Mume ni VVU mimi sina, nataka mtoto-Ushauri

"Hi Dinah
Mimi naitwa Tenisha-(si jina langu halisi) nimekuwa nafuatilia blog yako kwa muda mrefu na nimeona jinsi unavyosaidia watu kwa ushauri wako ,na mimi pia nikaona niseme yaliyoko moyoni kwangu.


Kwa kuanzia mimi nina miaka 25, niliolewa miaka miaka 4 iliyopita na sina mtoto (bado tulikuwa hatujapanga kufanya hivyo kwa wakati huo),ndoa yenye furaha na amani tele, mpaka mwaka 2008 mwezi April mambo yalipobadilika.


Mume wangu alipata ugonjwa kama unaofanana kabisa na Herpeszoster japo Doctor alisema huo ni mbaya zaidi , mimi nilikuwepo na nilimuuguza mpaka alipopona. Baada ya hapo Doctor alisema ingekuwa vizuri kama tungepima HIV, lakini kabla ya ndoa tulikuwa tumepima na wote tulikuwa negative.Lakini mimi nilikuwa na utaratibu wangu wa kupima mara kwa mara ninapopata nafasi ya kufanya hivyo.


Majibu yalipotoka yalikuwa ya kusikitisha, mimi nilikuwa na negative na mume wangu mpendwa alikuwa positive, nilillia sana sana (namaanisha hivyo ) lakini pia sikuweza kubadilisha ukweli.

Ikabaki hivyo tukaenda tena kupima Angaza na hospital tofauti majibu yakabaki hivyo kuwa mimi ni negative na mume wangu ni positive . Tokea hapo mpaka leo nimeshapima sehemu nyingi tofauti na majibu ni hayajabadilika.


Mume wangu namjua tokea tuko wachumba tabia yake naijua sio mtu wa kuhangaika na wanawake, nimekuwa namfuatilia sana nikawa najichosha mwenyewe (lakini ukweli zaidi anao mwenyewe kama ana nyumba ndogo mimi sijui).


Alikoupata sijui hata yeye mwenyewe alikiri hafahamu, ikabidi tukubaliane na ukweli, Sikutaka kumuuuliza sana kama alikuwa na mwanamke mwingine au la ! kwa sababu pia sikutaka akose amani na hali aliyonayo.


Basi ikabadi aanze dawa za kurefusha maisha (sio ARV)ambazo tulipewa na Doctor wetu. Wakati amepata huo ugonjwa tayari CD4 zilikuwa 200. Tuliongea na Doctor sana kuhusu maisha yetu na tulipenda sana kuwa na mtoto mwaka huu 2009, japo haiwezekani, njia aliyotuambia ni fertilization (nadhani wengine wanaijua)ambayo pia sio 100% .


Niliongea nae sana kuhusu mtoto yeye akasema alivyofikiria yeye nizae na kaka yake damu isiende mbali ,nilikataa hapo hapo nikamuambia sitaweza (never happen). Pia tulishauriwa asifanye mapenzi sana kwa mwezi kama mara 2 hivi au 3 asizidishe kwa ajili ya kulinda afya yake na huwa tunatumia condom na tuko makini sana kwa hilo.


Jamani kama nilivyosema hapo juu nina miaka 25, ninapata majaribu sana (kwa muonekano naonekana kama mdogo zaidi ya hiyo miaka na ni mzuri hilo nalifahamu hata mimi mwenyewe-hehe he hehe .) Kufanya mapenzi mara 3 kwa mwezi hakunitoshelezi pia nilizoea sana kufanya romace na deep kiss ila sasa hatuwezi kufanya hivyo ili kunilinda mimi asiniambukize.


Nampenda kumuacha naona siwezi, pia naona anahitaji mtu wa kumfariji kwa sababu bado anaona kama ni ndoto kwake. Na hatujawahi kumuambia mtu yoyote zaidi ya madoctor wanaotupima.

Naomba ushauri .
1.Nitafanyaje kuhusu mtoto , namhitaji sana mpaka huwa nakosa usingizi nikifikiria juu ya kupata mtoto wa njia ambayo hata mume wangu ataridhika na yeye na huyo mtoto (hataki nizae na mtu mwingine )

Jawabu: Hili linawezekana kabisa ila itabidi mchukue tahadhali sana na ni "risk" kwa mtoto. Kama mnaishi nchi zilizoendelea Mf-UK au US mnaweza kuliweka wazi hili suala la kuwa na mtoto huku mmoja wenua na VVU na wao watawaweka kwenye uangalifu mkubwa na kukukufanyia wewe mama (ukishika mimba) vipimo vya mara kwa mara ili kuhakikisha mtoto anakua vema tumboni bila hatari yakupata VVU, Mara nyingi mwanamke hupewa "course" ya madawa fulani kabla hamjanzakujaribu ili "kumimbana".


