Monday, 8 August 2011

Naogopa mkewe asije kujua uhusiano wetu, nifanyaje?

"Thanxs dada dinah kwa ushauri unaotupa wanawake wenzio. Ila dada naomba ushauri wako pamoja na wachangiaji wengine. Mimi nina mahusiano na mume wa mtu na nampenda sana naye ananipenda sana na pia ndio mwanaume wa kwanza kwangu.

Ila dada naogopa mke wake asije kujua, huwa namwambiai huyu mwanume lakini yeye ananipa moyo kuwa hilo halitotokea. Huyu mwanaume ananitunza vizuri tu na pia kaninunulia nyumba na full furniture. Nyumba hii iko mbali na anapoishi na familia yake.

Tatizo wakati ninapomuhitaji huwa simpati kwani unakuta muda mwingine yupo bisy na kazi au familia yake. Dada nifanye nini wakati nampenda sana?"

Dinah anasema:Natambua kuwa hii Post itawakera wengi, Mimi binafsi sikubaliani na tabia hii kwani kitendo cha kutoka na mume wa mtu ni Kosa kubwa. Lakini tukumbuke matusi na maeno makali hayatosaidia huyu dada kufanya uamuzi wa maana. Tafadhali mshauri kwa busara bila kum-attack huyu Binti.
Asante!

31 comments:

Anonymous said...

Mmhhhhhhh hiyo kali dada!!

Moto ukishakolea kwa kweli kuuzima ni mbinde sana, na hasa kwa kitu kinachoitwa "mapenzi" asikwambie mtu na kama ndio hivyo anakujali na kukutunza na kakununulia house.Hapo mwanamke hata umwambieje hatakusikia.

Na unacholalamika kama nimekuelewa vizuri ni kukosa muda wa yeye kuwa na wewe hasa unapomuhitaji akupe chakula chako cha usiku.Mambo mengine kama vile kuwa ni mume wa mtu hilo sidhani kama linakusumbua.

Ushauri wangu tangaza ndoa naye uwe mke wa pili maana mtafichana hadi lini dada?Ni afadhali kuhalalisha kabisa kuliko kuiba na kula kwa wasiwasi kila kukicha.
Sidhani kama kutakuwa na ushauri wa kukwambia achana naye halafu uone kama linakufaa hilo?Na umesema yeye ndiye wa kwanza,kwa kweli hata ukiondoka hapo bado utarudi tu bibie bora kujenga nyumba ya kutambulika kabisa.Kumbuka siku za mwizi ni arobaini.Hata ufiche vipi vitatokea peupe muda si mrefu.Wewe mwambie tu jamaa kuwa muweke mambo hadharani.Siyo peke yako unayekula bata wa waume wa wenzio mko wengi na kwa style tofautitofauti.Wanawake mko wengi sasa ukingoja wa kwako utampata wapi na lini?

Anonymous said...

Dada Dinah, mimi ninakubaliana kabisa na wewe kuhusu kukemea hii tabia ya kuchukua mume wa mtu. Ninachomshauri huyu dada ni kuwa kama yeye ni muislam, mwambie huyo jamaa akuoe uwe mke wa pili kuliko kufanya kwa siri kama hivyo unavyofanya. Jaalia ingekuwa ni wewe ungejisikiaje?! Mwambie huyo bwana kama kweli mmependana basi afanye taratibu akuoe ili muweze kujuana na huyo mke wake wa kwanza! Ni hayo tu.

Anonymous said...

inabid kuvumilia kwasababu n mume wa mtu nenda na mazingira akiwa busy inabid utulivu uchukue nafac yake...

Anonymous said...

