Ktk makala moja iliyopita nilielezea swala la kujiswafi ili kuondoa utoko nakupunguza harufu/shombo ya uke, vilevile nilisema kuwa kwa kufanya hivyo (kujisafisha huko chini) kunapunguza siku zako za hedhi ikiwa utaendelea kujiswafi wakati uko hedhini.
Sote tunatambua karaha ya hii kitu na baadhi hutunyima raha ikiwa wapenzi wetu hawezi kumudu kufanya ngono wakati uko huko mwezini japokuwa wewe unataka kuliko siku zote.
Sasa ni hivi; kuna uwezekano mkubwa kabisa kuwa siku zako ni kati ya 3-7 lakini wewe unakwenda siku 8-12 na huelewi kwanini wewe wakati wengine wanapiga siku tatu tu?
Unapokuwa hedhini damu huchirizika taratibu lakini si damu yote inayotoka nje ya uke na kujaa kwenye "Tampax" au "pads", sasa ili damu hiyo yote itoke yenyewe inamaana itakubidi uisubiri kutegemeana na uwingi wake.
Hivyo, ili kupukuza swala la kusubiri isaidie kwa kidole chako cha kati kuitoa huko iliko kama ambavyo nilielezea awali kwenye swala la kutoa utoko. Endelea kujiswafi mpaka uone maji yanachuruzika bila damu.....kwenye hedhi utahisi uterezi usihofu au kutafuta jitihada za kuumaliza, haumaliziki kwani wakati huo uke unakuwa laini ili kusaidia mabonge ya damu kupenya kwa urahisi (natambua sio wote lakini Mungu ndio alivyoumba hivyo).
Mara baada ya kujiswafi vaa kifaa chako kama kawaida na endelea na shughuli zako, kumbuka kujiswafi kila unapokwenda kuoga na hakika utajikuta unakwenda siku chache zaidi kuliko ilivyo awali.
Pssssss!Awali nilikuwa nakwenda siku sita (nilikuwa bikira so huruhusiwi kujisafisha) lakini tangu nilipoingia kwenye ulimwengu wa ulimwengu (mahusiano yakimapenzi) nikaanza kujiswafi napiga siku 3 tu na damu sio nyingi sana kama ilivyokuwa awali.....
Nakutamia siku njema na kila la kheri katika kupunguza siku zako za damu.
Ciao!
Comments
Napenda kazi yako kwani inaonyesha wewe sio mchoyo wa yale unayoyajua, nashukuru sana kwa somo la leo.
Kazi njema.
Hembu nifafanulie hapa maana wengine tunakinyaa saana na damu ya mwezi japo hatunajinsi yakuizuia.
Asante.
Nashukur sana kwa elimu yako kuhusu suala la kupunguza siku za hedhi, nimekupata na ntalifanyia kazi.
Asante dada.
Tunashukuru sana kwa darasa lako Dina.
Anony wa pili wa saa kumi na moj ana robo, damu ya hedhi hainuki vibaya inaharufu yake ya uanamke, lakini ikiachwa kwa muda wa masaa matatu ni kweli huvunda na kutoa harufu mbaya sana na kwa wale wanaobadilisha pads mara chache ndio balaa hasa.
Nakumbuka miaka ya 90 mwanzoni wakati niko shule ya Msingi (nilikuwa sijavunja ungo) wadada wakubwa walikuwa wakiambiana kuwa ukivunja ungo na kutosema unaoza.....sio kuoza bali unatoa harufu mbaya kwa vile unatwa huji jinsi ya kujiswafi na jinsi ya kubadilisha kipande chako ka Khanga au Pads au Tampax kwa wale waliondelea na wenye uwezo wa kununua bidaa hiyo.
Kufupisha hadithi ni kwamba, hedhi hainuki ikiwa unabadili kila baada ya masaa 2-3 (kutegemeana na uwingi wa utokaji), vilevile hakikisha unakoga mara mbili kwa siku (asubuhi na jioni)hivyo mkono/vidole vyako havitokuwa na harufu yoyote.
