Saturday, 27 June 2009

Mume Cheated, sasa anadai tupeane nafasi-Ushauri

"Hi, wadau mwenzenu nina shida, mnajua toka mume wangu acheat wakati nina mimba, sijamsamehe. Tunaongea vizuri na tunalea familia vizuri, ila tatizo nikikumbuka maudhi ya mume wangu basi naacha huduma zote na chumba nahama.

Nakaa hata wiki then tunaongea narudi, najaribu kumsamehe na kusahau nashindwa, nakuwa jeuri sana siwajibiki chochote kuhusu mume. Na hii jeuri inakuwepo muda mwingi zaidi kuliko amani.

Sasa eti kaja na solution, eti we need space from each other so mimi nirudi kwetu kwa atleast 3 weeks or 1 month.. Nikamwambia "mie siendi popote coz siwezi kuacha watoto wangu na I dont need any space. Kama he needs hata yeye ana kwao aende tu. Mi mi kama nitaondoka ni 4 good na naondoka na TALAKA yangu mkononi". Akasema hatuachani ila tunarekebishana. Hapo wadau nisaidieni kuna cha kurekebishana au ana yake?"

Dinah anasema:Pole sana Mdada kwa unayokabiliana nayo, watu hawaelewi ni namna gani kuwa cheated on inauma na ni ngumu kiasi gani kusahau. Unaweza kusamehe vema kabisa , well ukadhani umesamehe (huwezi kusamehe kama huwezi kusahau) na ukawa unazungumza na mumeo lakini uhusiano wenu ninyi wawili hautakuwa the same again unless huyo aliyekosa (kwa case yako Mumeo) afanye kazi ya ziada ili wewe uweze kumuamini tena na hatimae kusahau aliyokutenda......hebu bofya hapa kwa maelezo ambayo yanaweza kukusaidia kiasi fulani.

Sio kwamba unakiburi bali unahasira kutokana na kitendo chake kichafu na hujafanikiwa kusamehe kama ulivyodai mwenyewe kitu ambacho kinaongeza ugumu zaidi kwenye kusahau na kuganga ya mbele. Ingekuwa yeye ndio katendwa yaani kama wewe ndio ungekuwa ume-cheat on him sidhani kama angekuwa na wewe by this time.....angekutwanga TALAKA siku hiyo hiyo.

Nimekutana na watu wachache wenye tatizo kama lako na niliwasaidia na wakafanikiwa na sasa wako pamoja wakiendelea na ndoa zao, na huko ndiko nilikopatia uzoefu na hivyo kujiamini ktk kulielezea hili suala la cheating.

Kwa mtu ambae hajawahi kukutwa na tatizo hili ningumu sana kwake kujua ugumu na maumivu yake na hivyo kudhani kuwa wewe unakiburi tu na unachezea shilingi chooni, lakini ukweli unabaki pale pale kuwa, unampenda mumeo, unataka sana kuendelea kuwa kwenye ndoa lakini hujui how to 4get and move on, kwasababu 1)-huji kwanini alifanya hivyo(cheat), 2)-Je umenusurika dhini ya maambukizo? 3)- Kwanini yeye hana habari na anachukulia kawaida (kwa vile hajaomba msamaha) na maswali mengine lundo.

Wewe kuwa mjamzito ni moja ya sababu kati ya zile nyingi ambazo wanaume huzitumia kama sababu kwa nini hutereza nje a.k.a cheat,.

Tatizo lililopo hivi sasa si yeye ku-cheat japokuwa ndio sababu, ninachokiona hapo ni mume wako kuwa na Majivuno (proud of himself) kwa vile tu yeye ni mwanaume na wewe kuwa needy na muoga kudai haki yako. Kingine ni ukosefu wa maswalisiliano baina yenu.

Mwanaume yeyote ambae hana majivuno na anathamini ndoa yake hawezi kukaa ziku zote hizo bila kuomba msamaha kuhusiana na tabia yake chafu, unless huna uhakika na unahisi tu kitu ambacho kitakufanya ushindwe kuwakilisha hoja.

