Mimi nimeolewa miaka 25 iliyopita na nina watoto wakubwa tu, lakini kutokana na shughuli zangu nyingi za kikazi sikuwa na muda wa kuipa Ndoa yetu attention na matokeo yake tukawa tunaishi kama mtu na flatmate wake.
Mimi nikienda kulala mume wangu anaendelea kufanya shughuli zake kwenye Comptuter au kuangalia TV, yeye akiwa amelala mie nakuwa macho nikifanya shughuli zangu. Maisha yetu yakawa hivyo kwa muda mrefu sana.
Ikafikia wakati nikawa nakosa the attention kutoka kwa mume wangu lakini yeye akawa hajali kabisa, mwishowe nikaamua kujiunga na dating site ya wanandoa ambao wako bored (nilipewa habari na co-worker hapa kazini). Huko nilikutana na wake kwa waume na wote ni wanaume na wake zao nyumbani.
Nilikuwa muoga lakini baadae nikawa nafurahia attention kutoka kwa wanaume hao kupitia emails na hatimae nikaamua kukutana nao moja baada ya mwingine na nilikuwa nafurahia sana jinsi walivyokuwa wakinijali na kunipa the attention na sifa lukuki nyingine hata mume wangu hakuwahi kuniambia.
Kwakweli nilibadilika na kuwa mwanamke mwenye furaha sana na nikabadilika kimavazi kwani zile sifa zilinilevya ukizingatia wengine walikuwa wakiniambia nikivaa magauni ya hivi napendeza zaidi na umbile langu linaonekana vizuri zaidi, basi mie nikawa nanunua nguo kwa mitindo hiyo ili kupendeza zaidi kwa nje na kujisikia vizuri kwa ndani.
Pamoja na kukutana nao hao wanaume kwenye dates sikuwahi kushawishika kufanya nao ngono, siku zote niliishia kuongea kuhusu maswala ya kimaisha, matatizo ya ndoa zetu, wale wanaume waliokuwa wakijaribu kutaka kwenda zaidi ya maongezi mara nyingi nilikuwa siwapi nafasi ya kukutana na mimi tena na wala sikuwa nikiwajibu.
Kwa bahati mbaya Rafiki wa Mume wangu alijiunga kule na ndio ukawa mwisho wa maisha yangu ya ndotoni kwani aliliona profile langu na moja kwa moja akaenda kumueleza mume wangu. Mume wangu alikasirika sana na tukagombana sana siku hiyo, lakini mie nikamuambia mume wangu kuwa yeye ndio chanzo kwani alikuwa akiniona kama vile fenicha ndani ya nyumba, nimpikie, nimfulie, nimuandalie mahali pa kulala na yeye anachofanya ni kula, kulala, kwenda kazini nakurudi.
Mume wangu akaondoka kwa hasira huku akisema tunahitaji kupeana nafasi na atakuwa Hotelini, mume wangu tangu atoweke hapa nyumbani hajaongea na mimi bali watoto wake wetu tu ndio anaongea nao na huenda kumtembelea huko hotelini. Watoto wetu hunipa habari baba yao anaendeleaje.
Dinah mdogo wangu, mume wangu nampenda sana japokuwa alikuwa nakasoro zake na kweli nilijibu kwa hasira nikidhani kuwa atakubali kosa na kunipa nafasi nimueleze ukweli wa ile dating site, lakini hakunipa nafasi hiyo.
Namtaka mume wangu kuliko nilivyokuwa nikimtaka mwanzo, sasa ni heri niwe nae nyumbani na sipati attention kuliko kukosa vyote. Yeye simuoni na attention haipo mara saba zaidi.
Naomba wanablog na Dinah mnipe ushauri ili mume wangu arudi nyumbani."
Dinah anasema: Habari ni njema tu Mama Samirah, asante kwa mail yako. Natambua pea nyingi sana hujisahau au niseme husahau kuwa kuna uhusiano wa kimapenzi ndani ya ndoa yao mara wanapozingwa na shughuli nyingi za kikazi.
Kutokana na maelezo yako nimegundua makosa mawili, Mosi ni uamuzi wako wa kumsaliti mumeo na kwenda kukutana na wanaume wengine, haijalishi kama uliwapa mwili (ngonoana) au la! Muda ulioutumia kwenda kutafuta, kujiandikisha na hatimae kuwa unakutana na hao wanaume nje ya ndoa yako ndio muda ambao ulipaswa kuutumia kurudisha romance ambayo ingeokoa ndoa yako.
