Hivi huyu ananipenda au Mchunaji?-Ushauri!

"Hi Dinah mdogowangu hujambo?
Naomba msaada wa ushauri kwa wanablog wenzangu. Mie ni mama mkubwa kiasi kwa umri, Nilikua na mwanaume tuliokua dini tofauti na tumeachana kwa miaka miwili sasa.


Kuna kijana ambae nimemzidi kwa takriban miaka miwili alivyosikia kama niaeachiaka tu, hapo hapo akaniambia yeye ananitaka na dakika hiyohiyo akaniambia kama niko tayari basi anaweza kufunga ndoa hata kesho, nilibaki nashangaa kwa nini haraka?


Mie sikumpa jibu la ndio wala hapana lakini nikabaki kumuambia labda ananijoke asingeweza kunioa kwa kua mie mkubwa kwake. Hali yangu kiuchumi na hata assets sio mbaya sana, Yule kijana ana kazi , ila kiuchumi nimemzidi ana mke na watoto watatu, ni muislam ndoa ya pili inaruhusiwa.


Alikua anamwamko sana wa kwenda kuongeza shule (degree ya pili) lakini hakua na sponsor na mwajiri alimkatalia ruhusa na akataka kuacha kazi, nilimshauri asiache ambembeleze mwajiri ruhusa. Sasa nikajiuliza ana mapenzi huyu au anataka kunituma nimsomeshe?


Baada ya mawasiliano, tukapoteana kwa kipindi kirefu kidogo kwa kuwa nilikua nje ya nchi. Tumeonana mwezi wa kwanza ki-accidental, ile mada imeanza tena, Na sasa ameshapata admission IFM hana sponsor, mimi niko nje ya nchi tena ila yeye anasisitiza anataka kuowa hata kwa remote, (kwa waislamu inaruhusika).


Najaribu kumsihi kwamba sasa hivituwasiliane tu na tuchunguzane, lakini yeye ameng'ang'ania antaka jawabu la kukubaliwa tuoane au laa ajikate. Hakuwa moyoni mwangu sana lakini nilikua nahisi with time hasa ukizingatia umri wangu naweza kumpenda.


Lakini ameng'angania ananipenda na anataka jawabu. Kwa tabia kama mme ndani simjui vizuri, nilijaribu kumuuliza kijana anaefanya nae kazi akaniambia kazini hayuko-organized na yuko hash, kwa nyumbani sijuiiii.

Wana blog naomba mnisaidie mawazo huyu kijana ananipenda kweli, au anataka kunitumia? lugha zake za kusisitiza hilo suala sikuzipenda sana kwani kunasiku ashaniambia ukinikataa mimi hutapata tena mtu kama mimi au hutapata mtu atakae kupenda kama mimi, au kwanini hujiulizi ni nini nilikupendea nisipende wanawake wenzio.nk.

Naomba ushauri jamani, ananipenda huyu? nimkubali? nimemwambia tusubiri kwa kua sipo nchini hadi november tuyazungumze yeye kagoma. Ushauri jamani hili jamaa linataka nini?"

Jawabu:Mimi sijambo Dada'ngu, habari za wakti kama huu mpendwa!
Huyo isije kuwa ni mmoja kati ya wale "wezi watupu", dada unajua siku hizi hata wanaume tena walio na familia zao(wake na watoto) wanachuna wanawake ambao mambo yao ni safi kiuchumi?.

Tena siku hizi nasikia wanawake walio nje ya Bongo au wenye kujiweza ndio wanaoibiwa kweli kweli, unaweza teremka pale Yapoti (airport) ukapokelwa na vijana/babaz watanashati wakitoa "offers" tofauti tofauti za ndoa hihihihihi.....turudi kwenye somo.


Kwenye maelezo yako tangu mwanzo mpaka mwisho hakuna mahali umeelezea hisia zako juu ya huyo kijana. Huyu kijana ni kweli anataka mdhamini kwa ajili ya masomo yake ya juu na ndio maana akakurukia mara tu alipogundua kuwa wewe na mumeo/mpenzi mmeachana.


