Wednesday, 18 August 2010

Nafikiria kuachana nae lakini nashindwa, nifanyeje?

"Heshima yako dada Dinah.
Napenda kutoa pongezi kwako na kwa wachangiaje wote ambao wapo bega kwa bega kutoa ushauri katika topic mbalimbali. Mimi ni mmoja wa wapenzi wa blog hii, nimekuwa nikifuatilia kwa karibu sana mada mbalimbali na kujifunza mambo mengi kwakweli.

Dada dinah kama unavyojua matatizo tumeumbiwa nayo binadamu hasa katika barangeni hili la mapenzi. Mimi ni kijana mwanaume, umri miaka 22. Kusema kweli mpaka sasa mwenzenu nipo njia panda kuhusu msichana ambaye ninampenda sana ila simuelewi hata kidogo kama kweli ananipenda ama la.

Ni miezi sita tangu ni mueleze hisia zangu juu yake bahati nzuri alinielewa na akanipa jibu zuri ambalo lilinifanya nisijute kumpenda. Tangu hapo nilikuwa nimechizika kwake nilipenda kila wakati eidha nimuone au nisikie sauti yake tu. Hapo ndipo nilipo fikia uamuzi wa kumnunulia simu ili mawasiliano kati yangu na yeye yawe rahisi.

Tangu hapo nikawa nampigia simu mara kwa mara wakati mwingine anapokea wakati mwingine hapokei, basi ninaamua kumtumia sms ambazo pia hakuona umuhimu wake, nasema hivi kwasababu ninapo muuliza kama amepata sms yangu hunijibu sms ipi? Ilikua inasemaje? Basi tu ilimradi.

Haya yote sikuyatilia umuhimu kwa kuwa nampenda ila wasiwasi wangu umeanza kuja hapa, tangu niwe na mahusiano nae sijawahi kukaa nae tukajadili kuhusu mapenzi yetu kwa kuwa huwa anakataa na kudai kuwa anashughuli nyingi.

Pili sijawahi hata kumkiss shavuni achilia mbali romance nimejaribu mara kadhaa kumuomba tutoke out japo twende hata beach lakini huwa ana kataa sababu ni hizo hizo. Nimemjali kwa mengi bado haoni umuhimu wangu kama mpenzi wake. Pia nikakubaliana na yote hayo hivyo mapenzi yakawa ni ya kwenye simu tu hakuna kuonana.


Kikubwa kinacho niumiza mimi mara kadhaa ninaweza kukutana nae katika mizunguko lakini cha ajabu huwa hana muda na mimi hata salamu mpaka nianze mimi. Nikikaa kimya hunipita kama hanioni. Dada dinah kiukweli nimekuwa sina raha muda mwingi nawaza kwanini ananifanyia hivi lakini nakosa jibu, hata yeye mwenyewe ninapo muuliza huwa hanijibu chochote.

Sasa sijui amedhamiria au ndio mapenzi yenyewe! naweza kusema alibadilika pale tu nilipo mnunulia simu na ilikuwa ni wiki moja tu baada ya kunikubalia ombi langu. Anayo nifanyia ni mengi mno ila sipendi kuwachosha wachangiaji kwa kusema yote.

Hivyo mwenzenu mpaka sasa nipo njia panda, neno nakupenda limebaki kuwakumbukumbu kwangu. Nimeshajaribu kufikiria kumuacha niwe alone lakini nashindwa, je nifanye nini mwenzenu.
Ahsanteni".

32 comments:

Anonymous said...

MPE NOTICE, ASIPOOMBA MSAMAHA BASI ACHANA NAE MAZIMA COZ HATAKUFAA HUYO. LOVE IS TWO WAY TRAFFIC, GIVE AND RECEIVE. IF U THINK THAT U R GETTING LESS THAN WHAT U DESERVE GO ON WITH UR LIFE. OMBA MUNGU AKUPE MKE MWEMA HUJACHELEWA BADO, 22? DOGO SANA.

Anonymous said...

