"Samahani dinah mie kidogo niko nje ya mada ningeomba sana unifahamishe jinsi ya kuzuia mimba kwa njia ya kalenda kwani nimechoka kutumia midonge jamani tafadhali nifahamishe mpenzi ndugu yangu.
Yaani huwezi amini kitendo cha kuwa na mpenzi wangu kinanifanya niumwe kwa kufikiria mimba tu. Nimekua muoga mchezo nautaka ila tatizo kuingia kwa mimba hivyo basi nakuomba chonde chonde unifafanulie jinsi ya kuzuia kwa kutumia tarehe tafadhali naomba."
Jawabu: Asante kwa uvumilivu wako pia kwa ushirikiano wa kuuliza swali lako mahali hapa. Njia ya asili ya kuzuia mimba ni mbinu pekee ambayo wanamama wa miaka ile kabla ya madawa ya kisasa(kizungu) kugunduliwa. Njia hii inauhakika wa asilimia 96-mpaka 98 kama zilivyo njia nyingine za kuzuia mimba kama vile vidonge, sindano, patch, Coil. Njia nyingine asilia ni kumwaga nje (withdrawn), lakini hii unahitaji zaidi ushirikaino wa mpenzi wako, mawasiliano wakati wa tendo kwani akijisahau au kuchelewa ujue kitu na box.
Mipira (Condoms) ndio kinga pekee inayozuia mimba na magonjwa yote ya ngono kwa asilimia 99 na ile moja iliyobaki ni kwa ajili ya sababu za kisheria kulinda Makampuni incase mtu akatumia vibaya na kushika mimba au gonjwa la zinaa. Vilevile Kinga hii (Condom) ndio pekee ambayo ham-badilishi mwanamke kihomono au kimaumbile.
Njia ya asili ya kuzuia mimba hutumiwa na wanawake ambao kwa namna moja au nyingine hawataki kutumia madawa ya kisasa ili kuepuka mabadiliko ya miili yao kama vile kunenepa, kutokwa na majimaji ukeni na pia kuna tetesi kuwa yanaongeza uwezekano kwa mwanamke kupata Saratani ya Kizazi na Matiti.
Kuzuia mimba kwa kutumia tarehe inauhakika ikiwa mzunguuko wako ni uleule na sio mrefu (siku 32-35) wala mfupi (siku 18-24) bali ni ule wa kawaida ambao ni siku 28. Ili kutumia mtindo/mbinu hii ya kuzuia mimba unapaswa kuanza kuhesabu siku zako sasa na fuatilia kwa karibu mzunguuko wako na kuhakikisha kuwa una siku 28 sio chini wala juu ya hapo, kwa kawaida unaaza akufuatilia kwa miezi mitatu hadi sita (kama umewahi kutumia madawa ya kuzuia mimba) kabla hujaanza kuitumia njia hii.
Namna ya kuhesabu nitumiayo mimi-Ili kuwa na uhakika na urefu au ufupi wa mzunguuko wako unapaswa kuhesabu siku ya kwanza utakayo ona damu mpaka utakapo ona damu ya mwezi utakao fuata.
Mfn; leo tarehe 12 mwezi wa kumi na moja ndio umeanza hedhi basi hedhi ya mwezi ujao itakuwa tarehe 10 mwezi wa kumi na mbili.....hii ni kama mzunguuko wako usiobadilika (sio mrefu au mfupi) ambao ni siku ishirini na nane tu.
Siku ya kwanza ya hedhi mpaka siku ya tisa ni salama na huwezi kushika mimba, baada ya hapo mpaka siku ya kumi na nne (yai linapevuka) unakuwa hatarini, siku ya kumi na saba mpaka siku ya ishirini na mbili unakuwa salama tena mpaka siku ya ishirini na tatu mpaka ishirini na saba (yai pevu linashuka) hatarini lakini ile ya ishirini na nane siku ya hedhi nyingine unakuwa salama tena......comfusing ei?
Ili kuwa na uhakika kuwa uko kwenye mstari kuliko kuegemea kwenye tarehe tu unatakiwa kujua mabadiliko ya mwili wako. Unapokuwa hatarini kushika mimba mara nyingi utahisi nyege zaidi n avilevile utoko wako utabadilika na kuwa mlaini zaidi (kama lotion) na wakati mwingine utahisi ute unatoka (ule kama udenda/mlenda)....ukiona hivyo hakikisha unatumia Condom vinginevyo utashika mimba.
Unapokuwa salama mara nyingi hamu ya kungonoka inakuwa haipo sana unless "uchokozwe", vilevile utoko wako unakuwa mzito (kama cream/mafuta mazito)na mweupe sana yaani hata wakati wa kujiswafi inakuwa taabu na inaweza kukuchukua muda mrefu zaidi. Hali ikiwa hivi ujue uko salama kungonoka bila kinga ya kuzuia mimba.