Kama mgewasiliana kuhusu tukio lililotokea wakati wewe mjamzito na unauhakika kweli alikusaliti ni wazi kuwa angeomba msamaha na kuahidi kuacha hiyo tabia na kubadilika kuwa a loving hubby kwako na a great father kwa watoto wenu.

Cheating sio kitu kizuri na ni sawasawa kabisa na yule muuaji(inategemea na reaction ya mhusika), lakini haina maana kuwa ndio mwisho wa ndoa yenu au mwisho wa uhusiano wenu. Inawezekana kabisa kutokana na tukio hilo mkawa the best couple (am not asking u to cheat on ur lover ili kuwa best...hapana), ila kwa bahati mbaya ikitokea na uko kwenye ndoa kuna hatua za kufuata na kuna njia ya kukabiliana na hilo.

Nini cha kufanya:Kwanza kabisa unatakiwa kujua umesimama wapi na unataka nini out of ndoa yako?
1)- Je unampenda mumeo na ungependa ku-work things aout na mumeo ili ndoa iendelee kuwepo na iwe yenye amani na upendo?(Kuna mengi ya kufanyia kazi ili kufanikisha hilo)

2)-Je Penzi limepauka/chujuka ila unamheshimukwa vile ni baba wa watoto wenu na unahofia watoto wenu wasilelewe na mzazi mmoja ikiwa utatoka ndoani?(Mkiweka mipangilio mizuri watoto watalelewa na ninyi wote, lakini kujilazimisha kukaa kwenye ndoa wakati huna furaha sio afya kwako)

3)-Unahitaji muda zaidi kuponyeka kabla hujafanya uamuzi wa busara? (hapa utahitaji kutengana nae kwa muda ili ku-sort our ur feelings and ur head).

Sasa kutokana na kitendo chake cha kukusaliti unadhani kuwa ukiondoka na kwenda nyumbani yeye atahamishia makazi kwa huyo mwanamke mwingine si ndio? Vipi ikiwa yeye ataondoka nakukuacha hapo nyumbani? Unauhakikahuko aendako ni nyumbani kweli na je itakuwaje kama atabeba na huyo msaliti mwenzie kwenda huko wote? Mana'ke kuna nyumba za wageni na wanaweza kutumia.........

Sulihusho hapa ni kupeana nafasi (kama alivyodai mwenyewe) ili kuona kama kweli bado mnapendana na mnataka ndoa yenu iendelee kuwepo lakini kutokana na hali halisi ya uhusiano wenu itakuwa ngumu kwa vile wewe humuamini tena mumeo.

Mimi nashauri wote wawili msafiri na kwenda mahali ambako hakuna ndugu wala jamaa, mkakae hotelini na huko muende kujaribu kurekebisha mambo baina yenu, kitendo cha kukaa ninyi wawili pakeenu na kuwatumia muda wote pamoja kufanya mambo tofauti ya kufurahi (msihusihe ngono) itasaidia kujua hisia zenu na namna gani mnahitajiana ktk maisha yenu.

Pia itasaidia ninyi wawili kutaka kuzungumza kuhusu maisha yenu, kumbuka siku zote naamini kuwa mwanamke ndio mtu pekee anaweza kubomboa au kujenga ndoa yake......hivyo basi jukumu hili liko mikononi mwako kwahiyo ni wewe pekee ndio uko upande wa kulianzisha na kulizungumzia tatizo lililopo kwenye ndoa yenu hivi sasa.

Lakini je utamuanzaje ili akubali?-Ili kumpata kwanza kabisa muombe msamaha kwa kumtamkia Talaka na kubishia wazo lake la kutengana kwa muda. Mwambie kwa uwazi na kwa upole kuwa hudhani kama ni idea nzuri kutengana na unadhani kuwa mnahitaji kutumia muda mwingi peke yanu bila ndugu, watoto na marafiki ili kusort things out.

Sema kuwa, ikiwa yeye au wewe utasafiri na kuwa mbali mbali itaongeza matatizo badala ya kuyamaliza. Mueleze kuwa mnahitaji muda wa kutosha ili kuzungumza na kurudisha the romance kwenye ndoa yenu kwani unahisi imetoweka ghafla na unadhani inawezekana kabisa ni kutokana na vitendo vyako ambavyo unavifanya kutokana na sababu ambayo utamueleza muda ukifika (hii itampa hamu ya kutaka kujua), na kama kweli alikusaliti atang'amua then na kama hakukusaliti basi atasubiri au anaweza ku-demand umwambie....

