Saturday, 5 September 2009

Mume to be anuna kwa vitu vidogox2-Ushauri

"MAMBO VIPI JAMANI?
MIE NI MDADA WA MIAKA 29, NATARAJIA KUFUNGA NDOA HIVI KARIBU MUNGU AKITUJALIA TUNA MUDA WA MIAKA 6 SASA NA TUNAISHI PAMOJA KWASASA YAANI DADA TATIZO NILILO NALO NI HUYU MWANAUME ANAPENDA KUNUNA KWA VITU VIDOGO YAANI UKIKOSEA KITU KIDOGO ANANUNA NA ANAWEZA KUONGEA MANENO YA KASHFA MPAKA NAOGOPA YANI MIMI HATA SIJUI NIFANYAJE JAMANI ANAWIVU SANA YANI NIKIPIGIWA SIMU AU KUTUMIWA MSG KOSA UNAKUTA KANUNA MARA HANIAMINI YAANI MPAKA NAKEREKA YANI NI VILE BASI TU EMBU NISHAURI DADA NIMFANYAJE HUYU MTU JAMANI MAANA ANANIKWAZA MPAKA BASI."

Dinah anasema: Mambo poua tu mdada, hujambo? samahani kwa kuchelewa kujibu. Binaadamu tumeumbwa tofauti hali kadhalika ninyi wawili ni tofauti sana kitabia, kimalezi hata matakwa yenu ni tofauti natumaini hilo unalifahamu.


Huyu mchumba wako inawezekana hajiamini hali inayopelekea yeye kushindwa kukuamini wewe hasa unapopokea sms au hata kupigiwa siku, mara nyingi mtu mwenye au alikuwa na tabia chafu kupitia simu au hata Internet huwa anakereka "Kisaikolojia" (kwa vile anajua ndio zake au zilikuwa zake yaani anauzoefu fulani hivi ) na kuumia balada ya kuuliza kwa upole na upendo "ni nani huyo ulikuwa unaongea nae" au "nani amekutumia ujumbe.


Mmekuwa pamoja miaka 6, mnapendana na mnakwenda kufunga ndoa ili kuishi pamoja maisha yenu yote hivyo basi ni vema kuanza kurekebishana sasa. Natambua kila mmoja wenu anavijikasoro ambavyo havirekebishiki so u live with them na viji-habit vyake ambavyo vinarekebishika ikiwa mhusika atakubali kuwa anavyo na vinamkera mpenzi wake.

Nini cha kufanya:
Ni ngumu sana kuwakilisha issue hiyo kwake (Kwa wanaume wengi lawama zote anabeba mwanamke) hivyo unapaswa kutumia UANAMKE wako kuandaa namna/mazingira ya kuwakilisha issue, unaweza kutumia mapenzi ya hisia na mwili, unaweza kumromantisha (kumfanyia kitu romantic), unaweza kubadili mwenendo kwamba kila unapopokea sms unasoma kisha unamuonyesha au unaifugua karibu yake ili aione, na kama ni simu basi hakikisha unamhusisha.....MF-unaulizwa simuni, "unafanya nini" unaweza kusema nipo tu hapa na Mchumba/mwenzangu/mume wangu tunapumzika. N.k

Vilevile kama unajua kuna vitu vidogo vidogo vinamuudhi na vitu hivyo wewe ndio unaevisababisha basi unapaswa "kupumzika" yaania cha kuvifanya. Baada ya muda (wiki nne mpaka miezi 2) unaweza kuwakilisha tatizo lako kwake kwa upole na upendo, hapo hatoweza kukurushia lawama zozote kwa vile tayari ulimhusisha kwenye txts msg na simu unazopokea na ukaacha vile vitu vidogo vidogo vinavyomfanya anune.


