Mchumba anipenda mie Moyo mzito-Ushauri!

"Dear dinah, Natumaini hujambo na mwenyezi Mungu anazidi kukuongezea nguvu katika kazi yako ya kudumisha mahusiano ya watanzania wenzako. Dinah mpenzi mimi ni binti mwenye umri wa miaka 24.

Tatizo langu linalo nileta hapa leo ni ukosefu wa mapenzi kutoka kwangu mimi kwenda kwa mwenzangu. Labda nikuelezee scenario ya mapenzi yangu. Mimi na kijana mmoja tulikuwa majirani enzi za utoto wetu na tukaenda shule moja ya msingi, ila tulivokuwa wakubwa wakati tunaingia sekondari wazazi wa mwenzangu walihama mkoa tuliokuwepo na kuhamia mkoa mwingine.


Tukaja kukutana high school moja tena tukawa marafiki wa kawaida tu kwa sababu tulikuwa tukijuana kabla. Baada ya hapo kwa sababu mwenzangu kwao walikuwa na uwezo akaenda kusoma chuo kikuu nje ya nchi mimi nikabaki chuo kikuu hapa Tz.


Akiwa huko hatukuwahi kuwa na mawasiliano hata siku moja. Ikatokea siku nikapokea simu kutoka kwake akisema alinikumbuka na anataka kunisalimia tu hii ilikuwa mwaka mmoja kabla hajarudi nchini. Tangu hapo akawa anakawaida ya kunipigia simu kila siku.


Kikafikia kipindi akaniuliza kama nina mpenzi nikasema sina naye akasema hana tukaanza kuwa wapenzi kwa simu tu kama ilivyo kawaida ya wapenzi wa mbali. Tukaanza kuahidiana tutaoana akawa amejenga mawazo anamchumba Tz na mimi nikajua yeye ndiye mchumba wangu.


Lakini hapa katikati takribani miezi sita imebaki ili yeye mwenzangu arudi toka shule nikapata mtu (intruder) ambaye tulipendana ile ya mhemko kwa kuonana kwa mara ya kwanza.Wakati naanza mahusiano ya mapenzi na huyo intruder nilijitahidi kumfuta huyo rafiki yangu wa mbali katika mawazo yangu na nikafanikiwa.


Nilikuwa naona mapenzi ya simu ni kudanganyana tu hamna lolote. Ikafikia kwamba nikawa sina uhakika tena kama nampenda huyo rafiki wa nje(Ambaye tunapigiana simu) ama la. Mara nayo mahusiano yangu na intruder yakawa ya muda mfupi sana na wao walihama nchi kabisaa, kwani baba yake alikuwa Balozi nchini Tz kutoka nchi fulani ya nje.


Ilimbidi aondoke awafate wazazi wake na akawa amepata na shule ya masters huko huko kwa hiyo asingeweza kubaki Tz hata kama angependa, akanishawishi twende wote na wazazi wake watanitafutia shule nikakataa kwenda. Baadae nikashtuka na kuona kwamba huyu mtu atanipotezea wakati kwani sioni future kati yangu na yeye japokuwa mawasiliano yetu yalikuwa mazuri tu.


Sikuwa na la kufanya ikanibidi nimuache mwezi mmoja tu baada ya yeye kuondoka chini. Japokuwa kilikuwa kitu kigumu sana kufanya kwa wakati huo ukizingatia nimeshaharibu mahusiano na mchumba wangu wa nje.


Miezi miwili baada ya intruder kuondoka mwenzangu naye akarudi Tz. Na aliporudi alikuwa na higher expectations kuhusu mimi akataka sana kuniona nikawa namkimbia. Kijana wa watu haku give up na alikuwa akinifuatilia kila pahala, Sikuweza kumkimbia tena ikabidi sasa nimpe nafasi aweze kuonana na mimi.


Tukaanza kuzoeana kidogo kidogo. Ikafika siku tukaelezana story za maisha na nini kilipita hapo kati na kwanini nilikuwa sitaki kumuona, sikumficha nikamwambia ukweli kwani alikuwa na haki ya kuamua lolote na isingekuwa vizuri kuwa na siri kati yetu kama nimeamua kujitosa kuwa naye.


Mungu akasaidia hakuniacha na akanisamehe kwa sababu alikuwa akinipenda kwa dhati. Miezi mitatu baadae mpenzi huyu akapropose nami nikakubali. Lakini kusema ukweli ndani ya nafsi yangu nilikuwa nimeshamfuta wakati tunakutana ikawa najilazimisha kuwa naye na sikujua hata kwanini nilikubali hiyo proposal yake.