Kwa "case" yako ni rahasi zaidi kwa vile wewe huna VVU (japokuwa utakwenda through vipimo vingi na vya mara kwa mara kuhakikisha hilo, kuwa kweli huna kabisa-kabisa VVU), mwanamke akiwa hana VVU anaweza kuzaa mtoto ambae hana VVU tena bila kutumia madawa yeyote ya kumzuia mtoto kulikwaa gonjwa hilo kwa vile inasemekana kuwa mbegu za kiume hazibebi vijidudu vinavyosababisha upungufu wa kinga mwilini (UKIMWI) kuliko mwanamke mwenye VVU.....tafadhali bonyeza link hapo pembeni kulia mwa blog hii kwenye maandishi yakijanani chini ya Profile yangu kuna maelezo ya kutosha kutoka kwa madaktari na pia unapata nasafi yakuwauliza maswali moja kwa moja, tafadhali jiweke karibu nao kwa ushauri zaidi wa kitibabu.


Kitu kingine unapaswa kufahami ni kuwa HIV Virus ziko za aina 3 tofauti. Aina mbili ambazo ni hatari zadi zinanawiri nchi za joto hasa Afrika na aina ya nyingine inastawi zaidi nchi za Baridi. Inasemekana kuwa ukiwa na VVU aina ya tatu na unaishi nchi za joto kuonekana sio rahisi ukilinganisha na zile mbili za "kiafrika".


Ndio maana nikasema kabla ya kuambiewa wendelea na suala la kumimbwa huwa wanakupa vipimo vingine lukuki ili kuwa na uhakika....tafadhali soma Tovuti nyingine inayojihusisha na kuzuia VVU kwa watoto....bonyeza hapo kulia kwenye Logo ya mtoto kwa maelezo zaidi ya kitaalamu.


2.Mimi jamani bado mdogo nina mihemuko ya ujana nahitaji kufanya mapenzi nifurahie pia sitaki kutoka nje ya ndoa.


Jawabu:Kutokana nakilichotokea kwenye ndoa yako na kama ulivyodai kuwa unampenda mume wako na nyote mnaonekana ni waelevu basi sio mbaya kama utashauriana na mume wako na kukubaliana kuwa wewe uwe ukitumia "sanamu" kujiridhsiha pale unapohitaji zaidi. Matumizi ya sanamu za ngono sio kitu ambacho mimi binafsi huwa nashauri wapenzi kutumia kwavile naamini katika uumbaji wake Mungu, lakini kama "issue" ndio hii ya VVU ninafuraha kabisa kusema....tafadhali kanunueni sanamu ili wewe uweze kukabiliana na mihamko yako.


Utakachotakiwa kufanya hapa ni kuwa "mbinafsi" kidogo ili kuzuia kumtamanisha mumeo ambae kutoka na ushauri wa Daktari hapaswi kufanya ngono mara nyingi kama ilivyokuwa hapo awali kabla hajajua kuwa anaishi na VVU.*****


Nitashukuru wa ushauri /maoni kutoka kwako Dinah na wengineo. Nimejieleza kwa kifupi ila nina imani nitakuwa nimeeleweka na nitapata ushauri mzuri.
Tenisha"

Jawabu:Tenisha, asante kwa kuwa mfuatiliaji wa mahali hapa, shukurani kwa mail yako na kwa uwazi wako.

Pamoja na kuwa nimekujibu moja kwa moja ningependa nitoe maelezo kwa ujumla ili kuweka sawa au kujazilizia mengi na mazuri yaliyosemwa na wachangiaji. Inasikitisha wengi wamekushauri uachane na mumeo (kitu ambacho mwanaume actually angekifanya kama wewe ungekuwa na VVU).


Kuna wachangiaji wamgehusia suala la "rushwa", ni kweli kabisa watu wengi wanatoa "kitu kidogo" kwa madaktari ili wapatie majibu ya uongo (hawana HIV) lakini ktk hali halisi wanakuwa navyo na wanajua kuwa alikwisha vikwaa miaka ya nyuma, lakini kwa vile CD4 ziko juu, wanaendelea na maisha kama kawaida na zitakapo pungua na kudaka maambukizo wakati tayari yuko kwenye ndoa unaweza kusukumiwa wewe lawama kuwa ulikuwa "kicheche" ndani ya ndoa.


Kama ulivyosema ulijitahidi kumchunguza na kuhakikisha kuwa hana tabia ya "kuchomoka" nje ya ndoa yenu, inawezekana ni kweli kabisa hajaupata baada ya kutoka nje ya ndoa, kuna uwezekano mkubwa aliupata kabla ya ndoa na akafanya "makaratee" na Dk ili kupata majibu kama yako.


Kuna njia nyingine za mtu kupata VVU ambavyo sio lazima iwe Ngono (inategemea na shughuli zake) kama Nesi au Daktari anaefanya kazi na waathirika wa VVU. Vilevile kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu namna ya kuishi na watu wenye VVU ambao tayari wanaugua....kutokana na utu au ukaribu wa wahusika au ukosefu wa vifaa hapo nyumbani mtu anaweza kujisikia vibaya kuosha kidonda/kinywa kwa kuvaa mpira na badala yake akatumia mikono mitupu ambayo huenda ilikuwa na mkato/mchubuko ndani ya ukucha n.k.


Pia wapo watu ambao wanaambukiza wenzao kwa makusudi kwa kujichoma sindano kisha kuwachoma wenzao na sindano za kushonea, pini, kitu chochote chenye ncha kali au hata kuweka vifaa vya kunyolea walivyovitumia karibu au hata kuvibadilisha(kuonda visafi na kuweka vyao walivyotumia).



