Mazoezi ya Matiti yanayoanza kujitokeza!

Kama nilivyosema awali kuwa ikiwa wewe umechelewa(ulikuwa hujui hili wakati matiti yako yanaota) basi msaidie mdogo wako au binti yako anaekuwa hivi sasa, ili asije kujisikia vibaya pale wanaume watakapokuwa wakiponda/zungumzia matiti kwa kuyaita "malapa"...."flapy" n.k.


Kwanza kabisa hakikisha mtindo wa kulala ni kifudifudi (kulalia tumbo), kwa kufanya hivyo kunasaidia kwa kiasi kikuwa kufanya matiti yako yabaki/pumzike, kwamba hakuta kuwa na kuning'inia kama utakuwa umelala chali(lalia mgongo) au kiubavu.

Zoezi...1

Asimame wima dhidi ya mlango au ukuta kisha aegeshe matiti yake mahali hapo kwa nguvu kisha aachie (ajitoe ukutani), zoezi hili hufanya matiti yaume sana lakini wewe kama dada/mama mpe moyo kuwa avumilie. Afanye hivyo mara 20 kila asubuhi.


Zoezi....2

Simama wima huku mikono yako ikiwa imenyooshwa huku na kule kisha ipeleke mbele nakukutanisha viganja vyako alafu irudishe nyumba kadiri uwezavyo (sio lazima ikutane) ila utahisi maumivu fulani sehemu ya matiti (misuli yafanya kazi hapo)....fanya hivyo mara 10 na ongeza hesabu njinsi unavyokua.


Zoezi...3

Ukiwa umesimama wima na mikono yako imenyooshwa huku na hule inanyue taratibu kuelekea juu na kutanisha vidole vyako huko juu kisha rudisha mikono ilipokuwa (imenyooka huku na kule).


Baada ya hapo mimi nilikuwa nikienda kujiandaa tayari kwa kwenda shule nikiwa na hasira kibao kuwa nimeamshwa alfajiri.


Kila la kheri kwa hili...........sijamaliza hivyo usikose kutembelea tena.

ty.

Comments

Anonymous said…
hi dina mie huu wimbo wa Brenda naufananisha na wimbo fulani wa Jide,yaani sijawahi kuusikia kwa brenda,lol
Sasa haya mambo ya matiti ,mbona wanitia wivu du natamani ningekuwa kijana mdogo ningefanya hilo zoezi.mh manake huyu binti hapo kwenye picha acha tu saa sita kamili,her milk is standing wow teh teh teh kazi njema dia.
KKMie said…
Brenda aliuimba long time, kipindi kile alipokuja Bongo baada ya kupiga msamba kwenye KORA.

Si unajua tena mambo ya kukaa karibu na bibi wa miaka aliyezaliwa miaka ya mwanzoni mwa 1900.

Karibu tena.
Anonymous said…
Asalaam alleikum Dinah....ous!
mi nataka kujua yaani binti akifuata maelekezo hayo yote barabara basi 'malapa' hayatatokea tena hata akishakuwa mama watoto-yaani akijifungua na kunyonyesha?
Mimi Kibiriti Motto.
KKMie said…
Waalleikum Salaam Kibiriti...Ikiwa maelekezo hayo yatafuata vema binti anapokuwa na kisha kufuata melekezo mengine nitakayoyaelezea siku zijazo ambayo ni utunzaji wa matiti ktk umri mkubwa bilakusahau wakati wa ujauzito na wakati wa kunyonyesha basi hakika binti (kwa wakati huo atakuwa mama) matiti yake yatainama kidogo tu hali itakayomfanya ajiamini ktk kuyaonyesha matiti yake wakati wa kufanya mavituzi.

Kwa wale wenye matiti yaliyolala na hawajui jinsi ya kuyatumia ili kumpagawisha mupenzi muendelee kufuatailia makala zangu niwapange mbili-tatu sawa?

Karibuni sana.
Anonymous said…
Da Dinah ulikuwa wapi miaka yote ile wengine tulipokuwa tunakuwa? Yaani nasoma hapa nasikia uchungu kweli, matiti yangu yalilala kabla hata sijapata watoto.

Lakini nitahakikisha binti yangu hawi kama nilivyokuwa mimi lazima nimpe somo lako Dinah. Unatufungua macho kwa kweli yaani nashukuru kwa kuanzishwa kwa blog hii.

Keep it up!
KKMie said…
Anony hapo juu, Miaka yote hiyo nilikuwa mdogo....yaani nilikuwa nakuwa na uzoefu wala ujasili wa kuandika au kuzungumzia maswala ya ngono mpaka nilipokuwa na miaka 27.

Karibu sana tubadilishane uzoefu.