Pili ni kumsukumuzia mzigo wa lawama yeye mumeo wakati unajua kabisa kuwa wote wawili mlijisahau au mlikuwa mnategeana au oengine mlikuwa mnadhani kuwa mmekuwa wazee kupeana attention kama wapenzi.
Badala ya kumuambia kuwa yeye ndio chanzo ulitakiwa kumuomba msamaha kwani wewe ndio uliyemtenda mwenzio, hata kama alikuwa hakupi attention bado alikuwa anakuheshimu na kukuthamini na kutumia muda wake nyumbani.
Ni wazi kuwa Mumeo amehama hapo nyumbani baada ya kugundua kitendo chako ili kupata nafasi ya kufukiri kabla hajafanya uamuzi kwa faida yake na watoto wenu, sasa unachotakiwa kufanya ni kama ifuatavyo:-
Mosi, ni kuomba msamaha kwa kumsingizia kuwa yeye ndiye aliyesababisha wewe kuibua tabia chafu na kumsaliti. Kama alivyoshauri mmoja kati ya wachangiaji, unaweza kutumia Kadi, Emails au barua (kizamani) ambayo actually siku hizi ni more romantic kuliko emails na Kadi. Hakikisha unaandika maneno yako kutoka moyoni na sio kuCopy na kuPaste kisha unaPrint.
Pili, kubali kuwa ulikuwa mjinga, mbinafsi na mwepezi kushawishika kirahisi na kufanya ulichokifanya, jutia kosa lako na kubali lawama zote ikiwa atazitoa juu yako (kumbuka you want him back ukianza ubishi utakuwa unamuongezea hasira)
Tatu, wakati unakili kuwa wewe ndio wa kulaumiwa, tumia nafasi hiyo kusema ukweli kuhusu kile ulichokuwa unakikosa lakini pangilia maneno ambayo hayatamfanya ajisikie alikuwa kajisahau (again, kumbuka wewe ndio unamtaka Mume asikutaliki hivyo kuwa mwangalifu), Mf: badala ya kusema kuanzia sasa tupeane attention.....unaweza kugeuza kibao na kuahidi kuwa utajitahidi kugawa majukumu na muda wako kati ya kazi na yeye n.k
Nne, kamwe usizungumzie wanaume wangapi umekutana nao na wapi mlikuwa mkikutana au nini walikuwa wakikuambia. Lakini ikiwa atataka kujua kama ulifanya ngono nje ya ndoa yenu basi sema ukweli (hapa umesema hukukutana nao kimwili) mhakikishie hilo kwa kusema wazi hisia zako juu yake, namna unavyomthamini kiasi kwamba huwezi kutoa mwili wako kwa mwanaume mwingine yeyote, sema hakuna mwanaume yeyote anaestahili mwili wako bali ni yeye mumeo na mengine yote ujuayo kuhusu kumfanya mwaname ajisikie Safiii!
Tano, mpe muda wa kufikiri mara baada ya kumuomba msamaha na kumueleza ukweli. Usilazimishe aje nyumbani haraka na badala yake muonyeshe namna unavyompenda kwa vitendo zaidi (kumbuka ahadi ulizompa), hakikisha yote uliyosema unayafanya kwa vitendo.
Kuwa mvumilivu kwani haweza akaamua kukusamehe na kusahau hapo hapo, atahitaji muda. Pia kumbuka kuna mtu wa tatu hapo anahusika ambae ni rafiki yake. Huyu rafiki (inategemeana na urafiki wao) anaweza akajenga au kubomoa ndoa ambayo tayari inaufa.Hivyo basi, kama unauhakika kuwa huyu rafiki ni wa Damu basi unaweza kumtafuta huyu Bwana na kumueleza ni jinsi gani unampenda mumeo na watoto, ni namna gani ungepeda ndoa yenu iendelee kuwepo. Mwambie ni vipi unajisikia vibaya kwa kitendo ulichokifanya kwa rafiki yake ambaye ni mumeo, Weka wazi hisia zako za kimapenzi kwa mumeo mbele ya huyu bwana.