Kama ni bikira tafadhali usijaribu kujitia kidole wala kujiswafi kuondoa utoko au damu ya hedhi.
Nakutakia siku njema na mafanikio ktk kujaribu kupunguza siku zako za hedhi kwa kujiswafi vema.
karibu tena.
Nashukuru sana kwa ushirikiano wako na karibu tena!
Wengi mnaokwenda siku tano mpaka kumi namoja jaribuni na mtaona mabadiliko ya siku kupungua badala ya siku 5 zinaweza kuwa 3 na badala ya kumi namoja zinaweza kuwa 5.
Hii ni mbinu ya kiasili kabisa....kabla ya Biology haijaingia Tanganyika. Ni mbinu mabibi zetu walitumia.
Jiulize enzi hizo hakuna pads na kaniki/khanga walikuwa wakitumia nini kukabiliana na hedhi?
Shukurani kwa uchangiaji wako.
Mimi naomba uelezee swala la madawa ya kuzuia mimba faida na madhala yake na je tupe uzoefu wako wewe umewahi kutumia na kama umewahi ni aina gani ya vidonge unatumia?
Asante anti Dinah.
Mimi binafsi sijawahi kutumia madawa ya kuzuia mimba kwa zaidi ya Condoms kwa zile siku za hatari hii ni kwavile siku zangu za hedhi hazibadiliki-badiliki na vilevile sio wakati wote Mpenzi anamalizia ndani hivyo na-save mimba hapo ei? hahahha.
Kwanini basi sijawahi na sina mpangowa kutumia madawa hayo?
1-Inasemekana yanachangia kwa kiasi kukubwa kupata Saratani ya matiti au kizazi.
2-Inasemekana yanapunguza "libido" yaani haku ya kungonoana.
3-Inasababisha maji-maji mengi ukeni.
4-Inasemekana yanabadilisha homono za mwanamke nakusababisha "depression" mara baada ya kujifungua (ikiwa utaamua kuzaa).
5-Inasemekana inasababisha kunanenepa bila mpango na kupunguza unene inakuwa mbinde.
6-Unaweza usipate mtoto yaani mirija yako ya kupitishia manii ya mpenzi/mumeo inaziba na ili kuizibua utahitaji upasuaji ambao unaweza kuhatarisha maisha yako au hata kubadilisha mlolongo wako wa hedhi.
Ila suitie shaka, washiriki wa hapa watasoma na kutoa maelezo kuhusu madawa hayo ya kuzuia mimba kutokana na uzoefu wao.
Karibu sana.
Kumbuka Saratani inasababishwa na mlundikano au mkanganyano, mabadiliko fulani ya chembechembe zilizo mwilini mwako sio.....hivyo sidhani kama kutakuwa na swala la "unapata ikiwa tayari unayo Saratani"....bali inategemea na madawa unayotumia.
Kwamba kuna zile inasemekana ukitumia hupati hedhi sio? Sasa jiulize ile damu ya kila mwezi inakwenda wapi? Je madawa hayo yanagandisha mayai kutokupevuka?
Nikianzaga ku-type maelezo yanazidi kuja tu...mweee! sasa Bi dada unaonaje ukitoa ushuhuda kuhusu swala zima la madawa yakuzuia mimba ili wanaotak akufahamu wajue.
Asante na karibu tena.
Sina hakika kamanimekuelewa vizuri, unamaana kuwa hupati ule ute unaolainisha uke ili uume upite bila taabu na kusababisha maumivu sio? au huna hamu kabisa ya kufanya mapenzi hata kama jamaa akijitahidi kukunyegesha?
Maumivu makali wakati wa kufanya ngono/mapenzi husababishwa na mambo mengi ya "kibaiolojia" moja wapo likiwa mabadiliko ya mwili wa mwanamke baada ya kupata watoto(kuzaa),matumizi ya madawa yakuzuia mimba kwa muda mrefu, lishe, unene kupita kiasi,wembamba kupita kiasi, kutokuwa na mapenzi/huvutiwi, kutosisimuliwa kwamba mpenzi wako hajitumi vemakukufanya ujisikie kufanywa/kuwa na hamu, mawazo na mihangaiko yakimaisha, kuugua kwa muda mrefu n.k.