Kule kwetu tunapofunzwa huwa tunaambiwa kuwa mwanamke ndio pekee mwenye uwezo wa kubomoa au kujenga nyumba yako (not exactly ila wanatumia hii ili wewe mwanamke ujue nafasi yako na kuwa mwangalifu kwenye uhusiano ili kupunguza matatizo), Pia kumbuka maisha ya kimahusiano na ndoa sio lelemama, yanahitaji kufanyiwa kazi kila siku.


Bibi yangu aliwahi kusema kuwa "kukitokea tatizo ndani ya ndoa jiangalie wewe kwanza na jirekebishe kabla hujaomba mwenzio ajirekebishe"RIP........alitumia kuomba rather than kumtaka mwenzio ajirekebishe.

Usitegemee mabadiliko ndani ya siku au wiki moja bali muda zaidi kwa kuwasiliana, kushirikiana, kukumbushana na kuongozana.

Kila la kheri ktk kuweka sawa hili na kwenye kufunga ndoa.

14 comments:

Anonymous said...

Pole saaana ndugu! It pains alot, hapo hata ndoa bado je mkiwa ktk ndoa!

Mi naona uizoee tabia yake na uchukulie kuwa ndvyo alivoumbwa, huenda tbia yake ni inborn.

Mbona uktaka kla m2 awe kama utakavyo basi hutapata mchumba anayekufaa kwakuwa kla m2 ana kasoro. Basi jtahid kuyafkria yalyo mema anayokutendea kulko makosa. Hata ww una mapungufu meng tu ambayo mwenzio anayavmilia kwan wazan ww ndo huna kasoro kbsa. Hv wazan sifa zoote alizokuwa akhtaj mke wake awe nazo ww unazo? Sidhan!

Pia jiangalie huenda huwa unafanya mambo meng yanayomtia hofu ndo maana ana wivu! Usipende kufanya mambo mengi kwa siri kama vle kupokea cm c lazma ukaongelee pembeni au meseji co unasoma tu na kuifuta hapohapo kwan hvo n v2 vtakavyomtia shaka.

Fungeni ndoa haraka sana ili muepukane na zinaa.
Mwatima

Anonymous said...

Nikuambie ukweli mpendwa, hali hiyo ipo kwa wanaume wengi, na hii inasababishwa na kutokujiamini,au kutokumwamini mwenzako. Kwasababu gani, unakiona kitu hukipendi na labda umeshawahi kusema kuwa hiki sikipendi nataka iwe hivi, bado kinarejewa,sasa kwa udhaifu wetu hatuwezi kutumia fimbo, au kupigana, kwa wanaume wengine wanaishia kununa.
Kununa ni moja ya njia ya udhaifu wa kuonyesha kuwa kuna jambo limetokea ambalo hulipendi. Ni njia ya udhaifi kwasababu kuliko kununa unatakiwa useme kuwa kwaweli hili mwenzangu umeniudhi naomba iwe hivi, na wapenzi wanatakiwa wasichoke kuelezana ukweli, na kuelezana huku kuna mahali pake jamani!
Njia ya kulikwepa hili ni kujaribu kutokufanya kile kinachomuumiza mwenzako, na ukitaka kukifanya mueleze mwenzako kuwa nataka kukifanya hiki kwa sababu kadhaa.Na ni rahisi kwa nyie wanawake kumweka sawa mwanaume wako akakubaliana na unachokitaka,kama kweli unampenda na kumjali.
Kuhusu wivu, hii wengi tunasema ni sehemu ya mapenzi, ila tunatakiwa wivu usizidi sana.Hivi wewe utajisikiaje kama unafanya vitu viletavyo wivu na mume, au mkeo hakuulizi? Hapo kutakuwa na walakini, huenda jamaa hakuthamini tena,au ndio zake!
Kuna wivu mzuri na wivu mbaya,na wivu mzuri ni wakujenga pendo, kuwa usiibiwe au mwenzako asiende kinyume na taratibu za mapenzi au ndoa yenu.
Kwaushauri wangu, usijali hali hiyo ya kununa, wengi wa wanaume ambao sio waongeaji sana wanatabia hiyo, na wivu ni sehemu ya upendo, jamaa anakupenda muno ndio maana anawivu, anaogopa asije akaibiwa. Cha muhumu ni kutokuzidisha yale asiyoyapenda na muonyeshe kimpenzi kuwa yeye ni yeye peke yake, na hiyo iwe kweli usije ukawa unampaka mafuta kwa mgongo wa chupa kwani akigundua,huko kununa kutatoka nje na watu wa namna hiyo wanaweza kufanya jambo usilolitegemea.

