Mume wangu hataki tuzae-Ushauri!

"Habari dada dinah na wasomaji wengine, naomba msaada wenu wa ushauri na samahani kwa maelezo marefu. Mimi nina umri wa miaka 28 na mume wangu 37. Tunaishi Europe. Niko kwenye ndoa miaka 2.


Tulikubaliana na mume wangu tusizae kwa muda fulani kwasababu ya gharama tulizopata wakati wa harusi na pia ili tujenge. Muda wa kutozaa unaisha mwezi wa 12 hivyo ikifika muda huo natakiwa kutiana kwa nguvu zote ili nimimbike.


Kuna siku nilimkumbushia mume wangu kuhusu muda wa kupata mimba unakaribia hivyo tuanze kujiandaa, akawa mkali na kuniambia nisahau kitu kuzaa kwasasa kwasababu ana majukumu mengine ya kuwasomesha wadogo zake wawili ambao ni mtoto wa kaka yake na masikini mmoja anamsaidia na mtoto wake alimzaa na mtu mwingine alipokuwa chuoni.


Mimi nikamwambia anaweza kupunguza majuku kwa kuwaachia ndugu zake mdogo wao mmoja na yeye akabaki na mdogo mmoja kwasababu kwao wako 9 na huyo mtoto wa kaka yake amuachie kaka yake amsomeshe mwanae ili na sisi tuzae wa kwetu na tujenge na kufanya mipango mingine akanambia hatofanya hivyo kama siwezi kusubiri majukumu yaishe nitafute mwanaume asiye na majukumu nizae nae.


Ndugu zake wengine wanauwezo wa kawaida mbao yeye ameshawasaidia kwani alishawapa mtaji wabiashara, na kuwajengea nyumba ya familia na pia mambo mengi anawasaidia. Jamani nisaidieni sielewi nifanye nini. Na nimeshaambiwa nitafute mwanaume mwingine, kuzaa nataka na ndoa yangu sitaki ivunjike"

Jawabu:Asante sana kwa barua pepe yako, nadhani mumeo alijibu kwa hasira kwa kufikiria kuwa kwa vile tu amekuoa unataka asahau familia yake (kumbuka umeolewa miaka 2 tu) hivyo majukumu yake aliyonayo aliyaanza kabla yako na hivyo hana buni kuyamaliza. Yeye kama mwanaume tena wa Kibongo haitaji mwanake kumuambia nini cha kufanya hasa linapokuja suala la ndugu zake. Hivyo basi tamko lake la kutafuta mume mwingine usilitilie maanani.


Katika mambo yote kwenye uhusiano wowote wa kimapenzi hata siku moja usiingilie mambo ya familia ya mwenzio, hata kama atakuomba ushauri hakikisha unampa ushauri utakaomsaidia na kwamwe usiponde ndugu zake hata kama wamemuumiza mumeo na badala yake msikilize, mpe matumaini na kumtuliza hata siku moja usijarubu kujiingiza kwenye masuala ambayo wewe hayakuhusu......hujui makubaliano yako kama Familia.


Badala ya kumuambia mumeo apunguze majukumu ulitakiwa kumwambia kuwa "kipato changu" kinatosha kusaidia majukumu mengine yakiongezeka moyoni ukimaanisha kuwa unataka mzae, lakini kama kila kitu ni juu yake inamuuwia vigumu hasa ukizingatia kulea mtoto Ulaya sio lele mama kwa maana ya kiuchumi.

Natambua unavyojisikia na hofu yako ya kuchelewa kuzaa, wewe bado kijana ungekuwa na umri wa miaka 33 na ukawa na hofu hiyo ya kuzaa ningekuelewa, lakini kumbuka unaweza kufurahia maisha yenu ya ndoa bila kuwa na mtoto mpaka pale mtakapokuwa tayari na kuwa na uhakika wa kufanya hivyo.


Najua wanawake wa Kibongo kuzaa wanaona mwisho wa matatizo au njia pekee ya kulinda ndoa kama sio kum-keep mwanaume, yaani wewe kuwa mwanamke basi ni lazima uzae lakini wanasahau kuwa (1) Ni majaaliwa na (2) Ni chaguo la mtu. Kuzaa sio lazima na haijalishi una umri gani kama Mungu alitaka siku moja uwe na familia basi itakuwa hivyo.


