Utachumbiwa lini.......? Make him(II)

White Gold & Diamond!
4-Ni mwiko kuwa tegemezi, hakikisha unafanya kila uwezalo kuonyesha kuwa unaweza kufanya mambo yako kivyako bila kuomba-omba (vibomu) unless umekwama kweli kweli yaani malipo yamechelewa au biashara hajaenda vema mwezi huu na mwenye nyumba anatishia kukuweka nje, hakikisha tukio hilo halijirudii mara kwa mara.

Kumbuka kuzungumzia malengo yako ya baadae (sio ndoa) malengo yako kimaisha kwamba ungependa unatafuta kiwanja ili ujenge nyumba hata ya chumba kimoja Mungu akikujaalia, ungependa kununua shamba mahali na kufanya kilimo cha mboga-mboga n.k.

Sahau au usithubutu mambo ya kisistaduu uchwara ya ningependa kufungua duka la kuuza nguo, kufanya pati kubwa ya kuzaliwa kwangu au kununua Prado.....haitosaidia kwani ni kama vile unamwambia akupe mtaji.....zungumzia vitu vikubwa vya kudumu.....atakuona una akili ya kimaendeleo na unafaa kua wa milele Daima.


Sisemi kuwa usipokee zawadi au "mshiko" aki-offer si kajitolea bwana.....hiyo bomba lakini kale ka mchezo ka' kumfanya mpenzi wako kitega uchumi sio njema kwani kila mtu anamajukumu yake ujue! Mwanaume akionakuwa unaweza kujitegemea bila kuwa na kiburi (uswawa kwa sana)anakuwa na uhakika na maisha yenu ya baadae kama familia, na hivyo kusogeza swala la ichumbana ndoa karibu zaidi kuliko alivyopanga kuwa mpaka ajenge nyumba, kumiliki biashara kubwa n.k.


Kwani atajua wazi kuwa mtashirikiana na kufanikisha mambo haraka zaidi ikiwa mko pamoja kama mke na mume......ni kweli ukiwa mwenyewe kufikia malengo inachukua muda mrefu sana (kutokana na uzoefu wangu) lakini mkiwa wawili ktk ndoa malengo yanafikiwa chap-chap....kumbuka usemi usemao umoja ni nguvu na...........!

Hivyo mwanamke usibweteke fanya bidii ktk shughuli zako na onyesha kuwa unaweza kuweka tofauti ktk maisha yenu (ikiwa mtafunga ndoa) hali itakayomvuta mpenzi kutangaza ndoa.


5-Kamwe narudia tena kwamwe usiruhusu amalizie manii yake ndani hakikisha na ni mwiko kutumia madawa ya kuzuia mimba (kisa cha kubadili mwili/maumbile yako) kwa mwanaume ambae hajakuchumbia, hakikisha manatumia "condom".....Kwanza hurushisiwi kabisa kufanya ngono lakini kutokanana mfumo wa maisha wa sasa, wadada tunabaki shuleni kwa muda mrefu tofauti na miaka ile na kuizuia nature inakuwa ngumu hivyo inabidi tu ufanye ngono nje ya ndoa.

Sasa kama huruhusiwi kufanya Ngono b4 ndoa kwanini unamruhusu mwanaume akumwagie ndani wakati unajua kabisa uhusiano wenu sio "commited" kwa sasa....nina maana hakuna pete ya uchumba? Ukimimbika je?Kumbuka unafanya ngono kabla ya ndoa ili kufurahisha mwili na sio kujenga familia (which is the Main reason ya kukutanisha miili yetu kwamujibu wa Sayansi na Dini)......kama anakupenda kweli, yaani kafika mwisho wa Reli lakini unamzuia kumalizia ndani ni wazi kuwa ataharakisha mambo ya kutangaza ndoa ili apate uhuru.......wenyewe wanasema "kumiliki mwili wako nje na ndani".


Baada ya kufanya yote haya na mengine ya kumfurahsiha na kumridhisha kitandani na nje ya kitanda ktk mwaka mmoja na bado hajatangaza ndoa? Aaaah lazima kuna kipengele nimekiacha, sasa hebu niambie mpenzi wako anapenda nini zaidi yaani kama vipi anaweza hata ngono akaiweka pembeni ili amalize anachokipenda na ikiwa hakijaenda alivyotaka basi ngono inakuwa "out of the window".

Nikipata majibu yako then nitakupa Mbinu ya mwisho (nitaweka ktk mtindo wa Polls kulia kwa site hii) na baada ya hii (mbinu ya mwisho) ndoa haijatangazwa basi no matter how much you love the guy ujue you are not enough to be his wife acha kupoteza muda, tafuta ustaarabu mwingine, maisha mafupi atii!

Kila la kheri.

