D'hicious.....a Year on!



Shukurani za dhati kwako wewe msomaji kwa ushirikiano wako, Rafiki zangu wote walioiweka D'hicious kwenye site zao kwa moyo mkunjufu na wenye furaha nasema Mungu awabariki sana kwa kuthamini mchango wangu ktk jamii ya Kitanzania "mtandaoni".

Katika safari hii ya miezi 12 nimekumbana na vishawishi vingi as you can imagine, nimekutana na kutengeneza mafariki wengi kutoka sehemu mbali mbali za Dunia, nimejifunza mengi kutoka kwa watu wengine na hata kukabiliana na "bullies".

Nisingekuwa nakiburi cha kuvuka miezi 12 na kusema nilichokisema leo hii bila ya Rafiki yangu mpenzi na wa Siku nyingi, Geeque aambae mimi huwa napenda kumuita "Jiikyuu" au GQ ambae siku zote usiku na mchana alikuwa pale kwa ajili yangu, huyu bwana ni kimbilio, nguzo na shujaa ktk maisha yangu "mtandaoni" ambayo time to time nilikuwa napata wakati mgumu kutokana na vitisho, abuse na vishawishi.

GQ unaja kabisa kuwa bila wewe D'hicious ingekuwa hadithi.......Asante kwa yote na Mungu akubariki sana.


Comments

Simon Kitururu said…
Hongera sana Di!Moto huo huo dada
Anonymous said…
Hongera sana kwa kutimiza mwaka mmoja.
Anonymous said…
Hongera Dinah na kila lililo jema, nakumbuka mwanzoni kabisa ulinisaidia sana na tangu siku hiyo kila siku lazima nije kusoma mambo humu. Ubarikiwe.
Anonymous said…
Haya mama ongeza bidii kwani akina mama wanahitaji sana mchango wako.
Anonymous said…
hongera dinah, je unaweza kutuambia umepata mafanio au faida gani tangu umeanza kuweka mambo wazi hapa?
Anonymous said…
Hongera kwa kuadhimisha mwaka. Ile topic yako ya kujiswafi uke ndio iliyonileta hapa baada ya kuitafuta kwenye google na tangu siku ile siku haipiti bila kupitia hapa na sasa najua kujisafisha na chupi zangu zimekuwa kavu pia nimejifunza mambomengi kupitia kwa wachangiaji. Katika blog nyingi ninazopita nafikiri yako ikomakini na ya kujifunza zaidi kuliko kuburudisha au kujuana. Enedeza kazi nzuri.
Anonymous said…
Naipa pongez Blog yetu kwa kufikia mwaka huku ikiendelea kutoa somo zuri kwa jamii..ni hatua kubwa sana.
Happy Birthday d'hicious .
Anonymous said…
happy birthday dinahicious
hii blog imesaidia wengi sana,Mungu akubariki sana dina naamini imeokoa ndoa za watu hapa.
Anonymous said…
Dada Dinnah, Kwanza hongera kwa kutimiza umri huo unaoutimiza. Naheshimu sana kazi yako hii kwani ni ya msaada mno katika jamii.Pili mimi nina tatizo kidogo nahitaji kusikia ushauri wako na wa wasomaji wote wa ukumbi huu mzuri. Nina ndoa yangu kwa miaka sita sasa tuna mtoto mmoja na tunategemea mwingine Mungu akijaalia mwaka huu. Baada ya uja uzito wa kwanza tumbo la mke wangu halikurudi katika hali ya mwanzo, yaani alikuwa na kitumbo kinamna fulani. Lilipungua lakini si katika hali ya mwanzo au tuseme ya kawaida.Tumejaribu kutafuta tight ya tumbo lakini haikusaidia, ingawa labda haikuwa nzuri sana. Sasa tukafikiri na kuona labda kabla hajajifungua safari hii tujaribu kupata utaalamu wa jinsi gani tunaweza kupunguza na ikiwezekana kurudisha tumbo lake katika hali ya kawaida, maana hata yeye mwenyewe inamnyima raha kiaina. Sasa ni njia gani nzuri za kutumia zisizokuwa na madhara kwa afya? Nitafurahi mno kusikia ushauri na kama tutafanikiwa katika hili.
Anonymous said…
Hongera mupenzi... tunakuombe uendelee kuwepo kadri Mungu atakavyokuwezesha. Happy birthday dinahi..
Anonymous said…
Hongera sana dada Dinah.. Mungu akujaalie hakima zaidi ili nasi tuelimike zaidi kupitia kwako..ukweli ni kwamba watu wengi tunajifunza mengi hapa japo mara nyingi hatuchangii mada kama mimi ambayae leo ndio mara ya 1.tangu niambiwe kuhusu hii blog na my friend haipiti siku bila kuja huku ndani..keep pit up!Dear.lily.A
Anonymous said…
Hongera Dinah: tunakupa ahsante sana kwa mafunzo yako unayotufahamisha. tumejifunza mengi na faida tumeipata. Mungu akupe kila uzo idumu hii blog yako.
Anonymous said…
Kwakweli na udhati wa kutoka moyoni nakupongeza sana Dina kwa kunipa mafunzo ambayo kwa miaka yangu 34 nilikuwa sijawahi kuyapata. Hongera sana kwa kutimiza mwaka mmoja na Mungu akuongezee mika mingine mia moja ya kutuhabarisha.
Ama kweli siku hazigandi.
Kip it ap
crzyk said…
Nimejifunza vitu vingi sana kupitia blog yako na kila siku lazima nikusome,Mungu akubariki sana kwa kutimiza mwaka wa blog hii na aendelee kukupa uzima na afya njema..
Anonymous said…
Hongera sana dada umesaidia wengi kuwa huru na swala zima la ngono na kujiamini na mimi ni mmoja wao.
Anonymous said…
Hongera sana kwa kufikisha mwaka mmoja
Anonymous said…
siku njema ya kuzaliwa wa d'hicoius, wewe ni moja kati ya wanawake wachache sana ambao sio wachoyo kuchangia wayajuayo na wanawake wengine.Hongera sana.
Anonymous said…
Ulipoanza nilikuwa nakushangaa na kukuona unakiuka maadili na nilikuwa mmoja kati ya wale waliokuwa wakijaribu kukutatisha tamaa lakini baadae nikaja kugundua kuwa mimi ndio nilikuwa wa kushangaliwa kwani mengi nilikuwa siyajui na sasa nayajua Ubarikike dada.
Anonymous said…
Mungu akuzidishie Dinah kazi nzuri.
Anonymous said…
Kwa kweli unahitaji pongezi kwa kujitolea muda wako na kushea yale unayoyajua, uelewa wako mkubwa unaoweza kusikiliza na kuelewa matatizo ya watu na kuwapa ushauri au mawazo yako ambayo yanawafanya waweze kutatua kinachowasibu.Hongera sana na endelea kutuletea mambo.
Anonymous said…
Uko juu Dinah all the best
Anonymous said…
Hongera dia thats what i call "women power" na huwezi kuipata if hauna correct information lzm nikubaliane na wengine hapa nimejifunza mengi kutoka hapa pamoja na ushauri mwingi nimepata hapa pia
ubarikiwe zaidi na zaidi
dinahicious idumu
Anonymous said…
Hongera sana Dinah kwa kufikisha mwaka mmoja na Blog hii tamu sana ya Dinahicious. Umeanzia mbali na hapa ulipofikia ni hatua nzuri sana. Umekumbana na mengi katika kuendesha hii blog lakini kutokana na ushupavu wako uliweza kuhimili misukosuko yote na kuweza kuiboresha hii Blog na kufikia hapa ilipo.

