Ndugu wanahatarisha Ndoa yangu-Ushauri

"Habari za kazi dada yetu mpendwa, baada ya kusoma ile stori ya kaka aliyemsaidia mdogoe na kisha kumpindua, nikaona nami niseme yaliyonisibu.

Mimi ni mdada wa 29 umri, nimebahatika kuolewa miaka 8 iliyo pita. Namshukuru mungu nina amani na ndoa yangu. Nia ya kuja hapa ni kutaka kujua hawa ndugu wadogo wa damu, binamu, mashangazi na wengineo tunao wakaribisha majumbani kwetu na kuwaonesha upendo wa juu na baadae kuharibu je tuwafanyaje?


Dinah mimi naweza kusema mume wangu kidogo Mungu kamjalia si sana ila kiasi cha pesa kwa mwezi mshahara unaridhisha. Sisi katika hili nikaona kwanini nisimwendeleze mdogo wangu Juma nimsimamie mpaka atakapo maliza miaka yake 3 au 4 ya chuo bila kuchukua mikopo.

Nikampanga mume wangu naye akaona ok, huruma bado ikaja kwanini huyu Hadija naye nisimtoe, ok kutokana na mambo mengineyo kama mwanamke au matatizo ya kwenu si kila mara unakuwa unamwambia mumeo utacho kwa bure, basi nikawa nafanya siri nikampangia H, chumba pale makumbusho huku akiwa ni waiter kwenye hotel.

Basi ikawa ndio mtindo kodi ikiisha anakimbilia kwa daad, baadae H akajisahau akaamua kuacha Uweitress, ikawa ndio mzigo unaongezeka zaidi kwani pamoja na kumlipia chumba kila mara ilinibidi pia kumpa pesa ya matumizi. Baadae nikasikia anaboyfriend ambaye kula kulala hana kazi ila yeye H ndio anamtake care, sio siri dada, roho iliniuma sana yaani miim nimpe pesa ya matumizi tena akamuonge boyfriend wake wakati wazazi wangu kijijini wanakaa bila matumizi ya kutosha.


Si ikabidi nikae nae chini na kunimuliza H mbona nasikia hivi na hivi, unajua yeye anaongea sana na mtundu mtundu kuliko mimi ila utundu wake si wakimaisha, majibu aliyonipa ni "hee kwani wewe utombwi? unataka nisitombw? wewe ulivyomleta bwana wako nani alikushauri, mume mwenyewe sura mbaya".


Dinah, nilishindwa kuvumilia nikamjibu kwa hasira "sura mbaya mbona pesa zake wazifutafuta?" pia nikamjibu "hao mahandsome nikiwataka ni wapo kibao pesa ninayo nikiamua namchukua napiga pamba anatoka, pamoja na sura mbaya ya mume wangu ila hatulali njaa huyo handsome utakula sura yake huko ndani? kwanza kwa huhandsome gani kiboy friend chenywewe sura mbaya, pesa ya kula hana, wa nini ?" nikamaliza. Basi yakawa malumbano, kitu ambacho kiliniuma sana.


Basada ya muda kupitai tukayasahau hayo yote, akawa na interest ya saloon nikaona njia bora ni kumpatia mtaji wa hicho akipendacho ili azuie kuomba matumizi kwangu. Nikajikaza nikatoa kama milioni 3 anunue vifaa pamoja na kukodi sehemu, kwani baada ya mwaka tena si mkataba ukaisha akawa hana tena pesa ya kurudia kulipia.


Mimi nikauchuna nikamjibu ukitaka funga rudi kwa wazazi kijijini nimechoka. Mwaka ukakata hana chanel nikamwita nikamwambie kasome upendacho ,nikalipa ada ya miezi sita kaenda shule mwezi mmoja tu, nikamuliza kunani? Akasema "ooh mimi sitaki kusoma" kwa sababu alishanunua vifaa vya salooni nikamomba atafute tena frem nitamlipia mwaka na nitampa tena mtaji wa madawa ya saloon, kweli alipata frem sayansi kwa mwaka laki 8 pamoja na bla bla milioni1.2 .