Kila la kheri!
Comments
Hata njia ya kalenda inapoteza maboya usije ukajidanganya hata kidogo.kama kweli unaogopa kudaka mimba, basi oana na huyo jamaa au ndo mambo ya kuibiana hayo.Yatakutesa bure?kwa nini usingeacha tu huo mchezo.
Kama unaona vigumu kuuacha mchezo huo, basi mimi nakushauri tumia kondomu itakusaidia kuliko kalenda.Hako kamchezo kamewaponza wengi sana, ni katamu,lakini machungu yake utalani kitendo.
Kama ni mwanafunzi njia pekee ni kuacha.Kumbuka shule ndiyo mume/mke au ndiyo baba/mama yako kwa maisha yako ya baasdaye.Usije acha shule na kuanza kulea ambaye hukumweka kwenye mipango yako.haya yako maamuzi dada yangu.
Unaweza kutumia vidonge au sindani au kondom ila njia zote hazina uhakika nikujaribu hivyo usijisahau sana ila njia ya asili kwaupande wangu naona kama haina uhakika hakikisha siku zako za mwezi hazibadiliki na uwe makini kwakuruka siku za hatari.
Ushauri kwa muuliza swali nikwamba kuwa makini na huyo mchumba mambo yakuanza kuishi bila ndoa ni mashaka, wanaume wengi ukishamuonjesha haoni sababu yakutangaza ndoa sijui muwe mnapendana vipi napia maswala yakutumia vidonge au sndano ni uaweza kumeza mividonge ikakuletea madhara bdae
Kwanza ulificha mengi mara ya kwanza ulipouliza swali.baada ya kurushiwa makombora ndipo ukaja na maelezo mengine angalau.
sasa wewe dada kuna mabo kadhaa ambayo umezungukwa nayo.
jambo moja ni kwamba umetuambia mchezo unaupenda hutaki kuuacha.
Pili umesema unakaa na huyo jamaa na mnaendelea kutombana usiku kucha.
Tatu huyo jamaa yako anataka kukuning'inizia uzi ili ushone ndani na ndipo ajue kuwa uko fit.
Nne wewe hutaki mimba ingawa kuchapwa bomba(Kungonolewa)unakuhusudu sana.
(huo ni msamiati mwingine wale wasiojua.)
Kama unaishi na jamaa huyo, Je, nani mjinga asijue kuwa unachapwa bomba na outcome yake ni kubeba mimba?Je, ni nani unamwonea aibu kubeba mimba,lakini kuchapwa bomba unaona ni ujasiri?halafu ukipata hizo njia za kuzuia mbona mtatofautiana na huyo mpenzi wako na kama unampenda kama ulivyokiri mwenyewe Je, uatakuthibitisha vipi kuwa u fit ili akuoe?Je, kama sasa unaenda kijificho kutafuta njia za kuzuia mimba huoni kuwa njia hiyo itakugharimu hadi mtakapooana utakuwa unajificha kufanya mabo hivyo badala ya kukaa na kuzungumza muelezane uwazi na ukweli wa mambo?
Wewe dada amua moja tu kama hujaridhika na utungaji mimba achana naye kwa nini ujisumbue na jambo lililondani ya uwezo wako?Yaani kuchapwa bomba tu kunakutesa hivyo????
Haya nakutakia maamuzi mema.
Nimesoma comment za wadau mbalimbali, lakini kikubwa nilichobaini nikiwa kama mdau wa masuala ya uhusiano, mapenzi na ndoa nimebaini kuwa tatizo la huyu dada bado halijapatiwa ufumbuzi!
hivyo basi, nami brazatk mzee wa malavedave ninayepiga libeneke kwenye blog ya www.mwakilaga.blogspot.com na Jarida la Chombeza Time linalopatikana mitaani kwa Tsh 1500 tu likiwa limesheheni mada na meseji kali za mapenzi ninataka kuweka bayana machache kuhusianaa na tatizo la dada yangu na endapo wadau mtataka zaidi msisite kutembelea blog yangu ama kuwasiliana nami ofisini kwangu, kwa ushauri wa bure!
Kwanza nataka niwaeleze wadau juu ya athari za vidonge vya kuzuia mimba: Wanawake wengi hujikuta wanakumbwa na machafuko ya tumbo au kutapika wakati wa asubuhi, kuvimba matiti kama siyo kukumbwa na dalili za ujauzito mara wanapoanza kutumia vidonge kwa mara ya kwanza! Hii husababishwa na vidonge hivyo ambavyo vina hormones zile zile ambazo mwanamke huzitia kwenye damu wakati akiwa na mimba. Hata hivyo wataalam wanasema kuwa dalili hizi hufikia kikomo baada ya miezi kati ya 2 hadi 3.
