Mpenzi anaporudi "the old fashion"

Unakumbuka nilikupa maelezo ya mwanamke wa zamani alikuwa akifanya nini pale mpenzi/mume wanapokwenda safari? Nia na madhumuni ilikuwa ni kukupa nafasi wewe kuelewa nini kilikuwa kikitokea wakati ule alafu chukua moja au mbili (jifunze) kisha changanya na yale uyajuayo sasa (ya kisasa). Sasa leo hapa namalizia sehemu ya pili ambayo ni kitu gali kilikuwa kikifanyika mpenzi anaporejea kutoka safari ya mbali.



Kitu cha kwanza kilichokuwa kikifanyika ama kufanywa na mwanamke anapomuona mume wake kwa mara ya kwazna tangu walivyotengana (kwenda safari) ni kumsoma kwa macho yuko katika hali gani.....afauraha, ucchovu, hasira, mgonjwa, kukata tamaa n.k. alafu ndio anamlaki mumewe huyo kwa kutegemeana na hali aliyonayo mpenzi wake.



Kumbuka kuwa wakatihuo hakukuwa na mawasiliano kama sasa kwamba unajua kama sio kusikia kitu gani kinaendelea kabla hata hujamuona mtu hivyo unakuwa umejiandaa na jinsi ya kumpoke si ndio?



Sasa kwa mfano mume hana furaha au mchovu au amekata tamaa mwanamke alikuwa akimlaki kwa furaha lakini sio ile kumkimbilia na kutaka abebwe (jitu lina hasira/huzuni linaweza kukumwaga kwenye majani/chini)....baada ya hapo mume alikuwa akichukuliwa moja kwa moja bafuni/kwenye jiwe/kigoda/stuli kusafishwa kisha anafunikwa na blanketi, shuka au khanga (kaniki) alafu anakandwa sehemu ya pembeni ya kichwa chake kwa kutumia kitambaa kilicholowanishwa kwa maji joto ili kumpunguzia msongamano wa mambo/usumbufu alionao kichwani yaani kumfanya a-relax.



Baada ya hapo kilikuwa kikichukuliwa chungu kikubwa au karai leye maji ya joto yaliyochanganywa na mafuta ya karanga alafu unatumbukiza miguu yake humo na kuanza kuikanda nakuikausha mara tu unapomaliza shughuli ya ukandaji.

Mume anaongozwa chumbani kisha alawa kitandani ili apumzike wakati mwanamke unaenda kuandaa chakula (zamani chakula kilikuwa kikipikwa ukiwa nyumbani na sio kabla kwani hakukuwa na vitunza joto/moto) na wakati unaandaa chakula hicho basi unaweza ukawa unaimba nyimbo mbali mbali zinazoelezea unavyojisikia au kilivyokuwa ukijisikia kutokana na upweke au kuonyesha jinsi gani unampenda mumeo.

Pole kwa kukusolemba, tuendelee kama ifuatavyo!

Chakula kikiwa tayari mwanamke humfuata mumewe na kumkaribisha, kwa kuanzia anaweza mlisha tonge mbili-tatu kabla hajakaa na kuanza kula nae. Wakati wanakula ndio wakati wa kuanza kuongea na kuuliza maswali ya huko alikotoka, safari ilivyokuwa na jinsi ulivyotaabika na upweke bila kusaha furaha yako iliyoje kuwa nae tena.

Ulikuwa ukidhaniwa kuwa huu ni muda muafaka kwa vile tayari ameonyesha anamjali, umempunguzia stress na kumfanya awe-relaxed zaidi hivyo atasikiliza na kuelewa kile unachomwambia tofauti na kama angeanza kuwakilisha hoja na malalamiko (ya mama mkwe mfano hahahaha) mara tuu baada ya kumuona.

Pia ulikuwa ni wakati mzuri kuliko kusubiri mpaka mko kitandani, kwani ni wazi kuwa ktk ile nyanja kusikiliza na kumuelewa mwenzio huwa sio rahisi kutokana na wingi wa nyege as you can imagine mtu ndio kajitokea safari lazima mambo fulani yawe mambo.

Sasa baada ya mlo kumalizika ndio unafuata ule wakati wa kujimwaga ktk kufanya mapenzi na kuonyesha ufundi na manjonjo yako uliouongeza wakati yeye hayupo.

Ikiwa narejea akiwa mwenye furaha kabisa yaani yuko kawaida mwanamke alikuwa hajitumi sana kama ambavyo nimeeleza hapo juu.