Inawezekana kabisa kutokana na "kasumba" alidhani wewe utakuwa "desparate" kuwa na mwanaume au kuolewa kama inavyoaminika kwa wanaume wengi kuwa unapokuwa mdada mkubwa na kisha kuachika basi unakuwa huna "bahati", hivyo pamoja na kuwa ni mdogo kwako aliona utamkubali tu bila mizengwe.


Kwa upande wa pili huenda kijana kweli anakupenda, lakini je wewe unampenda? Tangu umetoka kwenye uhusiano mwingine ambao naamini ulikuwa wa muda mrefu na "serious" ni wazi unahitaji muda kuchuja hisia zako ili kuwa na uhakika vilevile kuwa tayari kujiingiza kwenye uhusiano mpya wa kawaida wa kimapenzi acha ndoa.


Kutokana na maisha ya sasa hakuna kitu kinaitwa kuchunguzana ili kufunga ndoa(ilikuwa miaka hiyo), siku hizi kupendana kwanza, ndio majuana taratibu na kuchunguzana na kuerekebisha kama inawezekana alafu unamalizai nakufanya maamuzi ya busara baada ya kugundua kasoro zake na yeye kugundua zako na kisha kujitoa mhanga na kukubali kuishi maisha yako yote (kufunga ndoa) bila kuzijali kasoro zake na utakachokifanya ni kumpenda mwenzio kila siku kama ndio mmeonana wiki iliyopita.....vinginevyo ndoa itakuwa ndoano.


Sasa, suala hapa sio kama yeye ni mchunaji au lah, kitu muhimu hapa ni wewe na hisia zako juu yake. Je unahisi kumpenda? kama sio je unadhani unaweza kurafikiana nae kikawaida tu? Vilevile unadhani siku moja unaweza kupendana nae na kuwa zaidi yamarafiki wa kawaida?

Nakuja....

Comments

Anonymous said…
hahaaaaaa jamaaa linataka hela yako mama, hana mpango na mapenzi yako yeye anataka akishakuoa umtunzie hata wale wanae 3.napia anataka umsapoti kwenye shule,achana na wanaume wa hivyo mama jitulize atakuja mwanaume mzuri.
Anonymous said…
Dada hakuna mapenzi hapo,mtu gani hajua hata tabia yako akurupuke tu akuoe?!.Mimi niu mwanaume lakini siamini kama kuna mapenzi hapo.Kuna mawili moja huenda ikawa anataka kukutumia ili apate hela pili anaweza kuwa anataka aje huko uliko.Hii mpya me sijaisikia.Halafu kama kweli anakupenda kwa nini akutishe eti "ukinikataa mimi hutapata tena mtu kama mimi au hutapata mtu atakae kupenda kama mimi, au kwanini hujiulizi ni nini nilikupendea nisipende wanawake wenzio.nk." wewe jiulize tu kwani anakaa na wewe kila siku,anajuaje labda huko uliko kuna watu wanakutongoza na kukupenda kiukweli.Kwa upeop wangu finyu I dont think hapo kuna love.Option uliyompa ya kumwambia asubiri mchunguzane ni nzuri na uliona mbali.Dada yangu hapo ukitereza umeingia mkenge,usije sema hatukukwambia bure.Jamaa anataka kuendesha na kukusaidia kutumia mali zako.Mwisho wa siku kazi kwako na maamuzi unayo mwenyewe.
Anonymous said…
wako wanaume wanakimbilia wanawake wenye hali nzuri siku hizi, kuwa macho. suala la ndoa sio la pupa. nafkiri ulishaliona hili kutoka bw mliechana. enewe we mpange mkutane mue mnaongea tu bila kumpa pusi kwa miezi zaidi ya 6 utaona mwelekeo wake.

jaba
Anonymous said…
Yaelekea huyo si mkweli na ana lake jambo lamani hata iweje ghafla bin vuu.Mpendwa huyo anataka kulelewa tu huo mzigo!
Anonymous said…
Mhhhhhhhh wewe dada acha utoto huo!!
Wewe mwenyewe umetuambia una umri mkubwa kumzidi huyo kijana, halafu eti unaomba ushauri kwa watu wakushauri nini dada?Hivi upendo nao ni wa kushauriwa au nunataka tu kuchezea nafsi yako??

