Je anaweza kumsamehe Ba'Mkuu?-Ushauri.

"Dada Dinah mie nakuja tofauti kidogo. Nimekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Kijana mmoja kwa mwaka na nusu sasa. Nampenda na pia nadhani yeye ananipenda kwani huwa ananifanyia yote ambayo mimi nahisi ni kwaajili ya mapenzi yake kwangu.


Kipindi cha mwaka tumeishi pamoja baada ya yeye kuja na idea ya kusave ili tufunge ndoa mwakani, maana yake huku tunakosihi maisha ni ghali sana. Kwa vile ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuishi na mwanaume nyumba moja nikamuomba mpenzi ahamie kwangu badala ya mimi kuhamia kwake na akakubali.


Nilifanya hivyo kwa vile nilikuwa naogopa kunyanyaswa kama uhusiano wetu hautofika mbali. Namshukuru Mungu tangu tumeanza kukaa pamoja maisha yamekuwa mazuri ukiachilia migongano ya hapa na pale na kupishana kwenye baadhi ya mambo. Tumefanikiwa kusave kiasi cha kutosha kwa ajili ya kufunga ndoa kuanza maisha kama mke na mume.

Kitu cha kushangaza Mpenzi wangu hajawahi kuzungumzia wanafamilia yake, mwanzoni nilidharau tu kwa vile sikutaka kumkorofisha japokuwa kuna donge linanikaa rohoni nikitaka kujua kwanini hazungumzii familia yake wala kunitambulisha kwao kwa simu!

Huwa nafikiria vitu vingi sana juu ya mpenzi wangu huyu lakini kwa vile nampenda huwa najipa moyo maisha yetu ya ndoa ni kati yangu mimi na yeye na sio watu wengine. Siku moja nikaamua kukaa nae chini na kuuliza kama utani tu.

Mpenzi wangu alicheka alafu akaniambia, alikuwa anasubiri mpaka baada ya kufunga ndoa ndio aniambie ukweli kuhusu maisha yake lakini kwa vile nimeuliza basi atasema na lolote nitakaloamua basi ataliheshimu. Akaendelea kuwa yeye hana ndugu wala wazazi na alilelewa na baba yake mkubwa ambae alimtesa sana.

Nilimuonea huruma sana na nikatamani kumkatisha lakini pia nilitaka kujua mwisho wa story yake. Mpenzi wangu ilimbidi atoroke pale nyumbani na kudandia treni kwenda kijijini ambako kulikuwa na bibi na babu yake, alipelekwa shule na kufanikiwa kufaulu na kuendelea na Sekondari lakini baada ya tu ya kumaliza kidato cha nne Babu akafariki Dunia.

Maisha yalikuwa magumu kwani bibi hakuwa akifanya kazi na wala hakupokea msaada kutoka kwa baba mkubwa. Akaamua kuacha shule na kuanza kufanya kazi ya kulimia watu mashamba ili aweze kupata hela ya kula yeye na bibi.

Baada ya miaka michache kupita bibi nae akafariki na yeye akabaki mkiwa, hivyo akaamua kurudi Dar ili kutafuta kazi na kwa bahati nzuri alipata kazi kwenye Ubarozi fulani kama mlinzi. Akajiandikisha Chuo cha ufundi lakini masomo ya jioni na kujilipia mwenyewe. Alifanikiwa kumaliza na kufaulu, akiwa na kiu ya kwenda Chuo Kikuu aliomba Udhamini kutoka kazini kwake kwani gharama za masomo zilikuwa juu sana.

Boss wake baada ya kusikia historia ya maisha yake na kugundua kuwa hana ndugu akamdhamini akasome nje ambako ndio tumekutana. Baada ya kuniambia yote hayo nilijisikia vibaya na kujuta kwanini niliuliza, nilimuonea huruma mwanaume mzima kutoa machozi.

Nilipomuuliza kwanini hakuwa wazi tangu mwanzo? akasema hakutaka niwe nae kwa kumuonea huruma kutokana na maisha yake ya zamani bali niishi nae kwa vile nampenda.

Je! Ni sawa kama nitamshauri mpenzi wangu amsamehe baba yake mkubwa na kurudisha uhusiano?"

Dinah anasema: Nimepitia ushauri na maelezo ya wachangiaji na wamegusia vitu muhimu ambavyo natumaini umevifanyia kazi. Nakubaliana na imani yake kuwa hakutaka umuoenee huruma kutokana na hadithi ya maisha yake ya zamani ambayo inauzunisha na alitaka umpende.