Njia nyingine ambayo mtu anaweza kupata VVU ni kunyoa, tengeneza nywele Salon, sio wahudumu wote wa sehemu hizo wanatumia bidhaa maalumu iliyothibitishwa kitaalamu ili kuuwa vijidudu vinavyosababisha UKIMWI na wanapofanyia kazi nywele zako sio wakati wote wanaikwepa ngozi, wakati mwingine inatokea bahati mbaya ngozi naguswa, sasa kama kifaa hicho kilimnyoa mtu mwenye VVU ni wazi unakuwa hatarini (Inashauriwa kwenda na mashine/vifaa vyako mwenyewe just incase)


Kutokana na maelezo yako nahisi mumeo alijua alichonacho mwilini mwake (VVU) na akawa muangalifu sana kila anapofanya mapenzi na wewe ili asije kukuambukiza, lazima alihakikisha unakuwa tayari kabla ya tendo na hakuwa akilazimisha ikiwa hauko kwenye "mood".


Ni vema jamii ikabadilika jinsi inavyolichukulia suala la VVU. UKIMWI ni gonjwa hatari kama yalivyo magonjwa mengine mengi ambayo hayana tiba bali dawa ya kupunguza makali yake Mf ni Pumu, Moyo, Kisukari, Saratani mbali mbali, Matatizo ya akili n.k tofauti yake ni kuwa UKIMWI unaambukiza wakati hayo mengine hayaambukizi lakini yote yanaua na ktk hali halisi baadhi yake yanakuondoa haraka kuliko yule mwenye VVU.


Tukumbuke kuwa hivi sasa tunamezunguukwa na jamii kubwa inayoishi na VVU, na kuwa na vijidudu hivyo haina maana kuwa wewe ni mgonjwa japokuwa unatakiwa kuwa muangalifu na kumuona Daktari wako mara tu unapojisikia tofauti (maumivu au kujisikia ovyo/vibaya), hii inasaidia wao kukufanyia vipimo na kujua tatizo ni nini....huenda umekumbana na maambukizo fulani na hivyo inakuwa vema kulitibu tatizo hilo kabla halijawa sugu kwani mwili wa mtu mwenye VVU hauna kinga za kutosha za kupigana na magonjwa/maambukizo mbali(sote tunalijua hili).


Elimu kuhusu UKIMWI in terms of kujilinda, unavyoambukiza na kujizuia imetosha lakini sasa inahitajika elimu kuhusu namna ya kuishi na VVU na kuishi na watu wenye VVU.


Kidokezo:Napenda kuwakumbusha rafiki zangu. Condom ni asilimia 100 lakini kutokanana sababu za kisheria hiyo asilimia moja ambayo inafanya bidhaa hii kuwa 99% inalinda Kampuni husika kwa utengenezaji wa bidhaa hiyo, ikiwa wewe utaitumia vibaya na kupata maambukizo ya VVU.

Unapoamua kutumia Condom, mnapaswa kuwa waangalifu kama sio kuziruka harakati nyingine za kuandaana kuelekea kwenye safari yenu kabla ya kuvalia vazi hilo maalumu. Kushikana nyeti, kugusisha nyeti zenu, kubusu, kunyonyana huko chini n.k....huwezi kufanya vyote hivyo kisha ukadai "nilivaa Condom au alivaa Condom hivyo sina HIV", kama ndio katabia kako ka kutumia condom baada ya kufanya yote hayo bila Condom......kapime!


Wapo wanandoa kama huyu Mdada (nawafahamu) ila wao walifunga ndoa wakijua kabisa mmoja wao ana VVU baada ya mkewe kufariki, pia ilithibitishwa baada ya Njemba kupima. Siku zote wanadai kutumia Condom na walipokuwa wanataka "mimba" ndio walikuwa wanakwenda nyama 2 nyama lakini kwa uangalifu na kwa kuzingatia lengo moja tu ambalo ni kusababisha mimba na sio mambo ya utamu au kwenda mwendo mrefu. Sasa wanawatoto wawili wenye afya na mkewe hana VVU huyo bwana yuko chini ya matumizi ya madawa.


Fafadhali mpenzi msomaji ukipata nafasi tembelea Tovuti husika kuhusu HIV ili kujifuza zaidi mabadiliko ya wadudu hao, kuishi navyo, kuishi na walionavyo, ngono na mpenzi mwenye VVU na mambo mengine mengi kwa faida yako, huenda sio wewe leo lakini kesho ikawa mdogo wako au hata rafiki yako kama sio mtoto wako.

Kila la kheri Tenisha, na hongera sana kwa kuwa na mapenzi ya dhati kwa mumeo. Mungu akubariki na nawatakia maisha marefu ya ndoa.