I would never call this love...I am sorry to say dadangu una tamaa tu! Na tamaa yako itavunja familia ya watu. Remember what goes around comes around, hata kama huyo mke wake hajui kuna siku na wewe utataka kuwa na familia yako na wewe utayaona! Mali utaziacha hapa hapa duniani dadangu,is it worth kuingilia familia ya watu for things you'll leave on this earth? Pesa na mali kwa sasa vinakupa contentment ila hii ni kwa muda tu, age kumbuka pia inaenda na kuna siku utahitaji zaidi ya hivi na ndiyo hapo sasa utakapoanza kujutia! Mkewe anajua tu mume wake kama ana affair, she might not know who it is yet na as long as ana huzunika huko alipo utaishia kwenye matatizo kwenye maisha yako! Binadamu wewe wasikie tu, who knows what kind of woman she is! Yani unajiingiza kwenye matatizo yasiyokuwa na msingi. Huyo mwanaume kwanza hakupendi lets be honest. He likes you kwa sababu wewe ni most likely young and beautiful na unamfanya ajisikie young pia. Ila kuna siku atakuacha tu, he is not stupid for knowing you want his money and he wants sex from you. Yeye kashajitengenezea maisha yake, wewe je? I'm sure he is very happy jinsi ulivyomjinga maana he still protects his family. Kwanini unaji degrade hivi? Hivi kweli huwezi pata wako? I'm very young na wala sijaolewa but I can tell you tamaa itakuua! Probably you're not even the only one, most men who do this get addicted. Enjoy your youth and do something for yourself siyo muda wa kuanza kutegemea wanaume!Hata kama huyo mwanaume akiamua in teh long run to leave his family for you, trust me utaingiain teh same problems as the current wife. Sana sana utampokea tu matatizo yake. You will reap what you sow. May God give you the insight and wisdom katika hili. Kila la kheri!

Anonymous said...

tafuta wako achana na waume za watu..kuwa na utu!!

Gise wa Mkoa said...

uuuuhhh hii kitu imekuwa ni kama fashion sasa katika jamii zetu jaman..!1 WAUME ZA WATU..!! WAUME ZA WATU..! WAUME ZA WATU..!! watatumaliza...!!

Anonymous said...

Amakweli adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzie. sasa wewe unajuwa kabisa huyo bwana anamke na wewe unangangana tu!!!! Bibie achana naye na wewe tafuta wako. utakuwa endelea kuwa 'that other lady' mpaka lini?

Anonymous said...

kwa ushauri wangu endelea kuwa nae kama mwenyewe unampenda na unamfurahia coz unaweza ukawa na mume na asikujali wala kukutunza, cha muhimu muheshimu huyo mzee na mkewe pia.

Anonymous said...

kwa kifupi huwa siwapendi wanawake wanaotembea na waume za watu, mimi mwenyewe niko ktk ndoa na kuna dada alitembea na mume wangu, yaani mpaka leo hii siwezi kumsamehe mume wangu na huyo dada aliyetembea nae natamani wafe tu wote wawili. sasa mimi binafsi kutokana na maadili yangu siwezi kumuua but kama ningeweza kungemuua kabisa, maana hakuna kinachouma kama mume. umetoka nae mbali, umempa moyo halafu siku unakuja jua anacheat hiyo feeling isikie tu watu wanasema, na ndo maana unakuta mtu anaua. achana na huyo mwanaume tafuta wako mbona huyo ameshawahiwa na mwanamke mwenzio, utahatarisha maisha yako. na pia hauwezi kutoka nae kwa uwazi yanakuwa mapenzi ya kufichana. mapenzi ni starehe unataka watu wote wajua huyo ni wako, sasa ana mkewe unadhani itakuwaje.achana nae kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.

Anonymous said...

chamsingi ww fanya juu chini hiyo uwe mke wa pili kwake kama ni muislam iliusije kosa maisha mazuri ya huyo kaka na kama ni mkristo mushauri akuache mali si kitu tamaa za mwili zinavita dada yangu vumilia utapata vya kwako

Anonymous said...

Bibie ng'ang'ana hapo hapo unataka kwenda wapi na huyo ndiye kakubikiri?

Hizo siku unazomkosa vumilia kwa sababu unajua ana mke mkubwa wewe ukipata moja kwa mwezi au wiki inatosha maadamu anakupa mahitaji mengine mengi.Kakununulia nyumba unafikiri mchezo?Huyo jamaa anakupenda mwenzangu!!!

Ukimwacha utavuna gundu wewe kaa hapo hadi kieleweke.Kama jamaa anakupenda na naamini anakupenda mwambie aingie Uislamu ili akuhalalishe na wewe uwe mke wa pili.
Mimi nadhani umebahatika umempata akupendaye na umpendaye,hilo la mume wa mwenzako potezana nalo nani alikwambi wanaume wanakuwa na mke mwanamke mmoja?Kama ana mke nyumbani , basi ana mwingine nje kwa kujivinjari.

