Tuesday, 22 April 2008

"Cheating" inaweza kuokoa uhusiano wako.


Umegundua kuwa mpenzi/mumeo/mkeo anatoka nje ya uhusiano wenu au yeye mwenyewe kaamua kusema kuwa hilo ndilo lililokuwa likitokea aukuendelea, unapanic, inakuuma, unakasirika, unalia, unamfokea na kuhoji maswali lukuki kwanini aruhusu hilo kutokea, kitu gani unakosa kwake mpaka ukatafute huko na hata kusema kuwa yule ananini ambacho wewe huna?

Hahahaha wakati mwingine huwa na-miss kugombana na mpenzi ni afya ujue ila sikutumi uka-cheat ili uongeze afya kwenye uhusiano wako.

Kwa kawaida hili huwa linasabaishwa na mambo mengi ambayo nimeshawahi kugusia ktk makala za nyuma na kwa bahati mbaya huwa halitokei mbali au niseme na mtu ambae humjui kabisa mara nyingi huwa ni mtu wa karibu kwa maana huwa unamuona mara kwa mara, kama vile maeneo ya kazini, baa, Salon, dukani/sokoni, mfanya kazi mwenzio.


Mimi binafsi naamini kuwa hili linapotokea huwa kuna na sababu ya msingi kabisa kwa nini mmoja wenu kaamua kwenda nje nasema hivyo kwa vile naamini ktk mapenzi ya kweli na ya dhati, na imani yangu hunifanya nijue wazi kuwa hilo haliwezekani unless kuna mapungufu fulani kati yangu na mpenzi (sio upande mmoja).



Lakini kwa bahati mbaya au niseme kwa kibinaadamu hili linapotokea wengi huchukulia tofauti na kujaza lawama wa yule aliyefanya kosa na hatujiulizi wenyewe kwanini ameamua kufanya hivyo towards me.


Baadhi huamua kwenda kuwaadhibu wale waliohusika na tukio zima the other woman/man kitu ambacho mimi sidhani kuwa ni busara.
Natambua hili jambo huwa linauma sana na kukufanya upoteze ile hali ya kumuamini mwenzio japo kuwa unampenda........upendo hauna maana ikiwa hakuna uaminifi, kwambahuwezi kupenda mwenzio kwa asilimia zote wakati huna imani nae tena kutokana na kosa alilofanya.


Najua kuwa kuna baadhi ya watu wanaamini kuwa wapo watu wameumbwa hivyo kwamba hata ufanye nini watatoka nje tu, ktk hali halisi hilo halipo japokuwa kuna matatizo ya kiakili (Manic Depression a.k.a Bipolar) ambayo yanaweza kumfanya mtu kufanya vitu vya ajabu ikiwa ni pamoja na kufanya ngono ovyo bila yeye kujijua yaani haamui kuwa sasa naenda kulala na fulani bali anajikuta anavutiwa na mtu nakutaka kufanya nae ngono on spot na atafanya hivyo......well hili ni tatizo la kiakili ambalo ni la kurithi na watu wachache sana wanalo.


“Cheating” imegawanyika, kuna wale wanaoafanya hivyo ili kuwa na mpenzi wa pili wa kudumu, kuna wale wanafanya hivyo ili kujaribu kupata mambo fulani ambayo hawayapati kwa wapenzi wao(hii huwa kwa muda mrefu) na kuna wale wanaofanya hivyo kwa bahati mbaya kwa vile kalewa, kashindwa kujizuia baada yakushawishiwa au alikuwa “high” kutokana na matatizo ya kiakili kama nilivyosema hapo juu.


Ni wazi kuwa hili linapotokea uamuzi wa kwanza kabisa na haraka ni kuachana na mpenzi wako, Lakini je unaweza kuendelea kuishi na mpenzi wako? Je utaweza kumuamini tena? Utaanzaje kufanya nae mapenzi? Itakuwa kama zamani au itabadilika n.k.

Pssst: Mpenzi anaekili kuwa ka-cheat mara nyingi huwa na mapenzi ya dhati, anajuati akosa lake na pia anaumia kama unavyoumia wewe au pengine zaidi kwa kile alichokifanya na uwezekano wa yeye kurudia kosa ni mdogo sana kwa vile hatotaka kuumua au kukuumiza tena na that's love! Lakini yule anaeficha mpaka umekujakugundua affair imekuwepo kwa zaidi ya miezi kadhaa au miaka hana tofauti na muuaji na ni wazi kabisa hana mapenzi ya dhati na wewe......

Endele akuwepo, nitakapo rudi nitakupa maelezo na mbinu za ku-cope na hilo na vilevile nitagusia kilichokuwa kikifanyika miaka ya akina bibi kwani cheting sio kitu cha karne hii. Usicheze mbali.

9 Wamechangia Mada, bonyeza hapa kwa mchango wako.:

Anonymous said...

