tag:blogger.com,1999:blog-3242810584517347839.post6671020093397682371..comments2023-06-04T11:15:25.464+03:00Comments on Dinahicious-Relationships, Love & Marriage: Mke asikiliza wambea na sasa tunaishi ki Juma na RozaKKMiehttp://www.blogger.com/profile/03913977764860036912noreply@blogger.comBlogger8125tag:blogger.com,1999:blog-3242810584517347839.post-11002816895655031032010-03-06T11:10:36.001+03:002010-03-06T11:10:36.001+03:00Ndugu yangu chanzo cha kuvunja ndoa ni wewe mwenye...Ndugu yangu chanzo cha kuvunja ndoa ni wewe mwenyewe. Kwanza hujaonyesha kujali tatizo linalomkabili mkeo, kama ungekuwa ulionyesha kujali basi hata hzo pombe ima ungeacha au ungenywea nyumbani. Vipi kaka try to analyse what makes ur wife not to trust u, then keep away frm that. Amiin nakwambia kilaji kinawatoa wa2 wengi kwenye nuru na kuwapeleka kwenye kiza, ikiwa wataka mkeo basi acha pombe na ikiwa wataka pombe basi kubali mkeo aondoke, kila m2 anahisia na cku zote m2 anaekupenda lazima aumie hasa akisikia habari za usaliti awe amethbitisha au laa. Mwisho wa yote ni kwamba chunguza pia mwenendo wa mkeo, kulikoni anakomalia kuondoka kuliko kutatua tatizo????? Take care bro that is bitter sweet of mariage.
MwatimaAnonymousnoreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-3242810584517347839.post-91068078184234789222010-03-04T12:39:49.328+03:002010-03-04T12:39:49.328+03:00ukisikiliza wembea siku zote mtagombana.kama huyo ...ukisikiliza wembea siku zote mtagombana.kama huyo mwananmke anakupenda kweli mwambie asisikilize watu otherwise hakupeni pole sana ndugu?mdauAnonymousnoreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-3242810584517347839.post-36720450772969124142010-03-04T11:37:18.441+03:002010-03-04T11:37:18.441+03:00UJIO MPYA WA DARHOTBOARD 'DHB FORUM'
ULIS...UJIO MPYA WA DARHOTBOARD 'DHB FORUM'

ULISHAWAHI KUWA MEMBER WA DARHOTBOARD ' DHB FORUM' SASA NI WAKATI WA KUKANDAMIZA UPYA TENA BAADA YA DHB KURUDI KISASA ZAIDI

HIVYO BASI UNAITWA KAMA ULIKUWA MEMBER INGIA KWA JINA LAKO LILE LILE AU LA JIANDIKISHE UPYA, TUANZA MAKAMUZI UPYA.

WAPI MASAKI,BABY KIBAKI, MSJACQUE,LIVECAT,MC ZOBIZOBI,GAIZKA,BIMKORA,DUMISANE,GEEQUE,MALIWAZA.MALISAK,FUNZADUME,NAILA,JANNY,LUCKY ONE,DR MUATHU, DINAH,MCHAICHAI,MADOIDO,PAPAK,TZKWELI,MTOTOWA MJINI NA WENGINEO WEEENGI NI WAKATI WAKUJUMUIKA UPYA NA KUANZA KUSOGOA KAMA KAWA

BOFYA
http://www.darhotwire.com/forums

KARIBU SANA

DHB TEAM

*****Madam nirushie hiyo plz kijiweni kwako maana najua wana wa mapenzi na mapendi washinda huku

zeze...udelete post sio upostshamim a.k.a Zezehttps://www.blogger.com/profile/13656930199966929799noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-3242810584517347839.post-14569728298480311942010-03-03T13:16:01.920+03:002010-03-03T13:16:01.920+03:00Inavyoelekea huyo bi dada anapalia nyumba yake mot...Inavyoelekea huyo bi dada anapalia nyumba yake moto sasa itakapoungua ibaki gofu ndo atakapoisoma namba kwa nyuma wakati hao mashostito wanaompa umbea wanamla kisogo na kumuona punguwani kwa kuharibu ndoa yake wakati wao wapo na wapenzi/waume zao wanakula bata tu.

Kaka mi naona ndoa yenu bado changa hamna haja ya kuachana au na wewe kumshushia varangati, ila sio siri na sisi wanawake tunamidomo michafu jamani yani mtu anaweza akakushushia mitusi mpaka unajiuliza hivi na huyu kazaliwa na mwanamke mwenzangu ama? halafu saa nyingine upeo wetu wa kufikiri umekuwa mdogo sana, inabidi tubadilike mambo yakusikiliza mashoga na umbea yamepitwa na wakati, uwe na shoga ambae mnakaa na kupanga vitu vya maendeleo, shoga wa kupiga umbea wa kazi gani anakuchosha tu na maneno yasiyokuwa na staha.

