa kumfikiria kuishinae pamoja kwani asipokuoa utaumia sana
pili kama ukipata mchumba aliye silias achana naye huyo anayekupotezea muda
tatu mjaribishe kuhusu kujitambulisha kwenu ili wamfahamu na ikibidi wamtambue ukiona anakataa ujue anakupotezea muda
nne mwambie yeye ni mpenzi wako na anatakiwa kuwa muwazi kwako
na mwisho kwa upande wa mawasiliano ukiona ni wewe tu ndio unapiga usipopiga anakaa kimya nawe amua kukaa kimya umuone ata akikupigia usimchangamkie jafanya kama huna taimu ili naye aumie kama naye hatajali ujue akupendi yupoyupo NA anataka kupoteze muda wako bure au kukutia tu akuache
Anonymous said…
Mhh!!!! hilo shushushu la Kimataifa dada na wala hana mapenzi ya dhati kwako. Mapenzi ya kweli hayachagui mtu wa aina gani, sasa huyo anataka mtu mwenye masters huyo hakupendi kama ulivyo anakupenda kwasababu unaelimu ungekuwa huna elimu usingekuwa wake.

Kula kona Dadaaa
Anonymous said…
hi dada walivyosema usinvest much on him. ww ni msomi jaribu kuwa mtafiti, But sidhani km apo kuna mapenzi mapenzi ni pande zote mbili na kuheshimu feeling za mwingine how come yeye yupo hivyo? mapenzi yako wapi? uyo sio future yako na hana mapenzi kwako kabisa.Sio ubavu wako na kumbuka mume mwema atoka kwa bwana.
Anonymous said…
mwombe Mungu tu kama ndie atakuwa wako tu haijalishi, mie dada yangu 35yrs sasa alikuwa na kiu ya ndoa akamwambia boyfriend wake sasavipi mbona sikuelewi, kumbe jamaa alikuwa bize na maisha kujijenga ndo alikuwa amepata kazi kama 2+ ndo anataka kwake papendeze,sister akazidi kumganda jamaa akamwambia nimekupa ruksa kama una kiu ya ndoa nimekuruhusu tafuta mume akuoe, hapo ilikuwa yapata uhusiano una zaidi ya miaka 7, sister alikata tamaa kabisa kuhusu huyo boyfriend wake mpaka ilipita miaka 2 ndo juzi tunashangaa huyo boyfriend wake ametangaza kumuoa jaman kila mtu anashangaa .
Anonymous said…
Wewe dada umeandika stori yako kwa ufundi na mtiririko mzuri sana.Your story is very interesting!! mimi nimenogewa hata nilitaka ingeendelea.

Nianze kwa kukupa pole na hayo yanayojiri katika dimbwi la mahusiano ya mapenzi. Kumbe wahenga walisema " kwako kukiungua basi jua kwa mwenzako kunateketea"

Kuna mambo mengi sana yakujifunza katika masuala ya mahusiano ya kimapenzi na hasa unapokuja katikasuala la kujua ni nini hasa unataka katika mahusiano hayo?

Ni muhimu sana kuweka lengo ambalo litakuwa dira ya kuelewa relationship unalolifakamia linafiti according to what you want/intend to achieve?

Kama huna plan yoyote basi utakufa na mapenzi na kukuletea msiba mzito sana.As far as I know, wadada wengi wanaingia kwenye mahusiano kwa mtazamo kwamba kuna kuolewa hapo.

Lakini imekuwa tofauti na wanaume kwani wanaume wengi mtazamo wao ni kufaidi ngono tu basi ndiyo penye tamaa yetu wanaume.

Kuoa si kipaumbele cha wanaume wengi walio katika mahusiano ya kimapenzi.

Kwa hiyo dada nakuomba kaa chini fikiri, tafakari juu ya lengo lako la kujiingiza katika mahusiano na huyo jamaa ni nini na nini unapata,then think of the future of your relationship, then come back to the reality what is going on right now, and how do you enjoy?

Usiteswe na kitu kinaitwa mapenzi!! Hasa ukijua kuwa hujaingia hasara yoyote kwa hilo, nikiwa na maana kwamba ni muhimu ujiachie huru na kitu kinachotesa moyo wako hasa kinachosababishwa na mtu mwingine asiyekuhusu kabisa katika maisha yako.

Ni afadhali uteswe na ndugu zako au wazazi wako waliokuzaa kuliko kuteswa na kupandikizwa na stress na mtu baki tu kisa eti mapenzi!!!

Wewe ni mdada mdogo tulia kabisa, mpe nafasi usihangaike naye tena fanya kama humjui wala hubabaiki naye.

Kusoma kupo na wala si maamuzi ya yeye juu yako bali ni maamuzi yako juu yako mwenyewe.Hapa nina maana mtu mwingine asikusinikize kufanya kitu fulani kwaniukifanya hakitanoga wala kuleta maana maishani mwako.

Utafikiri umesoma kumbe hukuelimika hata kidogo kwa sababu haikuwa ridhaa yako, kama jamaa yako ni mpelelezi ni kazi haina shida na wala hawezi kukuambia hilo ni kiapo kikubwa sana huko serikalini.

