Yaani hata sielewi nimjibu nini huyu EX-Ushauri

"Shikamoo dada Dinah, natumai wewe ni mzima wa afya na unaendelea kutusaidia sisi wenye matatizo mbalimbali ya kimapenzi. Hii ni mara yangu ya kwanza kuomba msaada kwako japo nimekuwa nikisoma article zako mbalimbali kupitia blog yako na kuona jinsi unavyosaidia watu mbalimbali.

Mimi ni msichana mwenye miaka 22, nipo masomoni nje ya nchi. Kabla sijaondoka hapo nyumbani nilikuwa boyfriend ambaye tulikutana kwenye pilikapilika za kimasomo (tuition). Sikuwa na uhakika kama kweli ananipenda lakini nikajikuta nimeanza nae urafiki na hatimaye kukutana kimwili.


Kwa nilivyouona uhusiano wetu nilihisi kama alitaka kuwa na mimi sababu ya uwezo wa kifamilia tulionao na si mapenzi sababu alikuwa na maisha ya kawaida sana (samahani kwa kutumia neno kapuku) na mara baada ya kufanya mapenzi nae alianza kunitreat tofauti na mwanzo. Hata nilipomwambia naenda kusoma nje hakurespond kama nilivyotarajia kwani hakuonyesha dalili ya kujali. Kwakifupi ilikuwa kama tumeachana japo hakuna alietamka.


Mara baada ya kufika huku nikamtumia namba yangu ya simu na tukawa tunawasiliana hadi niliporudi likizo yangu tukaendelea kama kawaida japo hali ya yeye kupenda kufanya mapenzi kila tukutanapo haikuisha. Alitaka tukutane kila wiki (ilifika kipindi hata nikiwa kwenye siku zangu alitaka tufanye na nikimgomea inakuwa ishu).


Niliporudi huku tuliendelea kuwasiliana tena kwa muda baadae akakata mawasiliano, nami nikaamua kukaa kimya nimuone atafanya nini lakini ndio akawa kimya moja kwa moja. Nikajua ndio tumemalizana.

Baada ya kuona kimya hicho nikaamua kuanzisha uhusianio mwingine na mtu mpya ambaye hakuwa mTanzania. Nilikuwa nae kwa mwaka na tulikuwa tunaendelea vizuri hadi alipo graduate na kwenda kwao na sitegemei kukutana nae tena.

Nilikaa kwa mwezi mmoja nikaanza kuwa na uhusiano na mvulana mwengine ambaye ni Mbongo mwenzangu. Najua dada unaweza kuniona somehow kicheche lakini naomba unisaidie maana nimechoka kubadili wavulana na tatizo langu kubwa siwezi kujizuia hasa mvulana akiwa mzuri.

Huyu mbongo nilienae sasa nilisoma nae O-level huko nyumbani. Kiukweli ni mzuri na historia yake ya nyuma alikuwa kigongo hasa kwa wasichana japo nilikuwa sijui wakati tunasomanae. Yeye mwenyewe ameniambia kweli alikuwa kicheche na akanipa album yake nimeona picha za hao wasichana wake wa zamani lakini kaniambia ameamua kutulia.

Nikaamua kujaribu bahati yangu kwa mara nyingine, nampenda sana huyu nilienae sasa na najaribu kumridhisha kwa kum-treat anavyotaka. (yeye ni out-going sana japo mimi si mtu wa viwanja kabisa). Yaani naona kama nimepata nilichokuwa natafuta kwa muda mrefu maana ana kila kitu nilichotaka mwandani wangu mtarajiwa awenacho ikiwemo elimu, uzuri, kujali na mambo mengine ndio maana najitahidi nim-keep ili tufike mbali na Mungu akipenda tufunge ndoa japo sina uhakika.


