Utunzani wa matiti wakati wa hedhi na Ujauzito!


Natambua kuwa uvaaji wa sidiria wakati matiti yanakua, wakati wa hedi na wakati wa ujauzito ni karaha sana na unahisi kubanwa tu (kwavile yanauma kiaina) na hali hiyo hutufanya wengi kuachana nazo na kuachia matiti yakining'inia bila "support".


Kama nilivyosema awali kuwa matiti wakati wa hedhi huongezeka ili kuwa tayari kutengeneza chakula cha mtoto ambae kwa wakati huo yai lako linakuwa likisubiri kurutubishwa na mbegu ya kiume lakini hilo lisipotokea basi matokeo yake ni wewe kupata hedhi.


Si wanawake wote wanaopata maumivu/ongezeko la ukubwa wa matiti wakati wanakaribia hedhi na wakati wa hedhi, lakini ikiwa wewe ni mmoja kato ya wale ambao matiti huongezeka ukubwa unapokaribia na wakati wa hedhi basi hakikisha unafanya mazoezi kama niliyoeleza kule mwanzo na pia zingatia kuvaa sidiria wakati wote isipokuwa wakati wa kulala.


Vilevile kwa wamama wajawazito ni vema kuvaa sidiria ili kuyasaidia uzito wa matiti yako usiyavute kwenda chini hali itkayopelekea kuwa na matiti ya liyolala mara baada ya kujifungua.


Nikirudi nitamalizia najinsi ya kutunza matiti wakati wa unyonyeshaji pia wakati wa kufanya ngono (mfundishe mpenzi wako jinsi ya kuyachezea na kuyanyonya.....si

Comments

Anonymous said…
mi nasuburi apo kwenye kunyonya na kunyonywa..af ivi kwani umme ukinyonywa sana nao 'huanguka' Dinah?
KKMie said…
Uume siku zote umeanguka (ndivyo ulivyoumbwa) na huwa mgumu time-2-time ikiwa mwanaume anapata haja kubwa (kunya), akiamka asubuhi, akishituka, akisisimka kimapenzi/ngono, akishawishika, akitamani n.k.

Nikijibu swali lako; hapana uume ukinyonywa hauanguki.....hahahahaha umenichekesha wewe!
Anonymous said…
Wewe dinah inakuwaje unajua mambo mengi hivi? Kwani unaumri gani? Navutiwa sana na kazi yako yaani kama inawezekana ungefanya Semina na wanawake ili wajifunze moja kwa moja kutoka kwako.

Wanawake wengi wa Kitanzania naamini wanahitaji kufahamu haya mambo moja kwa moja kwani wengi hawana mazoea ya kutumia Computer au hawajui kabisa ila ukifanya semina nakuwatembelea wanawake huko waliko itawasaidia sana.

Ni mtazamo tu Shangazi.
Anonymous said…
Mimi nina swali kuhusu matiti, hivi mwanaume anapata raha gani kuyachezea au kuyanyonya matiti yetu?

Ni hilo tu Dinah.
Anonymous said…
haya kamalizie apo kwen topiki chap chap tujue moja....kumbe uume haunguki ukinyonywa...LOL afadhali
Anonymous said…
Dinah U rock woman!