"MAMBO VIPI JAMANI?
MIE NI MDADA WA MIAKA 29, NATARAJIA KUFUNGA NDOA HIVI KARIBU MUNGU AKITUJALIA TUNA MUDA WA MIAKA 6 SASA NA TUNAISHI PAMOJA KWASASA YAANI DADA TATIZO NILILO NALO NI HUYU MWANAUME ANAPENDA KUNUNA KWA VITU VIDOGO YAANI UKIKOSEA KITU KIDOGO ANANUNA NA ANAWEZA KUONGEA MANENO YA KASHFA MPAKA NAOGOPA YANI MIMI HATA SIJUI NIFANYAJE JAMANI ANAWIVU SANA YANI NIKIPIGIWA SIMU AU KUTUMIWA MSG KOSA UNAKUTA KANUNA MARA HANIAMINI YAANI MPAKA NAKEREKA YANI NI VILE BASI TU EMBU NISHAURI DADA NIMFANYAJE HUYU MTU JAMANI MAANA ANANIKWAZA MPAKA BASI."
Dinah anasema: Mambo poua tu mdada, hujambo? samahani kwa kuchelewa kujibu. Binaadamu tumeumbwa tofauti hali kadhalika ninyi wawili ni tofauti sana kitabia, kimalezi hata matakwa yenu ni tofauti natumaini hilo unalifahamu.
Huyu mchumba wako inawezekana hajiamini hali inayopelekea yeye kushindwa kukuamini wewe hasa unapopokea sms au hata kupigiwa siku, mara nyingi mtu mwenye au alikuwa na tabia chafu kupitia simu au hata Internet huwa anakereka "Kisaikolojia" (kwa vile anajua ndio zake au zilikuwa zake yaani anauzoefu fulani hivi ) na kuumia balada ya kuuliza kwa upole na upendo "ni nani huyo ulikuwa unaongea nae" au "nani amekutumia ujumbe.
Mmekuwa pamoja miaka 6, mnapendana na mnakwenda kufunga ndoa ili kuishi pamoja maisha yenu yote hivyo basi ni vema kuanza kurekebishana sasa. Natambua kila mmoja wenu anavijikasoro ambavyo havirekebishiki so u live with them na viji-habit vyake ambavyo vinarekebishika ikiwa mhusika atakubali kuwa anavyo na vinamkera mpenzi wake.
Nini cha kufanya:
Ni ngumu sana kuwakilisha issue hiyo kwake (Kwa wanaume wengi lawama zote anabeba mwanamke) hivyo unapaswa kutumia UANAMKE wako kuandaa namna/mazingira ya kuwakilisha issue, unaweza kutumia mapenzi ya hisia na mwili, unaweza kumromantisha (kumfanyia kitu romantic), unaweza kubadili mwenendo kwamba kila unapopokea sms unasoma kisha unamuonyesha au unaifugua karibu yake ili aione, na kama ni simu basi hakikisha unamhusisha.....MF-unaulizwa simuni, "unafanya nini" unaweza kusema nipo tu hapa na Mchumba/mwenzangu/mume wangu tunapumzika. N.k
Vilevile kama unajua kuna vitu vidogo vidogo vinamuudhi na vitu hivyo wewe ndio unaevisababisha basi unapaswa "kupumzika" yaania cha kuvifanya. Baada ya muda (wiki nne mpaka miezi 2) unaweza kuwakilisha tatizo lako kwake kwa upole na upendo, hapo hatoweza kukurushia lawama zozote kwa vile tayari ulimhusisha kwenye txts msg na simu unazopokea na ukaacha vile vitu vidogo vidogo vinavyomfanya anune.
Kule kwetu tunapofunzwa huwa tunaambiwa kuwa mwanamke ndio pekee mwenye uwezo wa kubomoa au kujenga nyumba yako (not exactly ila wanatumia hii ili wewe mwanamke ujue nafasi yako na kuwa mwangalifu kwenye uhusiano ili kupunguza matatizo), Pia kumbuka maisha ya kimahusiano na ndoa sio lelemama, yanahitaji kufanyiwa kazi kila siku.