Wewe usimwambie mpaka mtakapo safiri nje ya mji au mkoa mwingine.....Kama mnaishi Tz basi Morogoro pale pametulia, Arusha pia kuzuri, Bagamoyo, Kigamboni kule kuna Hotel moja bomba kabisa kwa ajili ya kupumzikia mwisho wa wiki....lakini kuzuri kabisa nadhani ni kwenye Mbuga za wanyama kutokana na asilia ya nchi itawasaidia muwe na mood nzuri zaidi....


Weka wazi hisia zako zilizoumizwa ili mumeo aelewe kuwa bado linakuuma na huwezi kabisaa kusahau (ikiwa unauhakika na usaliti wake). Unajitahidi kusamehe lakini msamaha haukamiliki ikiwa yeye mumeo hajakubali kuwa alikosa na kukuomba msamaha.....kama mwanamke natambua unafanya vyote hivyo kwa kudhani kuwa yeye mumeo atang'amua unataka nini kutoka kwake.

Kwa bahati mbaya hawezi kusoma via vitendo vyako wala hawezi kujua yaliyokichwani mwako isipokuwa pale utakapoamua kuliweka wazi ktk mtindo wa kuwasiliana. Ukiendelea hivyo ataamua kwenda kutafuta amani sehemu nyingine na wewe utabaki unaumia even more.

Ikiwa hunauhakika na usaliti wake pia mueleze kuwa ulipokuwa mjamzito ulikuwa unahisi au kama uliambiwa bsi sema wazi kuwa kuna watu walikuambia kuwa mumeo anatoka na mtu fulani na tangu siku hiyo imani nae mumeo imekutoka na hunashindwa kumuamini tena.

Kama akikana kutokana na tuhuma hizo (ikiwa huna uhakika) then inabidi kuwekeana rules kama inawezekana ili kukuongezea au kukurudishia wewe ile hali ya uaminifu juu yake mume(kwamba uanze kumuamini tena).

Ndoa ni ngumu sana kama hakuna mawasiliano ya kutosha au hujui namna ya kuwasiliana na mwenza wako, ndoa ni ngumu kama hakuna uaminifu baina yenu, ndoa ni ngumu kama hakuna maelewano wala masikilizano, ndoa inaweza kuwa ndoano kama hakuna amani ndani ya nyumba yenu.

Ndoa ni our third job kwa wale wote wenye kazi, watoto na waume/wake pia ni our second job kwa wale wote ambao bado hamjazaa lakini mna wake/waume na kazi. Hivyo tukitaka ndoa zetu ziwe Imara, bora, nzuri, zenye furaha na amani hatuna budi kuwajibika na kuzifanyia kazi kila siku iendayo kwa Mungu kama vile unavyokwenda kazini kila siku ili kulipwa mshahara lakini tofauti ya ndoa ni kuwa haina mwisho wa wiki wala likizo ila malipo yake ni zaidi ya Mshahara ikiwa utawajibika vema.

Nakutakia kila la kheri ktk kurudisha ndoa yake kwenye track kama kweli unataka kuendelea kuwa ndani yake.

Ubarikiwe!

12 comments:

Anonymous said...

Pole sana dear, ni kweli kucheatiana inauma sana ila kama mwenzio alikuomba radhi na hukua na ushahidi zaid ya kushuku au kukamata kitu basi msamehe na usahau yaliopita kwani inaonyesha unampenda sana mume wako nae anakupenda ndio umevumilia kwa hiyo jitahidi sana kufikiria mazuri aliokutendea kuliko kufikiria mabaya hasa ya kucheat utajiumiza na kutesa watoto wenu! Believe me watoto ni wazee wao tu baba na mama na mkiachana watoto ndio mtawapa tabu! wahurunieni watoto wasiokua na makosa msiwatese!