Hii itasaidia sana kufikisha ujumbe kwa mumeo ambao utajazaia yale uliyokwisha mueleza mumeo, hasa ukizingatia yeye ndiye aliyepeleka ujumbe wa dating site.
Baada ya hapa, watumie watoto ili kupata date ya familia ikiwa ni pamoja na baba yao, watoto siku zote wanapenda baba na mama kuwa pamoja hivyo haijalishi ni uchafu gani umefanya na utawaumiza lakini kama nia ni kurudiana watoto watasaidia kwa kiasi kikubwa sana kufanikisha hilo.
Kwa sasa nikuachie hapa ili ufanyie kazi Ushauri wa wachangiaji wengine na ule kiasi niliokupatia live kwenye radio siku ya Kipindi.
Kila la kheri.
Comments
Ni mimi Mama Moses, Dar
Ukiangalia maelezo yako, utagundua wote mliamua kujenga hamnazo, kuishi kizungu,ambapo mnaweza mkawa kila mtu na chumba chake au kitanda chake. Hii sio vyema, mlivyofanya kwenu nyote.
Wewe umezidisha zaidi ubaya kwa kujiunga na huo mtandao wa kutafuta wenza, ilihali unaye ndani, tatizo ni kutokuwasiliana na kuambizana ukweli. Kwani uliwahi kumuomba kuwa sasa mwenzangu nakutaka akakutolea nje? Uliwahi kukaa naye kikao cha maongezi na kuelezana matatizo yenu? Hakuna.
Kosa kubwa tunalolifanya wanandoa nikutokuwa na mawasiliano. Utakuta mtu ni bosi ofisini kabla hajaanza kazi anawaita wafanyakazi wake wanakaa kikao, na kuweka mipangilio ya siku, au ya mwezi, lakini akifika nyumbani kila kitu shangalabaghala.
Mimi ushauri wangu, tafuta mbinu za kumuomba msamaha, mtumie meseji, au hata ikibidi rafiki wa karibu kuwa unataka maongezi naye, na wewe hakikisha umejikwatua vyema akija home au huko mtakapokutana. Muombe msamaha na mueleze ukweli. Hakikisha unanyenyekea, siunajua tena kubembeleza. Akikusamehe, basi siku kadhaa, jenga tabia ya kumuomba faragha, muongee hiki na kile kuhusu mipangilio ya shughuli zenu, kuwa isiingilie `haki za ndoa' Au?
emu-three
Mwenyez Mungu anasema Yote yanayotupata ni vchumo vya mikono yetu. Kwa hiyo uyapokee kwa mikono miwili kwakuwa umeyachuma mwenyewe!
USHAURI . Muombe msamaha kwa dhati acha kjifanya mjanja na hali ni mkosaji tena mpumbavu mkubwa! Ckutukani ila biblia ndo inasema kuwa mwanamke mpumbavu hbomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe, kama ulvofanya wewe! Mpigie magoti maana ulichofanya ni usaliti mkubwa! Tena omba radhi kwa Muumba wako. M2 mzima lkn mambo ovyo, USIRUDIE UPUMBAVU HUU! Kumbuka kumuabudu Mungu kunasaidia, maana kama ungekuwa unamwabudu hungefanya upuuzi huo,Eti dating site! Ndo nini!!
Mwatima
Je unadhani wewe ni mtu msafi sana?? Kama Mungu angeamua kuhesabu makosa yetu nani angebakia kutokuhesabiwa kosa huku duniani? Mimi nakuona bado ni mtoto mchanga unayenyweshwa maziwa tu.Nimekuwa nikisoma comments zako mara nyingi umekuwa ukiongelea sana habari za kumtii Mungu lakini cha ajabu unachanganyaq mno mambo.Huyu mama ameomba ushauri tena wa majuto kwa kosa alilolifanya ili asaidiwe, lakini wewe badala ya kumshauri kitu cha kufanya unamtwika matusi makubwa utafikiri kakuibia kitu wewe.Pia hujui chochote maana ya blog hii kuwa hapa na hata huyu muomba ushauri hujamsaidia kitu umebaki kumsakama na matusi tu wala hujui ulihitaji ufanye nini.Usichanganye mambo yako binafsi na mambo ya mahala hapa.Nakushauri usome kwanza makusudi ya bloger huyu kuiweka blog hii hapa.Ikiwezekana anzisha tovuti ya kwako itakayokuwa inazungumzia maadili ya kidini.Umepotea njia mkristo gani wewe kila mtu unamswagia matusi tu??hata Yesu alikufa kwa ajili ya wenye dhambi sembuse wewe???