Comments

Anonymous said…
ukweli ni kwamba huyu mme wako alikuwa muathirika siku nyingi alijua kabisa hata test ya kwanza kabla ya ndoa alijua kabisa ni mwasilika. ndio maana akawa hataki muzae kwanza, ila mungu si athumani ndio hivyo hujapata VVU, duuh dada pole sana

Mdau
Anonymous said…
Mh,hapa kuna kazikweli.nitakushauri kama ifuatavyo
1.pole sana dada cha kufanya usifanye mapenzi na mume wako kabisa hata kama una mihemko, ilakama unataka na ww kupata ngoma endelelea maana wanasema ndomu si 100% kinga.usimfurahishe mume wako kwa kuwa guilty bila sababu anajua yeye alikotoa huo mwiba.atasema hajui kwani unatoka kwa mungu huo au gafla tuu anao anakudanganya sana huyo.USIFANYE SEX NAYE TENA.
2.kuhusu mtoto tafuta mwanaume mwingine uzae kama kama unaona bila mtoto huna maisha unashangaza sana dada upo 25 bado yanki ww,mwambie mume sitazaa na kaka yako wala rafiki yako, nitatafuta mtu mwingine nizae naye kwa mapenzi yangu na wala si yako"mume wako"
USIFANYE MAPENZI NA MUME WAKO UNAJIUA NA WW KWA KUPENDA NGONO CONDOM SI 100%.
hiyo mihemko yako itakupeleka six under.
Anonymous said…
Sister umeshajua mume wako ana VVU na bado unafanya nae mapenzi hiyo condom inaweza kupasuka, halafu uaminifu hana, huyo alikuwa kicheche ohoo chunga sana, wanaume sisi heee wadanganyifu sn sn na nyinyi mkiambiwa kidogo tu munaamini roho zenu.
Haya kama ushachoka kuishi dada endelea kumpa mambo mazuri, japo ni mume wako but sababu ya maradhi basi epukana nae haraka iwezekanavo halafu duu una moyo kweli wangu mm achilia mbali kufanya mapenzi na mtu mwenye vvu basi kula nae sahani moja sitaki.
take care bado mdogo usijali
Anonymous said…
pole mdada,

hayo ndio maisha ukisikia, ndio majaribu ya kimaisha ukisikia. Mpeleke mume wako kwenye maombi kama una imani!!!. Miaka 25 sio mchezo, una nyege kibao.

jaba
Anonymous said…
Hey Tenisha(Jina la utani)!

Kwanza kabisa nakupa pole sana kwa hayo yaliyokuzunguka katika ndoa yako.mzigo ulionao kweli ni mzito unahitaji kutiwa moyo sana!

Kwanza, nikianza na swala la ugonjwa wenyewe ninakupongeza kwamba umejitahidi sana kuendelea kuwa na mumeo ili kumsaidia na kumtia moyo asije akaghadibika katika hali hiyo akafa mapema.maji ukiyavulia nguo huna budi kuyaoga kwa kweli.Pole sana dada, naamini maadamu umejua na mumeo amejijua hivyo mtaendelea kujikinga ili wewe dada usijeambukizwa,pia mumeo ataendelea kujilinda zaidi na masharti hayo ili aendelee kuishi.Hilo nadhani mumelivalia njuga vizuri kufuatia maelezo yako.

Jambo la pili ni lile la kuhitaji mtoto.Dada hili ni bomu kubwa sana. Kutokana na hali mliyonayo na mumeo mimi ningekushauri sana tena sana acha kwanza hilo jipe muda mrefu zaidi ili ujiepushe na madhara mengine yanayoweza kusababishwa na uhitaji huo.Unajua dada, maadamu Mungu amekunusulu wewe kutoathirika licha ya kwamba ulikuwa unafanya mapenzi na mumeo aliyeathirika,Basi hilo la mtoto hebu tulia kwanza ili usije kuchukua uamuzi usiyo sahihi na ukahatarishwa.Kwa mfano hata ukazaa na mtu mwingine hiyo dhamiri yako juu ya mtoto huyo itakuwa kwenye shida daima katika maisha yako kwa sababu umeolewa.Pia ukizaa na nduguze kama livyosema kaka mtu,hiyo pia ni hatari sana.Usiamini mtu yeyote hata kama utakwenda naye kupima, pia inawezekana hata wewe unavyo virusi licha ya kwamba vipimombalimbali vimekuthibitisha u salama.Nina maana usije chukua mimba na ikawa ndiyo ngoma kubwa.ushauri wangu tulia dada angalia kwanza tatizo lililopo na insi litakavyo endelea kutunzwa.

Kuhusu tatizo la minyege/mihemko hasa ukiwa mrembo mbichi kabisa of 25 yrs.Ndiyo dada mara 3 kwa mwezi inaonekana ni kama sawa na halkuna kwako kufuatia maelezo yako.tatizo lipo palepale,kwamba sasa unataka ukatimizziwe wapi?? Je, unataka uingie kwenye risk ya VVU? unayo nafuu kwamba unaipata hata hiyo mara 3 kwa mwezi ambayo ni kama mara moja kwa wiki.Ukijaribu kutoka nje utakuja shangaa filauni badala ya ya Musa.mtego wa mabo hayo upo katika kunogewa, hapo jitu upofu uchukua nafasi ukashangaa macho hayaoni tena wala hayachambui hata kinachoonekana katika udhaifu.Ushauri wangu katika hili, tafuta njia mbadala ambayo haimhusishi mwanadamu mwenzio.Bila shaka unajua. Au tumia njia ya maromance na mumeo bila kutiana alikini ukaridhika na mihemko ikapungua kama siyo kuisha.Pia njia nyingine acha kufikiria sana mapenzi kuwa unayakosa kwa sababu mwenzio kapewa restictions za kutongonoka mara kwa mara.nadhani kuna hisia zako zinajaribu kukuweka kwenye kumbukumbu za jinzi mumeo alivyokuwa anaweka sawa katika suala la mapenzi.