Anonymous said...

....pole sana hiyo ni challenge ya maisha..mapenzi ni sehemu ya maisha yetu....

Ni kazi sana kumuacha mtu unaempenda ila pia inawezekana...

Kutoka na mume wa mtu hatari yake huwezi jua mkewe akijua atakufanya nini au atamfanya nini mumewe..hatari sana...

Kama ni waislam basi akuoe uwe mke wa pili sheria ya dini inaruhusu ila kila upande uwe wazi na kupunguza kujificha ...

Pia tafuta mwanaume mwingine wa kuwa nae na achana na mume wa mtu..wanaume wa kupendana nao ni wengi..huyo hadi kaoa sio wako...

pia ni rahisi kupata maradhi kama ukimwi kwani ni hivi mwanaume anaetoka nje ya ndoa huwa hapati muda wa kuwa na mkewe hivyo mwanamke anaweza tafuta wa kumridhisha na matokeo yake anaweza leta magonjwa home na kumbuka wanandoa hawatumii condom na wewe ni wazi hutumii condom na jamaa..mtakufa na ukimwi

pia kuwa na roho ya huruma kwa mwanamke mwenzio..muachie mumewe wakae walee watoto..

Kama unakazi basi fanyakazi yako pata kipato na jiendeshe maisha yako..kukujengea house sio issue kwani wanawake wengi tuu wamejenga na kununua magari na wanasomesha kwa jasho lao ..punguza utegemezi kwa wanaume na jiamini kuwa unaweza jenga na kuendesha maisha yako kama utafanya kazi au business...

kama huna kazi mwambie akupe mtaji na atambae zake

..Ila jaribu kumpa nafasi mwanaume mwingine anaekupenda na achana na huyo kwani hayo ni mapenzi hatarishi kiusalama na kiafya...

karibu

Gluv Love

gluv100@yahoo.com

hamadi allai said...

unajuwa nyie mcwe wepec wa kudanganyika,unatongozwa na unajuwa mme wa m2 na anafamilia bado unamkubali,inamaanisha akimuacha huyo ulomnyang'anyia nawe akakuoa nawe ipo cku utafanyiwa hayohayo alafu upate kuona radha yake.r:tafuta asiyeoa uish nae baada ya kuona km anafaa au la! uSIONE VYAELEA VIMEUNDWA.

Anonymous said...

Eti unampenda sana,unapenda pesa huna lolote mwizi wewe,angekuwa hana kitu bila shaka usingekuwa naye,si unaona jamaa kakununulia hadi nyumba.km ni mwislam mwambie akuoe la sivyo achana naye.

Anonymous said...

POLE SANA DADA.MI NAKUSHAHURI JITAHIDI KUMTOA KWENYE AKILI YAKO KISHA PUNGUZA WAWASILIANO PIA JIONE KAMA ANAKUPOTEZEA MUDA WAKO COZ HAWEZI KUKUOA MDOGO WANGU PIA KUMBUKA MME WA MTU SUMU DADA.TAKE CARE MAMA.

Anonymous said...

Vitu vingine vinaboa. Huyo jamaa we humpendi wala nini, una shida pesa zake. Moyo wako umetawaliwa na tamaa ya pesa kiasi ambacho umeshindwa kutofautisha mapenzi na tamaa. Usijidanganye eti unampenda huyo jamaa, akifulia hapo sidhani kama utasema unampenda sana huyo mume wa mtu.

Anonymous said...

Je wewe ndo ungekuwa "mke" wa huyo mpenzi wako, ungefanyaje...? Just achana nae, tafuta mpenzi ambae atakuwa wa kwako pekeyako! Itakua bora kiafya na kisaikologia

manyagag said...

duh pole sana dada nagu kwa sababu tayari umeshaingia japo ningependa kujua umemkuta ndani ya ndoa au mlikua pamoja kabla ya ndoa yake?kiukweli hakuna marefu yasiyokua na ncha na watu husema mapenzi hayana siri hasa kwa sababu tayari amekwisha kununulia na nyumba that means hamtoachana leo wala kesho.swala la kua siri litakua kwa mda tu na sio milele kwani ipo siku yatakukuta.cha kufanya dada angu achana na huyo mme wa mtu kwan bado ni bint utapata mtu wa kukuoa tu usibabaishwena nyumba na mali za huyo mtu kwan aliyempa bado yupo na ridhiki yako ni pana.
NOTE:MME WA MTU NI SUMU(AND VISEVERSA)
asante from manyagag@gmail.com

Anonymous said...