Comments

Anonymous said…
Unajua nini nakupendea Dinah.. yaani unavyotufundisha akina sie hapa jinsi ya kujitambua, yaani kuwa ngangali na kuangalia mbele ili maisha yaendelee!! Paragraph ya mwisho imenikuna sana kwenye mtima wangu! Nimejifunza jambo zuri sana! unajua sometime hawa mashosti huwa wanatudanganya sana au niseme kwa njia nyingine huwa tunadanganyana sana!! kuhusu suala la kumng'ang'ania mwanaume akuoe hata kama haelekei. Jamani mashosti tuwe tunapeana ushauri unaojenga! Hii mambo ya kung'ang'ania sana wanaume watuoe hiii....
Anonymous said…
Heko dada Dinah, hapo sina dukuduku. Nafikiri umeweka kila kitu wazi, kazi ni kwetu. Ningepata nafasi ningetoka na wewe `out' weekend hii.(Sssssh, asijue wako wa moyo.)
Lakini hata wako wa moyo akijua kuna ubaya. Eti mfano, wewe umeolewa au tuseme hata hawo ambao hawajaoana lakini ni`wapenzi', hawawezi wakatoka `out' na mwingine, mfano mimina wewe tukatoka `out'. Lakini kwa wapenzi its ok, je kwa wenye ndoa? Naona hapo kuna mtihani.Hebu toa darasa moja kuhusu kutoka `out' na asiye mumeo, au mpenzi wako. Kuna watu wana-spend na mashemeji zao, ingawaje yametokea makasheshe ya ajabu. Je ni halali, tukaiga hili?
Kwa hii point, nafikiri tungeongeza ni `mwiko' kutoka `out' yenye kuchukua masaa mengi, hasa usiku na mtu ambaye hamjachumbiana, au mnasemaje. Well mnaweza mkapata `dina' pamoja, lakini,ile ya kuzidisha hadi kunywa na kunywa. Nafikiri hapo kutakuwa na utata. Sio kama naona wivu, mmmh, hata....
Kwa kipengele hicho pia tuongeze `mwiko' mwingine. Sivyema kumruhusu mwenzako kama hamjachumbiana, kupiga picha za ovyo-ovyo. Nazungumza hili kutokana na uzoefu. Wapo ambao baada ya kupendana sana, walifika hatua wakaaminiana, na iliyobaki ni kufunga ndoa. Lakini hawakuwahi kungonoana, waliahidi hiyo iwe zawadi yao `maalumu' baada ya ndoa. Raha sana kuvunjana `bikira' siku ya `fungate' Hii ni nadra kuipata siku hizi. Lakini wapo wachache...sijui.
Siku ya siku wakawa wametoka `out' na huko wakanywa na kunywa, na kwa vile walishafikia hatua ya kuaminiana hawakutiliana shaka. Siunajua tena kupenda-Wazungu wanasemaje `infatuation' au sio!
Dada Dinah, hiyo pete hapo juu, wabongo wakiiona watakukata kidole!
Tuendeleee...
Unajua tena pombe, pombe jamani, inaharibu akili. Wakaamua wasirejee nyumbani, wakatafute chumba cha wageni, au sio. Na huko kwa mara ya kwanza wakangonoana. Wakawa wamevunja ile ahadi yao,kwasababu ya `kilevi'
Na ili kuiweka kumbukumbu yao, wakaamua wapige picha zile za siri.
Unajua tena maisha ni kupanda na kushuka, licha ya upendo huo, licha ya kuaminiana kwao huko, ikatokea la kutokea binti akapata `schholarship'-masomoni nje. Bwana akawa anakula vumbi bongo.
Huko na huko, Binti huko masomoni akakutana na aliyemuona ni zaidi. Macho si yamefunguka, na dunia si ameijua, akili ikamtuma. `Ingawaje kweli nilitokea kumpenda `yule' lakini hapa nimefika. Na jamaa huyo mpya alikuwa hana muda wa kupoteza akamchumbia binti, na harusi ikatangazwa.
Jamaa Bongo hana hili wala lile, alipoona mbona mwenzangu siku hizi kimya, hanipigii simu tena, hanitumii e-mail, kulikoni. Akiwa anatafuta ukweli siku moja akakutana na ndugu wa `mpenziwe' na kwa vile mambo yalishafanyika, yule ndugu alimueleza ukweli ulivyo.
Jamaa alikaa mwezi hajiwezi. Nini alichokifanya, alichukua zile picha akazipeleka kwa wataalamu, ile sura yake ikaondolewa kinamna ikabandikwa sura ya mtu mwingine na kuipeleka alikoipeka.
`binti mrembo ajiuza' na maneno mengi ya ajabu. Siunajua tena kuchafuana majina. Mume wa yule binti akazipata hizo picha. Ikawa `shughuli' na ndoa ikawa ndoana. Yaliyoendelea baadaye hutamani kuyasikia.
Sasa ni mwiko' kwa hali ya sasa hivi `kupiga picha, hasa za uchi au kumruhusu mwezako, hata mumeo,(kwanini mpige picha za uchi)akupige picha za utupu. Kuna leo na kesho huwezi jua.
Huo nami ndio mchango wangu wa leo.
emu-three
KKMie said…
M3 hiyo inakuja kwenye kipengele cha mwisho kinachotegemea zaidi polls.Vuta subira. Asante kwa ushirikiano.
Unknown said…
asante kwa ushauri ni mwiko kuwa tegemezii