Hivi tutafunga ndoa au? Mawasiliano Sufuri...

"Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 25 ninamchumba ambaye tuna miaka 2 katika uhusiano wetu, anasema kuwa anatarajia kunioa ila sina uhakika kuwa ni kweli. Mimi nipo Arusha na yeye yupo Dar, ila sina uhakika maana naona siku hizi kapunguza mawasiliano na mimi sio kama mwanzo. Naombeni ushauri wenu kama kweli ananipenda au ananidanganya tu.
Ester."


Jawabu: Ester, asante sana kwa ushirikiano wako. Mchumba wako ndio amesema kuwa anatarajia kukuoa sio kwamba mmepanga (yeye na wewe) kuoana hivyo kufanya nyote wawili kutarajia kufunga ndoa na kuishi pamoja mpaka kifo kiwatenganishe?

Natambua kuwa ni kawaida au asili kwa mwanamke kusubiri mwanaume atangaze ndoa au atake kuoa lakini ktk hali halisi ndoa ni makubaliano ya watu wawili wanaopendana na wenye nia moja ya kwenda kuishi maisha yao pamoja, japokuwa kwenye baadhi ya Jamii wazazi wako ndio wanakubaliana na sio ninyi mpendanao.

Kwenye hili, naona mambo mawili ambayo yanaweza kusababisha hofu yako juu ya u-serious wa mpenzi wako kwako. Mosi, huenda yeye haamini kama kweli unataka kufunga nae ndoa kwani maelezo yako hayajaonyesha wewe kutaka au kutaraji akufanya hivyo bali yeye ndio anatarajia kukuoa.

Pili, umbali kati yenu na gharama za maisha hasa linapokuja suala la mawasiliano inazweza kuwa sababu kubwa ya ninyi kutokuwa na mawasiliano ya mara kwa mara kama ilivyokuwa huko mwanzo, pia kunauwezekano mkubwa kuwa unasubiri yeye ndio awasiliane na wewe na sio kuwa mnawasiliana kwa maana ya wewe una-check nae na yeye anafanya hivyo. Inaonyesha yeye ndio mtendaji mkuu kwenye uhusiano wenu hali inayoweza kusababisha uchovu na yeye kuhisi kuwa anafanya too much na wewe kazi yako ni kusubiri tu.

Uhusiano wowote wa kimapenzi unajengwa/boreshwa kwa kuzingatia nguzo kuu tano na moja kati ya hizo ni kushirikiana, ninaposema kushirikiana ninamaanisha kiuchumi, kihisia, kimwili, kimawazo na maamuzi. Nasikitikakusema kuwa kutokana na maelezo yako hakuna dalili ya ushirikiano kwenye uhusiano wenu na vile vile mawasiliano sio mazuri sana kutokana na umbali kati yenu.

Kitu muhimu cha kufanya ili ujue kuwa jamaa hakudangaji juu ya suala la kufunga ndoa na wewe, ni wewe kujitahidi na make an effort kwenye uhusiano wenu hasa linapokuja suala la mawasiliano, zungumza nae kuhusiana na ahadi yake na sasa ifanye iwe ahadi yenu kwamba mnaahidiana kufunga ndoa na hakikisha unamshawishi afanye kweli kwa kuchumbia kwenu na sio kuishia kusema tu "nitakuoa", "lazima nikuoe", "natarajiakukuoa" au "wewe mchumba wangu".

Suala la yeye kukupenda au kukudanganya nadhani itakuwa ngumu kwangu mimi na wasomaji wangu kujua kwani hujatueleza kwa undani na kwa uwazi zaidi, wewe Ester ndio mtu pekee unaeweza kujua kama Mchumba wako anakupenda kwa kuzisoma hisia zake, ukaribu wake kwako, anavyoku-treat n.k.

Tafadhali zingatia hayo machache niliyokueleza na mengine kutoka kwa wachangiaji wangu na ujaribu kuyafanyia kazi ili kufanikisha kile ukitakacho kutoka kwenye uhusiano wako. Kwa case yako ni ndoa basi hakikisha unafanyia kazi uhusiano wako ili kupata hiyo ndoa....kwa mbinu zaidi kama utahitaji basi unaweza kurudi tena mahali hapa.

Kila la kheri!

Comments

Anonymous said…
Ukishaona mabadiliko sheria mmoja ya penzi ni kufanya uchunguzi wako. Chungulia ndani kama kuna watu wanakulia urojo wako.

Miaka miwili na yeye yupo Tanzania kwa nini anachelewa? Jee mnaliongelea swala la ndoa na yeye anasemaje?
Anonymous said…
Kupunguza mawasiliano si kigezo cha moja kwa moja kumshuku mtu kuwa hakupendi. Mi nafikiri anaweza akawa yupo bize na majukumu yake ya kila siku.
Ushauri ni kwamba mpigie simu mida tulivu ambayo unahisi atakuwa kitandani saa 3 mpaka 4 hv usiku, na umuulize kwa upole nini hatma ya penz lenu coz unaona mawasiliano yamepungua, umri nao unakwenda muulize mipango ya kufunga ndoa maana huwa sichochei zinaa, katika yote anayoongea jaribu kupima ana mawazo gani kuhusu penzi lenu, u wil discover something.
Kwa upande mwingine angalia hata upande wako je huwa unapiga cm? Huwa unatuma sms? Sio unakimbilia kulaumu na wakat kaz yako ni kubp na kutuma tafadhali niongezee hela! Hapo sitakusapoti ndugu yangu.