Huo ushauri wa kuwa mbali ili mkumbukane na kusaha yaliopita siyo mbaya na pia kupatanishwa yaani kusevu problem lakini ndugu yangu dunia ya leo usiondoke ukaacha nyumba yako ujue unampisha mwenzio na mimi siamini sana dunia hii mwenzio akishakuingilia nyumbani kwako kwanza kabisa anakutilia nuksi katika nyumba yako ya machafu yake!

Kwa hiyo mimi nakuunga mkono kama unavyosema kama anataka break yeye ndio aondoke na uhakikishe ni kweli anaenda kwao na siyo kwingine!

Ila cha muhimu jaribu kumsamehe mwambie mimi nimekwishakusamehe haina haja ya kukaa mbali na onyesha kuwa unampenda na tafadhali ondoa kinyogo nae pia acha visa ujue kuwa unaharibu siyo kutengeneza

Ni mimi Salha

Unaweza kusoma yangu ya tarehe 18

Nipo navumilia na nimepata moyo kwa walionipa mashauri japo wengine wamenishauri nitoke lakini si unajua tena kupenda navumilia tu namuachia Mungu atakavyoamua ila nafurahia ushauri wa wengi pia nasubiri kwa hamu kuhusu Dinah majibu yake naona ni ngumu yangu lakini nina hope atanijibu vizuri.

Ndugu yangu kwenye ndoa au wapenzi kuna mambo mengi Mungu atusaidie!

Goodlucky

Salha

wahida shoo. said...

hapari yako shosti
pole sana ndugu kwa matatizo. naomba nikushauri kwamba usiende kwenu kaa ulee watoto wako. kwenye ndoa inaitaji uwe na msimamo wako shosti kama yeye anaitaji nafasi kwanini yeye asiende kwao aukuambie wewe ndio uwende. kwani wewe ndio mtu wakutangishwa
shosti nakupenda ukienda kwenu tu ukirudi utamkuta mwenzako kajaa ndani tele chamsingi lea watoto wako usimuwazie mwanaume ndio ukae ukijuka huyo hiyo ndio tabia yake usiumize akili yako pole sana mi naitwa wahida shoo.

Anonymous said...

Kumbe unajiongezea matatizo mwenyewe.tatizo haliko kwa mumewe hata kidogo.Nasema hivyo kwa sababu jambo lililotokea la cheating lilishaombewa msamaha.Sasa nini kuendelea na vizingiti vilivyopita?Huoni kama wewe ndiye unacheat sasa?Wengi wanadhani cheating ni katika mapenzi tu!! kumbe hata unapomtendea jeuri mwenzi wako ni the same thing as to have sex with another woman/man out of your marriage.

Unamtendea hivyo mumeo,na ndiyo maana anakuambia muepushane kidogo maana haoni faida ya kukaa na mtu anayefanya jeuri kama unayofanya.Kuna makosa mangapi umefanya wewe ameyavumilia?

Sasa unataka suluhisho gani hapa wakati wewe ndiye msababishaji mwenyewe,mbona jibu unalo.Kwa nini unazidi kuwaka hasira hivyo kiasi kwamba unataka kubomoa ndoa yako? Ungetuambia kuwa mumeo amerudia lile kosa,tungeelewa kitu hapo,Lakini sasa hujui kwamba utampa nafasi nyingine ya kutoka nje ya ndoa huyo mumeo?Halafu utalalama pasipo kuangalia kosa lako.

Kama wewe ni mkristo tafadhali sana muombe Mungu akusaidie kusamehe na kusahau.Hakuna kosa kama la kukumbuka mambo yaliyopita, tena uliyosamehe katika ndoa, vinginevyo hutakujajenga ndoa yako hata siku moja iwapo hata mumeo ataamua kukumbushia yale yote mabaya uliyomtendea.Please,please elewa kuwa unajichongea kaburi mwenyewe.Sahau kabisa mambo hayo.

Nimegundua kitu kingine kilichokukimbiza kuja tena hapa ni ile kauli aliokuambia mumeo kwamba muepukane kidogo.Hiyo ndiyo imekuwa mwiba mkubwa kwako.Mbaya zaidi hujui wewe ndiye unayasababisha yote hayo.Hii ni nafasi ya kutubu na wewe kwa mumeo kwa jeuri ulioendelea kumtendea.safisha mambo haraka acha kubangaiza mambo maktika ndoa.Elewa ile mihimili mnitatu katika ndoa" Samahani, pole,nakupenda.Hapo hakuna kulipizana visasi na kukumbuka yaliyopita.Ziba ufa utajenga ukuta usipokuwa mwangaalifu.