Siku zilivozidi kwenda ikawa nazidi kuona simpendi ikafikia hatua kila kitu akikifanya mie nakiona kibaya. Sasa nashindwa kuelewa what is happening to me. Mwenzangu ananipenda sana na anajionesha dhahiri kama ananipenda lakini mimi nimeshidwa kurudisha mapenzi, harusi bado miezi mitatu na bwana harusi simpendi nifanye?


Labda nimuelezee kidogo jinsi yeye alivo kitabia.. Ni mtaratibu anaongea kwa adabu, nimsikivu na anamapenzi kwa ndugu zake na ndugu zangu pia. Mapenzi anayajua vilivyo. Zaidi ya yote kusema ukweli kaka wa watu ni mzuri anamvuto wa haja, anapesa za kutosha hatuwezi kulala njaa.


Ukweli ni kwamba kumuacha sitaki nataka kupewa ushauri vipi nifanye nipate mapenzi nimpende yeye kama yeye. Maana yake sijawahi kupata mtu mwenye mapenzi ya dhati kama aliyo nayo yeye? Lakini moyo wangu umekuwa mzito kwake.

Please Help kuyajenga haya mapenzi na si kuyabomoa. Kwani niliambiwa we can learn to fall in love!
yours Tumaini"

Dinah anasema: Tumaini hadithi yako ni nzuri mpaka raha kuisoma, ulichonifurahisha ni kuwa wazi kw ampenzi wako na kumueleza ukweli ulivyokuwa ni wanawake wachache sana wenye uwezo wa kufanya hivyo, wako radhi kudanganya wapate "kumchuna" mtu kuliko kumpa mtu ukweli na nafasi ya kufanya uamuzi wa busara.


Kutokana na maelezo yako hakika mpenzi wako anakupenda na hata wewe unampenda kwa maana ya "love" lakini humpendi kwa maana ya "dislike", kwasababu kama ungekuwa humpendi kwa maana ya "love" basi usingefikiria kutaka kujenga nae mapenzi wala usingetaka ushauri wa namna ya kumpenda au hata kuhisi mapenzi na badala yake ungeachana nae siku nyingi.


Nadhani umeingia kwenye uhusiano "serious" mapema kabla hujamfuta yule mtoto wa Balozi a.k.a Intruder, sasa kwa vile bado hujaondokana na zile hisia za kimapenzi na yule mtoto wa Balozi itakuwia vigumu kuachiamoyo wako kwa huyu mchumba wako.


Unajua, Enzi zile za Bibi zetu pengine hata Mama zetu, wengi walikuwa wanajifunza kupenda ikiwa wanafungishwa ndoa na wanaume wasiowapenda. Hali kadhalika wanawake hao walikuwa wakitumia mbinu fulani-fulani (sio madawa/uchawi) ili kuwafanya waume zao kuwapenda ikiwa itatokea wameozwa kwa wanaume waliowapenda lakini wao mwanaume hawawapendi na wanaishi nao tu kwa vile wazazi walitaka iwe hivyo.


Kumdondokea mwenzio kimapenzi ni kitu nadra sana (haikupati kama vile hamu ya kula)hivyo basi kudondokewa na mwanaume ambae anakila kitu unachokitaka kwa mwanaume a.k.a "the one" ni sawa na miujiza na unapaswa kushukuru Mungu, kufurahi na kulienzi penzi la huyo mtu aliyekudondokea ambae anavyote utakavyo mwanaume kuwa navyo.


Nini cha kufanya; Msifunge ndoa wakati moyo wako ni mzito juu ya huyo Kijana na badala yake tafuta uwezekano wa kuisogeza mbele tarehe ya kufunga ndoa kwa kushirikiana na Mchumba wako ili upate muda wa kutosha wa kuufungua moyo wako ili kupokea penzi lake kama sio kujifunza namna ya kumpenda mumeo wa baadae.


Kumfanya mtu akupende ni rahisi zaidi kuliko wewe kumpenda yeye hasa kama huna kabisa hisia, lakini kwavile tayari mmekuwa pamoja kwa muda na sasa ni wachumba inamaana kuwa kuna hisia fulani kati yenu, pia kuna vitu umegudua ambavyo vinakufurahisha kuhusu yeye mchumba wako na vingine labda vinakuudhi lakini kubwa zaidi ni kuwa kuna mengi mnafanya kwa kukubaliana, shirikiana na mnafurahia "interest" za aina moja.