Jamani hata kufungua kinywa na kusema asante, nilibaki naduaa. Kuna siku anakaa na kumsifia ndugu yetu mmoja ambaye alishaolewa miaka 15 iliyopita ee wamejenga, wewe sijui utajenga lini? hao hao wamejisahau kuwa ndio chanzo cha kutokujenga kwangu kuwaangalia wao wamekula nini wamevaa nini watafua na nini, alafu mtu anakuja anakupitia wewe kimafumbo.


Mbaya zaidi huyu ni mdogo wangu wa damu toka nitoke hana udogo wa sana kupishana kwetu miaka 2 tu. Si huyu tu Dinah nimemtaja huyu kwasababu wa damu, nimemseidia binamu, akatoka kunisimanga kwa watu, ni wengi ndugu waliopata msaada wangu ila naambulia kutetwa na kusimangwa.


Hebu nielekezeni niishi vipi na hawa ndugu? Sometimes nasema hili nalifumbia macho ila utakuta roho inanisuta nkuona haifai, pia wanaponizidi nawaeleza mimi si tajiri wa hivyo wanvyofikiria siwezi kusaidia kila mtu, kwani hata Kikwete ana ndugu ambaao hawezi watosheleza itakuwa mimi kapuku?


Kuna baadhi ya Makabila wakiona na unaishi kwenye nyumba kubwa, gari 2, 3 zinapumua garden, basi kila mmoja anataka kuishi kwako.hususani kabila la ........ni hayo tu Dinah na wachangiaji wengine, naomba mnishauri nifanyenini ili dungu wasije haribu ndoa yangu?"


Jawabu:Hihihihi ni kweli kuna Makabila Fulani Fulani akyanani huwa wanaamia na ukishangaa-shangaa na mumeo wanachukua, tena basi wengine hata undugu wenye ulipoanzia wala hujui. Mbaya zaidi hawajali kama umepanga au umejenga, kinachoudhi hata kama unachumba kimoja wako radhi kulala jikoni au kwenye upenyo ilimradi tu wakuharibie uhuru na mumeo.....tuliache hilo!


Shukrani kwa ushirikiano wako na uvumilivu kwa kipindi ambacho nilikuwa nahamisha makazi. Suala lako sio geni miongoni mwetu au niseme kwenye sehemukubwa ya jamii nyingi za kiafrika, ndio kitu pekee kinatufanye tuwe tofauti na jamii nyingine Duniani kitu hicho ni “Family values”.


Ni wazi kabisa kama wewe ni mkubwa kwenye familia yenu unalelewa ktkmazingira ya kuwa mfano kwa wadogo zako, kuwa kiongozi wao na pale unapokuwa mtu mzina na kuanza maisha yako unahisi kuwa na majukumu Fulani juu ya ndugu zako na vilevile kuna kahatia Fulani unahisi ka kusaidia wazazi hasa kama hawana kipato au umri umekimbia (wazee).


Kitu ambacho huwa tunashindwa kukivumbua kama alivyosema mmoja kati ya wachangiaji ni kuwa kuzaliwa tumbo moja kwa maana ya baba na mama moja haina maana kuwa mtakuwa na uwezo wa kufikiri wa aina moja, upendo na kuthamini wengine in the same way.....ndio ni ndugu wa damu lakini tukumbuke sote ni “individuals” na tunafanya mambo “individually”.



Nia na madhumuni yako ilikuwa kumsimamamisha mdogo wako lakini kwa bahati mbaya hana shukurani na wala hathamini jihudi zako za kutaka kumsimamisha kimaisha ili ajitegemee nap engine awe na kidogo kama wewe au kama akiongeza bidii basi afanye makubwa zaidi ili asaidie wengine.


Kuna ndugu ambao huwa na mafanikio lakini huwa wawasaidii wenzo kijikwamua na badala yake huwapa samaki wenzao na sio nyavu kama alivyo gusia mchangiaji mwingine hapo kwenye maoni (nimependa sana msemo wako Kaka uliyesema mpe nyavu akavue samaki na sio kumpa samaki kwani atarudi tena kuomba samaki).


