Unatarajia nini unapoelekea kwenye uhusiano?





Kuna swala la wanawake kudhani kuwa "ndio imetoka hiyo" yaani ndio milele, mara tu anapoanzisha uhusiano na mwanaume……..

na kwa bahati mbaya wengi huishia “disappointment” na kuwaita wanaume wa kibongo hawana mapenzi ya kweli…….sio hawana mapenzi ya kweli bali wewe ndio ulikuwa na haraka au nyote wawili mlikuwa na haraka na hamjui nini maana halisi ya neno “mapenzi”.


Siku hizi vijana tunaharaka sana ya kufanya mambo ambayo hufanywa kwenye commitment relationships sasa sijui ni maendeleo au ni wanaume kutokuwa wazi pale wanapotaka kuwa na uhusiano fulani na mwanamke?


Napenda utambue kuwa kukutana na mwanaume/mwanamke na kuwa nae na kupena miili yenu haina maana huyo ni uhusiano tayari, uhusiano hujengeka baada ya kutoka na huyo mtu kwa muda fulani minimum miezi kama 3 hivi au zaidi……

Hata kama alikujia na gia ya “nataka uwe mpenzi wangu”…..huwezi ukawa mpenzi ktk siku chache……unahitaji muda kuwa na uhakika na hisia zako.


Unajua zamani watu walipokuwa wakikutana, walikuwa hawakimbilii kungonoana, walikuwa wanaheshimiana na kama ni kukutana basi inakuwa mahali peupe kuepusha vishawishi vya kungoana na hali hiyo iliwawezesha kuvuta muda na kuwa na uhakika na hisia zao kuwa kweli wanapendana.


Na ndio maana wakati huo walikuwa wakiamini (jua) kuwa mwanaume akikupenda kweli basi atavumilia na atakuja kuwaona wazazi na kufunga ndoa na wewe……ndio kungonoka kunafuata.


Tofauti na sasa ambapo tuna swala la ku-date ambapo penzi la huibuka....…kisha tunahamia kwenye Trial (move in together and all) na kuangalia mambo yanavyokwenda….je mnapatana? mnaendana ki-life style, kingono mko sawa n.k.


Alafu ndio penzi la dhati hujengeka vema zaidi kwa vile utakuwa unamjua mwenzio kwa undani na hivyo kufanya uamuzi wa busara kama unaweza kumvumilia na kushi nae maisha yako yote au la.


Natambua kuwa kuna watu wengi (hasa wanawake) wanaendeleza imani kuwa kama mwanaume anakupenda kweli basi atakwenda kujitambulisha kwa wazazi wako na atafunga ndoa na wewe……..


Kutokana na nyakati hizi za mwisho I MEAN SAYANSI YA TEKINOLOJIA a.ka maisha ya kisasa ni wazi kuwa hawajui tofauti ya kupendwa na uamuzi wa kuishi na wewe maisha yake yote na matokeo yake ni disappointment.

Zingatia haya.....
Napenda kukwambia kuwa unapoanza uhusiano na mwanaume chukulia mambo taratibu na usikimbilie kufanya ngono kwani kufanya hivyo automatically kutakufanya udhani kuwa tayari uko kwenye uhusiano,


*Angalia mambo ambayo uta-offer ikiwa utakuwa kwenye uhusiano na sio kutegemea afanye hivi au vile

*Weka 50-50 na sio asilimia mia moja kuwa uhusiano utakuwa kama unavyotaka kwani

*Usitegemee mambo makubwa yafanyike ndani ya uhusiano wako na badala yake acha yatokee yenyewe bila kulazimisha.

*Kuwa wazi na kuyazungumzia yale ambayo ungependa yafanyike ktk maisha yenu ya baadae lakini sio kwa kulazimisha au kununa ikiwa mwenzio anaonyesha kutovutiwa na mazungumzo hayo na badala yake wewe furahia kila siku kama inavyokujia……


* Kumbuka mapenzi ya kweli huchukua muda kujengeka na yakijengeka huwa hayabomoki……hata kama mtaamua kuachana baadae mahaba yataisha lakini penzi siku zote hubaki moyoni.

Nitaendelea……

Comments

Anonymous said…
Sawa kabisa Dinnah...
Anonymous said…
Nakubaliana na maelezo yako ila mimi naona tatizo la wanaume wa kibongo wengi huwa hawako wazi na waongo kusema wanakutaka uwe nao kivipi. Mfano kama unamtaka mtu kwa ajili ya kungonoana tu si umwambie ili kama hana mpango huo asiwe na wewe na kusubiri mtu atakae mtaka kama mpenzi wa kufanya kila kitu na sio ngono tu. Uongo wa wanaume ndio unafanya wanawake tudahini tunapendwa au ndio tumeisha pata wa kuishi nae milele.
Anonymous said…
dinah,i know i always comment on whatever u write.how do i even know if it right to start a relationship???especially wheni have a kid???im so so afraid of getting in bed with any men ,i ahve been single for 2yrs no any sort of relationship..im too lonely now and i feel like being with someone
what should i do???
KKMie said…
Anony wa 2:29am, kutokana na maelezo yako inaonyesha wazi kuwa uko tayari sasa kuanza/jaribu uhusiano kwa vile unahisi upweke na pia unahisi kuwa na mwenza.

Sio lazima ulale na mwanaume haraka mara tu baada ya kuanza kutoka nae......labda ungekuwa wazi kidogo....kitu gani kinakufanya uogope kulala na mwanaume (mpenzi), uwazi wako utanisaidia mimi kukujibu kiufasaha zaidi.

asante sana kwa ushirikiano wako.
Anonymous said…
dinah kinachonifanya niogope ni dissapointment,maybe i mit feel our relationship is based on sex,nikilala nae ninaongeza idadi tu ya wanaume?lot of thing sijui i cant explainit myself how i feel
Anonymous said…
wala haupo mwenyewe anony 2.22am, hata mimi nimeachana na mume wangu sasa ni miaka 2 na miezi kadhaa,(kwa sababu ya endless cheating, etc) lakini hata hamu ya wanaume sina, (not becoz of hurt, I am over that now)sometimes I feel labda I am not normal, sometimes I picture maybe to meet someone new lakini when I truly search my heart, I still feel I dont need anyone,I have observed when guys approach me for a relationship, I have a feeling that they r just a distruction, I am pursuing my career, have great friends, I hang out. Lakini hamu ya sex, its really gone, Iam 37.
Well, I cannot explain what is happening to me. But whatever it is, I am so much enjoying the peace and control of my life that comes with being alone.