Tangu nimeachana na wangu, sitaki Demu-Ushauri!

"Eti dinah wewe ni profesheno kwenye mambo ya LOVE???mi namatatizo kichizi ya kisaikolojia ,Tangu niachane na chick wangu feb 2007 mpaka leo sitaki demu na wala sijisikii kabisa kuwa na uhusiano vipi ninamatatizo gani???

Aalafu kwa nini simpati demu mwenye sifa ninazotaka?? best wishes"

Jawabu:Shukurani kwa kukubali ku-share tatizo lako hapa kwa faida ya watu wengine wenye tatizo kama lako au ambao watakumbana nalo hapo baadae.

Sidhani kama unatatizo, hiyo ni hali ya kwaida inatupata watu wote tunapoachana na wapenzi wetu ambao tulikuwa tukiwapenda sana au tumekuwa nao kwa muda mrefu. Inakuchukua muda mrefu kabla hujaondokana na hilo yaani kwa kifupi ni kuwa alikuumiza sana au uliumia sana kumaliza/ua uhusiano hali inayokufanya upoteze imani na wanawake kwa ujumla ukihofia wao kuwa kama yeye at the end. Japo kuwa sio kweli kwani wanawake tunatofautiana. Hivyo all u need is time to heal jeraha lako.


Sio rahisi kupata mwanamke mwenye sifa zote uzitakazo kwani huyo atakuwa "perfect" na "there is no such thing" hapa duniani, kwani hata Malaika hawako hivyo. Ukiwa tayari kupenda tena au kuwa kwenye uhusiano basi fuata moyo wako lakini suisahau akili yako.

Jiwekee sifa utakazo kwa mwanamke lakini ikiwa utamdondokea mmoja ambae ana-tick box 5 muhimu out of 10 mchukue nyingine utarekebisha ukiwa ndani ya uhisiano. Kitu muhimu cha kuzingatia sio sifa alizonazo bali hisia zako za kimapenzi juu yake na je utakuwa mtu mwenye furaha ukiwa nae karibu?

Sasa take your time to get over kilichotokea alafu ukiwa sawa/tayari mambo yatakuwa bomba kuliko ilivyo kuwa na EX, kumbuka kwenda taratibu, kuwa wazi na boresha mawasiliano ili ikusaidie kumfahamu mwenzio zaidi.

I hope nimekujibu vema na umenielewa.

Comments

Anonymous said…
Lazima ulikuwa unampenda sana au alikuumiza sana kiasi kwamba umekata tamaa na wanawake wote kwa ujumla.
Anonymous said…
Hiyo ni hali ya kawaida, na inamkuta kila mtu, pale anapoingia kwenye mitihani mizito, hasa ya kuachwa kwa namna yoyote ile. Lakini cha ajabu siku ukimpata umpendaye hutaamini, hali hiyo itaondoka na utadunda kama kazi.
Kitu kikubwa cha kufanya ni kuchukuliwa mambo yote `kama kawaida' na usiharakishe katika maswala haya ya mahusiano, labda kama umri umeenda. Na kama kweli hujisikii kuwa na demu katika karne hii, na kama kila kitu kipo safi, basi mshukuru Mungu na tuliza mawazo yako vizuri huku ukidadisi kwa undani, ipo siku utamkuta ambaye hukutegemea.
Kwa kusema kuwa humpati demu mwenye sifa unazozitaka, ina maana umeshaanza kutafuta. Hapo rafiki yangu kuwa muangalifu, wapo walioanza `kuonja' na hatimaye wakajikuta wamempata yule ambaye hafai kwake kabisa, lakini kumuacha tena ikawa haiwezekani. Siunajua tena pale unaponasa, kutoka hutoki ingawaje unataka.
Wasichana wazuri wapo na kila siku wanazaliwa wazuri, tatizo ni jinsi ya kumpata. Kitu muhimu wasiliana na watu kama dada Dinah, ambao wana mitandao mipana, ipo siku utampata.
Huo ndio ushauri wangu
emu-three
Anonymous said…
Hiyo ni kawaida katika mapenzi, kutegemeana na sababu iliyofanya mkaachana na jinsi mlivyokuwa mnapendana, na malengo yenu kwa ujumla. Hali kama hiyo hujitokezo uwe umeacha au umeachwa. Ila inazidi kuwa mbaya kama ulitendwa vibaya.

Cha kufanya sasa hivi ni kukubali yote yaliyotokea, kujikubali wewe mwenyewe na kufurahia maisha ya u-single. Nakushuri uendelee kufurahia tu na masela katika maisha ya u-single, na kuna siku bila kutarajia wala kujua, utajikuta umenasa kwa mtu mfulani. Hapo utaanza maisha mapya na kusahau yote yaliyotokea. Enjoy kijana, wenzako tunatamani kuwa single ila hatuna nafasi ya kuwa hivyo
Anonymous said…
ucjal hiyo ni kawaida,ht mi pia ilishawahi nikuta nliachwa solemba nikaona km dunia imefka mwisho lkn nlikaa kwa kipnd kirefu kla anaenifuta naona hafai,bt now am happy naenjoy life km kawa cz av find someone who fits me
Anonymous said…
ni kaiwada tu ukiachwa haswa kwa mtu uliyempenda pale inapokuwa ndivyo sivyoo. Nilishapitia huko, cha muhimu jiangalie kwenye kiooo na kujiona wewe ni mzuri tu wakuvutia na unauwezo wa kumvutia msichana yoyote. Jipende,jipe nafasi kwanza wewe, fanya nachotaka mfano kama ni mtu uliyekuwa unapenda mitoko (outing) nini? endelea wala usijifungie ndani. Jenga urafiki kwanza nawasichana ile kula nao story nini, usiangali negative things sana za wanawake. kwa ufupi usiwe pick sana mfano, kama unalisti ya vitu usivyopenda juu ya mwanamke. maan mie nilikuwa na list ya nisivyovipenda juu ya wanaume lakini, nikakuta hii type ya wanaume nisiyoipenda, ndo huyu niliyenaye na ananipa raha hadi sasa, na wale niliokuwa nawapenda waliishia tu niumiza moyo wangu (vibuti kwenda mbele nilipewa). Kwa ufupi huyu hakuwa kwenye hata 15 bora katika list yangu ya wanaume nao taka. Ila sasa nina raha, moyo wangu unaraha ingawa tunatofautiana sana tuuu, hadi mwonekano wetu.
Anonymous said…
Mimi sasa hivi jamani sio mchezo kabisa yaani sitaki kusikia kitu kinaitwa demu maana nimechanganyikiwa sana na nimemwaga hela sana sasa bora nile ninenepewe mwenye...nile zangu chips kuku maana nimeangaika vya kutosha na unaweza kufa hivi hivi yaani kwa ajili ya kitu kidogo sasa si bora kuvimbiana tu??Au kukaa kupumzisha akili maana mhhh nime salute kwa kweli nilikuwa mjanja kwa mademu lakini nimebanwa mimi jamani acheni mchezo mapenzi ni kitendawili kabisa.....
Anonymous said…
Dina Na wadau wote,thanks 4 maoni,mliyo nipa

i was a lil bit crazed,mmmH!!