Sasa wapo watu wanahisi fahari kuombwa-ombwa kila kukicha na ili kuhakikisha hilo linaendelea watakuwa wanakupa “samaki” badala ya kukupa “nyavu” ukavue Samaki utakao. Wewe dada yangu ulitoa samaki na kisha Nyavu lakini mdogo wako anazidi kukurudisha nyuma kimaendeleo na kuonyesha kuwa hajali anakucheka kuwa unashangaa tu wakati wenzako wana majumba.


Hey, hakuna radhi ya ndugu si ndio?!! Timua huyo mdogo wako asie na heshima, adabu wa shukurani, na sasa “focus” kwenye familia yako, linda ndoa yako kwa kutumia muda mwingi na mumeo badala ya kufikiria hao wanandugu wajinga-wajinga, andaa maisha ya watoto wako ambao ndio wajibu wako na ukishangaa sasa na jambo likatokea ujue hao ndugu zako watasimamnga na kusumbua watoto wako kama wanavyokufanyia wewe hivyo mama changamka na anza kuwarekebishia maish ayao ya baadae hivi sasa.

Huyo mdogo wako ni mtu mzima na anapaswa kuendesha maisha yake kivyake.

Kila lililo jema mdada.

Comments

Anonymous said…
ACHA KUBWETEKA NAO FANYA MAMBO YAKO UKIJA PIGIKA HAOHAO NDIO WATAKUA WA KWANZA KUKUSIMANGA
NDUGU KAMA HAO NI WAKUWAFUMBIA MACHO MPAKA WATAKAPOTIA AKILI
WEWE MWENYEWE UNAYATAKA HAYO WAMESHAJUA UDHAIFU WAKO
Anonymous said…
Pole sana dada yangu. Uvumilivu ni jambo la kheri,lakini lina mwisho wake hasa yule unayemvumilia anapozid kukubeza na kukudharau.
Msaidie mdogo wako msaada wa mwisho, ktk msaada huo muulize yeye mwenyewe anataka umfanyie nini? Na wala usimlazimishe fani kwani atakapoyumba atakwambia wewe ndio ulimchagulia.
Kuhusu ndugu na jamaa ni vema ukaendelea kuwasaidia tena wape msaada wa kuwaendeleza kimaisha sio uwasaidie kwa kuwajaza nyumbani na kuwalisha. Ikiwezekana wasomeshe fani wanazopenda e.g ufundi, si lazima uwapeleke secondari hata kama hawapendi.
Kumbuka kuwa kutoa msaada ni jambo la kheri kwani hata ukijilimbikizia hutakufa nayo hayo mapesa wala magari.
Kuhusu tabia ya kumbeza mumeo eti mbaya si jambo jema kwani utamu na uzuri wa mume/mke aujuae ni mke/mume. Kwa mantiki hiyo kama mumeo ni wako na ulimpenda ni waz utak uwa jasiri kusimama mbele ya kadamnasi kuutangazia umma kwamba huyo ni mumeo na unampenda. Huna haja ya kulifikilia hilo na hali wajua kuwa akipendacho yeye c lazima na wewe ukipende, na wala ukipendacho wewe si lazima na yeye akipende.
THE MESSAGE [ never pretend to love some one who you dont love because you will hurt him or her when a right person comes.]
BY Mwatima A.
Anonymous said…
Mhhhhhhhhhhhhh du! wewe dada hizo pesa mnazipata kifisadifisadi au ni zile mnazozipata kwa taabu na kujiumiza??

mdogo mtu umempa mamilioni ya mtaji,huyohuyo anakutukana na kumtukana mume wako amabye ni shemeji yake, tena kwa tusi baya, na wala hajamtendea jambo baya lolote.Yaani mume wako atukanwe hivyo na ndiye mhangaikaji?? na bado uendelee kumtolea mamilioni?