Nawe nakushukuru sana kwa michango yako mbalimbali kwangu binafsi, kwa Bongo Radio na EastAfricanTube. Umefunua macho watu wengi kutokana na mafundisho yako ambayo umekuwa ukiyatoa kwa ufanisi mkubwa. Hongera Sana.
Anonymous said…
Dah nimechelewa na pati imekwisha. Hongera dada Dinah blog hii ni muhimu sana.
Anonymous said…
Dah nimechelewa na pati imekwisha. Hongera dada Dinah blog hii ni muhimu sana.
hureeeeee party hii cake inaliwa wapi??? anyway naomba nichukue fursa hii kukupongeza saana dinah kwa kutupa masuala nyeti ya malavidavi kama ninavyopenda kuiita kwani ni nyeti saana na mengi tumejifunza kupitia huku....naomba nikutakie mika 100 zaidii mpenzi
Anonymous said…
Happy birthday Dinahicious Blog,hongera mpendwa kwa kutimiza mwaka, tunashukuru sana kwa mambo yote unayotuelimisha, yaani mmhu! we acha tuu tangu nimeanza kusoma hii blog mambo yangu ni safi sana
ubarikiwe mpendwa.
Anonymous said…
Mambo yako matamu Dadaaa endelea kutujaza mambo ambayo wanawake wengine wanatunyima wanaona tunafaidi, hawajui kuwa sio wote waliobahatika kuwa karibu na bibi zao ambao walikuwa makungwi. Hongera kwa kufikisha mwaka moja japokuwa nimechelewa mamaaa naona ulienjoy sana.
Anonymous said…
Oh, dada Dinah, nilikumiss sana, nilikuwa nikikukumbuka hata pale nilipokuwa kitandani nikigugumia kwa maumivu ya operesheni.
Hongerana sana kwa kutimiza mwaka!
emu-three
FunkHouse! said…
Message yako imenifanya nitokwe na chozi. Safi sana Dinah & keep it up!