Anonymous said...

DUH HUYO JIBABA UMVUMILIE TU KWANI NDO SILCA YAKE NA HUWEZI IBADILISHA KWA NAMNA YOYOTE ILE MAANA SILKA HAIBADILIKI ILA HULKA HUBADILIKA,PILI MTEGE SIKU MOJA UMWAMBIE MAMA YAKE AKUTUMIE SMS YA KIMAPENZI ITAKAYOMUUMIZA YEYE NA KULETA UGOMVI MKUBWA BAINA YENU ILA NAMBA YA MAMAKE UISAVE JINA LA KIZUSHI ILI LIMCHANGANYE KIMAWAZO THEN MUMUUMBUE AKOME TABIA HIYO NA PIA NAKUASA MWANGALIE SANA JAMAA AKO WENGI WENYE TABIA HIZO NI VICHECHE,MALAYA KOMA YAANI KAA NAO MBALI KABISA HIVO HUFICHA MAMBO YAO KWA KUTUMIA WIVU.
SHOSTISHO WA MBAGALA ZAITUNI

Anonymous said...

Dada mi nakushauri uwe mvumilivu nae coz ni mambo madogo tu ayo katika suala zima la mapenzi then ukiangalia umeshakaa nae sana , itakua ajabu ukimuacha kwa sababu iyo tu ndogo !
Cha msingi ni kujaribu kuepuka kufanya kile ambacho kitamkwaza coz kama ni kumsoma umeshamsoma.

Anonymous said...

NDO MAISHA HAYO, DADA WEWE FANYA YALIYO SAHIHI.KUNUNA KWA VITU VIDOGO INAWEZEKANA NDO ALIVYOKUZWA KWAO, HUWEZI MMBADILISHA SASA.UKIKWAZIKA MWELEZE.SIKU NJEMA

Anonymous said...

Wee ni mwanamke mkubwa sasa na unatakiwa ujue unachotaka. Kama unajua ukikosea huwa nanuna basi usikosee!! Hao wanaokupia simu/sms akina nani? lazima kuna sababu, kama ni minjemba basi uchague moja wao au yeye!! Mapenzi bila wivu sio mapenzi. Hebu nikuulize ivi huyo jamaa yako angekukuta umeshikwa tako na mwanaume mwingine halafu akakaa kimya asikuulize chochote ungesemaje?
au yeye akitumiwa msm/simu na wanawake unatajisikiaje? kama simu/sms sio za mapenzi uwe unashea nae kwani vipi? si mnakua mwili mmoja, mtiana, mnanyonyana n.k. sijui kama kuna siri zaidi ya hayo. Kama unataka maisha ya furaha na ndoa yako jirekebishe, uishi maisha ya mke wa mtu na sio kama ya mwanamke ambaye bado anatafuta soko!!

Mdau M2

Anonymous said...

Dada!

Naomba nikukumbushe kwamba umeamua kuishi na huyo mwenzako! Kitu kikubwa ni kwamba lazima uvumilie tabia ya mwenzako,kama unampenda na ukakubali kuishi naye basi ndivyo alivyo.Vilevile lazime unikubalie kwamba naye haridhiki na tabia yako anakerwa lakini anajaribu kuvumilia. Ukweli ni kwamba hawezi kuwa unavyotaka hata kidogo, na pia huwezi kuwa anavyotaka.NDOA NI KUVUMILIANA! Kazi unayo dada yangu, Pole sana!