Kinachopungua au kukosekana hapo ni wewe kuufungua moyo wako zaidi ya ulivyo ufungua hivi sasa na ili kufanikisha hilo basi fanyia kazi yote haya nitakayokueleza hapa chini, bila kujali mtiririko wake.

1-Kuwa mkweli na nafsi yako ilikujua unataka nini kutoka kwake in terms of mapenzi sio alichonacho.

2-Focus kwenye nini hasa uta-offer kwenye uhusiano wenu.

3-Jifunze kufurahia/kupenda na ku-appriciate kila effort anayoifanya juu ya uhusiano wenu.

4-Mfundishe/mwambie afanye vitu vile unavyopenda/furahia.

5-Jjitahidi ku-share moyo wako wote kwa mwenzio, kamwe usiachie nafasi kwa jaili ya mtu mwingine aliyepita (mtoto wa Barozi) au mabaya aliyokufanyia huyu Mchumba hapo mwanzo.

6-Weka wazi ndoto zako za kimaisha kwa mpenzi wako.

7-Weka wazi uoga wako au vitu unavyohofia kuhusu uhusiano wenu au maisha yenu ya baadae.

8-Tumia muda wako mwingi kuwa na mchumba wako, jinsi utakavyokuwa unamzoea kiukaribu zaidi ndivyo hisia zitakapoibuka.

9-Fanya shughuli pamoja, Mfano; kutoka kwa ajili ya matembezi, chakula, kuona ndugu, jamaa na marafiki, kujichanganya kwenye sehemu ambazo mara nyingi pea/couple huwa pamoja (hii pia itakusaidia kuzalisha hisia zaidi juu yake).

10-Ukipata nafasi ya kuwa pekeyako jaribu kum-fantacise anakufanyia mambo fulani matamu ambayo hajawahi kukufanyia.

Baada ya muda usiozidi miezi miwili utaona au kuhisi tofauti juu ya hisia zako....hilo likitokea au kutotokea basi nitafute tena.

Kila la kheri!

