Human Papilloma Virus (HPV) ni maambukizo yanayotokea sana wanawake na huambukizwa kwa kufanya ngono, unapata maambukizo haya hata ukitumia kinga (Condom). Baadhi ya maambukizo haya huweza kusababisha Saratani iitwayo "Cervical" au Saratani ya Kizazi ambayo inaweza kusababisha usiweze kushika mimba/zaa ktk maisha yako yote au maambukizo mengine huko ukeni ambayo sio yale ya Ngono tunayoyajua nakutajia kila siku.
Hakuna dalili zozote za Saratani hii ya kizazi lakini ukiwahi kujua kuwa unayo kwa kufanya kipimo kiitwacho "Smear" basi unakuwa umeokoa maisha yako kwani Saratani hii inaua wanawake sambamba na ile ya Matiti.
Mwanamke anaeanza ngono mapema (chini ya miaka 21) anakuwa kwenye hatari kubwa ya kupata Saratani hii na wale wanaoanza Ngono ndani ya miaka 20 huwa x2 kwenye hatari ya kupata Saratani hii.
Huu ndio ukweli wa Ijumaa ya leo kwa maelezo zaidi Muone Dk bingwa wa magonjwa ya kike, Madaktari hawa wanapatikana kila Hospitali kuwa Nchini.
Mwisho mzuri wa wiki.
Hakuna dalili zozote za Saratani hii ya kizazi lakini ukiwahi kujua kuwa unayo kwa kufanya kipimo kiitwacho "Smear" basi unakuwa umeokoa maisha yako kwani Saratani hii inaua wanawake sambamba na ile ya Matiti.
Mwanamke anaeanza ngono mapema (chini ya miaka 21) anakuwa kwenye hatari kubwa ya kupata Saratani hii na wale wanaoanza Ngono ndani ya miaka 20 huwa x2 kwenye hatari ya kupata Saratani hii.
Huu ndio ukweli wa Ijumaa ya leo kwa maelezo zaidi Muone Dk bingwa wa magonjwa ya kike, Madaktari hawa wanapatikana kila Hospitali kuwa Nchini.
Mwisho mzuri wa wiki.
Comments
1 comments
Nimetoka pale mawazoni kwa Simon Kitururu, basi nkawa napitia pitia viunganishi vyake mkono wa kushoto mwa blogu yake. Kiunganishi kimoja wapo kimenileta hapa.
Unafanya kazi nzuri, inayostahili pongezi. Ningeweza kuwa na sababu nyingi, lakini niiseme moja.
Tunahitaji kuwa na ladha tofauti tofauti tunapopita pita katika blogu za Kiswahili. Baada ya kusoma siasa sana tangu vuguvugu hili la blogu lilipoingia miaka ya 2004/2005, nadhani upepo unaelekea kukaa sawa. Kwamba sasa tunapata karibu kila aina ya maarifa yaliyo katika lugha yetu adhimu ya Kiswahili.
Sikuwahi kuona blogu iliyojikita katika ngono na viambata vyake, yenye kuandika masuala hayo kwa lugha ya “kawaida” kama blogu yako. Kwa hiyo kwangu mimi hii ni hatua muhimu katika ulimwengu wa kublogu nchini kwetu.
Vilevile, watu wengi wanajidai kuwa hawapendi kusikia wala kujadili habari za ngono hadharani. Lakini tunajua kwamba wanafanya hiyo kwa siri. Na wanapenda ngono kuliko habari nyinginezo. Na wanapofuatilia na jadili masuala hayo hawapendi hata wajulikane kwa majina yao. Ndio maana blogu kama hii naamini ina mashabiki wengi. Sababu ni kwamba watu wengi wanapenda kufuatilia masuala nyeti wasiyoyasikia yakijadilika hadharani.
Ni hivyo kwa sababu kila binadamu ana hisia za ngono tangu anapozaliwa.
Hivi unadhani ni kwanini watoto wachanga (kati ya siku moja na miaka miwili) wanapenda sana kunyonya kila wanachokiona? Jibu ni kwamba japo hawawezi kusema, watoto hawa wanaponyonya vidole ama chochote wanapata hisia kama za mtu mzima anapofanya mapenzi! …maajabu eeh?
Akikua kua, inasemekana mtoto anaanza kujisikia raha ya mapenzi anapokwenda haja kubwa! Haya si mambo ya kizushi, yamefanyiwa utafiti rasmi. Wakati mtoto anajisaidia anapata raha kuliko kitu kingine chochote.
Ninachotaka kusema ni kwamba ngono inatawala maisha ya binadamu tangu anapozaliwa. Hivyo ili tuweze kudhibiti hisia hizi, na hata kuzitumia ipasavyo tunapaswa kuijadili ngono bila wasiwasi wowote kama anavyofanya Dinah.
Samahani kwa andiko refu.
Kila la heri.
Mimi nimeshituka kidogo, kwani nilitegemea watu wengi wengekuwa na maswali kwa Dada Dinah. Mimi nina tatizwa kidogo, kuhusiana na mada hii.
Kama `gonjwa' hili au tatizo hili halizuiliki hata ukitumia kinga, ina maana linaingiaje? Kwa hewa, kwa kujamiiana, au....
Nilipitia mtandao fulani nikaona kuwa `uambukizaji wake' unaweza ukakupata hata kwa kugusana ngozi kwa ngozi, vyombo vya kulia, mataulo, na hata sakafu kama muathirika amepitia hapo na kuacha `virusi'.Mambo hayoo...
Sasa jaribu kukusia kama wenye matatizo hayo ni wengi, mbona wengi watakuwa na matatizo hayo! Tumuombe Mungu atunusuru!
Sijui dada Dinah unasemaje?
mimi
emu-three
Ugonjwa huu ni mmoja kati ya yale ya ngono (hayaambukizi kama kipindu-pindu au amagonjwa mengine)lakini hili haliwapati wanaume ni wanawake tu japokuwa kufanya ngono (na mwanaume) ndio kuna "triger" hasa kama binti ni mdogo.
Ni kweli kabisa kila mwanamke anaweza kabisa kuwa nalo lakini hajui na njia pekee ya kujua ni kwenda kwenye kitengo cha Kansa au Hospitali yeyote amabako kuna madaktari bingwa wa magonjwa ya wanawake nakuomba kufanyiwa "smear test".
Hili ni gonjwa la wanawake na linasababishwa na wadudu ambao wanaishi mwilini mwetu, kama zilivyo Saratani nyingine hakuna kuambukizwa bali ni mkanganyiko wa homono na chembe (cells) mwilini mwako.
Usininukuu kwa haya yafuatayo (ahhahaha) ila mimi binafsi nalihusisha na matumizi ya madawa ya kuzuia mimba ambayo mabinti huanza kuyatumia wakiwa wadogo 13-20yrs.
From A-town