Nakutakia kila la heri katika kuinusuru ndoa yako.

mdau USA

GODE said...

forgive your husband.
usahau yaliyo pita
BY GODE

Anonymous said...

Habari gani?
Dada mbona moyo wako umekuwa mgumu hivyo? Ni mangapi umemkosea mumeo akakusamehe? Je una uhakika gani kama hutamkosea mumeo kosa kubwa ktk siku zote za maisha yako?. Hicho ni kipimo cha mapenzi yako kwake, ni ukweli dhahiri kwamba watu wanaopendana kwa dhati huwa wepesi kuombana msamaha na kusameheana.
Kumbuka ya kuwa msamehe mwenzako ili apate kushukuru, na kwa namna hiyo hiyo nawe utasamehewa!.
Ikiwa mumeo kaomba msamaha basi msamehe, kwani unayoyafanya sasa ni kumkosea mumeo na ni kuharibu ndoa yako kwa mikono yako mwenyewe. Kumbuka usemi usemao MWANAMKE MPUMBAVU HUIBOMOA NDOA YAKE KWA MIKONO YAKE MWENYEWE.
Tazama Mungu wetu anasamehe wabakaji, wezi, walawiti, lesbians, wauaji, wazinzi, wachawi, waongo, waliomdharau , watesaji,na waliokomit bestiality, wote hawa huwasamehe mara tu wanapomwomba msamaha kwa kumaanisha ili tupate kumshukuru!, Ni vip wewe mwenzangu unashindwa kumsamehe mwenzako aliejikwaa ktk moja, je wewe umejikwaa mangapi ktk hayo? Na je ungependa Mola wako asikusamehe? Basi nawe pia msamehe mumeo ili apate kushukuru! Nawewe pia omba msamaha ktk vurugu ulizomfanyia ktk kipindi chote hicho.
KUMBUKA SUBRA NA UVUMILIVU NI MUHIMU KTK NDOA! Ninyi si MALAIKA Mpaka msikoseane maisha yenu yote.
Mwatima

Anonymous said...

Ndugu yangu mie binafsi naona tatizo lipo zaidi upande wako ingawa mumeo ndio aliyekukosea hapo awali. Nadhani utakumbuka alikuomba msamaha na wewe kukubali kuwa umemsamehe. Sasa fujo unayofanya sasa hivi ya nini? Kama hukutaka kumsamehe, kwa nini ulikubali? Inaonyesha una chuki na kisasi dhidi yake. Hapo mrembo utakoroga mambo mwenyewe. Mie nakushauri uondoe chuki dhidi yake. Usifanye mambo kitoto. Fikiria ndoa yenu zaidi kuliko wewe mwenyewe. Hayo ndio majukumu yenyewe. Make sure you unalinda ndoa na sio kubomoa kwa vituko. Halafu kuhusu wewe kwenda kwenu mimi siafiki coz inaweza kuwa huyo mume amekuona huna muelekeo wa kubadilika au kumsamehe, sasa anatafuta jinsi ya kujitenga nawe. Na ukitoka tu, i guarantee waharibifu wataingia. Na wewe utasahaulika. Be a strong woman who can face any challenges. Stay with ur family and focus on positive thinking. Goodluck

Anonymous said...

Mama, unabomoa ndoa yako kwa kiburi chako, huwezi kumkomesha mwanaume hata siku moja, unajidanganya. Mwanamke unatakiwa kujishusha, by the way ameomba msamaha what else do u want? na unavyofanya hivyo ndo anazidi kukucheat. Jirekebishe haraka iwezekenavyo, omba msamaha kwa matabia mabaya yote uliyomfanyia then anza upya na ubehave kama mke. Wenzio wanazililia hizo ndoa wewe unachezea!

Anonymous said...