Dada kiufupi nimeshakuwa na wavulana 6 kabla ya huyu wa kwanza(1) alitaka tu awe wa kwanza kutembea na mimi na baadae alinidump. Wapili(2) alinipenda lakini alikuwa na elimu ndogo and tulikuwa tunaishi mtaa mmoja so nikam-dump. Watatu(3) nilikutana nae thru marafiki wa kalamu na tulisex siku moja baadae tukaachana sababu alitaka ndoa nami umri haukuruhusu naye alinizidi miaka7. Wanne(4) nilikutana nae kupitia rafiki yangu na tulishindana tabia tukaachana. Watano(5) ndo huyo tuliekutana nae tuition na tumeachana kimya kimya. Wasita (6)niliekutana nae huku kutoka Taifa lingine ambaye ame-graduate na kuondoka na wasaba(7) ndio huyu nilienae sasa katika wote hao niliekaa nae sana ni namba 5 & 6 wengine nilikaa nao si zaidi ya miezi3.


Tangu nilipojua nia ya huyo wa kwanza nikawa na hasira na wanaume so nikawa nawabadili kama nguo kulipiza kisasi lakini baadae nikaona ni ujinga na kuamua kutulia na huyo namba 5 nikajua nimepata.

Mwisho kabisa dada Dinah. Hivi karibuni huyo namba 5 ameanza kunitumia msg kuonyesha kuwa bado anajali baada ya kuwa kimya mwaka mzima ambao sikurudi huko, anasema ananipenda na alikuwa busy sababu ya maisha. Mimi sitaki kumrudia na hajui kama nilisha move on na kuwa na watu wengine.

Ninachotaka sasa ni kuwa na huyu nilienae lakini sijui jinsi gani nimwambie huyo wa huko Tanzania. Pia nimesikia mkilingana umri ni shida kuelewana, naomba imaana huyu wa sasa tuko nae sawa lakini naamini tutafika mbali japo sasa tuna miezi minne.

Natumai utanisaidia dada yangu.
Ni mimi Ney de great."

Dinah anasema:Marhaba Ney, mie ni mzima wa afya namshukuru Mungu. Asante sana kwa mail yako na kwa kueleza kwa uwazi historia ya maisha yako ya kimapenzi. Hakika umeanza kujihusisha na masuala ya Ngono na mahusiano ya kimapenzi mapema na kwa kasi kubwa sana.

Kutokana na maelezo yako inawezekana ktk ukuaji wako ulikosa sehemu fulani ya mapenzi kutoka kwa wazazi wako, kama ulivyodai kuwa kwenu mnauwezo wa kifedha. Mara zote familia zenye kujiweza huwa "busy" na shughuli za kuhakikisha pesa zinaingia na miradi inakwenda vema ili watoto na familia kwa ujumla kuendelea kuishi comfortably.....


Hii hufanya wazazi kujisahau na kutowapa mapenzi ya kutosha watoto wao na hivyo watoto ku-miss hayo mapenzi na matokeo yake baadhi huwa na tabia kama yako. Kwamba wanakuwa na msululu wa wapenzi wa muda mfupi ktk umri mdogo na kwa muda mfupi.


Nakuelewa uliposema kuwa uliamua kutoka au kubadili wanaume mara kwa mara (hope u were and still using Condoms) kwa vile ulikuwa unadhani unawakomoa, kitendo cha wewe kufanya hivyo au kuamini hivyo ni wazi ulikuwa umeathirika Kisaikolojia kutokana na uzoefu wako mbaya uliosababishwa na Mpenzi wako......baadhi ya wanawake huathirika vibaya kiasi kwamba wanapoteza hisia juu ya wanaume na kuibua hisia juu ya wanawake wenzao!


Lakini wewe ni mwanamke, na kwa kawaida mwanamke anachagua nani wa kumpa mwili wake na lini hivyo basi suala la wewe kushindwa kujizuia ikiwa mwanaume ni "mzuri" sio sababu ya kutosha kukufanya wewe kujipelekesha kwa wanaume hao ambao kwa namna moja au nyingine hawana mapenzi juu yako.....anyway, hatuwezi kubadili yaliyokwisha tokea tusonge mbele sasa.


Pongezi za dhati kwa uamuzi wako wa busara wa kuacha "katabia kale kachafu ka kulipiza kisasi", kutokana na maumbile ya mwanamke kitendo cha kufanya ngono na wanaume wengi hasa ktk umri mdogo unaweza kusababisha mabadiliko makubwa sana ya mwili wako hasa sehemu nyeti licha ya hivyo pia unaweza kupata maambukizo ya Zinaa.