Kuna watu wanajenga mahusiano na hata kufunga ndoa na kuendelea kubaki kwenye ndoa kwa vile wanawaonea huruma na sio kuwa wanawapenda. Nikirudi kwa past yake nadhani naungana na wote waliosema chunguza ili kujua ukweli na kama kuna ndugu (watoto wa baba Mkubwa'ke) basi unaweza k uanza kuzungumza nao bila kuwajulisha wewe ni nani (unaweza kujifanya ulisoma nae n.k) ili kujua ukweli wa mambo.

Kama asemayo ni kweli basi heshimu uamuzi wake wa kujiweka mbali na Mzee huyo (kama bado yupo hai) lakini jitahidi kutafuta namna ya yeye kurudisha uhusiano na watoto wa mzee huyo aliyemnyanyasa ili kuepusha watoto wao na wenu kuja kutengeneza mahusiano ya kimapenzi n.k si unajua Dunia ni ndogo hii.

Mimi binafsi sina uzoefu sana na matatizo ya kifamilia lakini nashukuru wasomaji wamekushauri vema kabisa.

Kila la kheri!

Comments

Anonymous said…
hamna sababu ya kuendeleza uhusiano na huyo baba yake mkubwa hakuwa na msaada kwake kwa nini ajitese kama walimtesa kipindi cha nyuma hana kitu basi wanaweza wakawa tayali hata kumuua kwa sasa kwasababu hana kitu. ACHANA NAO WW MLEE KM MZAZI WAKE SASA
Kizito said…
Haina haja ya kumsamehe huyo baba mkubwa. Kila mtu ana maisha yake sasa...cha muhimu ni nyie wawili kupendana, kufunga ndoa na kutengeneza familia yenu....

Kama huyo baba mkubwa angekuwa na nia njema basi asingeweza vumilia kumpoteza mtoto wa mdogo wake kiasi hicho....
Anonymous said…
Wewe dada una akili nzuri sana.Unafaa kuwa mke wa mtu kwani reconciliation unayotaka kuivalia njuga ni ya muhimu sana.Tena umeonyesha jinsi usivyoweka visasi.Huyo jamaa amepata wife anayefaa kabisa.

jambo lingine ni kwamba huyo ndiye atakuwa baba mkwe wako.Umefanya vizuri kuuliza na kutaka ushauri juu ya jambo hilo.Hakuna lisilosameheka kabisa.Pia hatuwezi kujua labda jamaa yako naye alikuwa na kaukorofi fulani kwa hiyo kusameheana ni muhimu sana ili undugu usipotee.

Pia naona umuhimu wake mwingine kwamba wewe unahitaji pia ndugu wa Mumewe wajulikane hamuwezi kuishi kisiwani licha ya kwamba mko nje ya nchi lakini home is home na ndugu ni ndugu.So please go ahead to talk with your husband to be kwamba njia nzuri ya maisha ni kusameheana hivyo amsamehe huyo baba yake mkubwa.

Kama hasemehe ni wazi kwamba hata wewe ukimkosea hatakusamehe.Mwambie utajifunzia kwa huyo baba kuwa atakuwa ni wa namna gani pindi mtakapoana.

Narudia tena kukupongeza kwa kuwa na mawazxo yenye busara sana.Kila la heri dada.
Anonymous said…
Stori kama ya kutunga vile!? Kama ni kweli basi umepata mume, hongera sana. Unachotakiwa ni kumpenda huyu bwana kwa akili na nguvu zako zote ili aweze kusahau yaliyompata. Upendo huvumilia, upendo huusudi, upendo husamehe, upendo... upendo.... ukimpenda atawasamehe wote waliomkosea na atakusikiliza maana wewe ndie baba, mama na ndugu zake. Kaa chonjo usijenyanganywa maana huyo ni mume kutoka kwa mungu.