Sambamba na hilo watumiaji wengine wavidonge hutokwa na damu nyingi wakati wakiwa kwenye siku zao.
Athari kubwa anayoweza kuzipata mtumiaji wa vidonge vya kuzuia mimba ni kuganda kwa damu kwenye moyo, mapafu au ubongo!
Wadau naomba muelewe kuwa kwa wanawake wengine mimba pamoja na kutumia vidonge vya kuzuia mimba vina hatari kubwa zaidi kwao. Hivyo basi wanawake hawa ni lazima watumie njia zingine za kuzuia mimba! Hivyo sioni sababu za kumshambuklia dadan huyu aliyeomba kupewa msaada na dada dinah.
Baada ya kutanabaisha hayo naomba sasa nimjibu dada yangu jinsi yakutumia kalenda kujikinga na mimba!
Njia hii haina uhakika sana wa kuzuia mimba, lakini ni nzuri kwa sababu haigharimu chochote.
Njia hii huwafaa zaidi wanawake amabo taratibu za siku zao za kwenda mwezini ni kawaida mara moja kila baada ya siku 28, na ili iweze kuzaa matunda, njii hii huhitaji mtumiaji awe tayari kukaa bila kukutana kimwili kwa muda wa wiki moja kila mwezi!
Kwa kawaida kuna siku 8 tu kila mwezi ambazo mwanamke anaweza kupata mimba ambapo siku hizi zipo katikati ya siku zake za kwenda mwezini, na huanza siku 10 baada ya siku ya kwanza ya kupata damu ya hedhi. Hivyo basi ikiwa mwanamke yoyote hataki kupata mimba ni lazima aache kukutana na mwanaume kwenye siku hizi 8! Naamini hili linawezekana kwani siku nyingine zilizobakia wapendanao wanaweza kujiachia kama kawaida kwani hakuna uwezekano wa mwanamke kushika mimba!
Ili kuepukana na kutatanikiwa, ni lazima mwanamke aonyeshe kwenye kalenda zile siku ambzo hatakiwi kukutana na mwanaume. Hapa inaweza kuwa ngumu kuchora kalenda ya ukutani kwa kuwa inatumiwa na wengi lakini ni rahisi kutekeleza hili kwa kutafuta pocket kalenda [kijikalenda ambacho waweza kiweka kwenye pochi yako]
Kwa mfano: Unaingia kwenye siku zako tarehe 5 Desemba, weka alama kwenye tarehe hiyo kisha hesabu siku 10 na baada ya hapo pigia msitari siku 8 zinazofuata!
Kumbuka siku hizo nane utakazozipigia msitari ni hatari kwani ukikutana na kidume tu na kushiriki ngono bila kutumia kondom utashika mimba, hivyo ni vema usikutane na mwanaume hata kidogo, yani epuka hata akikubembeleza na lugha laini kuwa nitapizia nje sweetie, sijui nini na nini kama hataki tumia kondom kataa kwani kupizia nje ni bahati nasibu hasa pale mwanamke anapoamua kumpa mwanaume maujuzi ya kabatini ambayo ni adimu, yaani mwanaume hupewa kwa sababu maalum tu hali inayomfanya apagawe kwa huba na hivyo huweza msababisha ashindwe kupiziza nje!
Je, ni maujuzi yapi hayo ya kabatini?n Hahahah, endelea kusoma safu ya dinah na www.mwakilaga.blogspot.com sambamba na Jarida la Chombeza Time linalopatikana kwenye meza za wauza magazeti nchi nzima [Tanzania] uweze kumpagawisha umpendaye.
Tuendelee na mada, ukishapigia mstari siku hizo nane maisha yanaendelea na sasa tufanye mwezi unaofuata siku zako zinaanza tarehe 1 January. Weka alama ile ile kwenye siku hiyo.
NA kwa mara nyingine hesabu siku 10, na na piga mstari chini ya siku 8 ambazo hupashwi kukutana na mwanaume kabisa.
Naamini dad yangu nitakuwa nimekusaidia kidogo lakini endapo una swali zaidi usisite kuuliza iwe kwangu, brazatk au dada dinah kwani naamini akipata muda wakutosha atakujibu tu.
NB: Usikose kutembelea kila siku www.mwakilaga.blogspot.com kwa mahitaji yako ya marafiki/wachumba, mada na meseji kali za mahusiano, mapenzi na ndoa.
Asanteni,
Brazatk