Upendo hauwezi kusukmizwa na watu hasa kama huo wa kupendwa na mtu au la.Kwanza unaonyesha wewe unampenda huyo kijana,labda shida yako ni huo umri.Kama humpendi kwa nini usimwambie direct kuwa "hapana"(No).Iweje huyo aendelee kukusakama kama hujamwonyesha hisia kuwa nawe unampenda?Na labda umneishatombana naye mara kadhaa, sasa nini kimebaki?

Kuwa nje ya nchi kuna maana gani hasa?unataka kutuambia kuwa ndiyo sifa ile umesema unamzidi kiuchumi??Mimi niko nje ya nchi pia lakini haina maana namzidi aliyeko bongo kiuchumi.Kama kweli unampenda oana naye acha kupoteza muda eti upate ushauri.Kwa bahati nzuri wewe umeonja ndoa hiyo iliyoharibika,na bado unahaha kutafuta ushauri wa namna ya kumpenda mtu.Huoni kama unatupa picha kwamba wewe una kasoro, na ukishauririwa na watu hapa bila ridhaa yako ukaingia mkenge utasaga meno dada.Hivi una umri wa miaka mingapi dada?Mimi umenishangaa sana kwamba unataka wakuamlie watu wengi juu ya kitu kinaitwa upendo!!!
Anonymous said…
Mama yangu mimi ningependa nikufahamishe tu kwanza wanawake wengi sasa hivi wana pesa. Wanawake wanajituma kutafuta pesa zao wenyewe. Wanatumia akili, maarifa na nguvu zao wenyewe. Kifupi ni kwanza wanawake wanakuja juu kiuchumi kuliko wanaume.

Sasa wanaume wanalitambua hilo na wanataka kutumia fursa hiyo kujinufaisha kama ambavyo wewe unapata wasiwasi kuhusu huyo Serengeti boy wako. Hivyo dhamira yako ya kumchunguza kwanza ni nzuri lakini fanya hivyo iwapo tu unaona anakuvutia na kwamba unaweza ukapenda kuwa naye. Lakini kama hana mvuto kwako achana naye kwa ni kwa jinsi nilivyopata picha you're a very busy woman so don't allow him to waste your precious time.

Lakini mama yangu kumbuka kwamba mtu anaweza kukupenda bila kuwa na sababu yeyote. Kwa vigezo vyangu hiyo ndiyo really love. Nimeshawishika kukuandikia kwa sababu nipo katika the same situation. Nina kipato kikubwa kuliko my BF. Ndugu na marafiki zangu walidhani my BF yupo kwa ajili ya kunichuna. I was worried but to my surprise yeye anajitahidi kila anapoweza to supply for me. He is struggling to make sure he provides for me. Namtega kwa namna nyingi tu ili kugundua kama ana nia ya kunichuna sijaona dalili hizo. Ingawa watu husema kuwa anaweza kuwa mvumilivu mpaka atimize lengo lake. Nakushauri mchunguze uweze kugundua kama ana nia ya kukuchuna au anakupenda kweli.