Comments

Anonymous said…
We neng'eneka halafu uachwe uje upate play boy ndio utajua joto ya jiwe maana unaonekana hutaki heri unataka shari na kwa muumba kila aombalo mja humpa sasa na wewe unaonekana unaelekea huko. Mtazamo wangu hata ukishauriwa wewe bure sbbu ushamchukia huyo jamaa (mtazamao wangu huu sio wa wengine watakaotoa maoni yao) sbbu kwa mtu anaefikiri sawa sawa kwa jinsi ulivyomuelezea huyu mkuu hakuna sababu ya kukosa kumpenda huyo mkubwa lakini yote kwa yote linapokuja suala la mapenzi huwa "siri ya mtungi......" kwa maana hiyo nafsi yako ndiyo inajua kwa nini humpendi mtu ambaye naamini unaamini ana vigezo vyote vya kupendwa.
Ndiyo maana nasema we "neng'eneka tu"Wacha tuone wengine watashauri nini.
Anonymous said…
Uamuzi mkubwa utatokana na wewe mwenyewe,kwani hiyo ni bahati kubwa kwako kuwa wote wa marafiki zako wanakupenda, na wote walifikia ile hatua wengi wanayoitamani ya kuwa na uhakika wa ndoa(matarajio ya ndoa)!
Hiyo ni bahati kwako, cha muhimu ni wewe kukaa chini na kutafakari nini unachokihitaji kwa mume mtarajiwa. Unataka aweje, unataka maisha yako yaweje, na ni nani, yupi kati ya hawo wawili atakayefanikisha hilo, je ukiwakosa hawo una uhakika wa kumpata zaidi yao
Nasema hivyo kwasababu moyo wako umekuwa mzito kwasababu ya huyo aliyeondoka, kuna kitu ambacho alikufanyia au anacho ambacho huyu wa Ulaya hana, au kuna malinganisho na mwingine. Ukikijua na kujua hilo, kinachotakiwa ni kuwasiliana na mtarajiwa wako kama kweli anaweza akaendana na `matarajio yako’ na ikibidi umweleze kiundani kuwa `ningelipendelea iwe hivi’
Nikuambie ukweli, wengi wa wanawake walio-olewa walikutana na `mitihani’ hiyo, lakini baada ya kuolewa wameweza kuisawazisha hiyo mitihani na kuwapenda waume zao kuliko awali. Kuna ambao mpaka ule muda wakuulizwa je umempenda bwana huyu awe wako wa ….’ Wanakuwa bado hawajakubaliana kimawazo, mioyo inasita na kujiuliza `hivi kweli..’Cha muhimu ni kuwa wawazi, mawasiliano na kujitahidi `kupenda’ kwani yeye kama ulivyosema `anakupenda’, mengine muachie mola kwani ndiye mjuvi wa `future yako’
emu-three
Anonymous said…
Pole na kutojielewa. Mimi ningekushauri ujipe muda. Na ndani ya huo muda jaribuni muwe close in terms of kuspend pamoja kwa sana. Muweke karibu. Mfanye kama rafiki yako. Mwambie matatizo yako na jaribu kumjulisha kwamba u r not 100% sure juu ya kurush kwenye maisha ya ndoa na ungependa akuoneshe namna gani angeweza kukusaidia mupite haya maji marefu.
Ni lazima uelewe kwamba mapenzi sio upepo, hayakupigi ghafla, mapenzi ni mazoea, mapenzi yanakuja taratibu, na mapenzi yanayokuja taratibu ni mapenzi ambayo hudumu muda mrefu, kuliko yale mapenzi ya 'kuhemkwa'
Nikiwa mwanamke mwenzio nakushauri umpe chance huyo mchumba wako wa nje ambae ameonesha yuko serious na anakupenda. Acha kutafuta mapenzi ya kihindi na drama in your life. Mimi nimekupita miaka miwili na nishapitia hapo ulipo, hujui nini kizuri kwako, uko busy unataka machekbobu, lakini hao watakupeleka pabaya. Huyu mwanaume ni wako na usimwache. Na tena umpende na kamwe usimuoneshe hana thamani kwako. Mwanaume ni mfalme. Wanaume wazuri ni wachache sana, umempata huyo basi mpende na muheshimu.
LL
So much said…
Mi nakubaliana na anon wa kwanza,na wengine hapa uamuzi unao mwenyewe coz jamaa ana kila kitu unachotaka au mwanamke yoyote kuvutiwa nae lakini still humpendi.Kama hujisikii kama vile yeye anavyojiskia unampotezea muda wake kwanini!?.Sina nia ya kuvunja bali huo ndio ukweli manake kama mtu hufeel hata anachokifanya kwanini usimwambie.Shilingi mwanakwetu unaichezea chooni kumbuka ikishatumbukia mpaka uje kuipata ni miaka.Kama unampenda wewe mpende,kuwa nae karibu.All in all me hata sikuelewi kwanini humpendi yani naandika tu hapa ila naona unamzingu na kumpotezea muda jamaa ukizingatia humpendi.Ukiendelea kufeel hivyo muacha jamaa akatafute mwenzio atakayempenda.
Enjoy
Anonymous said…
Huyo kijana wa watu masikini ningempata mimi ningemuweka katika macho yangu moyo wangu ungekua kweke tu.Umemwambia ukweli kuhusu mwaname mwingine na still anakupenda ama kweli unabahati lakini hujiamini!

Mimi natafuta vijana kama hao kwangu imebaki ndoto hasa vijana wengi wa ulaya wanawekwa na wanawake muhimu wanawake wapata tu service na love that is all.

Please ukiamua kumuacha naomba uandike hapa tena na nimtafute mimi
sema japo anakaa mji gani huku ulaya mie nitamtafuta na nitampa mapenzi ya kweli.

Lakini embu toa picha yako na yake labda u mzuri kumshinda na unaona hapo ulipo utapata tajiri na mzuri utastarehe. Kama ni hivyo embu niibie siri ili angalau na mie niambulie kwani huku kwetu hamna tajiri wala masikini lakini wanawake wapo wengi kuliko wanaume na wanaume kwetu ni almasi!