Mdau MM
emuthree said…
Na vyema kama utamshauri hivyo, kwani kutokana na maelezo yake,huyo ndiye sehemu ya familia ambayo huenda imebakia, sijui labda wapo baba wengine.
Ni vyema ukamshauri kwani huwezi jua ipo siku atahitajika mzazi wa mumeo au ndugu wamumeo wa karibu, sijui kama na wewe itabidi udanganye kuwa hana ndugu?
Lakini kwa vyovyote iwavyo, kusameheana ni wajibu, hata kama umefanyiwa machungu kupita kiasi.Tusipende kuwekeana kinyongo,kwasababu kila jambo hutenda kwa minajili fulani, je fikiria kama huyu mpenzi wako asitendewa hivyo angefika hapo alipo. Kiimani tunaambiwa kama utakufa ukiwa hujamsamehe aliyekukosea unaweza usiione pepo. Huyu ni yule aliyekukosea(bado unatakiwa kumsamehe), sasa yule uliyemkosea itakuwaje, ina maana unatakiwa umwendee hata kwa magoti ili akusamehe.
Wewe kama mkewe ni mshauri mkubwa sana kwake, usichoke kumbembeleza ili afanye hilo,ila usimlazimishe,kwani yeye kama binadamu itafika mahali ataona umuhimu wa kufanya hivyo
emu-three
Anonymous said…
Pole sana Binti kwa hilo. Bali unaweza kumshauri ili aweze kumsamehe baba yake mkubwa kwani maisha ni kusameheana, na Pia iwapoi Mungu alitusamehe mengi sana na kutufia msalabani kwa ajili dhambi zetu basi nakuomba na wewe mshauri kwa kuongea nae taratibu na kupitia maandiko na Dini kwa ujumla ili aweze kukuelewa na aanze mawasiliana na huyo Baba yake mkubwa ili waweze kusameheana na kuanza maisha upya kama watu wazima sasa.
Anonymous said…
Mpe pole mpenzio, nimesoma mpaka nami nimelia, mpe moyo mliwaze.

Janie
Anonymous said…
hapo upime mama yangu we kwnai usije ukamlazimisha hadi na yeyey akakuona tena hufai maan unamletea machungu hivyo vitu taratibu kama yey hana habari fanya juhudi upeleleze kama hiyo stori nni ya kweli usijekuta huyu jamaa kakimbia familia?? wapo watu wa aina hiyo!! uwe mwangalifu ktk ushauri !! muulize tu kama huyo bamkubwa kama bado anaishi na wapi ili ufanye upelelezi mwenyewe kimya kimya!! wanaumeeeeeeeeee!! naona uchungu mama
Anonymous said…
Shosti naomba nikushauri kwa mitazamo yangu miwili.
1. Mapenzi ni mapenzi na yanahusisha watu wawili tuu, hivyo yeye kutokuwa na wazazi isikupe shida sana kwani hata wewe huna uhakika kama utakuwa na wazazi siku zote za maisha yako, ni vema pia umshauri amsamehe baba yake mkumbwa akikataa usimlazimishe sana muombe akupe japo chimbuko lao unaweza ukajua ndugu zake wengine kama binamu, wajomba nk ni vizuri kujua ndugu zake wengine nao wakujue pia. hatakama amepotezana nao mshauri na msaidiane kwa jinsi yoyote ile mpate mawasiliano.

2. Ni vema ukajaribu kuchunguza zaidi kuhusu maisha ya huyo mpenzi wako, kwani wako baadhi ya wanaume hupenda kutoa stori za kuhuzunisha huku wakificha mabaya yao, sio kwamba nataka kutomuamini mpenzi wako bali nataka uwe una uhakika kabisa wakati ukiwa haujaingia kwenye ndo kwani endapo utagundua mabo mengine baada ya ndoa utakuwa huna la kufanya bali kuvumilia.
Anonymous said…
Sikushauri umshauri arudiane na baba yake mkubwa! wewe hapo huna la ziada, ni yeye moyo wake ukimtume afanye basi sawa! alipotoka ni mbali, na usitake kumtonesha kidonda, mshauri tuu aendelee kusoma na kupata kazi nzuri watoto wenu wasiwe na maisha kama yake, na mshauri kumwalika aliyempigania kuja huko kusoma, hata kama hatokuja, ni kama asante. mpe sapoti, kuwa nae benet, usigusie jambo kuhusu familia yake! wewe ndo baba yako ndo babayake, hata pia familia yako isigusie kuhusu familia yake.
Anonymous said…
Heeeeeeee wewe dada una mawazo mema sana:

Ni kweli uwe mwangalifu kuna uwezekano mkubwa huyo rafikiyo kakupa tu hiyo story ili kukuwin.Sidhani kama hiyo ingekuwa sababu tosha kutokukuambia muda wote na watu mko kwenye serious relationship. Wanaume wengine wasanii kweli kweli.Inawezekana ameona umemuumbua hivyo akatafuta kisa hicho kupooza makali.

Ninaloweza kukuambia ni kwamba fanya chini juu upeleleze zaidi kama kuna ndugu wengine.Pia jambo la kumshauri kumsamehe baba yake mkubwa ni la muhimu sana.Usidanganywe na hao wanasema achaneni naye kila mtu ana maisha yake, hiyo siyo kweli binadamu tunategeameana sana.Kama alivyosema mchangiaji mmojawapo kwamba kuna siku ya siku mtahitajika kumtafuta ndugu atakayekuwa anahitajika katika mambo fulani ya mafanikio na mipango yenu halafu mseme uongo kuwa hatunaau mkachukua wa bandia akawachenga.Samehe nawe utasamehewa.

