"Abnormalitie" ktk uhusino wa kimapenzi....Ushauri!

"Asante sana dada Dinah kwa kutoa Elimu kwa watanzania wenzako. Samahani mimi naomba nitoke nje ya maada kidogo. Naomba niongelee suala la abnomaralities katika miili yetu na madhara yake katika mapenzi.

Abnormalities zenyewe ni mfano mwanamke kuwa na ndevu, wasichana au wavulana kuwa na mvi katika umri mdogo au wanakuwa wamezaliwa nayo. Kidogo mvi watu hutumia dawa( dye) kuzuia mvi, ila ndefu kwa wanawake imekuwa vigumu.

Nataka kujua je wasichana wenye ndefu na ambao hawajaolewa, wanapata wachumba? Swala la pili ni mimi mwenyewe: Mimi ni mvulana wa miaka 27. Nina mvi kiasi kichwani.

Nimekuwa na tabia ya kuzipata rangi ili zisionekane. Lakini girlfriend wangu wa kwanza siku moja aninikuta nikipaka rangi nywele zangu, then nikamwambie sababu, tangu siku hiyo akasema niache kupata rangi kuwa yeye haoni tatizo na hizi mvi zangu, akasema tena zinanipendeza sana.

Nilikaa naye miaka 4 tukaachana. Sasa ninaye girlfriend mwingine. Nimekaa naye miaka 2 sasa lakini hajui kama nina mvi kichwani kwani huwa nazipaka rangi. Tunapendana sana na mwezi ujao nina mpango wa kumvisha pete ya ndoa. Je niache kuzipata rangi mvi zangu ili azione au nifanyeje? Naogopa labda huenda akapunguza upendo wake kwangu.

Kwa ujumla mimi sijui wasichana wanamchukuliaje mvulana au mwanaume mwenye mvi katika umri mdogo. Dada Dinah na wadau wengine naombeni ushauri."

Comments

Anonymous said…
well ni vizuri ajue mapema sio baadae ndo ashangae, mweleze kiutani hivi unajua niana asili ya mvii kama mtu fulani kwelii huwa napaka dawa ila nimezoea kupka rangi hadi nasahau kusema,
kwa upande wangu nadhani ukifika umri wa 30 and above utakuwa sex zaidi ukicha mmvi zako, mie sioni ubaya, ilimradi uvae kuendana na umri wako na uwe active tu. Kial raheri kwenye kuvishana pete na uoe kabisa mapema.
Anonymous said…
Binafsi ningeona upunguze kujiamini,jaribu kuwa wewe kama wewe(ulivyo) na wala usijishtukie kimaumbile.Kua na mvi kabla ya umri si tatizo kubwa lakuweza kusababisha mapenzi kupungua.Watu wanakua na vilema mpaka mbooni lakini bado wanapendwa hivyo jiamini.Tena hiyo ndio nafasi ya kumsoma huyo mpenzi wako.Kama atapunguza mapenzi kisa una mvi basi huyo si wa kuoa,hakupenda kama ulivyo.Khs wasichana kua na ndevu ni hormone na hata hivyo wanaume wengine tunavutiwa nazo tena kama akiongezewa na dimpoz uuuuuh anakua bomba na unique!!

