Jinsi matiti yanavyokuwa ndio uzito wake huongezeka hivyo kama binti/mwanamke unahitaji kuyasaidia kwa kuvaa kitu ambacho kitayasaidia kubaki pale yanapopaswa kubaki......nina maana vaa sidiria.
Vest ivaliwe wakati ukifanya mazoezi au unaweza kujifunga khanga (nyepezi) chini ya matiti yako hali itakayosaidia matiti yasiume sana wakati unafanya unayasumbua(inategemeana na ukubwa wake).
Wakati nakuwa wanawake wengi walikuwa wakiamini kuwa kuvaa sidiria kunasababisha matiti kuanguka; sio kweli.
Kumbuka kutovaa sidiria wakati wa kulala kwani naweza kusababisha uvimbe (damu kujikusanya pamoja) ktk matiti yako na badala yake lala kifudifudi(lalia matiti yako a.k.a lalia tumbo)
Natumaini nyote mnalijua hili sio? kama mlikuwa hamjui sasa mnajua.
Nawatakia siku njema na karibuni tena nitakapomalizia swala zima la usafishaji na utunzajiwa matiti kwa wanawake waliondani ya mahusiano ya kimapenzi.
C ya!
Comments
Nafurahia sana blog yako.
Karibu kila upatapo wasaa online.