Dina unataka kusema nini?
Umeongea na umenigusa kweli dear. Imenitokea, sasa ukisema afya una maana gani? Kwenye mada hii unataka kusema nini? Tafadhali naomba ufafanue. Maana mimi nimepoteza kabisa imani na mpenzi wangu baada ya kugundua hilo na kuhoji sana, nilimuuliza maswali yasiyo na mwisho. Unajua tena ubinadamu kusamehe kazi kweli, imennichukua muda kweli na machozi mengi. Bahati nzuri tu sikupata hasira ya kumfokea. Iliniuma sana. Fafanua mada yako na utusaidie waathirika wa hili tafadhali.

Dinah said...

Nina mengi ya kusema kuhusu hili Anony @5:53:00 PM, nimesema Cheating can make ur relationship stronger sio kwamba always break it.

Huchukua muda mrefu sana lakini at the end baadhi yetu huwa tunajitahidi kusamehe lakini huwa tunasota kwenye kusahau.

Niliwahi kusema kwenye forum moja hivi kuwa mwanaume anapo-cheat wewe mwanamke/mke unatakiwa kujiangalia na kutafuta sababu kwanini hilo limetokea hali kadhalika mwanaume/mume anapaswa kutafuta nini hasa kimemfanya mpenzi wake afanye kilichofanyika.

Endelea kuwepo unaweza ukapata moja au mbili, kama vipi unaweza kuniandikia ili nikupe ushauri as an individual kwani cases zinatofautiana.....sijisifu lakini nimesaidia wengi.

Karibu sana.

Anonymous said...

Naweza nikasema katika vitu vinavyouma katika ndoa ni `kufumaniana’. Ni heri kusikia na ikaishia hivyohivyo kuliko umuone jamaa live na mkeo au na mumeo. Nafikiri tukio hilo halitaondoka haraka kichwani.
Nikuambia kitu dada Dinah, sisi binadamu tuna asili ya `uchoyo’ au niite `ubinafsi’ hii ni hulka, na ni wachache sana wanaojaribu kuikwepa, lakini huwa ni vigumu sana. Ingetakiwa kila kitu unapotaka kukifanya unaangalia `kama ingelikuwa wewe umefanyiwa hivyo ungejisikia-aje’. Uwe mkweli katika maamuzi, sio ile kutamka tu, uwe unaagalia yale maumivu unayopata ukifanyiwa. Je ni wangapi wanaoweza kufanya hivyo tuwe wakweli! Jibu ni hakuna…mara nyingi tunaweka `ubinafsi’ mbele.
Wapo jamaa zangu wa karibu wameoa wake wawili, wawili. Maongezi mitaani ni ya kuwashutumu hawa jamaa kuwa wana tamaa. `Wanaendekeza tama za kimwili tu’ na maneno kama hayo. Hebu jaribu kuwatembelea hawa jamaa ili ujue ni kwanini walifikia uamuzi huo, jaribu pia kufikiria hali ya mke wa kwanza ilivyokuwa, na je aliridhia kuletewa mke mweza? Jibu ni kwamba hakuridhia, kwani ni mmoja kwa bahati anayeweza kuridhia tendo hili la uke wenza. Kwasababu gani `ubinafsi’ Je ni kwanini huyu bwana akaamua kuoa mke wa pili? `asilimia kubwa ni `ubinafsi’
Yupo mmoja katika maongezi alisema `huo ndio mfumo dume’. Mwingine akasema ni aheri kwasababu wake tupo wengi, kama wanaume wataoa mke mmoja mmoja wengine wataolewa na nani…
Katika hali kama hii mjadala unaweza ukawa mrefu, lakini tunashindwa kukiri kuwa `hulka yetu ni ubinafsi’ Kama tungeliweza kujimudu, tukawa wakweli tukakaa na kujadili kila kipengele kwa umoja, `ni nini walakini’ ‘je tunahitaji mwenza’ `kwani imekuwa hivi…
Yupo jamaa na mke wake waliishi miaka mingi, katika kuishi kwao wakajihisi kuwa hawaridhishani tena, sababu hasa ikawa haijulikani. Walikaa kikao cha busara, nakujiuliza kulikoni. Mume akatoa wazo, labda nikuletee mwenza ili asaidie hili,…mke akatahayari, akasema na mimi je, nimlete bwana akusaidie… jamaa akakasirika na kuja juu, haiwezekani.
Well, kwasababu walikuwa watu wazima na busara zao, wakasema ili tuhakikishe kuwa tatizo hili lipo wapi tutoke nje ya ndoa(kwa kukubaliana), wewe kwa wakati wako tafuta bwana na mini nitafute bibi…tufanye mara moja tu halafu tukutane tena. Kama kweli tutaridhika basi tutagundua kuwa tuna walakini fulani.
Zoezi likafanyika, na bahati kila mmoja alimpata mjuzi. Walichokipata hawakuamini. `kumbe kuna utamu wa namna hii’.Unajua walipokutana walisemaje? Kila mmoja alificha kueleza ukweli. Na matokeo yake ikawa `kudanganyana’ Leo nitapitia kwa mjomba, leo kuna harusi, leo nitachelewa kazini, kumbe ni kulekule kwenye `utamu’ ….
Wandugu wapendwa, hali ya `mahusiano ni nyeti’ mjadala wake ni mpana, na `ufundi’ au `usanii’ wake ni muhimu sana, tuongee tusione soo. Wengi tunabeza na kuliona ni swala la uficho(mambo ya siri), hata kwa mke na mume ambao wameamuriwa kuwa kila mmoja ni vazi kwa mwenzake. Cha ajabu kabisa vazi hilo linavaliwa gizani!
Sasa fikiria mwenzako akiliona la yule kwenye mwanga si atavutika, si atalitamani , matokeo yake yatakuwaje...
Endelea dada Dinah.
Huo ndio mchango wangu
Emu-three