Anakupenda sana tuu siunajua sisi watoto wakike ni tofauti kidogo na wakiume moja niaibu inayomsumbua pili hajajua kutumia simu nenda naye taratibu.hata mimi boyfrend wangu alihangaika sana na hiyo yoteilitokana nilikuwa sina hata expiriensi na mwanaume.alijaribu tukaenda mpaka gest lkn hatukufanya chochote ni kwasababu miyenilikuwa bado muoga ila kiukweli nilikuwa nampenda ila sikuwa tayari kumvulia chupi alipeleka taratibu na baadaye nilikuja kujikutanimenasa kwenye 18 zake vuta subira kijana

Anonymous said...

Mh! pole kaka, kwani hadi nini ndo ujue anakupenda, mana unalalamika hata romance hujawai may b anapenda kujilinda thats y anakuwa mbali na ww coz keshagundua nia yako kwake ni x, so lazima ajihadhari na mazingira hatarishi km kwenda beach, au any place kwa faragha.pia huwezi jua kwann anakukwepa, may b anakuponya na k2 flani. c unajua cku hizi afya cyo njema sana. (eg. kuna mtoto wa 4m six mtaani kwe2 alifariki juzi kwa VVU na mzaliwa wa 1994 alipata maambukizi toka kuzaliwa from he mom, na usingweza kumtambua kwa kumwangalia, embu just imagine alikuwa na BF, na ameishi kwa 16yrs) so plz let her go usimng'ang'anie sana. km vp labda mkapime la cvyo labda Mungu ana mpango mzuri tu na ww.

Gg

Angel said...

pole sana ,ushauri wangu chunguza kwa makini maana vijana kama nyinyi bado ni wanafunzi na mpo chini ya ungalizi wa wazazi kwahiyo swala la kumnunulia sim inaweza imekua tatizo kwake kwasababu lazima kwa mzazi anaye jali atauliza sim umeipata wapi
na kusema ukweli kua umemnunulia ni vigumu ,na akachimbwa biti akaamua kuachana na wewe kuepusha shari, na kuku ambia ukweli hawezi kwakua inaelekea anakupenda lakini hawezi kwakua bado yupo chini ya wazazi na anaogopa kuwaambia ukweli ,fanya uchunguzi katika hili inawezekana ika ndio sababu hasa yakufanya hivyo .
maana nakumbuka hata mimi nilianza uhusiano nikiwa na umri kama wako nikutana ma mpenzi nilikua naogopa hata kumsalimioa maana naogopa mtu asije akaniona akapeleka umbea nyumbani ika tabu,hata busu nilikua sitaki akilazimisha basi nitaangalia kila upande nikiridhika kua hakuna mtu basi ndi kiss nasio kwamba nilikua sipendi lakini niliogopa sana kuwapa wazazi stress ,na hata swala la beach nilipinga vikali maana nilifikiria nitaaga vipi kwenda huko na sikupenda kuwa danganya wazazi wangu ,na nilijisemea hivi nidanganye kua naenda mahali alafu niende beach mara nikifika huko nikutane na mtu wa familia kaenda huko nitakua mgeni wa nani mimi ,kwahiyo sikuthubutu hata kidogo ,inawezekana na yeye akawa na tatizo kama hilo .uhusiano wenu bado ni mchanga humja juana vizuri ,jari kuchunguza kwa makini utaujua ukweli.nakumbuka mimi nilimwambia baba watoto wangu ,mashari kua mimi sitakuja kwako labda uwe una umwa ndio nitakuja kukujulia hali tena kwa muda wa dakika 30 tu ,sitapata muda wakutoka na wewe, sihitaji zawadi zako zaaina yeyote ile hasa durable goods kama sim ,nguo etc. kweli nilimpa wakati mgumu sana lakini nikua sina jinsi maana nilikua mwanafunzi japo wa kidato cha sita ,na wazazi hawana tabia za kizungu kwahiyo ilibidi iwe hivyo .kwahiyo inawezekana na yeye inashida hiyo. fanya uchunguzi

Anonymous said...