Hivyo mdada tulizana, acha kujipa mawazo bila sababu ya msingi, furahia maish ayako ya ndoa, Mpe ushirikiano mumeo ktk kukabiliana na Majukumu uliyomkuta nao ili kumpunguzia stress, fanya bidii kwenye shughuli zako kiuchumi ili kukusanya senti kwa ajili ya mtoto atakae zaliwa, pale mtakapo elewana kufanya hivyo.

Ukimuonyesha mapenzi, ukiwa mwenye furaha, ukijitahidi kumuondolea stress na kushirikiana nae ktk kila jambo bilakujiingiza sana kwenye masuala ya familia yake, hakika mumeo atapata ujumbe na kama ni mtoto ndio unataka basi atakupatia......tumia uanamke wako kupata utakacho.


Pssst! Usikute hana uwezo wa kuzaa ila anashindwa kukuambia, mana'ke wanaume wakikaribia miaka 40 huwa na haraka sana ya kuzaa no matter what kama unahisi the same basi baada ya mwezi wa 12 tumia ila mbinu ya "kumtegeshea" siku za hatari na usiposhika mimba utajua ukweli na ukishika basi utakuwa umepata ulichokitaka.

Ikiwa unatumia aina yeyote ya dawa za kuzuia mimba basi ni wakati wa kuacha na kutumia njia asilia au Condoms ili kujiweka sawa kushika mimba hapo baadae.

Kila la kheri.