Kwani wewe unachotaka ni nini? maana haueleweki. unataka muachane au unataka muendelee kuishi? kama ni kuachana kwa kuwa mmeshazaa na mna watoto nakuashauri muondokane bila ugomvi. mueleze umeshindwa kusamehe na huna imani nae tena muachane.

kama unapanga kuendelea nae basi samehe muendelee kuishi huo utoto unaoufanya utakusababishia kupoteza hii fursa uliyonayo.

leo unahama wewe utafika wakati atakapokuchoka atahama yeye sio chumba tu kama unavyohama wewe bali nyumba kabisa.

wewe mwenyewe umeshakosea mara ngapi bado unajihukumu hadi leo au unahukumiwa hadi leo?

Na kwa tabia hiyo unayomfanyia huoni kuwa wewe ndo chanzo cha yeye kucheat? nakushauri uache utoto.

Anonymous said...

7Pole sana. Kwanini unashindwa kusamehe? Kwani mwanao akikunyea mkononiutaukata mkono uutupe? au utauosha uendelee na maisha? Ni sawa na mumeo pia. Keshafanya kosa na kaomba msamaha. Msamehe yaishe na muanze upya. Jeuri haijengi daima inabomoa.
Kuhusu kwenda kwenu usiende. Aende yeye aone kama itasaidia. Niaminivyo mimi ni kwamba 'Tabia uliyonayo wewe au yeye ni tabia mlizotoka nazo kwenu na makuzi yenu* Kwenda nyumbani hakukufanyi ukapate tabia mpya au ukajifunze tabia mpya. *Mizigo huwa inafungwa mara 1 tu na ni siku ya kuhamia kwa mumeo kwa sisi waafrika. Unless kama umeolewa ulaya au USA talaka ni nje nje. Kama ni bongo Ng'ang'ana

Anonymous said...

Asanteni sana kwa ushauri wenu nashukuru, ila naomba niwaulize nyie aliewaambia mie huyo mume kaniomba msamaha kutokana na midudu yake n i nani???? hajawahi kuomba msamaha ni mei tuu nimeamua kujisahaulisha lakini nikikumbuka na nikiwaza kwanini hakutubu ndio hapo ninapoona nadharaulika ndio maana nakuwa hivyo, so nyie mnaonilaumu eti niliomwa msamaha naomba niwaambie SIKUOMBWA MSAMAHA

Anonymous said...

Kumfuma mwenzako akivunja amri ya ndoa inauma, mtu asikueleze, hasa ndio umkute katika kumalizia, weweee... unaweza ukaua, sembuse kuhisi tu. Hili swala ni nyeti ndio maana kiimani za kidini kwa wale waliobobea wanasema hapohapo umeshavunja ndoa. Sijui utaijengaje!
Lakini je wewe umsafi kiasi kwamba hujawahi kuvunja amri za ndoa? Kama umsafi mshukuru mungu na ni vyema ukaenda kwa kiongozi wako wa dini ukaomba ushauri zaidi.
Lakini kwa tahadhari kama utamkuta kiongozi wa dini ambaye naye yamemfika yakibindamu, maana haya yanaweza yakamtokea yoyote kutokana na udhaifu wetu, huyo anaweza akakushauri kama wengi tulivyokushauri hapo juu, lakini kama utamkuta yule ambaye imani imemkaa, oooh, sijui kama ndoa ipo!
Lakini tujiangalie wenyewe, usafi wetu, je kweli hatujawahi kufanya kosa ambalo linaweza likaendana na hilo. Kwasababu sio ngono peke yake inayoweza kuvunja ndoa, yapo mengine nafikiri wataalamu munaweza kutusaidia kwa hilo. Basi inapofikia hapo inabidi tufumbe macho tuseme yaliyopita si ndwele tugange yajayo, tu-sa-me-he-ane ja-mani. Ingawaje kwakweli ni ngumu na ngumu kumsamehe aliyechezea mali yako. Ni mali yako kwasababu mumeambiwa yeye ni wako na wewe ni wake!
Linapotokea lakutokea, mungu atuepushie mbali, kwanza ni vyema kama tunataka tusameheane tuangalie `ni kwanini mpaka mwenzangu aamue kufanya hivyo' zipo sababu ukichunguza vizuri, tabia ya mtu au udhaifu wetu wenyewe!
Mhh, naogopa kusema zaidi, nafikiri dada Dinah, keshamaliza kila kitu
emu-three

Anonymous said...