Anonymous said...

Shosti pole ila fahamu kwamba siku hizi tumeingiliwa na jinamizi gani sijui kwa wanaume, sio wewe tu unayekumbana na hilo tupo wengi yani mambo mengine hata wewe mwenyewe unakuwa hujui baadae unasikia anakwambia ahh mi nilinuna sababu uliniboa ukimuuliza kwa lipi mwenyewe anaona aibu hata kusema, wanaume wamejaa utoto utoto unaokera na wengine ni malezi tu mabaya sasa ukimwambia mbona unabehave kama mwanamke anakuja juu lakini ndio ukweli wenyewe roho zao nyepesi nakuna nuna juu kwa kweli inabore sana ila fanya kitu kimoja mie kimenisaidia. Akinuna we jifanye hujui kama ndo umenuniwa muongeleshe wala usimjali kumuuliza uliza na kumbembeleza jifanye hujui kama ndo kanuna, Tena huyo asiyetaka uongee na simu akinuna weka vocha piga simu kwa shosti ongea ucheke mpaka ugale ugale ataongea tu. Kwani wengi wenye tabia hiyo huwa hawapendi ufurahi wala hataki uwe na raha mtoto wa kike yeye huridhika kila siku ukikaa na majonzi/simamanzi ahh ndo raha yake anakushusha confidence ili ujione takataka. Kataa hii ni aina nyingine ya domestic violence tena inatoka kwa zimwi likujualo....

Anonymous said...

MIE NAKUSHAURI HIVI

KWANZA BADIRISHA LINE YA SIMU INAWEZEKANA BADO KUNA WATU AMBAO WANAKUTOGONGOZA SANA KUPITIA SIMU YAKO.

USIPENDE KUMPA KILA MTU NAMBA YAKO YA SIMU KUNA WATU WENGINE WANAPENDA SANA KUBOMOA KULIKO KUJENGA.

MAANA INAWEZEKANA KUNA SIMU ZA UTATANISHI AMBAZO UNAPIGIWA UNASHINDWA KUZIJIBU VIZURI UKIWA NA MCHUMBA YAKO HUYO.


MWAMBIE KILA KITU CHAKO CHA KUHUSU UHUSIANO WA ZAMANI HUYO MCHUMBA WAKO USIMFICHE KITU.

MSIKILIZE ANACHOKUELEZA NA USIPENDE KUWA MBISHI WA KILA KITU AU KUJUA KILA KITU HAPO LAZIMA ATAKUTILIA MASHAKA TU.

NI HAYO TU.

NI MTAZAMO TU WAPENDWA.

Anonymous said...

Jamani...Anony wa 4:33:00 PM umenikuna haswaa, mimi pia nna mchumba wangu....yani jamani inasikitisha, mimi ni very outgoing person,mwenzangu sio sana, sipigiwi simu usiku,siongei na simu usiku,si-chat ivyo na watu,ila unaweza kushangaa mtu kanuna tu, asa najiuliza...ni vipi....?..ukimuuliza,anasema hamna,mbona nipo normal tu...mimi nakerrrrrrrrrrreka to the maximum....na yeye anaweza sana kununa,hata siku 4-5,haongei jamani,i think ni tabia ya kike. hapa napoandika,kanuna!!,tangu jana...yani nimefikiria weee nimefanya nini hamna nililofanya ambalo juzi sikufanya,hata mimi naona its a way of putting us down, anaona nikiwa na raha kwa zaidi ya wiki ntafwaidi sijui...i dont know....na mimi nimeamua kukaa kimya, tuone mwisho itakuwa wapi coz kila siku wewe ku-assume lawama hata kama huzijui ni ujinga sasa,maana nnakuwa mwanamke kupita kiasi....nitawapa feedback, na mimi nakaa kimya sasa,na leo nalala kwanguuuuuuu.

Anonymous said...