Jambo jingine ni kwamba ktk ushauri wa mada hiyo chini, Aisha simsapot kabisa, hv hajui kuwa siku hiz wanawake wanaomba haki sawa eti wawe sawa na wanaume kwa kila k2! Mi nafikiri kama nyie wanawake mnataka wanaume wawahendo kama watoto au yai basi mkubali tu kuwa mwanamume ndio kichwa cha familia na in most case mwanamke ni mtoa faraja na ni mshauri wa karibu but mtendaji mkuu ni mume. Yatupasa tujue kuwa mke kupiga deki kujipamba mwenyewe na kupamba nyumba ni vitu ambavyo akivifanya yeye mwenyewe moyo wake huwa furaha but mens are not interested in such activities. Kwa mantiki hiyo mkubali kwamba tupo tofauti na muache tabia za kujifanya ladies first, hv we unapenda mumeo awe nyuma? Kumbuka mume akiwa na kipato hubeba jukumu la kusaidi famili 2 ya kwake na kwa mkewe, but fanya research ni wake wangapi husaidia upande wa mume mara kwa mara kama afanyavyo mume?
Pia mke akiwa na kipato basi huchukulia kama ni chake peke yake, but mume yeye kipato chake huwa ni cha wote yaani yeye, mkewe na watoto. Kwahiyo ukumbuke kuwa ukiona hupewi pesa na mumeo usichukulie advantage hiyo kutoka nje ya ndoa eti ili upate hela utakuwa chiz, kwani kile kinachotafutwa na mumeo ni chenu wote, usipopewa haimaanish amekunyima but ana malengo mema na maisha yenu ya baadae.
Sikupenda ushauri kwa yule mume aliokuta love sms kwa wif akiomba 5ooo
Anonymous said…
Mchumba, mawasiliano na ndoa. Maswali ya kujiuliza, je mumekutana mara ngapi kulijadili hili,na je wewe unampigia simu mara kwa mara, na mkiongea mnaongea vitu gani? Mikakati yenu ilikuwaje, kuoana baada ya muda gani
Wanaume wengi wanaogopa kuoa mapema, kwasababu moja kubwa kuwa mume akioa majukumu yanaongezeka, tofauti na wanawake, wao mara nyingi wakiolewa,majukumu yao yanapungua(huu ni mtizamo wa ujumla) kutegemeana na unapotoka.
Kitakachomfanya mwanaume avutike na wewe na kutangaza ndoa, dada Dinah, alitoa hilo darasa nyuma, lakini kwa mchango wangu, naweza kusema wewe mtoa hoja unatakiwa umshawishimwenzako kwa vitendo na mawazo. Mfano kumsisitizia, ili aone kweli wewe upo upande wake, lakini kwa vitendo,usiwe `muombaji mara kwa mara’, kila ukipiga simu `nataka hiki au kile’ hili litampa woga muoaji, atazani kuwa wewe unahitaji saana, kwahiyo anahitaji muda zaidi wakujiandaa.
Mwasiliano yanaweza au yasiweze kuwa kigezo cha kuachwa kwenye mataa,hii inategemea na mwenzako na anachokifanya. Zipo shughuli zinazoweza kumfanya mtu asipate muda wa kuwasiliana nawe mara kwa mara, uchumi pia na tabia ya mtu yote haya yanaweza kumfanya mtu awe `kimya’ lakini haimaanishi kuwa amekususa.
Cha muhimu, wewe mwenyewe uwe `mchokozi’ wa kumpigia, kumtumia meseji na vyema ziwe za mapenzi, ili jamaa ajue unamjali. Usiogope kumweleza ukweli, kuwa muda unapita na unahitaji `ndoa’. Kiukweli tukubali kuwa `nyote munatafuta’ wewe na yeye, wasiwasi mkubwa ni je unayemtafuta ni yeye au anayekutafuta ni wewe na ni nani wa kuthibitisha hili. Jibu ni wewe na yeye.
emu-three
Anonymous said…
Sasa w mtoto mzuri hivi unahangaika nini? ila n nyie some tyms huwa mnategea mpigiwe simu asb mch na usk,labda nikuulize swali moja we huwa nampigia? unaweza kumwelewa m2 kwa kumsikiliza tu anavyoongea, so cha kufanya toa sadaka mpigia kila mara mpaka yeye mwenyewe atajishtukia
Anonymous said…
Binti acha kutapatapa, kupunguza kupigiwa simu tu kelele mpaka majirani waje kusuruhisha? Je, itakapofikia mmeoana na siku moja bahati mbaya mkakwaruzana si utampeleka polisi?

Hapo juu umeshauriwa vizuri sana, hebu uwe na subira na kuendelea kujifunza mambo mengi ya mahusiano,hayako tu kwenye kupigiwa simu mama!!!

Jaribu kumhoji juu ya kuoana halafu uone ana dira gani,halafu ukiona mashaka zaidi exit,no need to complain.