Kuhusu hayo masomo yake kama unaweza kumsaidia msaidie tu bila kujali kwamba unakuwa naye au la na kama huwezi mwambie huwezi iwapo atakuapproach maana inanekana huwa anakwambia tu kama kukushirikisha lakini hajakuomba rasmi.
Mie nakutakia kila la heri katika kuanzisha mahusiano mapya ila kuwa very careful.
Kimberly - Arusha
Anonymous said…
Fata moyo wako unavyokwambia, kuhusu kutumiwa itakuwa hiyari yako. Huwezi jua jamaa amezimikia nini juu yako.
Anonymous said…
HAMNA KITU HAPO, CHA MSINGI ENDELEA TU NA SHUGHULI ZAKO! ANATAKA AKUTUMIE TU HUYO! LAKINI KAMA WEWE WAMPENDA ITS FYN.
Simon Kitururu said…
Kumbuka jamaa pamoja na kukusifia kama wewe spesho lakini lilishawahi kuoa na linamke ambaye kwa vyovyote kinamna alikuwa spesho kama wewe ndio maana kachoka na maandazi na anataka vitumbua. Jibu unalo mwenyewe katika swala hili kwenye machale yako ukiniuliza mimi.


@Di:Mbona umenitenga?:-) nipo lakini hapa kimyakimya!:-(
Iddy said…
I couldn't let this one go bila kuweka comment... Dada au antie yangu, kwanza kabisa pole na kazi.. PILI I WANT YOU TO READ THIS FROM I GUY, ME. Jamaa ni mnyonyaji (muchie) he just want to suck you umlipie ada. Hakuna mapenzi ya kuonana kwenye stop sign na kutangaza ndoa..