Kutokana na umri wako mdogo na bahati uliyonayo ya kuendelea na masomo ni vema basi ukazingatia zaidi masomo na kufikiria maisha yako ya baadae kama ambavyo baadhi ya wachangia walivyokushauri.


Pamoja na kusema hivyo sina maana kuwa uachane na huyo mpenzi wako, la hasha! Endelea na uhusiano wenu lakini usiweke effort yote kwenye mapenzi na kum-treat kwa kila anachokitaka na badala yake jifunze kuwa na mipaka ili usije umia baadae ikiwa uhusiano hautokuwa vile unavyotaka hapo baadae.

Huyo Namba tano achana nae, Block namba yake au wewe badilisha namba yako, huitaji kumuambia chochote wala kumhabarisha kuhusu maisha yako na mpenzi wako wa sasa kwani hausiki in what so ever!

Kama kweli mnapendana na mmetulia (wewe na Mpenzi No.7) endeleeni hivyo na furahieni maisha yenu ya ujana. Kumbuka kuchukulia uhusiano wenu kawaida na kama Mungu anataka ninyi wawili siku moja kuwa mume na mke basi itakuwa hivyo, usilazimishe.

Kuwa muangalifu, na kumbuka mwanamke ana haki zote juu ya mwili wake, hakikisha men dont abuse it kwa kujiheshimu nakuheshimu utu wako, pia maisha yako ya baadae yapo mikononi mwako usiruhusu mtu baki akupokonye!

Kila la kheri!

Comments

Anonymous said…
Wanaume sita na wote una uzoefu nao??Najua una uzoefu nao ndio maana umewakumbuka vyema. Nakuomba hebu tafakari uzoefu wako na kila mmojawapo, `kiraha'Je kuna tofauti gani? Nafikiri hakuna tofauti, tofauti ipo katika hisia zetu. Tofauti ipo katika `tabia' na pengine tofauti ipo katika `mitindo', lakini yote hayo yanajengwa na `mashirikiano, na maelewano' ambavyo hivyo unaweza ukavipata kwa yoyote yule kama mtashibana.
Nafikiri katika juhudi zako zote hizo ulikuwa hutafuti yupi atakayekukuna vizuri,nadhani nia yako ilikuwa kumpata mtakayeelewana. Na hicho ndicho kigezo chema,lakini hilo haliwezi kuwepo kama hakuna `uwazi'. Mwambie nini unakitaka, mwambie nini unapendelea hilo limekuwa mtihani kwa wapenzi wengi ndio maana hatufiki kule tunakokutaka.
Sasa kwa ushauri wangu, ni kuwa nafikiri baada ya kuruka huku na kule, na ukazipata za aina tofauti nafikiri ni vyema ukatulia, na kama ulivyosema wewe mwenyewe huyo wamwisho anaendana na wewe, basi jitulize kwake, na wengine wakikubipu wape ukweli kuwa sasa unaye, na wao watafute wakwao.
emu-three
Anonymous said…
Asilimia Kubwa ya vijana wenye umri chini ya miaka 25 sio watulivu, Hupaparika na kutaka kujia hiki na kile kwa muda mchache, mfano umejonea mwenyewe hali yako ilivyokuwa... Umechezewa na wanaume sita na huna ulichopata cha msingi.. wengi wataona au kudhani naongea kwa ukali lakini ukweli inabidi usemwe.. Huna Upeo na Fikra za kuwa na Mwanaume ukatulia naye. Wewe bado ni msichana mdogo sana, Tulia Tafuta maisha yako, jipange utakuja kupendwa na kupenda baadae, Ushauri mungine ninaoweza kukupa ni kwamba, Mapenzi hayauzwi na wala hayapimwi kwa kipato... Si kila mwenye uwezo atakutreat vizuri na si kila asiye nauwezo atakutendea mabaya.. ukiweka kipato katika utafutaji wako wa mwenza utakuwa unakosea sana kwani kuna leo na kesho, naamini fika kwamba bado hujaanza kujitegemea.. Hizo ni mali na mafanikio ya wazazi au walezi wako.. hivyo ukishakuwa na zako ndio utaelewa maisha hasa ni nini, Also uzuri wa wanaume ni kama wa wanawake, Mimi ni mwanaume na nashukuru Mungu Ni mzuri sana, yaani handsome vya kutosha, nishaambiwa na wengi na nishasobokewa na wanawake wengi kama wewe wenye kupenda wanaume wa tamthilia...Lakini kumbuka kwamba Beutiful men/women are invisible as we tend to be absorbed with the outer beuty and forget who is the actual person inside... Uzuri ni swala la mtazamo tu na si chaguo letu kuzaliwa wazuri au wabaya, Binadamu ni Ndani ya mwili sio nje...Kabla hujaanza kuchambua huyu mzuri huyu mbaya, jiasess mwenyewe uone kama una sifa uzitakazo au unaona wewe ndio mwanamke wa kwanza duniani kwa urembo> if not, basi kumbuka kuna wanaume wanakuona mbaya kama wewe unavyowaona wao...na kuna wengine wanakuthamini kama wewe unavyowathamini baadhi yao...
Ni hayo tu...
NB: mtoto una umri mdogo sana kuchanganua mambo haya, ukikua utaelewa nini nimesema...
Anonymous said…
Binti, kwanza umehangaika mno na wanaume kwa umri wako huo wanaume saba miaka 22 tu?