Ushauri wangu kwa sababu hali ni tete itisheni kikao cha wanandugu kila mmoja wenu aeleze matatizo yake, ninaamini mtasuluhishwa na ndoa yenu itakuwa shwari na mapenzi motomoto.Pole kaka ndo mitihani ya ndoa hiyo, wenyewe huwa tunaapa for better for worse, sasa vumilia tu hiyo worse but you shall overcome majaribu kaumbiwa mwanadamu.Anonymousnoreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-3242810584517347839.post-47142340355930323192010-03-03T09:42:12.067+03:002010-03-03T09:42:12.067+03:00Pole kaka manuel. Mimi naona huyo mkeo labda amesa...Pole kaka manuel. Mimi naona huyo mkeo labda amesahau msemo usemao Mwanamke mpumbavu hubomoa nyumba yake mwenyewe. Maneno ya kuambiwa ukiyasikiliza sana yatapelekea kuharibu ndoa yako, afterall hujapata ushahidi kama mwenzi wako anafanya kitu kibaya ni bora achunguze kwanza pia na wewe kaka badili tabia uwe nae mkeo karibu, onyesha kumjali hiyo itamfanya akuamini hata hao magossip wakimwambia kitu akifananisha na the way unampenda haweziwaamini.

Jinyenyekeze muanze upya ukurasa wa mapenzi.mamaBnoreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-3242810584517347839.post-58942868015211937932010-03-02T11:04:51.380+03:002010-03-02T11:04:51.380+03:00Pole kaka kulingana na maelezo yako mimi nadhani s...Pole kaka kulingana na maelezo yako mimi nadhani si kwamba anasikiliza ya wambea labda yeye kapata mtu mwingine ndio maana anatafuta sababu ya wewe kumfukuza.ushauri kaa na mkeo muongelee masuala yenu na umpe nafasi ya yeye kueleza kile kilicho moyoni mwake unajua unapotoa kilicho ndani unapunguza maumivu na pia ajue kwamba nyumba haijengwi na watu wa nje bali nanyi wawili na ndoa ina mlango wa kuingia tu hakuna wa kutoka. Pia mweleza ubaya wa kutoa maneno machafu(matusi) mbele ya mtoto kwani ubongo watoto ni rahisi sana kukata vitu kwa hiyo asije akampiga mtoto pindi atakapokuta mtoto wake akitukana, neno la Mungu linasema mlee mtoto katika njia inayofaa naye hataiacha hata atakapokuwa mzee. pia jenga mazoea ya kutoka naye hata kama hanywi pombe yeye atakunywa vinywaji laini ila atakuwa nawe hivyo kueposha maneno ya watuAnonymousnoreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-3242810584517347839.post-58921859269021935182010-03-02T09:10:41.046+03:002010-03-02T09:10:41.046+03:00mhh!hapo pagumu kaka,ila km unampenda mkeo tafuta ...mhh!hapo pagumu kaka,ila km unampenda mkeo tafuta njia mbadala muweze kutatua tatizo lenu.kusema kumuacha huo ni udhaifu labda km kweli naww unakimwanamke huko unapoenda kunywa pombe,na baada ya kuyaweka sawa mambo yenu hakikisha naenda wote huko unapoenda hata km hanywi pombe hiyo kidogo itasadia au sio lazima uende bar mbona unaweza hata ukanunua na kunywa kwako!ukiwa mnaongea na mkeo kuliko kungangania kwenda baa matatizo mengine unayasababisha we mwenyewe.kikubwa ktk maamuzi yenu mumuangalie mtt wenu ambaye bado mdogo na anayehitaji malezi ya wazazi wote 2.ni hayoAnonymousnoreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-3242810584517347839.post-64597248053946178242010-03-02T06:59:24.759+03:002010-03-02T06:59:24.759+03:00Heeeeee kumbuka kuwa penye wengi pana mengi.Huko k...Heeeeee kumbuka kuwa penye wengi pana mengi.Huko kilabuni unakoenda kunywa ndiko unakowakuta hao wambea wanaenda kummwagia radhi mkeo.Unajua hata ukicheka na mwanamke tu wanapeleka habari kwa mkeo.

Mimi nakushauri kama unataka kuwa salama na mkeo achana na pombe kabisaa au agiza nywea home.Hakuna njia nyingine kwenye michanganyiko ya watu wengi hasa kwenye mapombe haku na jema hata kidogo.Kimbia kabisa maeneo ya vilabuni.Kama kweli unampenda mkeo basi pombe si kitu cha kushikamana nacho.Tafuta kitu kingine mbadala badala ya pombe.

Kila mwanamke atakuwa hivyo tu amini usiamini hakuna anayetaka aibiwe.Hata kama kwa sasa hunywi sana lakini ipo siku utazidiwa.Mwambie mkeo kwamba umeacha pombe kwani ndicho chanzo cha kutokuaminiana ndani.Kwa sasa ukitoka ulikotoka wewe chonga hadi home na msaidie mkeo kazi hapo home panga kazi mbali mbali mwende pamoja jioni mkafanye mambo yatakuwa mswamo kabisa.Usimwelewe vinaya mkeo hali ya pombe si salama kabisa vinginevyo na yeye awe anakunywa mnaenda wote.

Pole dogo lakini achana na pombe ili unusuru ndoa yako.Anonymousnoreply@blogger.com