Lakini wewe chunga ustaarabu wako.Utakuja kujuta usipochukua uamuzi sasa.Usibembembeleze mwanaume utateswa sana naye.

Kuna siku utaambiwa na wewe sasa uoteshe mboo mara uwe na nywele kama za mumeo utayaweza hayo yote?Mungu akusaidie katika hilo.
Anonymous said…
story ni nzuri , ushauri wangu kwako dada ni kwamba usikate tamaa,kwani huyo jamaa kashaweka target zake za maisha hakuna atakae badili hilo ukimsikiliza nini anakitaka utafanikiwa,kwani kuna wengi wetu ndoa sio muhimu kama target zetu tulizozipanga hazijafanikiwa,just tulia msikilize anachokisema.Huyo jamaa ni mkweli ,hajakudanganya kabisa ,amemaanisha anachokisema.
Anonymous said…
Dada mie sizunguki! Kwa kifupi hapo hakuna mapenzi, Mimi ni mwalimu wa saikolojia na nasoma udaktari wa saikolojia ya mahusiano-US! Hakuna mahali mahusiano ya kweli yanakubaliana, wala kuelekeana na maelezo yako. Hakuna cha ushushushu, ambao hata...siku hizi mambo yako wazi tu, wali..bana enzi za nyuma, siku hizi ushushushu mzigo tu, tena ni matatizo dadayangu! Any way, kimsingi Hata ukiapa kufa, bado penzi la kweli halizuiliki! Penzi halina kanuni, penzi liko ranked highest among the naturally occuring behaviors in human being! Haliwezi kuzuiliwa kwa tabia za nje! Cant be controlled externally! Then, hakuna kitu kinaitwa privacy kwenye true love! Dada nakushauri kama mdogo wangu, chukua hatua mapema! Fikiri kuhusu maisha yako ya baadae!Usikubali maisha yako yawe pre-determined or determined by any other person under the sun except by you! sitaki uje kujuta mydr! Nataka siku moja ukumbuke blogu ya dada Dinna ilikusaidia! Na degree yako siamini kama hauko na vision yako ya maisha. Ebu uiheshimu. Sioni hata unachohitaji kuchunguza kwa sasa, kwani uchunguzi wa sasa utakuwa too artificial, ulishamjua siku nyingi, right now, uko na much more valid and reliable data,so its your time to analyse the man huku ukirefer kutoka kwa ushauri wa wadau! ILA MWISHO WA SIKU, UTAGUNDUA HUYO SIO MUME,kama ndio mpango wako, na WALA SI RAFIKI WA KIUME, ni MVULANA TU ANAYETAKA AKUTUMIE BASI MUDA WAKE UKIFIKA ATAJUA AMUOE NANI! Pole mdogo wagu!
Anonymous said…
Kwakweli Dada F hongera kwa kueleza uhusiano wako kwa kina. Maana wakati ulipo kuwa unajieleza umenipa picha ya watu wawili niliokutana nao nikatambua hapa na ambiwa toka lakini hakuna namna ya kutamka.

Urafiki kama huo lazima utajiisi mengi hadi utajikuta unashituka pasipo na sababu. F mimi ni binti wa miaka 23 kama wewe lakini niliyokutana nayo nilipoanza mahusiano katika umri wa miaka 18 nilijifunza jinsi mwanaume anavyoweza kukufanya ukajisikia wewe ni mdogo na tena huna maana.

Urafiki kama huu kama ukija kuishia unaweza kukutengenezea chuki kubwa sana. Unaweza kujikuta huna raha hata katika urafiki wako mpya.

Lakini mie nakushauri kama umeweza kuwa mvumilivu kiasi hicho naomba upige goti muombe Mungu akuonyeshe njia uliyomo kama ni sawa au la. Katika haya yote unayoyapitia Mungu anajua hata kabla huja omba walakini piga goti kupata kujua hili.

Lakini nakuomba uwe na uwezo wa kujibeba incase of anything.
Anonymous said…
jamani hakuna jambo zuri kama kusoma mshukuru mungu na watu wengine hawapendi mambo yao hasa ya uhusiano kuwa wazi na pengine huyo mwanume kajipanga kuwa anataka aoe mwamke msomi jitahidi usome juu ya usiri wake unatakiwa uwe makini sana.
Anonymous said…
mmmmmh my dr! nachelea kusema ila name yamenikuta kama yako japo si sana. napenda kukushauri kubwa zaid MUOMBE MUNGU CNA, pia simamia mipango yako ulopanga ifanikiwe, kuwa tayari kwa lolote zaid sana ukipata bf mwingne msogeze karibu ili uwasome nao kwan huyo siomchumba bal ni bf nikimaanisha hamjafika kipindi cha uchumba kwani hamjatambulishana nymbn. pia jaribu kufanya yako kwa asilimia kumbwa, wanaume wanatuzarau tu wanapoona kuwa ha2na mipango ya kueleweka na 2naruhusu kumegwa 2.
ila nna waswas naye nakushauri kujtengenezea manzingra ya kumweka hawara