Ujana umekuwa ukikupeleka mbio sana hasa katikasuala zima la mapenzi umeyapa kipaumbele mno.

Mimi ningekushauri kuwa maliza masomo kwanza ndipo uhangaike na mambo ya mapenzi.Amini usiamini hatanhuyo jamaa uliyenaye huko kwa sasa hamtafika mbali hata kidogo.

Kumbuka sana hadithi ya Biblia mabayo Yesu alikutana na mwanamke malaya amabaye alimuuliza una wanaume wangapi alisema alikwishakuwa na wanaume watano na sasa anaye mmoja.Yesu alimjibu akamwambia hata huyo uliyenaye si mume wako.Nataka kukuambia kuwa huyo jamaa unaye tu hapo kwa kuwa mko karibu, atakutomba hadi anakuacha soremba.Mpenzi wako atakayekuwa mume wako bado hajatokea machoni pako.Uliyonayo moyoni mwako sasa ni mahangaiko ya kimapenzi yanayokusumbua sana.Lakini usidanganganyike kuwa una mtu unayefanana naye katika sifa nyingi.

Kama unanielewa nakushauri achana na wote hao,jitulize kwanza,punguza hisia za mapenzi,fanya kama ndo kwanza huhitaji mboo yoyote ya mwanaume iingie huko chini.Jipe muda maliza masomo kwanza.Halafu baadaye utaona umuhimu wa kuwa makini katika mapenzi,ukipuuza hayo ujue kuwa hutapata mwanaume wa kweli ambaye atapenda kuwa mpenzi wako mwenye malengo halisi ya kujenga m,aisha na wewe, utabaki na hadithi ya kufanya mapenzi na msululu wa orodha ya watu tu.

Wewe ni binti mdogo sana kama ni maonjo umeyapata, kama ni utamu umeishaujua na umeufanya na umeufaidi,lakini kumbuka na geuka na upande wa pili uone ulichovuna katika mahusiano yote hayo kama si ufedhuri wa kujifuarahisha na kujishutumu kwa ulichofanya.

Nakutakia kila la heri binti ili umalize masomo kuliko kuhangaika na mapenzi,kwani hayana usalama kwako.Byeee poor girl

USA
Anonymous said…
Mdogo wangu ukiwa na 22 years muda mwingi huwezi jua nini unataka. Najua kusikia hilo kunakera maana hata sisi tulipokuwa na age hiyo tulidhani hivyo hivyo.

Ukweli ni kwamba past yako haiwezi kupredict future, lakini atitude yako inawaze kuspoil future yako. Sasa sababu umri wako ni sawa kabisa na mdogo wangu, nakwambia kwamba BE CAREFUL maana you might getting into something which you will not like.