Kwani wewe uliIngia na gear NUMBER NGAPI? Think twice and go back to the start! Kaa naye chini mpe plan zako; inawezakana akawa anakuona kama unataka kumchezea ndo maana anakaa mbali na wewe! Mueleza nia na malengo yako ya mbeleni - siyo neno NAKUPENDA tu. Unampenda then what next? That girl is so smart - big-up mdada, kama hujaweka wazi your abjectives - hapo sahau!

Dogo, go back and re-write your objectives

Anonymous said...

Akili ya utoto ndo inakusumbua. Huyo msichana anaye mtu mwingine, atakupotezea muda tu...wasichana wengine huwa hawawezi kukataa kwa kusema no, au sikupendi au siko tayari...ila huonyesha kwa vitendo tu na kujaribu kukukatisha tamaa ili usiwasumbue. Anachofanya huyu dada ndo hicho, kujaribu kukukatisha tamaa ili mwisho wa siku uchukue time zako.

Cha kufanya ni kukaa kimya, tulia look around utakutana na mwingine tu na mambo yataenda sawa. After all bado mdogo sana, 22 ni bora utumie muda wako kujisomea au kufanya mambo ya msingi ambayo yatakupa shavu baadae. Inawezekana anakuona mdogo ndo maana yuko hivyo. Kwa kifupi achana naye.

Anonymous said...

Kijana mnona unataka kujiua mapema hivyo?

Wewe pamoja na huyo mlimbwende ni wachanga mno kuparamia mastress ya mapenzi.

Miaka 22 uko mchanga huhitaji kujikita mno nayo,take mapenzi as simple as you can.usipoteze muda kujikita nayo yatakuaharibia mwelekeo hatimaye ukajikuta unajiumiza bure.

Huyo binti inaelekea kabisa ni mtoto sana na pia amekuona una papala naye sana kiasi kwamba unapoteza muda wako kummingulia saa zote.Wewe huoni anadhiriki kukupita bila kukusalimia?

Ushauri wangu ni kwamba kaa kando kabisaaaaaaaa fanya kama hummaindi kabisaaa atakutafuta yeye.Hata sielewi kama uko chuo au unafanya nini, nilitaka kukuambia kuwa mapenzi ni sumu hasa ukijirembesha na mtu asiyekujali kama hivyo.Achana nayo kwanza endelea na mipango inayokuhusu wewe kama wewe tu hasa shule kama unasoma chuo au vipi.

Mbona watoto wa kike wamejaa kibao, ni vile labda hujatembea mahali pengine upo hapo ulipo hivyo umejifunika blanketi zito hata huwezi kuona wengine kando yako.Mbaya zaidi msichana akigundua kuwa unampenda sana atakutesa hadi ujinyonge.Achana naye tulia kwanza.

Anonymous said...

Hakupendi huyo kaka, au ana matatizo mengine kisaikolojia na hajui nini kinamsumbua, fanya bidii UONGEE nae ili ujue tatizo lake ni nini!?, kupewa denda , romance, au hata ngono haimaanishi ndio anakupenda jaribu kujua wazo lake kwanza juu ya mahusiano yenu mazima, kama vp achana nae tafuta mweingine pole sana kaka 22yrs bado kijana sana usikate tamaa...

Anonymous said...

nayaelewa maumivu ya kupenda usipopendwa,nami yamenikuta. kwa kifupi huyo mwanamke hakupendi,na wewe mwenyewe unaelewa,isipokuwa kwa kuwa unapenda,unajaribu kujipa hope maybe mambo yatakuwa mazuri,kiukweli hayatokuwa{yameshanikuta}.ukimpenda mtu ambae hakupendi,unajihisi na maumivu makubwa ambayo hayasemeki,wakati mwenzako anakula vizuri na analala vizuri,wewe unaishia kuwaza tu.The best way achia taratibu kwa kupunguza mawasiliano ingawa ni ngumu{mimi nilijaribu simu yangu kutoitia cr. kabisa ili nisitume msg au kupiga simu}kwani simu yangu nikiitia hela tu na huapa simpigii,basi napiga na msg natuma.achia taratibu,baadae kitonda kitapona,raha ya mapenzi,mpendane.umri bado mdogo utakuja kupata wako na akakupenda na wewe ukampenda,ila usifanye haraka kumpenda mwengine,it will take time.

