Nikirudi Bongo ndio itakuwa basi?-Ushauri

"Dada dinah pole na kazi, naomba niingie moja kwa moja na kile kilichi nileta hapa.
Dinah nina mpenzi ambaye tumeahidiana kuoana ingawa wote tuko shule mimi niko mwaka wa mwisho yeye bado kama miaka miwili hivi, na wakati wote huo tuko karibu sana kama mke na mume na tuko ughaibuni.


Tatizo ni kwamba tumekua tukigombana mara kwa mara na tunapatana wenyewe bila kumshilikisha mtu na kibaya zaidi huyu mwenzangu hua hajui kusema samahani hata kama anajua amekukosea, kiasi kwamba mtu unapata hasira.Mtu amekukosea halafu haombi msamahaa.


Siku zingine hua tunapigana kabisa kutokana kwamba yeye hataki kujishusha na mimi kama mwanaume sipendi kudharaulika mwisho wa siku tunaanza kupigana, Mbali na hayo inaonyesha kila mtu anampenda mwenzie kiasi kwamba hayuko tayari kumuacha.


Na kingine ni kwamba huyu mpenzi wangu ameumbika kidogo mungu kamjaalia.Na kipindi chote hiki nilichokua nae kweli tumefurahia mapenzi ingawa kuna ugomvi wa hapa na pale. Wanaume wengi wamemtaka lakini wote huishia kugonga patupu na wengi wanasubiri mimi niondoke baada ya kumaliza shule ndo wamtake kwani wanamwambia laivu ku wanasubiri niondoke.


Hapo ndio ninapoingiwa na wasiwasi je nikiondoka ataweza kuvumilia kweli?au ndo ahadi yetu itakua imekufa? pamoja na hayo namwamini sana lakini najua kuna kutereza, na mimi sipendi kuchangia hasa ukizingatia tumekuwa pamoja kwa muda wa miaka miwili na miezi sita sasa na baadhi ya ndugu wanajua uhusiano wetu.


Kipindi chote hicho wote tumekua sio watu wa kujirusha sana na wala hatutumii any alchohol. JE DADA DINAH NIWE NA MATUMAINI AU NDIO BAI BAI MAANA NATAKA KUJUA ILI NISIPOTEZE MUDA.

Naomba ushauri dinah na wadau wengine wa blog hii
thanx".

Jawabu:Asante sana kwa pole zako kwani zimefika wakati muafanya kwa vilemajukumu yameniandama sana tangu mwaka huu uanze lakini najaribu kujigawa kimtindo.

Sasa jamani mapenzi gani hayo ya kupigana magumi kwa vile mmoja hataki kudharauliwa na mwingine hataki kuwa chini? Hata siku moja haiwezekani mtu ajiweke chini kwani akifanya hivyo utamdharau kama ambavyo wewe hutaki. Kwanini wewe usiwe mstaarabu ukakaa kimya wakati yeye analalamika na akimaliza mpe jibu zuri, kwa upole na upendo badala ya kuinua mkono na kumdunda mwenzio ambae ni mwanake?.....tuliache hilo.


Suala la wewe kutaka kujua kama ni kweheri au usubiri unapaswa kumuuliza yeye mpenzi wako. Zungumzzeni kuhusiana na maisha yenu ya baadae na mipango yenu kama wapenzi. Weka wazi hofu na wasiwasi ulionao juu yake pale utakapokuwa unarudi Nyumbani na kumuacha yeye huko.

Mawasiliano ndio njia pekee ya kujua umesimama wai kwenye uhusiano wenu, mazungumzo yenu yakina yatakusaidia kufanya maamuzi ya busara iwe ni kusubiri au kuendelea namaisha yako kivyako.

Kuwa na mpenzi au kuwa kwenye uhusiano hakuzuii watu wengine kukutamani, kama mzuri anavutia na amejaaliwa umbile zuri kwanini asitamaniwe?!! Kutamaniwa haina maana kuwa mpenzi wako atatereza na kila atakae mtamani.....jivunie uzuri wa mpenzi wako ambao unavutia watu wengine.
Kila la kheri!

Comments

Anonymous said…
Mambo dada dinah,mi nilikuwa niombe ushauri sasa naomba nielekeze jinsi ya kutuma stori yangu mana hata sielewi nianzie wapi?naomba nisaidie mana nina matatizo na nahitaji ushauri wako na ndugu zangu wengi wa blog hii.....!
jackline
Anonymous said…
Kama kweli anakupenda atajituliza na kukusubiri wewe,lakini kama ilikuwa poteza wakati, basi `asiyekuwepo na lake halipo'.Hiyo ndiyo hali halisi ya ujana, na mwanzo wa urafiki hadi mke, kugombana, kufurahi, nk na muda ukifika, umefika.
Kinachotakiwa ni wewe na yeye kukubaliana `uchumba' kama umri wenu unaruhusu. Lakini kwanini msijitulize katika masomo mpaka muda muafaka?. Kama umri unadai, na unauhakika na mipangilio yako, basi vishaneni pete hii itamuweka yeye katika tahadhari, kuwa anaye mtu na akijirusha itakuwa skendo.
Lakini hata hivyo, haihakikishii moja kwa moja kwa yeye kujituliza kwa ajili yako, kama kweli hana mapenzi ya dhati na wewe.
emu-three
Anonymous said…
Kijana wangu, kama ugomvi ndiyo huo umesema huwa mnagombana na kupigana, katika urafiki tu,je, una uhakika kwamba kweli huyo mtakujaishi kiusalma?Pamoja na kwamba umesema kila mmoja anampenda mwenzake, lakini ugomvi mkubwa namna hiyo unatoka wapi? Labda nabaini kwamba bila shka nyote ni wachanga na hamjui nini kinawafanya muingie kwenye mahusiano hayo.

Kuhusu kumwacha huko ukiondoka, kwa kweli hiyo ni patapote,umekiri mwenyewe kwamba wanamtaka wengi lakini anakataa,basi jua kuwa ukiondoka hatakataa, atataka wa kuli-place tena akikumbuka na ugomvi wenu wa mara kwa mara forget it man, nothing with bework otu on your side.Lakini usife moyo maana umemsifia kuwa ameumbika, na labda hilo ndilo nguzo kubwa inayokufanya uone anafaa kuwa mke wako wakati unajua kuwa kitabia hamuwezi kuivana.

Uamuzi uko mikononi mwako wewe ukirudi bongo tulia tu subili huyo mlimbwende wako atakavyotunza maamuzi yenu na makubaliano yenu.

Kila la heri poor man.