Cheeting inayomuumiza zaidi mwenzi ni ya emosion kuliko hata vitendo. Haswa pale mwenzio akigundua na kukumbuka yote uliyokuwa ukimwambia kwamfano yakuwa unampenda sana. Na akifikiria hilo anajihisi yakuwa amedanganywa kwa muda mrefu kwani alikuamini.
Mara nyingi sisi wanawake tumekuwa tunajitetea kusema tunahitaji atension wakati sisi hiyo atension hatutoi. Je kwa kweli tunaitaji kuambiwa kila siku tumependeza au ni wazuri ili kuweza kuhishi kwa furaha. Je tuko tayari kuharibu ndoa zetu na heshima kwa watoto wetu punde tu atakapotokea mtu na kutuambia yakuwa tumependeza? Je unafikiri kweli hao waliokwambia yakuwa umependeza walikuwa wanakuambia ukweli au walikuwa wanatafuta njia ya kutafuna kitumbua chako tu.
Wanaume wengi wanaamini yakuwa wakimwambia mwanamke kuwa yeye ni mzuri sana na anapendeza basi wanakuwa wamfungua njia ya kutafuna kitumbua na kweli imejithihirisha mara nyingi.
Muombe mumeo msamaha na kwa kweli naomba wakati unapofanya hivyo usitamke neno kama "nia yangu haikuwa kufanya ngono bali attension". Kwani wewe unafahamu fuka kuwa hiyo haikuwa nia yako.
Unawezaje ukamhukumu mtu katika jambo ambalo yeye hajakuambia alilifanya?Na unapata faida gani kumwongezea mzigo mwingine ambao hahitaji na wala hajawahi kuubeba?
Hebu kueni wastaraabu mnapokuja kwenye tovuti hii kusoma na kushauri watu!!! Inakuweje mnajitwika mihasira isiyowahusu hata kidogo.mtu anaomba ushauri kwa kujutia kosa alilolitenda ili atafute ufumbuzi wa kina kurejea katika katika mahusiano na mumewe watu wanakuja kumponnda na kumtamkia hata yale ambayo hakutenda hivi inawasaidia nini mkifanya hivyo?Hamwoni kwamba sasa ninyi ndiyo mnaingia kwenye upotofu zaidi kuliko hata yule muomba ushauri.
Eti hukufikia tu kwenda out hata ngono ulifanya!! Je, ulikuwepo na uliona hayo??? kuweni wastaarabu jamani fanya kile kinachohitajika maadamu mtu amejitokeza na ameeleza yote ya nini wewe kuanza kumkosoa wakati amejikosoa mwenyewe.Wewe mpe ushauri wa namna ya kuondoa doa hilo basi!!!
Ni matusi yapi nliyotukana?. Neno pumbavu sio tusi, je unajua kswahili ww? Au umedandia gari kwa mbele?
Hata hvyo kufa kwa Yesu kwajili ya wenye dhambi haikuwa tketi ya ww kuwa huru ktenda dhambi.
Na pia mimi c msafi sana kama ulvosema! Mimi nlikuwa nawakumbusheni 2 ktk yaliyo mema. Pia kumbuka ya kuwa kla mmoja ni mchunga na ataulzwa juu ya alichokchunga! Na wala haimaanish kuwa mchunga ni msafi kwani naye ni mwanadamu.
Nisamehe sana mama yangu mpenzi na wanablog wote nliowaudhi, kwani ni dhahiri na ni kweli nmetumia lugha kali sana isiyopaswa ku2mia ktk ushauri. Nilipitiwa na kusahau kuwa naandika kama mshauri na baadala yake nkaandika kama Mtendewa[ mumewe], nkajikuta nimepata hasira kali as if mke wangu kanitendea. I regret 4 what i iv done and please my dear blogers na mama ambaye cjamtendea haqi.
Pia nashukuru kwa chalenji zenu kwani nmejfunza k2 muhimu sana!. But kosa ulilolifanya ni kunponda na kunfukuza baadala ya kunielimisha. Tazama, nami cjawa na mwenza hivyo cjakumbana nayo haya nami cjajua ugumu wa ndoa. But nashukuru pia kwa wote walosema nkue niyaone, kwani mmethbtisha dhahir kuwa nlofanya n kutokujua haya. I appriciate ur challenge and its ma duty kujrekebisha.