Kama hiyo haitoshi, ni huyohuyo unampa matumizi na yeye anahonga lijamaa la kumtomba, linakula kuma yake, linakula chakula chake, linalala chumbani kwake, na bado unamvumilia kumwongeze mamilioni ya pesa!!!

kama hiyo haitoshi, umempa nafasi ya kusoma na kutoa mamilioni ya pesa, kakatiza njiani hataki,mapesa yameyoyoma bure, na bado ukatoa tena mamilioni ya pesa kumwanzishia tena mradi wake.Na bado hana shukrani!!!
na bila shaka anaendelea kubeba limboo la mtu wake,na pesa juu.Loo hiyo kali.

Bila shaka huyo mdogo mtu anajua hayo mamilioni na ninyi mnayatoa kifisadi na ndiyo maana anajaa kiburi na kwamba labda nanyi mnaogopa atawatoa kimasomaso mkimfanyia stop.

halafu kama kweli anajua mnamhangaikia yeye na bado awasemeseme kwamba hamjajenga mbona fulani kajenga, du hiyo ina sababu.

Kama kuna watu wavumilivu wewe dada umejitahidi, lakini lazima ujue kuwa hayo unayafanya ksiri bila mumeo kujua, hivyo kwa minajiri hiyo lazima ujue unacheze pesa tena vibaya mno kwa mtu asiyejua nini mnamhangaikia.Ni dhambi kubwa kuchota mipesa hiyo bila idhini ya mumeo, tena unayemsaidia ndiyo huyo anakutwika mituzi juu,mbaya zaidi anatukanwa hata anayekesha kuyatafuta!!!

Huyo mdogo wako achane naye kwanza ulimwengu umfunze, kwanza ni mtu mzima na anatamani kutombwa tu ndiyo raha yake.kwa nini uumize kichwa kwa kuwa eti mdogo wa damu asiye na akili huyo mpuuzi?? tena msichana!! hiyo sijaona maana wasichana wanakuwa watulivu sana anapojua anasaidiwa ile ajiendeleze kimaisha tofauti na wanaume.

Mimi niko hapa ughaibuni, ninachofanya ni kusaidia ndg zangu kusoma tu hakuna cha biashara.mtu asome ili ajifunze na apate ujuzi.Huyo mdogo mtu kakimbia shule atabaki bwege siku zote,biashara gani itaendeshwa kigizagiza tu katika utandawazi huu????Pole sana dada.Achana naye huyo!!
Anonymous said…
Nadhani hii nikasumba ambayo ipo Tanzania lakini lazima mjue jinsi ya kukomesha.. Mimi nimejifunza mengi sana baada ya kuishi nje ya Tanzania, na mmoja ni kuwa accountable kwa maamuzi yako. Yaani kukubali matokeo ya maamuzi unayofanya.. Sasa kama wadogo zako watakuwa wanamess around kisha wanarudi kwako kuchukua tena pesa na wewe unawapa, hapo hakutokuwa na la kujifunza.

Nitakupa mfano wa wadogo zangu, nimewaambia kwamba sasa mnakwenda college wote mtapa laki 2 kwa mwezi, kwa miaka yote mitatu. Condition ya pesa ni kama ifuatavyo grade zote lazima ziripotiwe kwangu, pass ya C kwenye somo lolote means ni deduction ya 10,000 kwenye posho yako ya mwezi kwa mwaka mmoja. Shule nalipa miaka 3 maana yake kusup sio option. Na mwisho kila atakaye maliza anatakiwa kumuweka mama yake kwenye bajeti yake kwa miaka 2 ijayo. Hii ni njia muhimu ya kuwaambia kwamba hakuna FREE LUNCH. Mimi nilisoma degree kwa kubeba box. So, wao watakwenda bila box wala mkopo lakini lazima walipe fadhila.