Bibi yangu aliwahi kusema kuwa "kukitokea tatizo ndani ya ndoa jiangalie wewe kwanza na jirekebishe kabla hujaomba mwenzio ajirekebishe"RIP........alitumia kuomba rather than kumtaka mwenzio ajirekebishe.
Usitegemee mabadiliko ndani ya siku au wiki moja bali muda zaidi kwa kuwasiliana, kushirikiana, kukumbushana na kuongozana.
Kila la kheri ktk kuweka sawa hili na kwenye kufunga ndoa.

Comments
Mi naona uizoee tabia yake na uchukulie kuwa ndvyo alivoumbwa, huenda tbia yake ni inborn.
Mbona uktaka kla m2 awe kama utakavyo basi hutapata mchumba anayekufaa kwakuwa kla m2 ana kasoro. Basi jtahid kuyafkria yalyo mema anayokutendea kulko makosa. Hata ww una mapungufu meng tu ambayo mwenzio anayavmilia kwan wazan ww ndo huna kasoro kbsa. Hv wazan sifa zoote alizokuwa akhtaj mke wake awe nazo ww unazo? Sidhan!
Pia jiangalie huenda huwa unafanya mambo meng yanayomtia hofu ndo maana ana wivu! Usipende kufanya mambo mengi kwa siri kama vle kupokea cm c lazma ukaongelee pembeni au meseji co unasoma tu na kuifuta hapohapo kwan hvo n v2 vtakavyomtia shaka.
Fungeni ndoa haraka sana ili muepukane na zinaa.
Mwatima
Kununa ni moja ya njia ya udhaifu wa kuonyesha kuwa kuna jambo limetokea ambalo hulipendi. Ni njia ya udhaifi kwasababu kuliko kununa unatakiwa useme kuwa kwaweli hili mwenzangu umeniudhi naomba iwe hivi, na wapenzi wanatakiwa wasichoke kuelezana ukweli, na kuelezana huku kuna mahali pake jamani!
Njia ya kulikwepa hili ni kujaribu kutokufanya kile kinachomuumiza mwenzako, na ukitaka kukifanya mueleze mwenzako kuwa nataka kukifanya hiki kwa sababu kadhaa.Na ni rahisi kwa nyie wanawake kumweka sawa mwanaume wako akakubaliana na unachokitaka,kama kweli unampenda na kumjali.
Kuhusu wivu, hii wengi tunasema ni sehemu ya mapenzi, ila tunatakiwa wivu usizidi sana.Hivi wewe utajisikiaje kama unafanya vitu viletavyo wivu na mume, au mkeo hakuulizi? Hapo kutakuwa na walakini, huenda jamaa hakuthamini tena,au ndio zake!
Kuna wivu mzuri na wivu mbaya,na wivu mzuri ni wakujenga pendo, kuwa usiibiwe au mwenzako asiende kinyume na taratibu za mapenzi au ndoa yenu.
Kwaushauri wangu, usijali hali hiyo ya kununa, wengi wa wanaume ambao sio waongeaji sana wanatabia hiyo, na wivu ni sehemu ya upendo, jamaa anakupenda muno ndio maana anawivu, anaogopa asije akaibiwa. Cha muhumu ni kutokuzidisha yale asiyoyapenda na muonyeshe kimpenzi kuwa yeye ni yeye peke yake, na hiyo iwe kweli usije ukawa unampaka mafuta kwa mgongo wa chupa kwani akigundua,huko kununa kutatoka nje na watu wa namna hiyo wanaweza kufanya jambo usilolitegemea.
SHOSTISHO WA MBAGALA ZAITUNI
Cha msingi ni kujaribu kuepuka kufanya kile ambacho kitamkwaza coz kama ni kumsoma umeshamsoma.
au yeye akitumiwa msm/simu na wanawake unatajisikiaje? kama simu/sms sio za mapenzi uwe unashea nae kwani vipi? si mnakua mwili mmoja, mtiana, mnanyonyana n.k. sijui kama kuna siri zaidi ya hayo. Kama unataka maisha ya furaha na ndoa yako jirekebishe, uishi maisha ya mke wa mtu na sio kama ya mwanamke ambaye bado anatafuta soko!!