Anonymous said...

huyo anakuzingua achana naye wanawake wako wengi huyo mwanamke inaonyesha ana mwanamme mwimngine hivyo hawezi kuongozana na wewe kwa kuogopa jamaa atashitukia mahusiano yenu. nakushauri jikaze kiume msahau kabisa. utapata mwanamke ambae anakupenda kwasababu huyo si mkweli bali anataka kukuchuna tu. wala usihangaike kumunyang'anya simu uliyomununulia hilo linaweza kusababisha ugomvi na mkatia aibu mitaani. karne hii kugombana sababu ya kuma siyo issue wanawake kibao.

gudchaz said...

bro...!! huyo bana hakupendi wala nini kwa matendo anayokufanyia inaonyesha dhahiri kwamba hana mpango na wewe na unampotezea muda tu..........achana nae na atakuja kukumbuka tu,wanawake kama hao wapo tu duniani kwani huko anapopategemea atajutia.........ushauri wangu ni kwamba achana nae we bado kijana mdogo sana utapata umpendae na atakaekupenda kwa dhati na kuwa na furaha.....

Anonymous said...

pole sana kijana mwenzangu najua maumivu uliyokuwa nayo jamani haya mapenzi sijui hata yametolea wapi!! Tatizo siku hizi haw watoto wa kike wakipndwa hawapendeki wanadanganyika na vitu vidogo tu .Ndugu yangu chakufanya jaribu tena kuomba mkutane japo kwa muda tu halafu umuulize enafikiria nini juu yako!! na anakuchukuliaje!! hapo utapata jibu kama hataki hata kuonana na wewe hajali hisia zako huyo hakufai utakuja kuunia bure kaza roho tafuta mwingine wapo wengi ambao nao wanapata shida kama hizo!! kaka pole sana.

Anonymous said...

Pole sana kaka, nakuonea huruma sana huyo msichana uliyempenda anaonyesha ana maringo pamoja na hilo yaonyesha hajakuweka moyoni,kwa kuwa wewe umezimikia hapo emu anza kwa kumtesti kwanza kama kweli anakupenda jaribu kukata mawasiliano nae na asijue unawaza nini juu yake, ukiona hashtuki basi achana nae, na kama atashtuka na kukuuliza usijirudi haraka, mchunguze kwanza nia yake ipo kwenye mapenzi au kukuchuna. alafu umweleze awe mkweli kama hakupendi akwambie usipoteze muda, waschna tupo wengi kweli

Anonymous said...

be crful kaka..may b anakutest..au yuko intach na mwngne..bt umesema ulimpenda sana ila cjaskia umesema if she loved u b4,,isije ikawa uliovadose filngs juu yake then akuone bwege.umempa sim sawa,je yeye ashawahi kukupa hata bthday kad??its me alphonce[0765069691]

Anonymous said...

she has sm1 else intach kaka

Anonymous said...

kiukweli ni kwamba huyo demu hakupendi yaani ana mtu wake ambaye yeye anampenda na kumfanya awe na furaha ilo unapaswa kulijua then achana naye wewe bado mdogo tafuta mtu mwengine ambaye atakuwa na upendo wa kweli kwako.

Anonymous said...

Achan nae anaupotezea muda, ALAFU MI NAHISI WEWE BADO UKO SHULE KAMA SIJAKOSEA MIAKA 22 BADO MTOTO KUJIHUSISHA NA MAMBO YA MAPENZI AU NDIO UTANDAWAZI? PAMOJA NA HAYO ASIKUPOTEZEE MUDA COZ IT SEEMS SHE WILL NEVER LOV U BACK, SO WHY BOTHERING URESELF? TAKE UR TIME FIND THE OTHER LADY IN TZ(THER ARE PRENTY OF THEM).BUT SERIOUSLY CONCENTRATE ON URE STUDIES FIRST,THEN HAYA MAMBO YATAKUJA TU YENYEWE SAWA MKAKA?