Kuna dakitari mmoja aliniambia kuwa kila kitu kina dawa yake, dawa ya njaa ni kula, dawa ya usingizi ni kulala, dawa ya KUNUNA ni KUCHEKA.
Kwahiyo akina mama ambao yanawakuta hayo, tafuteni njia ya kuondoa huo ugonjwa. Kukaa kimya nakudharau kutazidisha nakuleta mengine. Ujue huyo ni mume wako, na kinachomuumiza yeye hata ukae kimya lazima kitakuathiri kindani-ndani, `kwanini kwanini' huko kujiuliza kunajenga `presha'
Najua wengine watasema kwanini kumdekeza, unampa kichwa nk. Hapana, huyo ni mtu wako, na ni mtu mzima, utakavyomtendea mema(yale anayoyataka), itafika muda na yeye atajiuliza na kujiona amekosa. Na hapo ndipo pakuelezana ukweli(unajua mume wangu hivi na vile bla-bla, nakupenda, ningependa iwe hivi, dume hoi. Jamani siri ya wanaume ni ndogo, lakini mnashindwa kuitumia. Acheni kutegeana au kuwekeana visasi).
Mimi ni hayo tena
emu-three

Anonymous said...

pole kwa hali hiyo iliyokukuta.
me ni mwanaume naishi na mchumba angu but sikai san nyumbani bse ya kazi za site.naweza kukosekana home kwa mda hata wa mwezi mzima.sasa basi ukirudi home we unakuja na hamu na mke na umepamiss home ila unakuta mke yale maneno alokua anyazungumza kwa simu kwamba ur missing here honey hayana ukweli wowote yani ni WORDS WITHOUT MEANING,
anarudi kutoka kazini ye ndo kwanza anaanza kuchat ukiuliza we vp? majibu ooh hawa ni mashoga zangu tulikua nao kazini ndo nachat nao!
mwanamke hana mda wa kukaa nawewe MKAPANGA HATA MIPANGO YA KESHO NA KESHOKUTWA full yuko busy na simu kama mwanafunzi alonunuliwa simu jana.tukisema ooh mwanaume una gubu,me ananikera n.k.Asikwambie mtu LAZIMA UHESHIMU UWEPO WA MUME HOME.
If you think anakukera na umeshinda kulitatua hili, pls dont go for marriage itakusumbua sana bse utakua huaminiki hata kidogo bse alishaanza kukutilia shaka toka mwanzo ama show/prove to him kwamba simu yako si kwa ajili ya kumcheat ili awe na amani, akuamini hata kama ukiongea na simu ajue ni mambo ya Amani kwa ndoa yake.
Be a woman to your husband not a competitor kama vile ni mke mwenza.
Anonymous wa 12:01:00 AM i like your comments.

Anonymous said...

Dada mleta mada, leo ni mara yangu ya kwanza kuchangia humu ninaomba nikueleze kitu kimoja. Kama unaumia sana na minuno ya mchumba wako mweleze na asipobadilika USIFANYE KOSA LA KUOANA NAYE- Hao wanaokwambia uvumilie dada ukishaingia ndoani ni wewe wa kulibeba zigo hilo. Ninaongea kutokana na uzoefu dada wangu mie nadhani anaongoza kwa kununa, kunihisi vibaya, kunidhania dhana mbovu, jeuri, kiburi, dharau na mbaya zaidi wivu uliopitiliza. Wangu mie ananuna mwezi, mwezi na nusu. Na akinuna hata kama mama mkwe wake kaja hatocheka hadi watu wanamwogopa. YAani ninakereka na hadi ninachoka cha moto ninakiona. Shost kama una roho ndogo usifunge hiyo ndoa nakwambia utajajuta!

Anonymous said...

Hicho kimeo dada wanaume wa kweli huwa hawanuni, akikuoa itakuwa disaster, kama moyo wako umeanza kusita tupa baharini atakusumbua maisha yako yote kama mimi, kama inakunyima furaha kwanini uishi bila furaha? uamuzi ni wako