Comments

Anonymous said…
dada Dina naomba nitoke nje ya maada yaan mimi ni msichana wa miaka 25 nimeanza mapenzi hvi karibuni tatizo langu ni kwamba yaan nimejaribu kutumia condom lakini maumivu ninayosikia ni ya hali ya juu sana. pia hata sijisikii raha yoyote nimejaribu njia zote ili nisikie raha lakini wapi. nifanyeje?? nahitaji msaada wako dada yangu.
Bye.
Anonymous said…
Dada Dina unaojiandaa kuja kumalizia mada hii, nomba pia uwe unatuweka sawa. Je, mwanake akisafiri walikuwa wanafanyaje? Huduma hizi naye alikuwa anazipata? Unawashauri nini wababa leo ambao wake zao wanasafiri sana. Maana dada Dina, wanaume tulio nao leo, wengi ukirudi anataka suna kwanza, ndio akae chini kukusikiliza. Yaani somo halipandi bila kupata kwanza. Nadhani hii iko kwa wengi wetu.
Hebu tusaidie, maana akina mama tunatamani sana huduma kama hii pia. Ni binadamu ati!
Tunakungoja dada Dina.
KKMie said…
Anony @5:17:00 PM,ungenisaidia kukujibu kwa ufasaa kama ungesema hizo nji zote ulizojaribu na hukufanikiwa kusikia/pata raha ya kufanya mapenzi/ngono.

Nitakuji kama ifuatavyo kwa kuanzia wakati nasubiri maelezo ya "njia zote ulizojaribu".

Nafikiri hii inaweza kusababishwa na kuchelewa kwako kidogo kuanza "mambo fulani" na itakuchukua muda mpaka kuja kuzoea mchezo swala muhimu ni kuhakikisha kuwa unafanya mapenzi mara kwa mara (tumia condom) na hakikisha mpenzi wako anakufanya taratibu na kwa mapenzi.

Achukue muda mrefu kukuandaa na wewe mwenyewe jaribu ku-relax badala ya kuhofia maumivu, maambukizo, kubambwa/fumwa (kama unaibia au mnafanyia ktk mazingira ya chuo, chumba cha rafiki au nyumbani kwa wazazi)n.k.

Asante kwa ushirikiano wako.
Anonymous said…
Jamani kulikuwa na raha yake, ingawaje wenzetu wanasema ni `mfumo dume kwa maneno kama `kwanini wanawake wao walikuwa hawafanyiwi hivyo...'.Inaweza ikawa hivyo, lakini hayo yalikuwa ni `mapenzi yao' , na kujaliana kwingi kulikuwepo. Nakumbuka wake walikuwa hawaendi vitani...
Wewe kwa hivi sasa umesoma, umeendelea, una uwezo wako, hata wa kum-miliki mume,unaweza ukaenda hata vitani, au sio? Lakini hapo awali mke ni mke na wengi walikuwa wake wa nyumbani. Walilelewa na adabu zao.
Leo hii wote mpo kazini, ingawaje kipato kikipatikana, cha mke hakionekani! `si umenioa wewe bwana, toa hela ya matumizi...'ukigeuka upande mwingine, `kwanini hivi wewe hufanyi'
Anyway tuyaache hayo!
Katika mchango wangu wa leo, ni kiushauri tu kidogo. Kwamba tusipende `kulinganisha kila kitu' kwamba ili tuwe na usawa basi kila kitu mume/mke akifanye. Hatutafika!
Vipo vitu vya kuchangia, lakini vipo vitu ambavyo vitabaki kuwa vya kiume/kike. Huu ni utaratibu mwema ambao tukianza kusema `kwanini' tutakuwa hatufiki...
Nisingependa kuingia ndani sana na kusema hili au lile linatakiwa liwe la upande wa kike/kiume, ila wenyewe wale wenye busara zao, ndani ya nyumba watajua hiki a kile akifanye nani, au mtapanga,ingawaje vingine vipo tu na vinajulikana. Haya ni mapenzi yetu ya asili yana raha yake, ni kiasi kidogo tu cha kuyaboresha, ili yanoge zaidi, ila isiwe ni kwa `msuguano'.
Zipo nyumba nyingi au wapenzi wengi sasa hivi hawaivani, kisa `usawa'. Jamani sehemu ambayo inatakiwa `usawa bi sawa' ni kwenye kung'onoana tu. Hapa kila mtu anatakiwa achangie, lakini ule utaratibu wa kimaisha ulivyo unajigawa wenyewe. Hiki anafanya mke, hichi anafanya mume. Au nimekosea wajameni?
Ni vyema mhurumiane, mjaliane ndipo upendo wa dhati utakuwepo.
Mimi yangu ni hayo tu kwa leo

emu-three
KKMie said…
Anony @ 6:20:00 PM, wakati ule bibi yangu alipokuwa ameolewa au walipokuwa wakiolewa mwanamke alikuwa hafanyi kazi wala kusafiri peke yake.