STRAWBERRY

Anonymous said...

Kama vip mpige chini ukifosi atakupa tabu baadae so mchunie kwa muda then mcheki kama atabadilika.kama hatabadilika jua kwamba anajamaa.mwingine ndio maana anashindwa kua karibu na wewe.

emu-three said...

Usihamanike haraka kiasi hicho kwasababu kwanza huyo ni mwanamke na hulka ya kike ni kuringa hata kama anapenda.
Pili nyie ni marafiki tu, usikimbilie yale ya uchumba na ya ndoa kabla hamjaewana. Nasema hivyo kwasababuu mapenzi wkati mwingine ni kama ulimbo, ukikunasa itachukua muda kuubandua, na athari yake inaweza kukuumiza kabisa.
Cha muhimu kikujuana kwanza, na kujuana sio lazima kuingiliana kiundani, hapana, kujuana tabia,na kama ikiwezakana kuelezana nini wewe wapenda na nini mwenzako apenda.
Huyu mwenzako anaweza akawa anakutega ili ajue msimamo wako kwake, kwahiyo hapo na wewe unatakiwa uwe makini, kama utataharuki kuwa hataki mapenzi ya undani basi atagundua uzaifu wako mapema, kuwa wewe nia yako sio njema kwake.
Peaneni muda, na ikifikia muda hutaamini, mabo yatakuwa saafi kabisa. Tusipaparikie makubwa kwanza, tufanye subira, kwani subira huvua heri

Anonymous said...

Vitu vingine acha ujinga hupaswi hata kuuliza yani kimbia, huyo hana hisia kwako hata chembe. Sasa kama hata mkikutana mpaka salamu uanze wewe unafikiri pana mapenzi hapo??? Kifupi ni kuwa huyo mtu hathamini chochote toka kwako isipokuwa simu uliyomkabidhi.
Kuhusu maswala ya kumkiss na romance achana nayo kwani yaweza kukupelekea kufanya zinaa, na sote twajuwa kwamba zinaa ni haraamu. Take care and be happy always.

Anonymous said...

Achana nae huyo kwa nini akufanye mtumwa wa mapenzi? hayo uliyomfanyia yanatosha pia anaonyesha hana mapenzi ya kweli kwako ni bora ukajua ustaarabu wako mapema mbona wazuri wapo wengi na wanazaliwa kila siku kuliko yeye! asikutese mtoto wa mwanamke mwenzie.

Anonymous said...

MH! huyo anakuonyesha live kuwa hakupendi anajitahidi kwa vitendo na wewe huelewi.maadam kaanza mwache endelea na maisha yako MUNGU atakupa wako huyo si wako usipoteze muda ukomboe wakati kaka bado unaweza

Anonymous said...

KILA LIKUEPUKALO LINA HERI KWAKO. SHUKURU MUNGU. UNATAKIWA UOMBE SANA, USIWE NA HARAKA NA MAMBO HAYO. MUNGU ATAKUPA MWENZAWAKO MWEMA. HAYO MAMBO HAYALAZIMISHWI, LAH SIO UTAKUJA JUTA MAISHA YAKO YOTE. NAJUA UMRI UNAHITAJI LKN JARIBU KUJ-CTRL. NDIO MAANA ULIMPENDA HUYO MDADA. KUMBUKA KUWA KILA VING'AAVYO SI DHAHABU. KARNE HII SI YA KUKIMBILIA INA MAGONJWA MENGI, MATAPELI WA MAPENZI NK. KUWA MWANGALIFU SANA. MSHUKURU MUNGU KWA KILA JAMBO. SALI SANA UMKABIDHI MUUMBA SWALA HILO. UTAPATA YULE ALIYEKUCHANGULIA YEYE.

Anonymous said...