Mshukuru Mungu kwamba wewe umebainika ni mzima.Utakayemjaribu ndiye atakayekuambukiza.achana na ngono bila kinga.Usikuamini sana kupima huko, tahadhari iko mikononi mwako mwenyewe hadithi za akina mjomba palikuwa pakawa du!!! ni hatari.
Nakutakia kila la heri dada na nakuombea sana Mungu azidi kukutia nguvu ili uyashinde hayo majaribu.
Syajujo@yahoo.com
Anonymous said…
HABARI YAKO MSICHANA MZURI TENISHA.KWANZA NAKUPA POLE SANA KWA HAYO YALIYOKUSIBU.NINGEPENDA KUJUA NI KIPINDI GANI KIMEPITA TANGU MARA YA MWISHO KUGONOKA NA MPENZIO HADI MARA YA MWISHO KUPIMA?JE NI ZAIDI YA MIEZI 3-4 TANGU ULIPOGONOKA KWA MARA YA MWISHO NDIO UKAPIMA? OKAY BASI KABLA SIJAPATA HIZO DETAILS NAKUSHAURI MAMABO YAFUTAYO:

1.NAKUOMBA UWE MWANGALIFU SANA KATIKA KUFANYA TENDO LA MGONOKO NA MUMEO KWA SASA KWANI KWA KWELI NI HATARI SANA KWAKO KUAMBUKIZWA KAMA UJUAVYO UKIWA KATIKA MAHABA HAYO MNAWEZA JISAHAU NA UKAONA KWANI NINI BWANA WAMEKUFA WANGAPI?ETI AKU1 MIE NAMPENDA MUME WANGU UKAMPA NYAMA KWA NYAMA AKAMALIZA VI CREAM VYA MOTO MOTO MUMO KWA MUMO BAADAE MAJUTO.

2.KWENYE SWALA LA MTOTO NA MUMEO HILO NAKUOMBA SANA ULITOE AKILINI KABISA JE WATAKA KUFA NA WEWE? PAMOJA NA HICHO KIUMBE UNACHOTAKA KUKILETA DUNIANI? KWELI KUTAKUWA NA UMAANA WOWOTE?

3.MIMI NADHANI LAZIMA MUMEO ALIKUWA NA KIMADA NJE HIYO AKUBALI ASIKUBALI HAIWEZEKANI UKAPATA VVU KWA NJIA YA MBU AU VUMBI OKAY?KWA HIYO KWA USHAURI WANGU KAENI CHINI ULIONGELEE HILO NA MUMEO KWA MAANA YAKWAMBA UZAE NA MTU MWINGINE NA HIO NDOA MUIVUNJE MBAKIE MARAFIKI TU.UNLESS LABDA UWE UMEAMUA NA WEWE UWE NA VVU KAMA YEYE KUMBUKA DADA ANGU MAISHA NI POPOTE PALE NA MAPENZI SI KWA MTU MMOJA UTAMPATA MWINGINE UTAAKE MPENDA KAMA MUMEO WA SASA HILI NALISEMA KWA AJILI YA KUHOFIA USALAMA WA MAISHA YAKO YANI NAJUA TU IKO SIKU MTAGONOKA LIVE TU YUESU WANGUUUUUUUUUUUU!KWA KWELI NI HAYO TU KWA LEO DADA ANGU.
Anonymous said…
pole sana mdogo wangu,mimi ni miongoni mwa walio mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya maambukizi ya vvu na mdau mkubwa wa blog hii.Napenda kusema yafuatayo.1.ni kweli kwamba condom haitoi kinga ya 100% lakini kwa sasa ndo njia pekee iliyothibitika kuweza kuzuia maambukizi ya vvu kwa zaidi ya 97%(kama itatumika kwa usahihi)2.nina wafahamu wanandoa wenye tatizo kama lako (kitaalam tunawaita discordant couples) ambao wameendelea kungonoka kwa kutumia condom for more than 10 years na bado alie kuwa negative hajaambukizwa! Endelea kumpa haki yake mumeo kwa kufuata tahadhari zote ambazo naimani umeshaelezwa na counselor wako.3 Kwa ufahamu wangu,hutaweza kupata mtoto na mumeo kwa njia ya kawaida bila kukuweka wewe hatarini,njia pekee inayoweza kukusaidia ni 'in vitro fertilization',muulize dr wako atakuelewesha zaidi.4.Nimefurahishwa na upendo ulionao kwa mumeo,endelea kumjali na kumtunza kwani anakuhitaji sana sasa hivi kuliko kipindi kingine chochote.5.Unaweza kuishi bila ngono KAMA UKI-TUNE AKILI YAKO,nakushauri utumie njia za kujiridhisha kwa kutumia mbinu mbadala(masturbation,vibrators etc) ili kumtunzia uaminifu mumeo.mungu akusaidie katika mapambano uliyonayo.MAYAK-ARUSHA.
Anonymous said…
HAYO NDO MAPENZI,UNAMPENDA MTU SIO KWA SABABU NI MZIMA ,BALI KWA KILA HALI.
MTOTO NI MWEPESI KUPATA,SIO KILA MNAPOFANYA NGONO ANAWEZA KUKUAMBUKIZA,NI ASILIMIA CHACHE SANA KUKUPA NGOMA KWA KUAMUA KWENDA NAE TENDO MOJA LA KUKUZALISHA,KISHA RUDINI KATIKA KONDOM.
AU NENEDENI MKAFANYE INSEMINATION, HUWEZI KUPATA INFECTIVE DOSE KISHA NGOMA.
TAFADHARI KAWAONENI USHAURI NASAHA.
Anonymous said…
pole sana dada,