Hivyo dada yamgu, dawa ni mmoja tuu. Muachishe mtoto ziwa, yaani muite mwambie mama mdogo kwa miaka 2 nimekuweka kwenye payroll yangu nikitegemea utasimama mwenye, lakini naona matokeo yake ni umerudi kutambaa hivyo, naomba nikwambie rasmi kwamba kuanzia leo mimi na wewe tutaendela kuwa ndugu bila kuombana pesa. Msaada wowowte nitatoa na si pesa. Thanks. Baada ya hapo muache aende akaone dunia kama ina fadhila.
Anonymous said…
Hakika imenigusa kama vile unanisema mie,yamenitokea na nakabiliana nayo kwa uwezo wa Manani.Ushauri kaa na mwenzio muelezane kinagaubaga kuhusu misaada yenu kwa wanandugu iwe kwa kiasi na kiasi kikubwa iwe kwa familia yenu na si kwa familia zenu(Ndugu)Kila siku ukisaidia utaonekana mpumbavu kwa wale unaowasaidia.Watakudharau na kukucheka
Anonymous said…
Kwakeli hili swala la wandugu kuwa mzigo ni la wengi, na tatizo kubwa ni pale unapojitolea kujinyima kwa ajili yao, nabado hawana shukurani, au hawathamini kile unachowatendea. Na wengine wanakuwa na tabia za ajabu za kukudidimiza, kwa kupotoka na kujiunga kwenye Makundi ya kuvuta bangi na umalaya.
Hali hii inawafanya wengine waonekane wabaya pale wanapoamua kumtimua au kuwa mkali kwa ndugu zake. Lakini mbaya zaidi ndugu hawo wanaweza wakachangia kuharibu ndoa za watu kwa uchonganishi au hata kuwa na mahusiano ya siri na shemeji zao. Zipo ndoa zimevunjika kwa dada mtu kumkuta mdogo wake akingonoka na mumewe, au kaka mtu kumkuta mdogo wake akila uroda na mkewe. Fikiria mwenyewe hli kama hiyo ikikukuta wewe utafanyaje. Kwa wanawake wengi wanaamua kuondoka , sasa wewe mwanaume utafanyeje, talaka, na mdogo wako umfanyeje?
Kwahiyo ni vyema, kama una nafasi ya kusaidia uangalie mambo mengi kabla, na ujaribu kutoa shule na sheria za mahali kwako. Tusichoke kukanyana kuhusu yale yanayoharibu hata kama wanandugu watakasirika, kwani kwa kufanya hivyo utasaidia mengi.
Mimi nakushauri ujikune pale mkono utakapofikia, weka malengo ya kusaidia yakitimia basi, na wewe ujiangalie msimamo wako, kwani ukiendelea kutoa tu, utazidi kumlemeza mlengwa, na mwisho wa siku utakwama na wakati huo huna ulichofanya.
Kusaidia ndugu ni vizuri na ndivyo jamii zetu tulivyokulia, lakini usaidie kwa malengo, huku na wewe unajiangalia maisha yako ya baadaye.
emu-three
Anonymous said…
Mpendwa Mdada,
Pole kwa yaliyokukuta huyo nduguyo H sio wa kumchekea kabisa! kwanza hana shukrani wala adabu hana akumbuke kuwa wewe ni dada yake unayemuweka mjini (pamoja na jeuri yake yote)kwanza unamuendekeza tu coz wasichana wa umri wake wana waume na watoto yeye bado anasubiri kufadhiliwa na dada then analeta jeuri!!??. Me naona usitishe msaada kwake na akija tena kukulilia shida mwonyeshe njia ya kijijini kwenu mpe na nauli akawasaidie wazazi kulima akaone maisha yakoje, hapa mjini naona anajidekeza akijua yupo wa kumuokota akiishiwa amekufanya wewe kama ATM yake. Na nakushauri misaada kwa ndugu iwe basi labda ile ya muhimu sanaa, uanze kufikiria kufanya vitu vya maana kama kuwa na assets kwa ajili ya watoto wako. Kumbuka kuna leo na kesho manake hauwezi kutegemea ndugu yako ndo atakuja kusaidia watoto wako ndugu wenyewe ndo kama hao wenyewe kujibeba issue!.
Anonymous said…
Mpendwa Mdada,
Pole kwa yaliyokukuta huyo nduguyo H sio wa kumchekea kabisa! kwanza hana shukrani wala adabu hana akumbuke kuwa wewe ni dada yake unayemuweka mjini (pamoja na jeuri yake yote)kwanza unamuendekeza tu coz wasichana wa umri wake wana waume na watoto yeye bado anasubiri kufadhiliwa na dada then analeta jeuri!!??. Me naona usitishe msaada kwake na akija tena kukulilia shida mwonyeshe njia ya kijijini kwenu mpe na nauli akawasaidie wazazi kulima akaone maisha yakoje, hapa mjini naona anajidekeza akijua yupo wa kumuokota akiishiwa amekufanya wewe kama ATM yake. Na nakushauri misaada kwa ndugu iwe basi labda ile ya muhimu sanaa, uanze kufikiria kufanya vitu vya maana kama kuwa na assets kwa ajili ya watoto wako. Kumbuka kuna leo na kesho manake hauwezi kutegemea ndugu yako ndo atakuja kusaidia watoto wako ndugu wenyewe ndo kama hao wenyewe kujibeba issue!.
Anonymous said…
cjawai kuchangia kwenye hii blog,me waga nasomaga tu,ila matatizo yako yamenikuna,kuna kipindi nilisoma interview flan ya hayati tupac shakur,alikua anasema "just bz some1 is born in to ur family daz not mean u will stay family all your life" kwaiyo hata hao si ndugu we angaika na mambo ya familia yako,mumeo na watoto,ukikunwa sana kumfadhili mtu mfadhili mbwa,mana binadam hawana shukurani
Anonymous said…
Pole sana Dada.Mie sina mengi ya kusema ila wewe umemlemaza huyo mdogo wako.Pili na yeye hana shukrani kabisa, cha kufanya jaribu kuendelea kutafuta mbinu ya kumsaidia ila usimtupe huyo ni damu moja sio mtu baki.Na ni vigumu san kumsaidia kwani yeye ni mvivu na hana akili kabisa.Tafuta mbinu usimtupe ila ni kazi ngumu sana.Pia usisahau kumwomba Mwenyezi Mungu atakusaidia.Watu wengi wamemsahau Muumba,ebu jaribu kuomba,na mweleze Mungu matatizo yako pia hata mdogo wako amemsahau Mungu anafanya mambo kama Limbukeni.Nakutakia maisha mema na yenye amani.
GOD LOVES US:

Happiness.
Anonymous said…
Pole mdogo wangu,

Ndugu ndo walivyo ! Mbona wewe unajibiwa vibaya na kusimangwa kuwa hujajenga, kuna wengine wanaitwa wachawi kisa eti mume anampenda na wana hela.

Muumini aliimba kuwa: NDUGU LAWAMA.
Wewe endelea tu kuwasaidia Mungu atakulipa tu, na wenyewe hawatakuwa na amani wa maendeleo yoyote kwa kuwa wamejibweteka tu.
Anonymous said…
Aiseee, Pole sana!!!
Napenda tu kukutia moyo kuwa hao ndugu tegemezi wako kila mahali. Ila unatakiwa mwanamke kuwa na akili kichwani. Dunia ya leo si kama ya baba zetu. Sote tunasaidia lakini kwa ujanja sana.
Kosa ulilofanya ni kuwaendekeza. Unachofanya ni zaidi ya kawaida. Ndio maana hujengi. Hapo umemtaja tu H, bado binamu, kaka, dada, wanao je! Masikini.
Sikufundishi uchoyo. Kama hujajenga na mipesa yooote uliyo nayo sioni kama unabarikiwa kwa kuwasaidia ndugu kama hao. Inakusaidia nini kama una gari tatu halafu unapaki kwa jirani! Inakusaidia nini kumsaidia mdogo wako ambaye siyo productive!?
yaani, mpaka nashindwa kuongea. Mimi ni mwanamke mwenzio. Na nina kazi nzuri na tegemezi kibao. Nawasaidia na maendeleo yangu naangalia. Nafanya hivyo kwa kutambua kuwa baadae nitachekwa.
Kalagabaho!
Pengine wengine watasema zaidi.
Mkereketwa tu.
Anonymous said…
Mh Dina mie nna yangu ila ya mwenzangu balaa. Ninachowezakumshauri ni kwa yeye kuwa jasiri na kuwakalisha hao wadogo zake na kuwaonya. Hakuna mtu aakayemlaumu kama akiamua kuwafukuza hapo nyumbani au kuacha kuwasaidia kwa sababu amejitahidi sana ni kiburi chao tu. I wish ningekuwa na mume mwelewa kama wako maana ni mvumilivu ila angalia waogo zako wasijekukufanya mkagombana na mumeo bure.