Kutokana na nyakati tulizo nazo nadani mambo ni tofauti sana kwani jinsi zote mbili (mume na mke) tunashughuli zetu zinazotufanya wakati mwingine tusafiri na kukaa huko mbali hata miaka 3 na tunachokitegemea kutoka kwa wenza wetu ni zawadi na "atanikoma" akirudi ngono wise.

Nawashauri wanaume wa nyakati hizi ambao wanawake wao wanasafiri kuliko wako kuwa waelevu zaidi na kuangangali hali aliyonayo mwanamke akitoka safari kuliko kukimbilia ngono kwa vile hujafanya siku nyingi.

Ofoz una haki kabisa ya kufanya hivyo aukutaka kufanya hivyo lakini jaribu basi kumuandaa mwanamke huyu ili awe ktk hali ya ku-relax kutokana na misongamano ya mawazo na uwingi wa kazi huko atokako kwani si wakati wote unarudi nyumbani ukiwa self normal.

Kama umeishi nchi za magharibi wewe na mume wako utagundua kuwa wanaume zetu huwa wanajitahidi na kubadilika kiasi nakukupa huduma ambazo zamani zilidhaniwa kuwa ni wao tu (wanaume) ndio wanastahili. Hii ni kutokana na hali halisi ya maisha huko (sio kuiga) bali ktk kusaidiana kwani wakati mwingine mke unatumia masaa mengi kazini kuliko mwanaume ambae ni mume/mpenzi wako.

Lakini kwa tulio ndani ya mbongoa mabo ndio wengi hali ni tofauti kwani wanaume wanataka kufanyiwa kile kilichofanyika miaka hiyoo (ya akina bibi) na hawajali kama sio hawajui kuwa nyakati zimebadilika sana.

Nafikiri elimu zaidi kuhusu hili inahitajika na je ni nani basi ananafasi yakufanya hivyo? Ni mimi na wewe....tuweke wazi hili swala bila kuwa feminist na hakika tutafika.

Asante sana kwa suhirikiano wako.
Anonymous said…
Ninashukuru sana kwa jibu lako lililoenda shule. Bravo Dina, nakuaminia, hakuna kinachokupiga mweleka.
Safi sana.
Anonymous said…
Asante sana dada yangu nilivyokuwa nasema kila namna nilikuwa naamanisha style zote nimejaribu lakini wapi ila mwenzangu anakojoa hata mara saba kwa siku .nampenda sana mpenzi wangu ila naogopa kwa sababu na yeye pia anawasiwasi kwa sababu anashindwa kunifikisha.
KKMie said…
Anony @ 9:05:00 AM, style zote? Hahaha mitindo iko mingisana kuliko mikao ambayo ile common iko kama mia moja na tatu hivi na kila mkao unaweza ukawa na mtindo(stlye) tatu au nne tofauti mfano mdogo ni kifo cha mende kima mitindo kama mitano hivi na doggy ina mitindo kama sita hivi hivyo sidhani kama umemaliza yote any way that is not the ace hapa.

Jaribu kusoma Makala zangu zilizopita hapo upande wa kulia kwenye ukuraha huu kisha chukua muda na kufanyia kazi yale unayodhani ni mapya kwako, hilo moja.

Pili jaribu kumuomba mapenzi wako akufikishe kileleni kwa kutumia ulimi au uume wake kusugua kisimi wakati mwili wako unaendelea kuzoea swala zima la kungonoana na jinsi mnavyofanya mara kwa mara ndivyo utakavyokuwa ukiujua mwili wako na kujifunza kufurahia tendo.

Natumaini utapata maelezo ya kutosha kutoka Makala zangu za awali na pia utachukua muda wako kufanyia kazi/kujaribu.

Kila la kheri.
Anonymous said…
Dinah naomba ufikishe salamu zangu kwa 'emu three' amenikuna sana apo juu!

Papaa