Ni usawa au Kiburi?

"After thousands of years of male dominance, we now stand at the beginning of the feminine era, when women will rise to their appropriate prominence, and the entire world will recognize the harmony between man and woman". The Rebbe.

Unakumbuka ule Mkutano wa wanawake kule Beijing au unatambua kwanini wanawake wanaitwa "wabeijing"?

Swala la usawa baina yetu wanawake na wanaume lilizua au linaendela kuzua utata kutokanana baadhi ya wanawake ku-abuse maana halisi au nia na madhumuni ya Usawa huo......na matokeo yake wanawake wamekuwa kama wanaume, wamejawa na viburi mbele za wapenzi/waume wao n.k. hii ni kutokanana kutoelewa kwanini hasa wamama wale walikusanyanakule "Beijingi" kudai Usawa.

Ukweli ni kwamba hakuna mwanaume anataka kuwa au kuoa "mwanaume mwenzie" kwa maana kwamba unatakiwa kubaki mwanamke no matter how much you earn, no matter how educated you are, no matter how tall you are.....having said that sina maana kuwa ndio uwe kila kitu "sawa/ndio bwana/mume wangu" type.


Usawa tunaotakiwa kuutolea mcho ni ule wa kujitahidi ktk elimu, ufanyaji wa kazi kwa bidii (kupata cheo kutokanana uwezo wako sio kwa jinsia yako), kuchangia maendeleo ya familia zetu namaisha yetu kwa ujumla, kuongoza aukushika nyazifa mbali-mbali ambazo awali zilidhaniwa kuwa ni za kiume tu n.k.


Sio kuwa mlevi kwa vile wanaume wanalewa, kuwa na wapenzi wengi wengi kwa vile baadhi ya wanaume wanafanya hivyo, kutongoza kama wanavyotongoza wanaume kwa vile tu "tuko sawa", kula kiasi kikubwa cha chakula kwa vile tu wanaume wanakula kuliko sisi (hushangai kwanini wanaume wanakula sana lakini hawana pot bellies eti?) na mambo mengine mengi ambayo wanaume wanayafanya kwa sababu zao binafsi kwa vile ni wanaume au kulinda ego zao.

Ukikutana na mwanaume ambae anapenda au vutiwa na "kiburi chako" ukidhani ndio usawa ujue huyo ni Player.

Ndio "fact" ya leo......unamchango? swali je?

Mwisho mzuri wa wiki.

Comments

jameskchurch said…
Kwa jumla nafikiri nimekuelewa vizuri tu. Uliposema kwamba inatakiwa mwanamke atafute au afuate uwezo wake mpaka mwishoni kwa ajili ya hiyo tu na siyo kwa ajili ya kitu kingine... sijui nini... kama Usawa mwenyewe. Nimekubali. Au siyo?

Lakini. Unajua kwamba siyo rahisi kuyabadilisha maoni ya jamii. Tuangalie mfano labda. Tuseme tunaye mwanamke mwenye akili. Amemaliza shuleni. Amepata kazi nzuri ya uwezo wake, lakini, amegundua kwamba wanaume wenzake wanafanya kazi ileile, lakini wanachuma hela nyingi zaidi kuliko za kwake. Maana yake nini?

Tatizo hili lipo hapa marekani pia na wanawake wanapiga vita vibaya kupata usawa wao. Pia, tatizo hili ni sawa na tatizo la ubaguzi. Waamerika weusi (jinsia zote mbili) wanafanya kama ulivyosema. Wanafuata uwezo wao lakini, wanashindwa kuchuma pesa kama wazungu. Inatakiwa vita iwepo. Uangalie historia. Bila vita, hakuna mageuzi.

Mimi mwenyewe natafuta mwanamke ambaye anavyo vita moyoni na akili sawa na yangu. Bila hivyo, na pata udoro kwa rahisi sana. Bila maongezi mazuuuuuuuri, kuna mapenzi tu. Na mapenzi ni mazuri! Sisemi siyo! Nasema mambo mengine yapo tu. Mara kwa mara inaonyesha kwamba labda mimi ni "player" kwa sababu nakuwa na wanawake kwa muda mfupi halafu na waacha... lakini natafuta mwanamke ambaye ataweza kunifaa kama ninavyomfaa yeye.
Anonymous said…
Dinah kama ulivosema 'mtihani' upo katika kukubali kuwa unawea kuwa na mafanikio sawa na mwanaume na bado ukaendelea kuwa mwanamke

Bahati mbaya mfumowetu, hadi leo unamwonyesha mwanamke kama kiumbe dhaifu, asiye na uwezo sawa na mwanaume kiakili, kiuchumi, etc, kitu ambacho si kweli, na
bahati mbaya zaidi baadhi ya wanawake wamechukulia hii hali kama kulipiza kisasi kwa waume zao pale wanapokuwa wamepata nafasi zaidi iwe kiuchumi , kijamii au kielimu, kitu ambacho sio sahihi!
Kuna ubaya gani kwa Profesa mwanamke kujikubali kuwa ni mwanamke mbele ya mume wake ambaye hana sifa kama za kwake?
Anonymous said…
Wewe mama unaonambali sana mimi nilidhani wewe ni mtu wa kufunda watu mambo ya kitandani tu kumbe kila kitu uko imara. Nakunyooshea mikono kwa kuwaelimisha wenzio.
Anonymous said…
Mimi naamini kuwa tafiti nyingi ambazo nimesoma zinaonyesha kuwa mwanamke ni tofauti kabisa na mwanamme katika vitu vingi sana kuanzia maumbile, mahitaji, akili (maana ubongo wa mwanamke umeumbwa tofauti na wa mwanamme), nk.

Na wengi waliosoma shule watakubaliana nami kuwa kuna baadhi ya masomo ya darasani ambayo wanawake wengi (sisemi kuwa wote) hawayawezi na yanawasumbua sana wanawake na si kwa sababu eti hawana juhudi za kutosha ila ni kwa sababu ubongo wa mwanamke na jinsi unavyofanya kazi ni tofauti na ubongo wa mwanamme. Ningeweza kutoa takwimu nyingi tu katika hilo.

Cha msingi ninachokiona ni kwa pande zote mbili (yaani mwanamke na mwanamme) kukubali kuwa tofauti hizo zipo na inapofikia kwenye hatua ya kifamilia kila mtu ni lazima ampe nafasi mwenzie bila kujali una elimu ya kiasi gani, una uwezo wa kutengeneza pesa kiasi gani na una wadhifa gani.

Moses J.