Age sio tatizo mimi mke wangu kanizidi two years, lakini hapo hakuna muoaji... So just stop it and go ahead with your life.
Anonymous said…
pole sana kwa yalio kukuta mimi yalinikuta kama hayo na mwanaume anawatoto3 kama wewe na alikua na haraka kama za huyo mwanaume but nikwamba alikuwa ananiaharakisha kumuoa na kuwa karibu nae ili usijue matatizo aliyokuwa nayo hapo nikwamba ukishaolewa nae ndio unakuta matatizo yake nakuwa inachukua process refu kwakua mko kwenye ndoa cha muhim nikuwa very smart na kumjua tabia zake b4 getting ur self into trouble mwanamme ambae anakuharakisha while haumjui nikuwa anaficha mambo au matendo au tabia zake chafu anataka zikukutie kwenye ndoa while mtakuwa mko so commited
so be careful mjue tabia na mambo yake b4 haujarukia uka regreat mwache ajikate hana sera
Anonymous said…
Mdau wa kwanza jaribu kuchangia point ya maana sio upuuzi wewe.........Au hiyo bahati unaitaka wewe???Anyway mama nadhani hapa hamna atakaye kupa ushauri nasaa zaidi wewe ndio utapata raha ya mapenzi na sio mimi au dinah so your choice zaidi..
Anonymous said…
Nafikiri hata kabla watu hawajakushauri, jibu kubwa unalo mwenyewe. Nasema hivi kwasababu wewe umeshaolewa na kuachika, kwahiyo unajua siri ya mapenzi ndani ya ndoa, na sidhani ungefurahi kufanya makosa mara mbili, labda kama unapenda huo mtindo wa kuolewa na kuachika. Uwezo unao, au sio lakini sidhani kuna mtu anapenda hali hiyoya kuolewa na kuachika. Kwanza kiheshima sio vizuri, pili utakuwa unajifikiria wewe mwenyewe, bila kuwafikiria watoto wako.
Hili la watoto tuliangalie mara mbili, wengi haatulipi kipa umbele hili swala. Mkioana na kuachana mnawajengea taswira mbaya watoto, na huenda kukawa na kizazi kisichokuwa na msimamo. Una watoto watatu kila mmoja na baba yake! Jenga familia yako ya leo ili iwe baraka kwa vizazi vijavyo.
Pia wewe kiumri ni mkubwa kama ulivyosema kwahiyo wewe unatakiwa uitumie hekima ya ukubwa wako katika mashauri mema. Ndio wanaume mkiwa ndani ya familia anatakiwa awe kichwa cha familia. Hii ni kawaida, kwasababu kila mkikutana wawili mmoja anatakiwa awe kiongozi `by default ni mwanaume’, lakini sio wanaume wote wanauwezo huo, kunahitaji busara ya pamoja ili kulielewa hili. Tumia umri uliomzidi huyo kijana kwa kumpa ushauri, nini maana ya ndoa, athari zake ,maisha ya uke wenza na matokeo ya baadaye.
Baada ya kusema hayo,mimi kama mimi siwezi kukushauri moja kwa moja kuwa olewa na huyo kijana au la khasha, kwasababu kama nilivyosema awali, jibu kubwa unalo wewe mwenyewe. Lakini cha muhimu ni kuvuta subira, huku unaangalia uwezo wako wa kuishi katika uke wenza, kwani uke wenza una-mashariti yake, usije ukaolewa ukaanza kuleta kichwa ngumu kwasabu uba uwezo, na huenda jamaa mke wake wa kwanza ni mke wa nyumbani, unatakiwa umuheshimu kama dada yako. Nafikiri hilo unalielewa.
Mengineyo, ni hayo ya upendo, je kweli unampenda kijana, au unataka tu kuolewa. Na kuolewa ni vyema, kwasababu kuishi peke yako ili-hali umri umepwelea sio vyema, kwahiyo bahati hiyo usiiachie. Wangapi wangapi ambao wanatafuta waume wa kuwaoa hawajawapati, hii ni dhahiri na kweli. Kipato chema maisha mazuri ni ridhiki ya mola, kuna leo na kesho.
Mimi ndio yangu
emu-three
Anonymous said…
Dada nami nilikuwa katika hali kama hiyo jamaa mdogo kuniliko nikakubali kuolewa naye haraka haraka sasa yamenikuta anasoma nje kwa msaada mdogo niliyompa lakini ni matusi dharau na kejeli zisizofaa. Nakushauri usitishike na suala la umri kuwa umeenda tena jamaa ana watoto watatu? Hiyo itakuwa burden yako. Nimejifunza sana kutuika kwa jamaa wangu sikuminvestigate alizaa na mwanamke mmoja na hamtunzi mwanae so naona anataka afaidi tu na ujue chanzo kikubwa cha ndoa kuharibika ni ubinafsi ubinafsi ni tabia ya mtu haibadiliki kwa siku moja so usiende huko mama tulia atakuja ambaye siyo 100 per cent perfect lakinimcha Mungu na mwenye kufahamu majukumu yake kama mme siyo kujifikiria jinsi ambavyo anataka kujiendeleza nk
Azrah hanafy said…
MAAMANGU MPENDWA, WENZANGU WAMEONGEA MENGI ALHAMDULILAH, ILA MIMI NINALOTAKA KUSEMA NI KUA, HUYU DOGO AMBAE MWENZANGU AMEMUITA SERENGETI BOY, MCHUNGUZE BT JAMA MUSISEME KIJANA ATAKA HELA, HUEZI JUA ROHONI MWAKE, ND UHUSIANO WAKE YEYE NA HUYU AUNTY, CZ HATA AJE AKWAMBIE ATAKA KUKUOA HATA KWA REMOTE, LAZIMA KUNA UHUSIANO ULIKUA WAENDLEA HAPO AWALI, PLUS MWAMPONDA HUYU DOGO ILE NOMA, SIVIZURI WASHKAJI, NYANYANGU MCHUNGUZE BT KIROHO SAFI, HILO LAKUTAKA HELA, C DHANI CZ BINADAMU WAKO TAFAUTI, KAMA YULE ALITAKA HELA, HUYU HUEZI JUA, TC OL, SHUKRAN JAZAKILAH, HANMIXER@GMAIL.COM
Anonymous said…
Mh dinaa mdogo wangu, hapa ndio umeshatia kapuni au uanakuja? nimefuatilia wee ila naona jee. Haya kila la kheri