Kuna mawili, yawezekana anakupima kama kweli unampenda kweli japokuwa hicho kipimo chake kimezidi, hata salaam? AU amegundua kuwa wewe ni muhongaji mzuri hivyo anaamua kukufanyia hivyo akiamini kuwa utatua pesa/kumuhonga kitu kingine ili umvute karibu. Ni hayo tu, ila usisahau kutembelea 'www.bongo21.blogspot.com'

Anonymous said...

kaka usipokuwa makini unaweza kuchizika kumbuka ni mara chache sana hutokea kumpenda mtu anayekupenda mara nyingi unayempenda wewe hakupend.
huyo mpenzi wako amshapata mtu mwingine ndio maana kaamua kukubadilikia au alikuwa naye kabla ya kuwa na wewe na kaamua kukuficha tu mdogo wangu umri wako bado ni mdogo sana mi nakushauri achana na hayo mambo yana muda wake kwa sasa kama ni mwanafuzi soma au kama unajishughulisha na shughuli binasi kuwa busy na kazi kwanza mambo mengine yanafuata baadaye

Anonymous said...

EBWANA POLE SANA, USIJALI HIZO NDIZO BAADHI YA CHANGAMOTO ZA KWENYE UHUSIANO. SOLN NIZIFIKIRIAZO
1.Mtafute mkae muonge mueleze mabadiliko yake kwako, hata akijidai yuko rightway jaribu kumkumbusha alivyo kuwa mwanzo na alivyobadilika sasa
2.jiulize kwani amebadilika sasa wakati mwanzo alikuwa poa pengine kunavitu anavikosa sasa kutoka kwako achiliia mbali zawadi nalega sana mahabati au havutiwi na unavyo ilipuka(pamba) maana mabinti wanavutiwa sana mwanaume nadhifu
3.jaribu kufuatilia historia yake kwani ni vema kujua background ya mwenzio HALAFU KUMBUKA KUTATUA TATIZO SIO KULIKIMBIA BALI NI KUKA CHINI WOTE 2 NA KUTAFUTA SULUHISHO.TONY

Anonymous said...

huyo dada hakupendi na isitoshe anawapembeni. Iweje akupite utafikiri we ukuta? communication is a key in any relationship, without it mnagidanganya tu! na kama mwezio hawezi kukuanza japo kwa salamu, basi hapo tatizo ni kubwa. mketishe muongee ikishikana move on. huo ndo ushauri wangu

Thadei said...

DUUUUH!Hiyo kali ndugu yangu!!Hivi ni nani anaepotosha maana halisi ya mahusiano??Hivi ni kweli mahusiano ni lazima Romance?au Kiss?Mimi nadhan mahusiano ni zaid ya hivyo!
Lakin anyway jaribu kutafuta faragha uongee nae ujaribu kumweka wazi nini unapenda!!
Ikishindikana move on kwanza wewe ni kijana mdogo una mambo mengi ya kufanya tena ya msingi kuliko kuumizwa na mapenzi ambayo kwako muda wake bado!!!!!!!!!!

Anonymous said...

great site keep, it up

Anonymous said...

hakupendi hata kidogo, ana mwanaume mwingine, nadhani anafurahisha na kitendo cha wewe kuwa crazy over her, it make her feel beautiful and loved which is selfish coz love has to be from both sides. achana naye tafuta mwanamke mwingine anayeona umuhimu wako. unaweza dhani huwezi kumpenda mwanamke mwingine ila unaweza na utashangaa mwenyewe. time heals leave her dont waste your time on her.

Jannel said...

huyo dada hakupendi kabsa ni bora uache mawasiliano nae bila ht kumtaMkia km mmeachana
na kama anakupenda basi atakutaft ila ukiona kakaa kimya ujue hakupend na yuko na mwanaume mwingine,namalza kusema kuwa mwanaume mwenye roho km yako ni kumi kwa mmoja,ila pole sn kaka yng amin ipo cku na ww utapata yule unayemhitaj

Anonymous said...

usikute na wewe unamsumbua mno.. kaa kimya kwa mda uone kama hata kutafuta.. msichana ukiwa unampigia pigia anakereka, we simu kila saa ma message ndo nini? tulia kijana, take it slow...