mimi nimeshangaa kidogo watu wanasema usifanye tena mapenzi na huyo mumeo kwa kutumia condom, wanasisitiza uache. ni washauri hao hao ambao mara nyingi wamekuwa wakiwashauri watu kutumia condom kwa sababu ni kinga dhidi ya maambukizi ya ukimwi, sasa leo ndio nimejua kumbe condom sio kinga kama tunavyoiongelea mara nyingi. mimi ni mmoja wa watu ambao huwa sio wepesi wa kuamini kwamba condom ni kinga na leo nimethibitisha kutokana na jinsi washauri walivyosema hapa.

kwako dada, hata kama unatumia condom, mimi naona ni hatari tupu labda kama umeamua kufanya vile wanavyosema "kwa shida na raha", hapo ni sawa na kuingilia kuogelea na panga kwenye mto wenye mambo tena umeshawaona.

Omba Mungu sana dadangu, upo katika kipindi kigumu mno, umejaribiwa na hapo ndipo imani inapopimwa.
Anonymous said…
Mh makubwa haya,mbona kama movie
tena ya ki nigeria au dengerlous desire ile ya kibongo,
mh si yakucheka lakini kama ni kweli pole sana sana tenaa kwasababu upo katika hard tym kuamua na hongera ur strong woman na ni mdogo sana tu kwa yaliyokukuta,tunajua unampenda sana mume wako lakini inabidi umuepuke tu uyo alikua malaya tena si wa mwanamke mmoja wala wawili full kicheche utake ustake anajua akikwambia ukweli utamuacha na sisi wanawake zaifu tuna huruma sana ndomana wanasemaga mwalimu wetu kipofu samtym kweli kabisa,kwanza ivi unajua wanaume wana roho ngumu sana iswear kama majibu yangeonesha wewe ndo muathirika na yeye mzima wallahi ungekula mabuti wewe kuanzia hospital adi nyumbani ukifika virago vyatupwa nje na wewe kwenu kila mtu angejua namajina yote machafu ungeitwa lakini ndo ivo,ushauri wangu ebu control nyege zako kwasasa ningumu lakini jitaidi msifanye tena ikishindikana mwambie ata doctor wenu awaite wote aseme ivo muache kabisa ata kwa condom,kaa naye chini kwa upendo na upole kiubinaadam mwambie mimi ntaendelea kukujali kukusaidia kwakila hali lakini kama ndugu au marafiki ila muachane tena kidini akuandikie talaka kabisaa ili wewe uishi kwa usalama umtafute mtu utakaemuamini na kumpenda mwenyewe mkapime tena mara 3 mana umeponea kwenye tundu la sindano unaweza ukawa around bado unakutafuta mana umekuvalia njuga hahahahaha ukimwi nae noma,kisha uamuzi wako kama utataka ndoa tena au ushatoa nuksi na ndoa ya mwanzo iliyobaki kungonoka tu hiari yako huyo ndo unaweza kuzaa nae mambo taratibu ata kuoana pia apo badae kama ukikosa mtu nikupe kaka yangu hahahaha lol {JOKES)ila mammy plisssssssssssssssss kinga bora kuliko tiba achana nae, ni hayo tu

tukijaaliwa inshaallah
kila kheri shostito
Anonymous said…
is it possible?huw mume nega mke positiv?inamaanisha hawa walikuwa wanangonoka na cd?au vp sijaelewa bado
Anonymous said…
Bidada u r so funny
Ok back to ushauri yaani we dada pole sana ukisikia majaribu ndo hayo,what i can i advice u ungeacha tu kungonoka na mme wako cos watu condom huwa zinapasuka,sometimes zinavuka,but kama u dont care na unampenda mumewako zaa nae,but kama unaona hutaki VVU its better usingonoke nae cos it is so risk.
Na kuhusu mtoto bora uzae na mtu mwingine ambae ndo utangonoka nae mara nyingi kama utakavyo, am pretty much sure huyo mume wako alikua na kimada mwingine hata kama unasema hakua nae but trust me alikua nae,Mens are so brave kwa upande wa kucheat.
ok then take care cos ur still young

Baby!!!!!!
Anonymous said…
Asanteni sana wote mlionipa ushauri , naomba nimjibu aliyeuliza hapo juu mimi jamani ni negative na mume wangu ni positive its almost a year now tokea tumegundua hivyo na tumepima sehemu nyingi sana tofauti ila majibu ni hayo hayo .
Anonymous said…
na pia tulikuwa hatutumii condom kwa miaka 4 tokea tumeoana.
Anonymous said…
Nimesoma majibu ya wengi humu nimeshikwa na butwaa. Yaani sikujua kama waTZ (au tuseme watu wengi waongeao kiswahili) wako mis-informed kiasi hiki kuhusu HIV and AIDS.