Good lukcy
Anonymous said…
LISTEN MY FRIEND WE KAMA NI MKRISTU OMBA MUNGU AKUPE MATUNDA YA ROHONI ILI UWEZE KUMPENDA HUYO JAMAA MAANA KAMA IMEBAKI MIEZI 3 NDO HARUSI WHAT DO U EXPECT WACHA UJINGA BAHATI UMEIPATA WATAKAICHEZEA GO TO CERTAIN CHURCH FOR DELIVERENCE SO THAT U WILL BE FREE GAL. GODBLESS U.
Anonymous said…
Habari zenu. Jamani unajua hakuna kitu kibaya kama kulazimisha mapenzi, athari zake ni mbaya sana na mara kwa mara zinajitokeza wakati mmeshazoeana kupita kiasi au tayari mkiwa kwenye jiwe, hapo ndio cha moto utakiona. Anyways point yangu ni kuwa mtu anaweza akawa na vigezo vyote vya mpenzi mzuri lakini kwako visikuvutie, au vinaweza vikakuvutia kwa kiwango fulani lakini zile inner feelings za mapenzi hazipo kabisa. Anaweza akawa mpole, mnyenyekevu, anayejali na mwenye mapenzi ya kweli lakini ndugu zangu kama feelings za mapenzi hazipo kwako hazipo tu, hata ufanyeje! cha ajabu unaweza ukawa attracted na mtu mwingine tofauti, pengine ana mtoto nje, hana hela, hajui kuvaa vizuri na huyo ukampenda kuliko almasi. Kwa hiyo mnaosema aangalie eti labda hataki heri anatafuta shari, au eti aangalie labda atakuja kupata playboy ajute mnataka ang'ang'anie kwenye kitu ambacho hakimsisimui??? hayo maneno ni rahisi kusema kama situation hii haijakufika. Mapenzi yako very complicated na mara nyingi yanabakia kuwa ni mystery, kuna watu wanapenda wazee, yaani hata umwambie nini hakuelewi. Ushauri wangu mimi ni kuwa kama unaona huna feelings na huyo mtu pliz pliz achana nae, tafuta yule utakayempenda maana ukilazimisha utaja juta huko mbeleni, kila la heri.
Tina.
Anonymous said…
Tatizo lako ni common tuu, kwani wengi wetu hatujui tunachotaka mpaka tukikosa tulichonacho. USHAURI NAMBA MOJA USIKUBALI KUINGIA KWENYE NDOA KATIKA HALI HIYO KWANI NDOA WILL NOT SOLVE THE PROBLEM INSTEAD IT WILL ESCALADE IT. NOW WHAT NEXT?

Nadhani ukweli ni kwamba unaitaji value test kuangalia kama kweli unampenda huyu jamaa au laa? Au kama utaweza kubuild love nae au laa? Jee utafanyaje value test? Kwanza andika chini nini unataka kutoka kwa mwanaume, Yaani moja mbili, tatu na nk. Ukisha andika unavyo vitaka kutoka kwa dream men, then andika alivyo navyo Mpenzi kutoka Ulaya, kama hana hata nusu ya unavyo vitaka then NO LOVE baina yenu, sorry but SUCK IT and let the sweet talk Mr Mpole Goo. But kama ana hata nusu ya uvitakavyo kutoka kwa mwanaume then find a way to build a bridge.

This is how: Muombe date, i prefer place ambayo mtakuwa private with less distruction. Kaa nae chini, kisha mwambie kwamba una worry sana kuhusu longtime committement baina yenu, mwambie nini kinacho kuogopesha and then see atasema nini. Na dhani yeye atakacho fanya ni kuconfort kama anataka kuwa na wewe. Then baada ya hapo you need to start build Love. Kuwa unajali tafuta vitu ambendavyo then mfanyie, surprise zinawakamata wanaume wote.... Things like unatoka saa ngapi kazini then una msurprise. You can build love kama kuna potential ya kubuild it. Kama hakuna Please Muachie kaka wa watu kabla huja muhurt feeling zake wakati is too late....

Ed
Anonymous said…
Binti, kama moyo mzito kwa huyo jamaa, tafadhali sana usilazimishe jitahidi kuvuta subira usije ukaenda mbio mambo hayo ni mazito sana.Kitu kuoa au kuolewa na mtu fulani usikichezee wala kukiendea papala, na wala usivutwe na mambo ya juujuu tu au ushawishi wa watu.majuto ya ndoa ni sawa na msiba mkuu, tena afadhali hata msiba mtu akifa amekufa utasahahulakini siyo kitu ndoa.

Mimi nimekuelewa sana, ana wala sifikiri hata kidogo kuwea labda unampenda yule mwingine, ninachojua ni kwamba bado unahitaji muda wa kutosha kulitafakari jambo hilo.Mtu asikudanganye akalinganisha na nyakati za mahusiano ya mapenzi akafikiri ndo ndoa inaweza kulazimishwa.Please be carefuly, unaingia kwenye mnyororo wa kufungwa ambapo utakuwia vigumu mno ukishaingia hapo.Chukua muda mrefu kidogo kutafakari na zaidi ya yote muombe Mungu akupe jibu sahihi katika jambo hilo.