Focus on your future, get your education going and don't sleep around. I know it sound hard kuamini kwamba unachofanya leo kinaweza kuathiri future yako, but trust me kinaweza.

Kuhusu huyo mpenzi aliyepotea mwaka mmoja sasa amerudi. Mwambie Excuse me, too little and to late cause i already move on.

Ed
Anonymous said…
Naona mdogo wangu bado hujaweka wazi wewe unapenda kuolewa au unapenda mauhusiano tu ya kawaida au unapenda ngono.
Lakini kutokana na maelezo yako unakaugonjwa kakutoridhika na kupenda ovyo.
Kwa hiyo kuwa makini lasivyo utajiukuta unaharibu future yako hivi hivi kwa kuukwaa ukimwi na ikawa kazi bure.
Kuwa makini tulia maisha yapo na utayakuta na kuyaacha kuwa makini usipende pende ovyo utakuwa kicheche.
Mdau Fidel,
jitonyile@yahoo.com
Anonymous said…
Sitaaa! Hata aibu huoni, eti nikamdump! yaani hata kuolewa bado mboo sita zimesha kupenyeza. Ama kwele tajiri kuingia peponi ni sawa na ngamia kupita ktk tundu la sindano!

Kwa taarifa yako tajiri anapata heshima kwasababu maskini yupo, laiti maskini asingekuwepo basi tajiri asingeheshimiwa, vivyo mzuri hapati heshima illa asiye mzuri awepo. Yaani wewe na bf wako wote ni hamjatulia ni vizuri mkioana ninyi kwa ninyi, we unataka umpelekee nani k iliyotumika sana!

Iyo k yako lazma itapta madhara.Usipojiangalia utapata tabu sana hapa duniani pamoja na elimu uliyonayo! Wenzio wanajuta kupoteza bikira zao kabla ya kuolewa wewe mboo sita na hiyo ni ya saba.

Hebu fikiria baadaye unaanza kumuomba mumeo akunyonye kinembe, laiti angejua kuwa hapo kuna mboo saba zimepita asingenyonya. Kifupi ni kwamba wewe una hulka ya ukicheche na unapaswa kuacha haraka sana.

Kama unapenda kutiwa basi olewa na kama hutaki kuolewa basi subiri, Dont u know that believing in God isn't a dogma but scientific?
Bora uoane na huyo huyo kicheche mwenzio.

Kwa taarifa hii ni blog ya watu wema na ndio maana wanahusiana ktk mema kama vile kuoana au kuboresha maisha ya wanandoa. Wee unafikiri wanaoshiriki humu hawamuamini na kumuheshimu Muumba wetu?
Be careful usijekuwa ajenti wa shetani hapa duniani, wenzio tunamuogopa Mungu kama wewe humuogopi basi endelea unayofanya.
Anonymous said…
Umri wako ni mdogo sana kulingana na wanaume uluokua nao, bt usiogope wala kukatishwa tamaa na wanaokuponda. Kila mtu anaudhaifu wake. Sasa, achana na wote anza upya. tulia, concentrate na shule na kumuomba Mungu. Utubu kwa yote uliyofanya na umrudie Mungu, then omba upewe mume. Hao wote wanapita tu, mume kumpata si rahisi hivyo.Huyo anatafuta pumziko. By the way, unaharaka ya nini? ndoa si rahisi my dia, jipe muda upate kilicho bora. ila tulia kabisaaaa. Yan ukiendeleza hako kamdenenge, my dia unadestroy future yako kabisaaa na trust me hutaolewa, utahangaika mpaka kufa, hakuna anaetaka kuoa kicheche
Anonymous said…
Huyu ni mfano tu wa jinsi huu mchezo wa mapenzi na mahusiano ulivokuwa na hatari.....Miaka 22 wanaume sita, na unajionea kabisa ufahari kwa jinsi ulivokuwa unawadump....nadhani tungekuwa tunaulizana list ya nyumba ndoa nyingi zisingekuwepo...kama hali yenyewe ndiyo hii.

Hongera kwa kutupa uzoefu huo, na zingatia waliyokwisha kusema wachangiaji wengine.....

PapaaK