Nampongeza mdau Mayak wa Arusha hapo juu 7:56:00PM kwa ushauri mzuri na kwa ufahamu alionao. Ni jukumu la kila binadamu kuhakikisha anakuwa "well informed" kuhusu mambo yanayomzunguka na ambayo yanaweza kumu-affect iwe negatively au positively. Hivyo ni jukumu letu sote kujua kuhusu HIV AIDS kwa undani haswa.

Dada mpendwa hongera kwa moyo mwema. Wewe si wa kwanza na wala hautakuwa wa mwisho kuwa na partner ambaye ni +ve ilhali wewe ni -ve. Unachofanya ni sahihi na ufuate moyo wako kama kuwa na mumeo ndio furaha yako.

Mimi ni Dr mtoa ushauri. Nimekutana na couples wengi sana wenye situation kama yako. Ni jambo la kuhuzunisha tu kuwa mara nyingi ikiwa mwanaume yupo -ve basi uhusiano huvunjika lakini wanawake ni tofauti kabisa.

Ni juzi tu nimepima wapenzi wawili waliokuwa wanaingia kwenye ndoa, na kabla ya kupima nilimuuliza kila mmoja wao je kama mwenzake ameathirika atafanya nini. Mwanaume aliniambia kuwa hawezi kusema chochote mpaka baada ya majibu lakini mwanamke alijibu kuwa anampenda sana fiancee wake na hivyo majibu yoyote yatakayotokea hayatamfanya abadili uamuzi wa kufunga ndoa. Walipopima, mwanaume alikuwa ameathirika. Mnaweza mkafikiri ni hadithi lakini mwanamke alikubali hali ya fiancee wake na wakafunga ndoa na sasa wako kwenye honeymoon. Nimetoa kisa hiki ili kujaribu kuelimisha umma.

Siwezi sema mengi mpendwa mdogo wangu, naomba upitie website hii
http://www.thebody.com/
utapata majibu mengi ya maswali yako.

Na link hii
http://www.thebody.com/Forums/AIDS/Couples/
ina maswali kutoka kwa watu mbali mbali na majibu kutoka kwa wataalam jinsi ya kuishi na ku-enjoy life kwa couples wenye mixed status kama ninyi.

Na pia naomba wadau wote mliojibu hapo juu msome pia hiyo website na mjitahidi kuwa informed kuhusu issues mbali mbali si hili tu la HIV AIDS maana kama wasemavyo wajuzi "INFORMATION IS POWER"

All the best
Anonymous said…
Dear mdada,

Pole sana kwa yanayoendelea kukusibu mpaka hivi sasa. Ukweli ni kwamba huyo mumeo alikuwa na wanawake wa nje ambao alikuwa anatembea nao bila wewe kujua na akapata maambukizi. Una bahati sana wewe mshukuru mungu wako. Mimi labda ningekushauri tofauti kidogo na wenzangu kwamba kwa kuwa wewe ungali bado mdogo na unahitaji kupata watoto akupe talaka yako kihalali ili uwe huru kuolewa na mwanaume mwingine lakini baada ya nyie wote kupima. Au uwe mvumilivu mpaka hapo mungu atakapomchukua kitu ambacho mimi naa wewe hatujui ni lini. Kuhusu tamaa yako ya kufanya ngono mbona hiyo mara tatu kwa mwezi mie naona inatosha ambapo ni kama mara moja kwa wiki? Tulia dada na jaribu kuelewa tatizo la mwenzio na msharti yake.

Pole sana na zidi kumwomba Mungu.

Mdau.
Anonymous said…
huyo mumeo kwanza majibu yake ya awali yalikuwa ufisadi mtupu yani watu wanaleta ufisadi hadi kwenye majibu ya ukimwi hapo awali alitoa mkwanja huko sijui ndio angaza wakamtolea majibu mazuri.Na huyo mumewe bora angekueleza tu ukweli ukajua kuliko kusema hajui ukimwi ulikotoka muongo anajua sana.
pole sana na hongera sana kwa kukutwa hauna ukimwi ila wewe ni jasili sana japo kuwa umri wako mdogo ningekuwa mie ningetoka nduki Hospital sio mchezo ukimwi unatisha sana ila ndio hivyo kiubinadamu tena.