Dada yangu kumbuka kuwa mawazo yako ya katika jambo hili ni muhimu na mimi pekee nimekuona ni mtu wa pekee sana.Nikuambie kitu dada yangu, leo mumewe anaweza kuona amefanikiwa sana,lakini maisha ni safari ndefu mno ina mawimbi mengi, ina tufani nyingi, ina nyufa nyingi, wakati fulani yanafananishwa na maua yachanuayo leo na kesho hayapo.Kwa hiyo usipime mafanikio yako ya leo ukaona ndiyo utakayokuwa nayo mbeleni.Muhimu jiweke kwenye chati nzuri na watu, na ndugu nk.

Ipo siku ys siku haja ya kumtaka baba kama huyo itafika.Binadamu husameheana na kurudiana kwa sababu hakuna asiyekosa.na kama alivyosema mchangiaji mmoja inawezekana huyo rafikiyo ndiye alikuwa chanzo cha yote hayo ingawa hawezi kusema kwako peupe.Moja ya mafanikio ya mtu ni kupitia kwenye magumu kwa hiyo mapito yana faida na hivyo usichukie mapito hayo maana ndiyo njia ya mafanikio yako.Kusoma ni kugumu sana kwa mtu kama mimi niliyesoma kiwango kikubwa cha elimu yangu najua hilo.Lakini baada ya kumaliza unaona fulani na mafanikio makubwa,kwa hiyo sipaswi hata kidogo kuchukia kusoma.Hivyo mshauri rafikiyo amsamehe baba yake mkuwa kama Mungu alivyokuongoza kuleta wazo hili hapa ili upate ushauri.Usisikie mawazo ya wajeuri hao wanasema chunga maisha yako.hakuna mwanadamu anayejitegemea mwenye katika jamii.Upo kwa sababu watu wapo na watu wapo kwa sababu mtu yupo.

Mwisho nakupongeza sana kwa kuwa na utu wa namna hiyo.nakuona kuwa mdada mwenye busara sana.Mungu akusaidie sana katika hilo ulifanikishe.