Kumbuka kuwa kila penye kufuka moshi pana moto!!!usiangalie kuwa jamaa anakupenda sana, kwa sababu upendo ni kama moto unaoweza kuwaka na kuzimika.Moyo ukisita heshimu na chukua tahadhari.nakutakia kila la heri katika jambo hilo na nakuombea Mungu akuwezeshe kuamua vema.
Anonymous said…
MIMI NINACHOKUSHAURI HUYO MWANAMME ANAKUFAA SANA..KWA SABABU KWENYE UHUSIANO MAELEWANO NDIO SILAHA YA MAISHA MAZURI KATI YENU. HUYO KAKA ANAONEKANA NI MUELEWA SANA NA ANAEJALI.
KAMA ANONY MMOJA ALIVYOSEMA, KINACHOKUSUMBUA WEWE NI KULINGANISHA NA YULE ALIYEONDOKA NCHINI..KUNA KITU ULIKUWA UNAPATA KULE AMBACHO KWA HUYU MTARATIBU HUKIPATI. KUMBUKA HAMNA MWANAMUME ALIYE PERFECT..KUNA VINGINE HUYU MTARATIBU ANAVYO AMBAVYO YULE MWINGINE ALIKUWA HANA. SASA HILI LISIKUSUMBUE SANA NI KITU CHA MUDA MFUPI....
MIMI SIAMIN LOVE ITS ON FIRST SIGHT, LOVE INAJENGEKA NA MUDA. JINSI MNAVYOKAA PAMOJA NA KUFANYA KILA KITU PAMOJA KAMA KUNA MAELEWANO NDIPO UPENDO WA DHATI HUJENGEKA. KWA HIYO USIOGOPE, UPENDO UTAJENGEKA TARATIBU KWA SABABU HUYO KIJANA ANAONYESHA ANAKUFAA. INGIA TU KWENYE NDOA, JISAHAULISHE MAPENZI YA ALIYEPITA NA NDOA YAKO ITAKUWA YA FURAHA SANA. AU KINGINE NI KWAMBA UNA WASI WASI LABDA ATAKUJA ALIYEBORA ZAIDI YA ULIYENAE..HILI KOSA USILIFANYE. ANAWEZA AKATOKEA MWINGINE UKAHISI HUYU NDIYE ROHO INATAKA, SIKU UKIINGIA KWENYE HUO UHUSIANO ROHO ITAKUSUTA UTAANZA KUFIKIRI LABDA NINGEBAK NA YULE WA UTOTONI MAISHA YANGEKUWA MAZURI..WAKAT HUO MAJI YAMESHAMWAGIKA.
SO DEAR OLEWA TU..JITAHID UWE KARIBU NAE NA UPENDO BAINA YENU UTAKUA TU..KITU KINGINE
Anonymous said…
my dear pole sana kwa yaliyokukuta lakini naomba kukwambia kitu kimoja kua usikubali kabla moyo wako hauko tayari kuingia kwenye ndoa coz itakuja kukuumiza sana baadae. kama watu wengine walivyokoment jaribu kukaa nae kuongea nae na uone kama anashaurika ili muweze kuongea na kushauriana ili aweze kukusaidia nawe kuondoa hiyo hali. naongea hivi si kwa maana naongea tu i have experience this myself na bado naumia mpaka sasa huwa silali niko na mawazo tu kama hii hali itakuja kwisha ama this iz going to be my life style. i have story like urs kwamba kuna mtu alinipenda sana na akawa tayari kunioa na amenioa na nina miezi miwili sasa tangu anione. mimi alikua ni mtu wangu wa kwanza kuwa kwenye relation kwa sababu sikutaka kuwa na mtu na kutunza heshima yangu mpaka niolewe na anikute niko salama nashukuru nimefanikiwa hilo. nilikua simfeel sana nikasema kuwa nitajaribu kuwa nae karibu na kufanya vitu ambavyo nitampenda zaidi. lakini imekua tofauti. nakushauri kama anaweza kuongea nawe akusaidie juu ya hilo itakusaidia sana hata wewe mwenyewe kurudisha upendo kwake kuliko hivyo ambavyo moyo wako bado haujaridhika