Ni mimi ITEITEI
Anonymous said…
Yes kuhusu hali
isiyoyakawaida kimaumbile ipo, na watu wote tunatakiwa tukubali hivyo. Wapo wenye `hali hii au ile' ambayo huenda kazaliwa nayo au imemtokea katika ukuaji wake. kwangu mimi sioni kuwa kuna tatizo gani kwa hili, kwani mapenzi yanajengwa toka ndani, na nje ni kama vikorombwezo tu.
Kama mtu anakupenda kikweli haijalishi wewe ni mfupi au mrefu, una ndevu au huna. Kama kakupendea kwa `ndevu zako' basi muelewane kwa hilo. Na ni vyema mukaelezana ukweli mapema. Usifiche kasoro iliyopo mwilini mwako, hayo sio mapenzi ya kweli! Siku akigundua ataanza kuondoa imani nawe.
Wakati nasoma haya maelezo yako, nikakumbuka jamaa mmoja ambaye jana alitoa mpya. Wapo hawa jamaa wenye magonjwa ya ajabu. Nayaita magonjwa kwani watu wanayajenga wenyewe bila kujijua. Kuna kitu kinaitwa `chabo'.Nani kawahi kusikia hiki kitendo cha ajabu, kiitwacho chabo!
`Chabo' ni hisia za kujijengea mwilini kama ilivyo `usagaji na usenge'. Hali hii inajengwa na hisia za kujiendekeza, na matokeo yake unavyokuwa mkubwa hali hiyo inakuwa haitoki!
Jamaa mmoja alifumaniwa akiwa kwenye dirisha la nyumba akiwa anajishughulisha kumaliza haja yake akiwa anawachungulia wapendwa wakifanya vitu vyao ndani. Jaribu kufikira mwenyewe mtu wa namna hii yukoje.Ni ajabu na kweli. Ipo mifani kama wale wanaochafua nguo za watu wakiwa wamebanana kweny daladala. Ukisikia huwezi kuamini, lakini vipo na watu kama hawa wapo.
Ninachotaka kusema hapa ni kuwa yapo mabadiliko ya kweli kama hiyo ya kutokwa na mvi, wanawake kuwa na ndevu nk. hivi ni vitu vipo nje ya uwezo wetu, na haviathiri `mapenzi ya kweli'! lakini vipo vitu vya kujiendekeza, ambavyo baadaye vinaharibu `ubinadamu wa mtu' hivi tunatakiwa tuwaelimishe watoto wetu. Kwa mfano, unapomuona mtoto wako anajenga tabia ya kuchunguliachungulia madirishani anza kumkataza kihekima! Pia wakatazeni watoto wenu kwenda kuangalia mikanda ya video inayoonyoshwa mitaani, na vitu kama hivyo. Hali hizi huanzia hapo.
Naona niishie hapo
emu-three
mahusiano mengi yanashindwa kudumu kutokana na watu kuto kuwa wawazi tangu mwanzo wa mahusiano.

Kuna watu unakuta hawapendi kabisa pombe.Ila kwa kuwa anashida na mtu atajilizimisha kuipenda pombe.Mimi naamini kama mtu ukiwa wazi tangu mwanzo,mwenza wako ataamua KUSUKA au Kunyoa.

Unaweza kukuta huyo uliye naye kwa sasa hapendi mvi.Ila kwa kuwa wewe umejitahidi kuvifa mpaka unamvisha pete.Basi anaweza kukuvumilia na baada ya muda akawa anatumia muda kutafuta aisiye na mvi.Ila iwapo angetambua tangu mwanzo basi nafikiri kungekuwa hakuna shida.

Ni sawa na basdhi ya watu.Walishajaaliwa kupata mtoto au watoto kwenye mahusiano ya mwanzo.Anapata mpenzi mpya anaficha ile siri mpaka mahusiano mapya yanakuwa sehemu nzuuiri ndio ana mwambia mwenzake nina mtoto.
MY GOD! anaweza kukuridhisha kakakuelewa huku akikutafutia na wewe revange kwa hilo.

Hivyo kuwa wazi jiamini..mtu kama anakupenda ndefu,mvi,kitambi,unene sio tatizo.

Jiamni.
Tutafika tu.siku njema D na wadau
Anonymous said…
Mdau kweli umefanya vizuri sana kuweza kueleza ukweli wako lakini sasa mimi sidhani kama etii ukiwa na mvi mwanamke anaweza akakusumbua lakini ina depends huyo mwanamke yupo vipi na mwanamke wa aina gani sasa mimi kwa ushauri wangu ni kwamba wewe hizo mvie endelea kuweka dawa usikate tamaa ila sasa ukishamvisha pete unaweza kuacha hakutakuwa na tatizo na pia si afadhali ya wewe una miaka 27 ni mkubwa lakini wengine wanazaliwa nazo hizo mvi mtoto anakuwa na miaka 12 au 13 na anakuwa nazo sasa mimi hapo naona kama wewe za kwako ni za ukoo kwa hiyo wala usisumbuke kuhusu wanawake kabisa wewe endelea kuweka dawa kama ulivyo sema alafu hapo baadae hakutakuwa na tatizo kabisa au sio mdau poa tunashukuru kwa kuweza kutoa mada yako lakini sijui kama nimekujibu vizuri au vibaya have nice day....
Faisal Mahrez said…
Mapenzi yanayojengwa kwa ukweli na kuaminiana ndio hudumu na si vinginevyo.
Usikubali kumpenda msichana au kupendwa na msichana kwa ulichonacho aidha kihali au kimaumbile. Siku zote mapenzi yanayodumu ni yale yanayojengwa na wewe kama wewe na yeye kama yeye. Mpendane kwa vile mlivyo.