Wewe dada umenishtua na kunisikitisha sana. Huyo mwanaume hakupendi, anakupotezea muda tu, wewe si mke wake na hauna haki yoyote, siku mkikosana atakunyang'anya kila kitu alichokupa. Naona hujui wanaume wewe. Nakushauri uachane naye mapema kabla hujapoteza muda zaidi. Kumbuka unahitaji kuwa na familia yako. Tulia na muombe Mungu, atakubariki na mume mzuri atakayekuwa na wewe muda wote. Binafsi ninaomba Mungu mwenye uwezo na nguvu afungue ufahamu wa huyo mwanaume haraka ili akuache mara moja, kwani wewe unamuharibia ndoa yake.

Anonymous said...

dada hiyo tabia si njema sidhani kama unategemea kuna mtu atakupa ushauri kwamba uendelee na mume wa mtu inavyoonekana haujiheshimu unawezaje kuanzisha mahusiano na mume wa mtu unajua kuna mwanamke kama wewe upande wa pili anaeililia hiyo ndoa yake ambayo wewe unaiharibu,fikira usemi mtenda akitendewa kama ungekuwa wewe unachukuliwa mume wako ungefurahi halafu unadiriki kuomba ushauri kutoka kwa watu unataka nini wewe.

Anonymous said...

Let me hold my pemper back. Binti kweli umekubali mwanaume wako wa kwanza awe mume wa mtu??? Kweli umejiona huna soko la kupata wa kumuita wakwako??? Dada fikiria upya uamuzi wako. Umeona mwenyewe kuwa nyumba alokujengea haitoshi; unahitaji kuwa na mtu wa kwako utakayekuwa nae muda wowote unapomuhitaji. Pole mdogo wangu; kama umri bado unakuruhusu nenda katubu dhambi zako; anza upya maisha yako.

Ila nina wasiwasi kwani wengi ambao walifikia kujengewa majumba huwa CV zao zinakuwa zimeshaenea mitaani hivyo kupata mwanaume wa kukumiliki jumla inaweza kuwa ngumu. Uamuzi ni wako. Ila ulichifanya si kizuri dada na kama na wewe unaamini kuwa si kizuri basi anza sasa kufikiria kuacha hiyo tabia. Kuna magonjwa. Kukununulia nyumba haina maana mko wawili tu (na mkewe). Kuna wanaume wana pesa ya kujengea nyumba jata wanawake wanne. Fikiria magonjwa mdogo wangu. What if the wife is also a cheater??? Chan hiyo ndugu. Huoni kinyaa kuchangia??? Huoni wivu kuwa the other woman??? I wish ungekuwa mdogo wangu I would have stopped you from the beggining. Anyway I hope it is not too late.

Anonymous said...

Jamani hii tabia ya kutembea na wake/wanaume wa watu ifikie pahala tuone ni kama sumu, wewe wajua kabisa huyo jamaa yako ni mume wa mtu kwanini isifikie pahala utumie akili tu ya kuzaliwa na kujiondoa ktk matatizo yasiyokuwa ya msingi? hiyo tabia ni mbaya sana jaribu kujitoa ktk huo uhusiano ndugu yangu hata kama anakupenda sana ipo siku wewe na huyo mmeo wa pembeni mtakuja kuumbuka tu.

Anonymous said...