Kwanza kabisa pole kwa kuchitiwa lakini mbona sijaona sehem uliozungumzia kuwa alikucheat wakati una mimba?Je uliwahi kuandika na ni lini ili tukipitie kisa chako vizuri.Kama hujawahi kukiandika je alikucheat vipi na vipi ulijua na una ushahidi gani?

Halafu kama tu unahisi na huna ushahidi mimi nakushauri bora uiache hiyo issue ya kutka msamaha kwangu mimi ni kuwa unataka akuhakikishie kuwa kweli katombana na mwanamke mwenzio sijui wewe mwenzangu lakini mimi ingeniuma zaidi pindi anihakikishie kuliko kuhisi! Kuomba samahani ni kukubali kosa alilofanya ambalo siyo dogo!

Ngoja nikupe mfano mwenzio mume wangu aliambiwa tu maneno ya uongo na marafiki zake kuhus mie na siyo kucheat ni kumsema vibaya mume wangu kwa mambo yasiyo ya muhim!Mimi nilijaribu kumwambia ni fitina lakini mwenzangu hakubadilika sasa ikabidi mie nikubali makosa na kuomba samahani kumbe ndio nimeharibu ni kama vile nimehakikisha kuwa kweli nimesema!

Unaona hapo hadi leo hatusemi vizuri mtu na mke na pia tuna mtoto sasa hata mtoto wake hamjali
unajua ndugu yangu wengi tunaojali watoto ni wanawake kwa vile wametoka matumboni kwetu lakini wanaume wanajua wanaweza kumpata mwanamke yoyote na akampatia watoto kama siye so huwa hawajali sana kuhusu watoto ndio maana tunakshauri usamehe tu na kufungua kitabu kipya kuliko kukazania kuombwa samahani ya kukuhakikishia kuwa wewe kuwa una mimba yake baada ya kukuenzi zaidi kwa ajili ya mtoto wake amekuponda na kumtafuta mwingine mwenye kuma ya Almasi inaechezewa na wenzake pia kuliko yako ambayo ni kama yake peke yake!

Wengi hawajui kwa nini umeumia ni kuwa watu wengi wanaumia kuhusu kitu ni kuwa wao wanajiamini kuwa hawacheat wenzi wao ndio maana imekuuma na mambo mengine wanayosema ni mambo ya kawaida kucheat ni kungonoka kwingine kinyume na mpenzi wako!

So mimi nakushauri kama bado unampenda mumeo samehe na achana na kutaka akuombe radhi kwanza kuna mijanadume mingine imeumbwa haijui kabisa kuomba samahani na mingine ukimkosea wewe na kumuomba samahani hapo ndio utakua umejiponza ni bora uache tu maisha muhim yanakwenda!Maji umeshayavulia nguo huna budi kuyakoga means mmeshaowana na mna mtoto so wewe vumilia tu ulee mtoto wako na madam hakurudia tena kwani wengine hawajui kabisa kuomba samahani na siyo kuomba samahani ndio muhim ni angalau akatae na kukuelekeza pia kukuliwaza hadi usahau kama ni just feelings zako tu ajue ni kweli unampenda na umeumia na kuhisi tu amefanya so akuhakikishie kuwa mimi siwezi kufanya kitu kama hicho kwani nimekosa nini kwako na kuongea na maneno mazuri.

Kama hafanyi hivyo mmeo ni type za ile midume yenye dharau, kibri na kujithamini wenyewe bila kujali feeling zako pole dear na vumilia pia sahau kuhusu samahani kabisa utazidi kuumia!

Pole na take it easy na mjali na kumpenda mwanao na yeye umchukulie tu kama alivyo ila visa bora acha kwani mijitu ya hivyo ndio itaona kero na kukupa wewe hila ili apate sababu ya kutafuta mwingine ndio maana badala ya kukusemesha vizuri amekwambia nipishe maana sasa anakuonea kero!!!Wanaume wee acha tu Mungu atupe moyo mgumu tuweze kuyamudu maisha yetu.

MotherQueen