pole sana ila mie naona bora usingonoane tena condom inaweza kupasuka ikawa balaa.
Anonymous said…
Mchangiaji Dokta wa saa 8:55:00 AM hiyo link Dinah aliiweka tangu alipoanzisha blog hii lakini sema watu hawafungi. Hapo chini ya Profile yake upande wa kulia maandishi ya kijani kuna maelezo mazuri ya jinsi ya kuishi na VVU.Kama alivyosema mwenyewe kuwa tunaishai na jaamii iliyoathirika hivyo hatuna budi kujifunza namna ya kuisha na VVU kwani kuzuia karibu wote tunajua lakini bado tunaambukizana.
Angekuwa mwanaume hana alafu mkewe navyo angemuacha huyo mdada na VVU vyake lakini wanawake wavumilivu.Hili swali ni changamoto kwetu wote.
Anonymous said…
nimeguswa sana na tatizo la huyu dada na coments za dr hapo juu,ni ukweli unaosikitisha kwamba watanzania wengi wanaufahamu mdogo sana kuhusu mambo mengi ya msingi likiwepo hili la HIV/AIDS,nadhani hili linachangiwa kwa kiasi kikubwa na tabia tuliyonayo ya kutopenda kujisomea baada ya kuhitimu masomo,nazidi kumshauri mdogo wangu azidishe upendo kwa mumewe na azingatie kwa makini maelekezo ya dr na counselor anayemhudumia,MAYAK-ARUSHA.
Anonymous said…
mume mume ......... hata ngedere ana mume kama wataka kufa baki ungonoke naye kama wataka kuishi anza mbele.
Anonymous said…
mtu anaweza kuwa na partner mwenye ukimwi ila yeye asiupate?kivipi?nahitaji maelezo on this. na je kama dada ulingonoka for 4 years na hujapata si uendelee tu ivo ivo kwani kilichosababisha usipate those years ni nini kije kusababisha leo?si hukuwa unajua na ukawa unaenda kavu?basi wewe hutapata so endelea tu kungonoka.na ushike zako mimba.
Anonymous said…
POLE SANA TINASHE,NAKUPONGEZA PIA KWA MOYO WA UPENDO ULOJALIWA BIBIE,
ILA PLS ACHA KUFANYA MAPENZI KWA KUTUMIA ZANA ZA KILIMO HAZIAMINIKI KWA 100% INSHORT ACHA KABISA MAWAZO YA MTOTO KWA SASA, U BETTER WAIT KWANZA MBONA UMRI WAKO MDOGO WANGU UNALIPA SANA TU 25YRS UR STILL YOUNG WATU WANAZAA MPAKA 35YRS- 38 SO PLS MUOMBE MUNGU AKUPE MOYO WA UPENDO SUBIRA NA AKUPE MAISHA MAREFU HUKU UKIMHUDUMIA MUMEO, LETS BE HONESTY JAMANI KIAPO CHA NDOA SI KINASEMA WEWE NI WANGU KWA SHIDA NA RAHA??HAIJALISHI ALIUPATA WAPI WHO KNOWS??PENGINE VIWEMBE AU SINDANO,ANYWAY SIO KAMA NAMTETEA NACHOTAKA KUSEMA TUSIMLAUMU HUYU KAKA KWA SASA HALI ISHATOKEA KILICHOPO NI KUMSAIDIA HUYU YOUNG GAL,USHAURI WA DOKTA NI MZURI SANA NA MIMI NAONA MDADA NENDENI KWA MACOUNCELL WATAWAPA USHAURI MZURI ILA PLS DONT GIVE BIRTH WITH ANYBODY FOR THE MOMENT PLS!POLE SANA!
Anonymous said…
Hebu wote kila mmoja lipokaa na kama ameolewa au kuoa, tujaribu kujikumbushe kiapo cha ndoa,....

emu-three
Anonymous said…
Nimesahau tana dada Dinah, nilikuwa najaribu kuperuzi maandiko matakatifu kuhusu tendo la ndoa,...naona mengi ya maandishi yanasisitiza `kutokunyimana tendo la ndoa, mmoja ni nguo kwa mwingine...' kwa mantiki hii, changamoto ni kwetu na je imani zinasemaje pale mmoja anapoathirika, na mwingine bado? ni vyemakwa swalahili tukapata ushauri wa kidini.

emu-three
Unknown said…
Kweli inasikitisha sana tu,ukizingatia bado mdogo na vile vile siajabu hata huyo mumeo hakutoka nje alipata katika hizo njia nyingine,mimi nakushauri dada yangu ujaribu hiyo njia ya kupandikizwa mbegu za kiume japokuwa sina hakika kama hiyo huduma ipo hapa kwetu ila nadhani unaweza ongea na huyo daktari wenu pia,hongera kwa kuwa na upendo wa dhati kwa mumeo kweli kumuacha itakuwa si vema kabisa ni vigumu kujua amepataje na kummuliza ni kumnyima raha na kumsononesha kwani haitosaidia chochote.Kuna mjumbe amesema wapo wanandoa ambao wamepeana mimba kwa njia ya kawaida na mke kubakia salama inawezekana ila yote ni mapenzi ya mungu kwangu mimi naona ni risk sana.Mungu akutangulie dada.
Anonymous said…
Nashukuru sana Dinah kwa ushauri wako na wengine wote mlionishauri .
Lakini nataka tu niwaambie mlionishauri kuhusu kumuacha kamwe sitaweza kufanya hivyo; jiulize wewe ukipata utaachwa? au utajisikiaje kuona unaachwa kwa sababu ya matatizo?.Ni kutumia tu njia salama kama zinavyoshauriwa ili usipate maambukizi.zaidi ya yote namshukuru sana Mungu aliyenipa nguvu ya kuyashinda haya yote.
asanteni
tenisha mimii