Anonymous said...

hii ya leo kali.personally with all my respect to you dinah,sikubali kamwe kama cheating inaweza kuokoa uhusiano wako.Just think about it shoshti.Katika mida na nyakati tulizonazo za hatari ya kutupwa (AIDS) ,Please sitaki kukubaliana na wewe kwa hili.Kwa nini tusijitahidi kuwa waaminifu tukaishi kwa furaha.Anyway at the end of the day thats the way you see it and i figure it this way.Thanks

Anonymous said...

dinah hii mada ni nzuri ila ni very sensitive sana sababu ina touch personal feelings za watu especially mtu ambaye kumtarajia anatoka na mwenzi wako ni kweli kabisa. nasubiria maelezo yako zaidi kuhusu utatuzi wa hili ila kweli kwa mtu ambaye ulimwanimi sana then akacheat tena na rafiki au jirani au wengine hata ndugu, housegirl/ houseboy/shambaboy. mmh ni kasheshe lakini watu wanavumiliana tu na wanaishi ila kasheshe ni kwenye kuaminiana.

Anonymous said...

Dina kawakweli hili jambo linatokea sana katika mahusiano mengi japo ni jambo ambalo watu hatuko wazi kuliongelea. Lakini nafikiri likiongelewa litasaidia kupungua na kutovunja mahusiano ya watu. Kwa mtazamo wangu ni kwamba cheating ni indication ya mapungufu katika mahusiano ya kimapenzi. Na hii mara nyingi inatokea watu wanapo jenga mazoea katika mapenzi,matokeo yake akshi za mapenzi na vionjo vya kuridhishana vinaanza kupungua. Hapo basi mwenzio akikutana na anayempa ma-care hata suna tu nirahisi kuanguka na ku-cheat.Mimi Dina hii mada naichukua kama somo kuwa kuzuia cheating kati yenu dawa ni ku-sustain mahaba kati yenu and mostly kwa kuwa wazi/open.

Anonymous said...

Dina mimi umenigusa sn kwani yamenitokea mume anarudi saa 8 ucku namuuliza anasema alikua msibani alivyolala sms ikaingia yeye alikua amelala nikasoma sms inasema asante mpenzi wangu umeniacha na raha manake leo umenipa ufundi wooote ucku mwema iliniuma sn nilipouliza badala ya kuijbu swali amekazana kwa nini umesoma sms yangu na hii c mara moja kurudi uck mwingi tulifunga ndoa knsn na tuna miaka 3 ya ndoa mtt 1 nifanyeje na mimi hanpi unyumba yapata mwezi sasa wote ni wafanyakazi nisadie kwa mawazo

Dinah said...

Anony @ 1:23:00 PM, Pole kwa yaliyotokea. Kitu kama hicho kikitokea hupaswi kuulizia kuhusu sms kwani ni kawaida kwa mkosaji kujaribu ku-cover up nakurudish akosa kwako ili aweze kukimbia kujibu shutuma. Ulichotakiwa kufanya ni kutafuta namna ya kuwakilisha hofu zako juu yake.

Nakushauri uzungumze nae na uwakilishe hoja zako kwa upole na upendo (sio kwa hasira) kw avile umegundua kuwa hupewi unyumba basi uliza kwanini hampeani mambo fulani au unaweza ukajaribu kutafuta muda na kufanya usiku wa mahaba na uume pamenzi hajawahi kuyaona au hujawahi kumpa kisha ndio wakilisha hoja yako bila kumrushia shutuma za sms.


base zaidi kwenye nini uta-offer kwenye uhusiano wenu, uliza maswali mwengi lakini sio kwa njia ya maswali bali kuzungumza na hakika ataweka wazi anachokitaka kutoka kwako amabcho kinampeleka nje.

Kwa vile umesema nyote mnafanya kazi ni wazi kuwa wewe mara nyingi huwa unachoka zaidi kuliko yeye au kutokana na msongamano wa kazi (stress) hujisikii khamu yakufanywa/fanya na hivyo unakataa tendo kutokana na uchovu au yeye ana "libido" kubwa kuliko wewe na hivyo haridhiki na ngono kwa kipimo.

Kila la kheri.

Anonymous said...

kazi nzuri but cheating isikie hivo hivo,unaweza jiua bure