Kutokana na hayo niliyoyataja kuwa wazi na uniambie wapi panakuhusu pia nitashukuru ikiwa utaniambia kuwa kati ya hayo niliyoyataja wewe haumo kwa kufanya hivyo nitakuwa na uhakika na majibu nitakayokupa.
Natumaini umenielewa.
Asante na karibu sana.
Ni Hayo tu .Nilikwua nadhani kunawanawake wenzangu wanaopata shida kama hizi baada ya kujifungua wanipe moyo heheehh.
Ni mie mwenye kasheshe za kuumia wakati wa mavituzz. Nimesoma maelezo yako kwenye makala yaliyopita na ya sasa (styles kippepeo sultan nk) nilitaka kuadd kuwa style nazo zachangia kuvuruga shughuli na kuumia zaidi. hii ya kifo cha mende ndio naumia sana ila ya pembeni inakwua nafuuu naona style pia zinachangia.Asante wka maelezo ya style maana wengine ndio tunajisavia sasa hivi ubaya tu mpenzi wangu naye mvivu ila nitajitahidi kumconvinse tujaribu hizi mpya.Ila nasubira maelezo yako labda kuna mengine yatanisaidia namie ninogewe.
Ila ungemuuliza Doc mishipa hiyo italegea vipi nina maana kunanjia yoyote ya kuilegeza n.k.
Nakushauri usitumie mpira(kondomu) natumani uko kwenye uhusiano wenye uaminifu sio? Mwambie mumeo atumie Ky Jelly kupaka uume wake na pia kukupaka wewe kwenye uke mara baada ya kuwa tayari hiyo itasaidia uume kuingia bila kukusababishia maumivu.
Mwambie atumie zile ky jelly zilizotengeneza maalumu kuongeza utamu (zinapatikana kwenye matuda ya madawa sambamba na kondoms).
Kitu kingine mwambie mpenzi wako ajaribu kucheza na kisimi zaidi kwakutumia kidole na mate, ulimi, uume (katerero au brush) ili angalau upate ile ya juu-kwa juu badala yakutegemea mpaka aingine.
Nakutakia kila la kheri ktk kujaribu mbinu nilizoeleza hapo juu.
Asante kwa ushirikiano wako.
Ikiwa makao wa kifo cha mende unakusababishaia maumivu basi uume wa mpenzi wako utakuwa mrefu sana au kina cha uke wao ni kifupi, kwani ktk mikao yoote mkao rahisi na comfy ni kifo cha mende mwanaume juu.
Lakini kwa vile umegusia swala la uvivu wa mpenzi wako (mimi naita ubinafsi)huenda inachangia sana kwani ni wazi kuwa atakuwa akijali kufurahia yeye au amalize haraka ili alale/pumzike.
Kama ni mvivu inamaana hata mahaba kabla na wakati wa kufanyanana huwa hayapo sio?
Mpige mkwara huyo aache uvivu, mwanume gani mvivu? Mwambie there are men out there wanaweza mchezo akishangaa watamsaidia(sikutumi ukatafute nje nakupa mkwara wa kumpa)......uone kama hatojirekebisha.....ukikaa kimya nakuvumilia utakosa raha ya utukufu wa tendo takatifu.
Kila la kheri na asante kwa mchango wako.
KWa sasa natumia mpira ila naacha nitatafuta vilainisho .Mie sipo bongo Ky jelly hata siifahamu ila nitatafuta vya hukuhuku nilipo. Daktari amesena ni hali ya kuzaaa chini kunajirudi sana kunakaza kutokana na kushonwa hivyo nijitahidi kwa vilainisho na maromance kwa sana nilowe itasaidia .Nitampa mkwara mzee maana naona ananisukumie mie sikubali heheheh
Asante na mchana mwema na ubarikiwa kuwa na moyo huu kwa kujibu maswali yetu.