Thanx all, Wasaalam
Mwatima
D'hicious inaamini ktk kuboresha mahusiano na sio kubomoa, hivyo basi natambua kuna baadhi ya wachangiaji wanashindwa kuzuia harira zao ikiwa kunatokea suala la usaliti wa mapenzi/ndoa.
Samahani kwa kuto hariri (edit)baadhi ya post kutokana na ufinye wa muda unaosababishwa na uwingi wa shughuli.
Neno Pumbavu sio mara zote linatumiwa kama tusi, wakati mwingine linaweza kutumiwa kama "mjinga" au "hamnazo". Mf- acha upumbavu wa kufuatilia maisha ya watu n.k
Kama ilivyo "mshenzi" linapotumiwa kama sifa....Mf jamaa anajua kuimba kishenzi au ninampenda kishenzi n.k.
Malaya ni tusi ikiwa mhusika hana tabia hiyo ya kungonoana na wanaume/wanawake wengi tofauti.
Hatumjui mhusika aliyeuliza swali hivyo hatuwezi kumhukumu kuwa yeye ni malaya kwani hatujashuhudia hilo.
Asante wote kwa ushirikiano.
Thanx Dinnah, i appriciate ur work. Kwa hakika ni njema, japo kuna sehemu huwa unakosea lkn ni makosa ya kbinadamu tu. Otherwise I acknowledge ur work kwakuwa ni njema, ndoa nyingi tumeshudia zikirudi kwenye track yake kupitia d'hicious. Hongera. Wasalaam!
Mwatima
Baada ya yote hayo utaona mabadiliko yakiingia taratibu moyoni mwake. So ni jnjia mwafaka kwa wewe kuwatumia tena watoto kujua ni hotel gani yuko room no ngapi nk. Ukishajua jitahidi ujue mda wake wa ziada na ratiba zake. Ukishayajua yote hayo yafanyie kazi ipasavyo. Nenda bila taarifa mpaka pale onana nae pasipokumtaarifu ukiwa katika mavazi, pafyumu, mtindowa nywele ule aupendao. Jiweke katika utayari wa kukabiliana na lolote lile toka kwake. And please kuwa chini. Zungumza nae kwa utulivu zaidi lakini kwa kujiamini. Kuwa na hoja na msingi ambazo hazitamfanya akuchukie zaidi. Mweleze jinsi gani unammiss, unampenda, umejuta kuwa mbali nae kwa mdawotehuo. Utamwona mwelekeo wake we unamfahamu zaidi ukimwona kalegea tu hapohapo kitu na box usimpe nafasi fanya yale ulomfanyia siku ya kwanza mlipoanza ku do. Then majibu utayaona.
Ma Jonny.
Mza.
Kutokana na uzito wa maisha ya sasa na bado sijafikiria kuoa huwa napendelea zaidi kuvisit internet dating ili kujiliwaza na huwa natafuta haswa wanawake walio katika ndoa zao (kwani hawawezi kuning'ang'ania baadae), walio na matatizo na wapenzi wao(kwani ni rahisi zaidi kuwadanganya) na inakuwa rahisi kwangu kufanya nao tendo la ndoa kukizi mahitaji yangu na baadae siwi na string atached. Kwa njia hii nimeweza kufanikiwa sana.
Hayo ni maisha ya sasa na wanawake wengi pia nilioshawai kuzungumzanao wapo ambao wanapendelea sex tu na hakuna kufuatana fuatana na commitment haswa hapa ugaibuni.
Kwa kuwa umekiri ya kuwa unampenda mumeo, ni vizuri ukaongeza nguvu zaidi kumuonyesha yakuwa bado unampeda kuliko kutafuta maliwazo nje kwani huko ni kumfanya awe mbali zaidi na wewe. Mkaribishe nyumbani katika shere za watoto kama birthday na umuonyeshe ya kuwa hapo ndipo anapobelong. Natumai yakuwa mlishawahi kupata matatizo mengine ya kindoa huko nyuma na kufanikiwa kuyatatua. Hivyo hata hili linawezekana.
asante