Mdau M2
Naomba nikukumbushe kwamba umeamua kuishi na huyo mwenzako! Kitu kikubwa ni kwamba lazima uvumilie tabia ya mwenzako,kama unampenda na ukakubali kuishi naye basi ndivyo alivyo.Vilevile lazime unikubalie kwamba naye haridhiki na tabia yako anakerwa lakini anajaribu kuvumilia. Ukweli ni kwamba hawezi kuwa unavyotaka hata kidogo, na pia huwezi kuwa anavyotaka.NDOA NI KUVUMILIANA! Kazi unayo dada yangu, Pole sana!
KWANZA BADIRISHA LINE YA SIMU INAWEZEKANA BADO KUNA WATU AMBAO WANAKUTOGONGOZA SANA KUPITIA SIMU YAKO.
USIPENDE KUMPA KILA MTU NAMBA YAKO YA SIMU KUNA WATU WENGINE WANAPENDA SANA KUBOMOA KULIKO KUJENGA.
MAANA INAWEZEKANA KUNA SIMU ZA UTATANISHI AMBAZO UNAPIGIWA UNASHINDWA KUZIJIBU VIZURI UKIWA NA MCHUMBA YAKO HUYO.
MWAMBIE KILA KITU CHAKO CHA KUHUSU UHUSIANO WA ZAMANI HUYO MCHUMBA WAKO USIMFICHE KITU.
MSIKILIZE ANACHOKUELEZA NA USIPENDE KUWA MBISHI WA KILA KITU AU KUJUA KILA KITU HAPO LAZIMA ATAKUTILIA MASHAKA TU.
NI HAYO TU.
NI MTAZAMO TU WAPENDWA.
Kwahiyo akina mama ambao yanawakuta hayo, tafuteni njia ya kuondoa huo ugonjwa. Kukaa kimya nakudharau kutazidisha nakuleta mengine. Ujue huyo ni mume wako, na kinachomuumiza yeye hata ukae kimya lazima kitakuathiri kindani-ndani, `kwanini kwanini' huko kujiuliza kunajenga `presha'
Najua wengine watasema kwanini kumdekeza, unampa kichwa nk. Hapana, huyo ni mtu wako, na ni mtu mzima, utakavyomtendea mema(yale anayoyataka), itafika muda na yeye atajiuliza na kujiona amekosa. Na hapo ndipo pakuelezana ukweli(unajua mume wangu hivi na vile bla-bla, nakupenda, ningependa iwe hivi, dume hoi. Jamani siri ya wanaume ni ndogo, lakini mnashindwa kuitumia. Acheni kutegeana au kuwekeana visasi).
Mimi ni hayo tena
emu-three
me ni mwanaume naishi na mchumba angu but sikai san nyumbani bse ya kazi za site.naweza kukosekana home kwa mda hata wa mwezi mzima.sasa basi ukirudi home we unakuja na hamu na mke na umepamiss home ila unakuta mke yale maneno alokua anyazungumza kwa simu kwamba ur missing here honey hayana ukweli wowote yani ni WORDS WITHOUT MEANING,
anarudi kutoka kazini ye ndo kwanza anaanza kuchat ukiuliza we vp? majibu ooh hawa ni mashoga zangu tulikua nao kazini ndo nachat nao!
mwanamke hana mda wa kukaa nawewe MKAPANGA HATA MIPANGO YA KESHO NA KESHOKUTWA full yuko busy na simu kama mwanafunzi alonunuliwa simu jana.tukisema ooh mwanaume una gubu,me ananikera n.k.Asikwambie mtu LAZIMA UHESHIMU UWEPO WA MUME HOME.
If you think anakukera na umeshinda kulitatua hili, pls dont go for marriage itakusumbua sana bse utakua huaminiki hata kidogo bse alishaanza kukutilia shaka toka mwanzo ama show/prove to him kwamba simu yako si kwa ajili ya kumcheat ili awe na amani, akuamini hata kama ukiongea na simu ajue ni mambo ya Amani kwa ndoa yake.
Be a woman to your husband not a competitor kama vile ni mke mwenza.
Anonymous wa 12:01:00 AM i like your comments.