Mdau Ughaibuni USA
Anonymous said…
MH
HUO NI MTEGO P'SE KUUTEGUA LAZIMA UFUNGE MKANDA, IWE ISIWE NI LZM UIJUE HISTORIA YAKE MAANA NAONA KAMA INAMISS HIVI AMETAJWA BABA MKUBWA TU, INAAMA YEYE HANA KAKA, DADA,BABA MDOGO,MAMA MDOGO,SHANGAZI,BINAMU NK SASA KWELI WATU WOTE HAO WASIWE NA MAELEWANO NAYE KAMA BABA MKUBWA, P'SE USIOGOPE KUMUUMIZA KWA SASA IMEKUWA STORY MAUMIVU YAKE SI SANA KAMA HAPO AWALI ENDELEA KUMUHOJI KWA INTERVAL ILI UPATE UKWELI, YOU NEVER KNOW AKIKUFIA SASA INAKUWAJE? THINK TWICE!! PATA UKWELI NA HIVI MMEANZA MCHAKATO WA NDOA, ONGEA HATA NA RAFIKI ZAKE LZM UTAPATA UKWELI HAKUNA SIRI YA KUFICHA UNDUGU ANAWEZA AKAWA NDUGU YAKO WA DAMU KUFICHA SI KUZURI HATA KIDOGO TAKE MDOGO WANGU, NAKUOMBEA MEMA KTK LIFE ULIYONAYO.
Mama T said…
Mwenzangu huwezi kujua huyo baba mkubwa alimfanya nini?Kama alikuwa akimnajisi sidhani kama jamaa atasamehe.Kama walivyosema wengine wewe fanya uchunguzi kuhusu watu wengine waliobaki kwenye familia yake kwani lazima baba mkubwa anawatoto.
Ila kama ingekuwa ni mimi wala nisingejali maisha yake ya kale ningeangalia ya sasa na kusonga mbele kwa kumpa mapenzi nakumfanya ajisikie kuwa ndugu zangu ni ndugu zake.
Anonymous said…
Mwanamke mwenzangu, samahani mimi najiunga na hili kundi la pili lenye mashaka na hadithi aliyokupa mmeo mtarajiwa. Kwa kweli sehemu kubwa ya wanaume hawasemi uongo, unaweza kuta mwenzio ana mke huku bongo anakutungia hadithi za huzuni. Mlazimishe, narudia mlazimishe uongee na huyo baba yake mkubwa kama bado atakataa lazima ipo namna. Anataka kusema kuwa ukoo wao ulikuwa wazazi wake, ba mkubwa, bibi na babu mwisho? Mbona haongelei mashangazi, wajomba, ma wadogo, binamu nk? Kwa maisha yetu ya kibongo extended families ndyo zetu asilete hadithi za kusema hana ndugu! MWANAMKE KATAA KUDANGANYIKA
Anonymous said…
mi hapa hataa,inawezekana kweli alikuwa na matatizo na baba mkubwa so what about other ndugu,hapana mdogo wangu,maisha hayaendi hivyo ,lazima ujue undani wake,kama alivyosema mmoja wa wachangiaji je bahati mbaya akikufia siombei ila kwa tahadhari mwenzangu utaanzia wapi wewe,basi hata majirani ,mi nina wasiwasi kuna kitu zaidi ya hicho.
Anonymous said…
kwa kweli hata mm naeza sema nna mashaka na huyo mumeo mtarajiwa coz haiwezekani mtu akawa na familia ya watu 3.sio kweli ndugu yangu funguka macho!ninachokushauri fanya uchunguzi wa kina kisirisiri huyo bwana kuna kitu anachokificha,inawezekana amekimbia familia(mke)ili kukupata ww kiulaini akaanza kukupa hadithi za magazetini au kuna kitu anachokitaka toka kwako thn akukimbie.so mdada kuwa na busara na mvumilivu mbembeleze amsamehe huyo ba ake mkubwa na akupeleke ili uwajue ndugu wa mumeo mtarajiwa ,huwezi jua kuna leo na kesho mtawahitaji hao ndugu. kinngine ni kwamba km atamsamehe baba ake amwangalie ana respond gani,km ataendelea kuwa km alivyokuwa basi ni wazi kuwa huyo baba an walakini so msijiweke nae karibu sn anaweza akawaharibia tn maisha yenu kwa hata kumuua ili kumiliki mali.ni hayo tu dada.bt nakusisitiza kuwa mwangalifu sn(makini)dunia imeharibika
Anonymous said…
Hata usijaribu kumwambia wapatane..labda huyo uncle wake ndio aje kuomba msamaha cause yeye hakuna kosa lolote alilomfanyia bali huyo uncle wake ndo mwenye makosa na hanashida yoyote kama maisha yake yapo sawa chakufanya wewe mwenyewe mueke karibu kiasi cha kwamba asijisikie mpweke ahisi wewe ndo mpenzi wake na wewe ndo ndugu yake..Hiyo itakuwa poa zaidi
Anonymous said…
HUYO LAZIMA ANA MKE BONGO!
CHUNGA NAMBA.
Anonymous said…
Yeah its too good to be true!

But lets give him the benefit of our doubts!

Hongera kwa kuwa mwanamke kamili! Jamani ee hawa wanawake wanatufaa sana; the way ulivyoelezea ni sawa na yaliyotokea in my family; mie ninashare baba na mama in both ways! Na kwa bahati mbaya huko nyuma sikuwa na good terms na my siblings haswa wale wa kwa baba! Huwezi amini mwenzangu ndio amekuja kuwa mpatnaishi mkuu! hatua ya kwanza aliyoifanya ni kuwa befriend wote wifiz na shemz na ikaishia hata sie tukaona aibu tukamaliza kuchuniana na tunawasiliana na kupeana habari! hivyo hili lako dada nakuunga mkono kwa asilimia mia ila nakuasa utumie hekima! kama baadhi ya wachangiaji walivyosema inaweza uwa cooked up story! ukitumia hekima utaujua ukweli! Na pia wewe unaweza kuwa ndo mpatanishi wao! Achana na nadharia za kizungu wanazokushauri wengine hapa kuwa as long as you have each other then basi! Hell no; Jamani waaafriak wenzangu haswa nyie mulioko hukoo out! Nanai asiyeujua utamu wa extended families! We acha tu hata siku ya harusi watu hulia machozi akimuuona shangazi wa mbali anavyopiga vigelegele! Achane mwenzenu aunganishe ndugu ndio faida za yeye kuingia kwenye familia mpya!
Asante na pole kwa kuwachosha!
Anonymous said…
dah mimi naona wewe ni mkarimu na wafaa kuwa mke wa mtu na upo tayari kuwa mama. kwani sioni jinsi mtu anaweza kuwa tayari kuwa mzazi wakati hayupo tayari kusamehe...nadhani ni vyema kuweka wazi mawazo yako kwake na atakalo amua iwe juu yake lakini wewe umeshaweka wazi kile kilicho moyoni mwako