Hayo ni maisha yako kama unamsaidia mtu asiyetaka kujisaidia and then anakulaumu kwa kweli hizo ni shukrani za punda mtimue kabla hajakupiga mateke.

Suzanna
Anonymous said…
ndugu yangu wee, siku zote watu wanasema mpe mtu nyavu za kuvulia samaki na si samaki, kwa sababu samaki wakiisha kwake atarudi umpe samaki mwingine.
Kwanza mdogo mwenyewe naye anaonekana ana jeuri, wala hajitambui kabisa. Kwa sababu angejitambua angejijua kuwa alikotokea ni wapi na ili asirudi alikotoka basi angefanya juhudi kwenye kile akifanyacho. Umeshawahi kukaa naye chini mkasaidiana kueleweshana kwamba ni nini hasa anachotaka kufanya in life? Kwa sababu unaweza kukazana kumjazia hivyo vifaa vya saloon kumbe hata biashara yenyewe hana interest nayo. Na mwisho wa siku, kuliko kuhangaika na tupa pesa yako bure, bora angepelekwa shule aweze hata kufumbuka macho kuwa hiyo biashara ya saloon aifanye kwa upeo gani. Hofu yangu ni kuwa, inaonekana toka mwanzo ulimuonyesha hisia kuwa mko matawi ya juu (usikwazike, ni msemo tu), kwa hiyo na yeye akafuata mto unakotiririsha maji. Mpe hali halisi, kwamba hana utoto wowote wa watu kuacha shughuli zao kumsaidia mtu asiyetaka kujisaidia mwenyewe....huku sura kavu, na wala usimuonee haya kwa sababu mwisho wa siku asipoweza kusimama kwa miguu yake mwenyewe, utakuwa mzigo wako kweli kweli...Tena muambie na yeye afikirie kujenga nyumba yake mwenyewe na siyo kazi kuonyesha majumba waliyojenga wenzake (hana haya kweli huyo mtoto!)
Anonymous said…
Dinnah hiyo msg ya mwisho ya 11.54.00 AM, niliyotuma ilikuwa nimechangia kwenye kisa cha asif king "MKE WANGU ANANIFANYA NITAKE KUOA MARA YA PILI" nashangaa nimeikuta huku sijui nilituma vibaya, naomba uihamishie kule
Anonymous said…
To whoever this may concern, this is rubbish huwezi msaidia bogus kama huyo just bcoz ni ndugu wa damu.....ndugu lawama nakejeli kama huyo hana mana hafai hata bure, huyo inaonekana ni muuzaji tu wa K, yaani nime boreka na hii habari basi tu, kusaidia kuzuri lkn sio kwa bogus kama huyo. eti wenzenu wamejenga!!!! duh!


Aidha wewe muuliza swali badirisha namna ya kumsaidia huyo mpumbavu,nimependa presentation ya kumpa nyavu sio samaki, thts brilliant!!! hongera kwa aliyetoa! ila nasikitika kupoteza fedha zako bure tena za kuiba bila mtafutaji kujua??!! ni risk sana unafanya wewe dada, huyo husband ni ngumbalo nini hajui hata mgt ya hela zake au fisadi?? au kipofu?? hizo bila shaka hazina jasho, huwezi tumia ovyo hivyo fedha zenye jasho bana lol.anyways ndo hivyo lkn huyo dogo ndo wale cheka na kima utavuna mabua! muache auze tu ndo atajua maisha nini, so stupid!

lajk
Anonymous said…
Mara nyingi watu wa namna hii hawabadilikihata kama ungempa nini! The only valuable help ambayo alipaswa kuitilia maaanani ni elimu! Kama ameshindwa kusoma mnunulie jembe na umpeleke kijijini akalime shamba la matikiti biashara inalipa sana! Ushauri wa bure!