Nilikuwa nimesamehe,lakini sasa unakuja kutafuta msaada huku kwenye mtandao,nitakukomesha,huu mmwaka ukiisha labda sio mimi,maana naona sasa unavuka mipaka,kwa taarifa yako kila unakopita na mimi nipo,wether utamuacha au no,lazima nikukill mbwa wewe,by any means NITAKUUWA

Anonymous said...

wewe anony wa 11.35 acha mikwara ya kichaa cha dog. Ujije kuua mtu bure kumbe wala sio mwizi wako huyo

Back to the topic; mie ni m/ume na nimeshawahi kutoka nje ya ndoa ila nakiri kabisa kuwa ili ni tatizo kubwa na ninajutia sana kwani w/wake siku hizi utongoza w/ume hasa wakiona ana kipato kikubwa. Binti achana na mme wa mtu inaleta mtafaruku sana kwenye familia ya m/mke mwenzio maana usaliti uonekane kwa wasiwasi tu wa m/ume si lazima akujue sasa kama huyo dada akihamua kufuatilia nyendo za mme wake atajua tu na unaweza kufanyiwa kitu kibaya hivyo vyote ulivyofanyiwa vikakutokea puani

Anonymous said...

honestly i hate when some1 is cheap.
me natamani wanawake wote wanaotembea na waume za watu wapate what they deserve kwa sababu kiukweli inauma sana mumu wako kutembea na mwanamke mwingine..
isitoshe unajidhalilisha sana kuvunjwa bikira na mume wa mtu you are so cheap
am sorry am being so harsh but that the truth though it hurts the only way to escape being called someones' misstress is to quit the relationship with him kwa sababu hapo hakuna real love ni money love na ikiisha utacheka kichina my dear. Pole

Liz

Anonymous said...

Mdau hapo juu umeniacha hoi. Kweli mume wa ntu sumu

Anonymous said...

Kwanza nataka nijue hati ya nyumba na document muhimu za kumiliki hizo mali alizokununulia zimeandikwa jina lako na unavyo mkononi??nasema hivo kwa sababu siku kikinuka anaweza akakuacha na kukunyang'anya mali hizo akampatia hawara mwingi,utachina mtaani nakwambia. Kwa sababu kwa tabia ya huyo mwanaume itafika kipindi atakuchoka atabeba mwanamke mwingine tofauti na mkewe atamfanya hawara kama wewe. Kama huyo mwanaume ni mkristo ni ngumu kuachana na mkewe. Mwenzangu weka mambo yako sawa ameshakutumia hata siku akikumwaga utatuliza machungu na vijimali alivokununulia kuwa macho. ohoooooooo.

Anonymous said...

we anony wa 11.25 kichaa cha dog unacho wewe,simtishi na mwenyewe anajua,kama ni mambo ameshaanza kuyaona na hiyo ni trela tu bado picha.si mmekutana mara tatu na mboo haikusimama,na bado nakuvutia speed tu,nakupa muda na subiri period ya mwezi huu,utarudi hapa kuomba ushauri ustopishe vipi,malaya wewe,na mkundu simpi,we endelea tu kumpa wewe maana ndio sifa yako kubwa kwa mume wa mwenzio,pumbavu wewe!!

Anonymous said...

we acha uchandudoa walahi mie siku nijue mtu anetoka na mme wangu ,i will deal with her mme /mke wa mtu sumu,imagine wewe ndo umeolewa harafu limalaya jingine linatoka na mmeo
Umeniboa kama nini huna adabu
myzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzz

Anonymous said...

umeniboa natamani kukutukana sema ndio hivyo dada dinah amekataza ila kimoyomoyo nimekupa moja kubwa. siwezi kucoment zaidi.

PS: wisen up! utakuja kuolewa wewe siku moja na mumeo atafanya ivyo ndio utajua utamu wake ***** (nimetukana hapo). haya bye

Anonymous said...

jipe moyo utashinda.kutolewa bikra sio sababu.wengi huolewa bila bikra wanaume ambao sio waliowatoa bikra.sasa tafuta kijana wa makamo yako,ambaye atakuoa na umfahamishe huyo mme wa mtu kuwa unataraji kuolewa.mfahamishe unataka kuwa na mwezi.akihitaji nyumba yake mrudishie na umkabidhi nyumba kwa raha.utapata nyumba yako.km ni mwanaume mwenye akili na kama alikuwa nawe kwa mapenzi tu hatadai nyumba na atakukubalia uolewe.CHAKO NI CHAKO DADA hata usiku wa manane unapata haki ya ndoa.