Comments

Anonymous said…
your husband is not serios with life.try kuomda hata viongozi wa dini au watu wazima wakusaidie.umru unaenda.wakwenu nani atawasaidia kulea?
Anonymous said…
dada pole na majukum yako yakila siku huyu baba naisi alikuoa kwa sababu ya kitu fulani, kwasababu yeye ana mtoto lakini wewe hataki upate mtoto hiyo cio haki hata mungu hapendi. nakushauri utafute watu wa karibu naye wamshauri kiutu uzima ili aweze kuelewa soma.
Anonymous said…
Jaribu sana kumshauri kuhusu hilo swala, kwani umri kama huo mnatakiwa muwe na mtoto ili muendane na mipangilio ya kiumri nyie na m(wa)toto wenu. Lakini hii inategemeana na kipato chenu na mlivyojiwekeza kwa ajili yao.
Mfano mkibahatika kuzaa sasa, baada ya miaka 20,ambapo angalao mtoto wenu atakuwa anaweza kujisaidia, baba mtu atakuwa na miaka 58. Mtu mzima wa kuanza kutulia!
Hoja ya kumueleza,ni hiyo,kuwa tukizaa sasa tutakuwa na muda mzuri wa kuwasaidia watoto wetu tukiwa bado na nguvu, kuliko kusubiri sana, hatimaye watoto watatuita babu!`Babuuu,oh baba, shikamoo...'
Ni vyema kusaidia ndugu na jamaa zetu,lakini hawo hawo baadaye wanaweza kuja kukusimanga, kuwa `kwanini ulichelewa kuzaa'
Tafuta muda muafaka, mfurahishe na hatimaye tia hiyo hoja kwa vielelezo makini.
emu-three
Anonymous said…
Pole dada kwa mawazo yaliyokupata kwa ajili ya kutamani mtoto, Kwa ushauri wangu maelewano ni bora zaidi na pia msaidiane kwa kila kitu means wewe uipende familia ya mumeo na yeye aipende familia yako kwani madam mmeshaoana mmekua kitu kimoja. Kuwasaidia hao wanaohitajia msaada ni kitu muhim kwa hiyo ukiridhika ndio itazidisha mapenzi. Na kuhusu mtoto hilo siyo mikononi mwenu kwani kila kiumbe kaandikiwa lini atazaliwa na lini atakufa kwa hiyo ndugu yangu nakushauri usipoteze mapenzi yako na mume wako kwa ajili ya kutaka watoto kwani Mungu akipenda na wakati wao kuja watazaliwa tu na huyo mume wako pia ataona wakati umekwenda na yeye anatakiwa kuwa na watoto kwani mtumai cha ndugu hufa masikini na ndugu akizaa na wewe zaa kwani at the end huyo mtoto akikua wa kwanza kuwajua ni wazazi wake. So poa zidisha mapenzi na toa unyumba kama kawaida na raha zikidi na wakati ukifika na wewe au nyie mtazaa watoto wenu na mtapata baraka na uzoefu zaidi kutokana na hao mnaowalea au kuwasaidia.
Anonymous said…
Anony wa 4:01Am, ni rahisi kusema hayo uliyoyasema lakini nadhani you are very wrong na kama ni mwanamke mwenzangu nadhani umechemsha, biological clock ya mwanamke iki tick rafiki yangu asikuambie mtu hapataeleweka kitu hapo,yaani unamshauri huyu dada eti atulie Mungu ndio mtoaji na avumilie tu, ni kweli Mungu ndio mtoaji lakini tusiwe wapumbavu wa kujibweteka tu, we need to play our part na Mungu nae atatubariki, sasa kama Mume hataki mtoto, hata huyo mtoto akizaliwa si atakuwa ana mihasira tu ya kila saa, ndio hapo utasikia ooh wewe umelazimisha mtoto. Kwa hiyo point ni kuwa aendelee kumconvince huyo mume wako mpaka akubali, ikibidi kuhusisha wazazi hata viongozi wa dini. Mwanamke ana special bond na mtoto, kitendo cha kubeba mimba miezi tisa, kuzaa, kunyonyesha etc ndiyo ndoto kubwa kwa wanawake wengi wakishaolewa asikuambie mtu, labda kama ni tasa na hawawezi kupata watoto, tena huyo dada anakosa selfconfindence kwa sababu anaona mume wake ana mtoto na mwanamke mwingine yeye hana, connection kati ya mume na mke ni watoto, ndio wanaoleta baraka kwenye nyumba, basi hakuna haja ya kuoana basi, maana matunda ya ndoa ni watoto, sasa kama wote ni wazima wa afya kwanini wasizae? kuna watu wanatafuta watoto usiku na mchana yeye Mungu kamjalia uzazi anakataa, that is a load of bullshit, samahani Dinah nimekasirika sana. Ushauri wangu, kama jamaa hataki kuzaa nae na amedhamiria hivyo bora kuvunja ndoa akatafute mwanaume anaetaka kuzaa nae na kutunza familia, hawezi kuendelea kukata kiuno kila siku halafu asiwe na mtoto wake na yeye wa kujivunia, wanaume wengine bwana very selfish!!
-Maggie.
Anonymous said…
Mbona mnaishi kizungu? Kidini Mwenyezimungu mnapoowana anapenda muwe na familia sema Kuzaa au kuzalisha ni majaliwa ya mwenyezimungu muumba. Ila msiseme kwamba hatutaki kuzaa sababu fulani ni zambi, kama mkiweza mwenyezimungu atawafungulia watoto inshallah. Mie na Mke wangu tuna miaka 5 bila mtoto ila hatujakata tamaa inshallah mwenyezimungu atatufungulia. Mwanzo tulijuwa wote tunamatatizo tumeenda kwa madaktari wote tumeambiwa tupo fine. Swalini muombeni mwenyezimungu kwani kutokuwa na watoto sio mwisho wa dunia. katika siku ulizotowa ushauri mzuri DINAH basi leo. Msikate tamaa mwenyezimungu yupo nan yie.

wanadamu wengine hata miaka 10 wanachukuwa.
Anonymous said…
Maggie umeongea kwa hasira sana, lakini naombanikukumbushe kuna mambo ambayo huwa hayalazimishwi, hivi ukizaa mtoto halafu usipate ushirikiano na mumeo utakua na raha na huyo mtoto? mimi kiukweli kabisa namshauri huyo dada awe mpole hakuna raha kama mtoto atazaliwa huku wazazi wote wawili wakimsubiri kwa hamu zote, mana hata wakati wa ujauzito mama atapata ushirikiano wa 100% toka kwa mumewe lakini ukilazimisha utakutana na vikwazo vingi ambavyo utapoteza hata raha na huyo mtoto, wewe shaurianana mumeo na ifike mahali mkubaliane bila kulazimishwa kumleta huyo kiumbe dunianina na ikibidi kusubiri nahsauri usubiri, ila kama una uhakika wewe mwenyewe unamudu gharama za hyo mtoto baso muombe mumeo muhakikishia ua una uwezo wa kugharamia hilo jambo na iwe kweli una huo uwezo